Ufalme Wako Uje
Kuona na kuamini miujiza ya Bwana katika kuendeleza ufalme Wake hapa duniani kunaweza kutusaidia kuona na kuamini kwamba mkono wa Bwana unatenda kazi katika maisha yetu wenyewe.
Tunapokuwa tunaimba, nilivuta kwa kina na wazo kwamba dakika hii hii mamia ya maelefu, labda mamilioni, Watakatifu waaminio katika zaidi ya nchi 150, na kushangaza lugha 75 tofauti,1 wamekusanyika tunapopaza sauti zetu kwa Mungu, wakiimba:
Njoo, Ewe Mfalme wa Wafalme!
Tumekuongea kwa muda mrefu,
Na uponyaji kwenye mbawa zako,
Uwaweke huru watu wako.2
“Njoo, Ewe Mfalme wa Wafalme!”3 Sisi ni familia kubwa ya waaminio duniani kote, wafuasi wa Bwana Yesu Kristo..
Tumejichukulia jina Lake juu yetu, kila wiki tunapokea sakramenti, tunaweka ahadi kwamba tutamkumbuka Yeye na kuweka amri Zake. Sisi tuko mbali sana na ukamilifu, lakini sisi hatuna uholela katika imani yetu. Tunaamini katika Yeye. Tunamwabudu Yeye. Tunamfuata Yeye. Tunampenda Yeye. Yetu ni kazi kuu katika ulimwengu wote.
Tunaishi, akina ndugu na dada, katika siku zinazotangulia Ujio wa Pili wa Bwana, uliotarajiwa sana na waminio katika vipindi vyote. Tunaishi katika siku za vita na uvumi wa vita, siku za majanga ya kiasili, siku ambapo ulimwengu unavutwa na mkanganyiko na vurugu.
Lakini pia tunaishi katika nyakati tukufu za Urejesho, ambapo injili inapelekwa ulimwenguni kote---wakati ambapo Bwana ameahidi kwamba Yeye “atainua … watu halisi”4 ambao Yeye atawaami “na wema na nguvu za Mungu.”5
Tunafurahia katika shangwe na kuridhika kwetu, na tunatumaini kukabiliana kwa ujasiri na masumbuko na dharura. Mambo magumu wengine ni makali sana kushinda wengine, lakini hakuna yeyote aliye na kinga. Mzee Neal A. Maxwell wakati mmoja aliniambia, “Kama kila kitu kinaenda vyema sana kwako sasa, ngoja tu
Ingawa Bwana ametuhakikishia tena na tena kwamba sisi “tusiogope,”6 kuweka mtazamo msafi na kuona zaidi ya ulimwengu huu daima si rahisi wakati tupo miongoni mwa majaribu.
Rais Thomas S. Monson alinifunza somo muhimu kuhusu kuweka mtazamo wa milele.
Miaka kumi na nane iliyopita nikiwa ninasafiri na gari moshi katika Switzerland na Rais Monson, nilimuuliza kuhusu majumuku yake mazito. Jibu lake liliimarisha imani yangu. “Katika Urais wa Kwanza,” Rais Monson alisema, “tunafanya kila kitu tuwezacho kuendeleza kazi hii mbele. Lakini hii ni kazi ya Bwana. Yeye anailekeza. Yeye ndiye aliye katika usukani. Sisi hushangaa tunapotazama Yeye anapofungua mlango ambao sisi hatuwezi kufungua na kutenda miujiza ambayo kamwe hatuwezi kuifikiria.”7
Ndugu na kina dada, kuona na kuamini miujiza ya Bwana katika kuendeleza ufalme Wake hapa duniani kunaweza kutusaidia kuona na kuamini kwamba mkono wa Bwana unatenda kazi katika maisha yetu wenyewe pia.
Bwana alitamka, “Ninaweza kufanya kazi yangu mwenyewe.”8 Kila mmoja anajaribu kufanya sehemu yake, lakini Yeye ndiye msanifu mkuu. Chini ya maelekezo ya Baba Yake, Yeye aliumba ulimwengu. “Vitu vyote vilifanywa naye; na pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.”9 Jinsi tulivyo macho na hadhari kiroho, tunaona mkono Wake duniani kote na tunaona mkono Wake katika maisha yetu binafsi.
Acheni nishiriki mfano mmoja.
Katika mwaka wa 1831, pakiwa na tu waumini 600 wa Kanisa, Bwana alisema, “Funguo za ufalme wa Mungu zakabidhiwa kwa mwanadamu duniani, na kutoka huko injili itaenea hata miisho ya dunia, kama vile jiwe lililochongwa mlimani bila kazi ya mikono litabiringika, hadi litaijaza dunia yote.”10
Nabii Nefi aliona kwamba kungekuwa na waumini “wachache” wa Kanisa inapolinganishwa na idadi ya ulimwengu lakini kwamba wangekuwa “kote ya usoni mwa dunia.”11
Mifano mitatu mizuri ya mkono wa Bwana katika kuendeleza ufalme Wake ni mahekalu yaliyotangazwa leo na Rais Monson. Miongo michache, nani angedhania kunaweza kuwa mahekalu katika Haiti, Thailand, na Ivory Coast?
Eneo la hekalu siyo uamuzi rahisi kijiaografia. Unakuja kwa ufunuo kutoka kwa Bwana hata kwa nabii Wake, kuonyesha kazi kuu itakayofanyika na kuthibitisha wema wa Watakatifu ambao watathamini na kuitunza nyumba Yake katika vizazi vyote.12
Mke wangu. Kathy, nami tulitembelea Haiti miaka miwili tu iliyopita. Huko juu mlima ulio juu ya Port-au-Prince, tuliungana na Watakatifu wa Wahaiti kuadhimisha kuwekwa wakfu nchi hiyo na Mzee Thomas S. Monson miaka 30 tu mapema. Hakuna yeyote kati yetu atakayesahau mtetemeko haribifu wa 2010. Waumini waaminifu na kundi la wamisionari wajasiri la karibu Wahaiti, Kanisa katika hili taifa la kisiwa linaendelea kukua na kuimarika. Inainua imani yake kuwaona hawa Watakatifu wema wa Mungu, wamevalia mavazi meupe, wakiwa na uwezo wa ukuhani mtakatifu kuongoza na kufanya ibada takatifu katika nyumba ya Bwana.
Nani angedhania kuwaweza na nyumba ya Bwana katika mji maridadi wa Bangkok?, Wakristo ni asiliamia moja tu ya nchi ambao kwa kawaida ni ya Kibudha. Kama Haiti, tunaona pia katika Bangkok kwamba Bwana amekusanya wateule wa ulimwengu. Nilipokuwa huko miezi michache iliyopita, tulikutana na Sathit na Juthamas Kaivalvatana na watoto wao. Sathit alijiunga na Kanisa alipokuwa umri wa miaka 17 na akahudumu misheni katika nchi yake. Baadaye alikutana na Juthamas katika chuo, walifunganishwa katika Hekalu la Manila. Mwaka wa 1993 familia ya Kaivalvatana waligongwa na lori ambalo dereva wake alikuwa anasisinzia. Sathit alilemaa kutoka kwa kifua chake hata miguuni. Imani yao kamwe haijayumba. Sathit ni mwalimu anayependwa katika International School Bangkok. Anahudumu kama rais wa Kigingi cha Thailand Bangkok North. Miujiza ya Mungu ipo katika kazi Yake na katika maisha yetu binafsi.
Muujiza wa Kanisa katika Ivory Coast haiwezi kusimuliwa bila kutaja majina ya familia mbili. Philippe na Annelies Assard, na Lucien na Agathe Affoue. Wao walijiunga na Kanisa kama wana ndoa vijana huko Uropa, wa kwanza Ujerumani na wa pili katika Ufaransa. Katika miaka ya 1980, bila kujuana Philippe na Lucien walihisi kuvutwa warudi katika nchi yao kuzaliwa ya Kiafrika kwa madhumuni ya kujenga ufalme wa Mungu. Kwa Dada Assard, ambaye ni Mjerumani, aliacha familia yake, na kumruhusu mume wake aache ajira yake kama mhandisi mashuhuri, kulihitaji imani isiyo ya kawaida. Hizi familia mbili zilikutana mara ya kwanza katika Ivory Coast na wakaanza Shule ya Jumapili. Hiyo ilikuwa miaka 30 iliyopita. Sasa kuna vigingi vinane na waumini 27,000 katika hii nchi maridadi ya Kiafrika. Kina Affoue wanahudumu kwa heshima, vile vile kina Assard, ambao hivi majuzi wamemaliza misheni katika Hekalu la Accra Ghana.
Je! Unaweza kuona mkono wa Mungu ukiendeleza kazi Yake mbele? Je! Unaweza kuona mkono wa Mungu katika maisha ya familia ya Assard na Affoue? Je! Unaweza kuona mkono wa Mungu katika maisha yako mwenyewe?
“Na katika lolote mwanadamu hamkosei Mungu ... isipokuwa wale tu wasiokiri mkono wake katika mambo yote, na wasiotii amri zake.”13
Miujiza ya Mungu haitendeki tu katika Haiti, Thailand, au Ivory Coast. Tazama karibu nawe. .14 “Mungu ni mwangalifu kwa kila watu … ; ndio, huhesabu watu wake, na ana huruma za kutosha kwa ulimwengu wote.”15
Wakati mwingine tunaweza kuona mkono wa Bwana katika maisha ya wengine basi tukashangaa, “Ninaweza kuuona vyema mkono Wake katika maisha yangu mwenyewe?”
Mwokozi alisema:
“Usiwe na shaka.”16
“Usiongope.”17
“Wala … hata [mashomoro] mmoja … haanguki chini [asipojua] Baba yenu. …
“ Msiogope … basi; bora ninyi kuliko mashomoro wengi.”18
Kumbuka kijana ambaye alimlilia nabii Elisha katika walipokuwa wamezinirwa na maadui: “Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje?”19
Elisha akamjibu:
“Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.
“[Kisha] Elisha akaomba, … Bwana, … mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana [akamfumbua] macho yule mtumishi; naye [akaona kile] kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.”20.
Unapoomba kwa imani ili uone mkono wa Bwana katika maisha yako, nakuahidi kwamba Yeye afumbua macho yako ya kiroho kabisa, na utaona wazi zaidi kwamba wewe hauko peke yako.
Maandiko yanafundisha kwamba tunapaswa “[kusimama] imara katika imani kwa yale yanayokuja.”21 Ni nini kitachokuja? Mwokozi alisali:
“Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe,.
“Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.”22
Sisi sote tumeimba “Njoo, Ewe, Mfalme wa Wafalme.”
Imani yetu hukua tunapotarajia siku tukufu ya kurudi kwa Mwokozi ulimwenguni. Wazo la kuja Kwake huchochea nafsi yangu. Itakuwa jambo la kushusha pumzi! Uwezo, na ukuu, upana na utukufu, utazidi chochote kile macho ya mwanadamu yameshapata kuona au kuzoea.
Siku hiyo, Yeye hatakuja amefungwa na nguo amelala katika hori,”23 bali Yeye atatokea “katika mawingu ya mbinguni, amevikwa nguvu na utukufu mkuu; pamoja na malaika wote watakatifu.”24 Tutasikia “sauti ya malaika mkuu, na … parapanda ya Mungu.”25 Jua na mwezi vitabadilishwa na “nazo nyota zitaondoshwa kutoka mahali pake.”26 Wewe nami, au wale wanaotufuata sisi, “watakatifu ... kutoka [pande zote] za dunia,”27 “watahuishwa na ... kunyakuliwa mawinguni kwenda kumlaki yeye,”28 Wale walifariki katika wema, wao pia “watanyakuliwa kwenda kumlaki yeye katikati ya ... ya mbinguni.”29
Basi, tukio ambako kabisa ni vigumu kufikirika: “Wote wa mwili”, Bwana asema, “wataniona kwa pamoja.”30 Itatendeka vipi? Sisi hatujui. Lakini itatendeka---kabisa vile ilivyotabiriwa. Tutapiga magoti kwa staha. “Na Bwana atatoa sauti yake, na miisho yote ya dunia itaisikia.”31 Na itakuwa ... kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu.”32 [Kisha] Bwana, … Mwokozi, atasimama katikati ya watu wake.”33
Kisha yatakuja kukutana kusikosahaulika kwa malaika wa mbinguni na Watakatifu juu ya nchi.34 Lakini cha muhimu sana, Isaya alitangaza, “Na ncha zote za dunia zitauona wokovu wa Mungu wetu,”35 na Yeye “naye atatawala juu ya wote wenye mwili.”36
Katika siku hiyo, wenye shaka watakimya, “kwani kila sikio litasikia … , na kila goti litapigwa, na kila ulimi utakiri”37 kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu.
Leo ni Pasaka. Tunasherehekea katika Ufufuko Wake Mtukufu na katika ufufuo wetu wenyewe ulioahidiwa. Na tujiandae kwa ujio Wake, kwa kuyarudia haya matukio matukufu tena na tena katika akili zetu na pamoja na wale tuwapendao. Na maombi Yake yawe maombi yetu “Ufalme Wako uje. Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.”38 Mimi nashuhudia kwamba Yeye yu hai, “Njoo, Ewe Mfalme wa Wafalme.” Katika jina la Yesu Kristo, amina.