Ubaba---Majaliwa Yetu ya Milele
Natuweze wote kufurahia wingi wa baraka za Baba katika maisha haya na utimilifu wa kazi Yake na utukufu Wake kwa kuwa akina baba milele.
Baba yangu alinifundisha somo lenye maana nilipokuwa kijana. Aligundua kwamba nilikuwa ninavutiwa sana na mambo ya dunia. Wakati nilipokuwa na pesa, mara moja nilizitumia---takribani kwa matumizi yangu binafsi.
Siku moja alasiri alinichukua kwenda kununua viatu vipya. Kwenye ghorofa ya pili ya duka, alinitaka niangalie nje ya dirisha pamoja naye.
“Unaona nini?” aliuliza.
“Majengo, anga, watu” lilikuwa jibu langu.
“Mangapi?”
“Mengi sana!”
Ndipo alitoa sarafu hii kutoka mfukoni mwake. Alipokuwa ananipatia, aliniuluza,”Hii ni nini?’
Mara moja nilijua: “Sarafu ya fedha ya dola!”
Akitumia ujuzi wake wa elimu ya kemia, alisema, “Kama utayeyusha dola ile ya fedha na kuichanganya pamoja na viungo vifaavyo, utaweza kupata naitreti ya fedha. Kama tungepaka dirisha hili na naitreti ya fedha, ungeona nini?”
Sikuwa na wazo, kwa hiyo alienda nami kwenye kioo kizima na akaniuliza,”Sasa unaona nini?”
“Najiona mwenyewe”
“Hapana,”alijibu, “Unachoona ni fedha ikiakisi mfano wako. Kama ukizingatia kwenye fedha, vyote utavyoona ni wewe mwenyewe, na kama pazia, itakuzuia kuona kwa uwazi majaliwa ya milele Baba wa Mbinguni ametayarisha kwa ajili yako.”
“Larry,”aliendelea, “usitafute mambo ya dunia hii lakini tafuta … kwanza … ufalme wa Mungu, na asisi uadilifu [Wake]; na vitu hivi vyote utaongezewa”(Tafsiri ya Joseph Smith, ya Matayo 6:38 [katika Mathayo 6:33, tanbihi a]).
Aliniambia niitunze ile dola na kamwe nisiipoteze. Kila wakati nilipoiangalia, nilikuwa ninafikiria kuhusu majaliwa ya milele ambayo Baba wa Mbinguni anayo kwa ajili yangu.
Nilimpenda Baba yangu na jinsi alivyofundisha. Nilitaka niwe kama yeye. Alipanda katika moyo wangu hamu ya kuwa baba mzuri, na tumaini langu kubwa ni kwamba ninaishi kufuatana na mfano aliouweka.
Nabii wetu mpendwa, Rais Thomas S. Monson mara kwa mara amesema kwamba maamuzi yetu yanaamua majaliwa yetu na yana matokeo ya milele (ona “Decisions Determine Destiny” [Church Educational System fireside, Nov. 6, 2005], 2; lds.org/broadcasts).
Hatupaswi basi, kukuza ono wazi la kudra yetu ya milele,, zaidi hasa lile moja Baba wa Mbinguni anatutaka tufanikishe---ubaba wa milele? Wacha kudra yetu ya milele, iwe kipengele cha maamuzi yetu yote. Bila kujali ya jinsi ugumu matatizo hayo yanaweza kuwa, Baba atatuhimili.
Nilijifunza kuhusu nguvu ya ufahamu kama huu wakati nilipojiunga na wana wangu wa umri wa miaka12 na 13 kwa mashindano ya 50/20. 50/20 ni sawa na kutembea maili 50 (kilomita 80) chini ya masaa 20. Tulianza saa 3.00 usiku na tulitembea usiku ule mzima na karibu siku ya pili. Yalikuwa masaa 19.00 ya kuchosha, lakini tulifanikiwa.
Tuliporudi nyumbani tulitambaa haswa kuingia nyumbani, ambamo mke wa ajabu na mama alikuwa ametayarisha chakula cha mchana kizuri sana, ambacho hatukuweza kukila. Mwana wangu mdogo alijibwaga, akiwa amechoka kabisa, kwenye kochi, huku mwana wangu mkubwa akitambaa kuteremka ngazi kwenda kwenye chumba chake cha kulala.
Baada ya mapumziko yangu ya maumivu kiasi, Nilikwenda kwa mwana wangu mdogo kuhakikisha alikuwa bado mzima.
“Uko sawa?” Niliuliza
“Baba, kile kilikuwa kitu kigumu sana nilichowahi kufanya, na kamwe sitaki kukifanya tena,”
Sikuwa karibu kumwambia kwamba kamwe sitafanya tena vilevile. Badala yake, nilimwambia jinsi ninavyojivunia kwamba alikamilisha kitu kigumu kama kile. Nilijua kingemtayarisha kwa vitu vingine vigumu atakavyokabiliana navyo hapo baadaye. Pamoja na wazo lile, nilisema, “Mwanangu, niruhusu nikupe ahadi hii. Wakati utakapo kwenda kwenye misheni yako, kamwe hutatembea maili 50 (kilomita 80) katika siku moja.”
“Vyema, Baba! Kwa hiyo ninakwenda”
Maneno hayo mepesi yalijaza roho yangu na shukrani na furaha.
Kisha nilishuka ngazi kwenda kwa mvulana wangu mkubwa. Nililala karubu naye---kisha nilimgusa. “Kijana, uko sawa?”
“Baba, kile kilikuwa kitu kigumu sana nilichoweza kukifanya maishani mwangu, na kamwe sitaweza aslani kukifanya tena.” Macho yake yalifunga---kisha akafungua---na alisema, “Isipokuwa mvulana wangu ananihitaji pia.”
Machozi yalitiririka wakati nilipoelezea jinsi nilivyokuwa na shukrani juu yake. Nilimwambia nilijua angekuwa baba mzuri sana kuliko nilivyokuwa. Moyo wangu ulijawa na furaha kwa sababu katika umri wake mdogo tayari alitambua kwamba moja ya kazi zake muhimu sana za ukuhani mtakatifu ilikuwa kuwa baba. Hakuwa na woga wa jukumu lile na cheo---cheo sahihi ambazo Mungu Mwenyewe anataka sisi tutumie wakati tunaposema naye. Nilijua nilikuwa na wajibu wa kulea matamanio ya ubaba ambayo yalikuwa yanawaka ndani ya kijana wangu.
Maneno haya ya Mwokozi yalikuwa na maana ya kina zaidi kwangu kama baba.
“Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe, ila lile ambalo amwona baba analitenda: kwa maana [yote ayatendayo yeye], ndiyo ayatendayo Mwana vile vile (Yohana 5:19).
“Sifanyi neno kwa nafsi yangu; ila kama Baba alivyonifundisha” (Yohana 8:28).
Ninapenda kuwa mume na baba---nimeoa binti mteule wa wazazi wetu wa mbinguni. Ninampenda. Ni mojawapo ya sehemu za utimilisho wa maisha yangu. Matumaini yangu usiku ule yalikuwa kwamba wavulana wangu watano na dada yao wataweza kuona siku zote ndani yangu furaha ambayo inakuja kutokana na ndoa ya milele, ubaba, na familia.
Akina baba, Nina hakika mmesikia msemo “Hubiri injili wakati wote, na inapobidi tumia maneno”(kutoka kwa Fransis wa Assissi). Kila siku unawafundisha watoto wako nini inamaanisha kuwa baba. Unajenga msingi kwa ajili ya kizazi kijacho. Vijana wako watajifunza jinsi ya kuwa waume na mababa kwa kuangalia jinsi unavyotekeleza wajibu huu. Kwa mfano:
Wanajua jinsi kiasi gani unawapenda na kumtunza kwa upendo mama yao na kiasi gani unapenda kuwa kuwa baba yao?
Watajifunza jinsi ya kufanya mbele ya wake na watoto wao wa baadaye wakati wanakuangalia mnavyowatendea kila mmoja wao sawa sawa kama Baba wa Mbinguni angefanya.
Kupitia mfano wako, wao wanaweza kujifunza jinsi ya kustahi, kuheshimu, na kulinda umama.
Ndani ya nyumba yako, wanaweza kujifunza kuongoza familia zao kwa upendo na haki. Wanaweza kujifunza umuhimu wa maisha na ulinzi kwa familia zao---kimwili na kiroho (ona “The Family: A Proclamation to the World,” Ensign or Liahona, Nov. 2010, 129).
Ndugu, kwa nguvu zangu zote za moyoni, Nina kuombeni kufikiria swali hili: Je! Vijana wenu wanawaoneni mkijitahidi kufanya kile Baba wa Mbinguni angependa wao wafanye?
Ninaomba kuwa jibu ni ndio. Kama jibu ni la, hamjachelewa sana kubadilisha, lakini ni lazima muanze leo. Ninashuhudia kwamba Baba wa Mbinguni atawasaidieni.
Sasa vijana, mnajua mnajitayarisha kupokea Ukuhani wa Melkizediki, kupokea ibada takatifu za hekaluni, kutimiza wajibu na majukumu yenu kuhudumumisheni ya muda, na kisha bila kungojea kwa muda mrefu, kufunga ndoa ndani ya hekalu na binti ya Mungu na kuwa na familia. Ndipo unatakiwa kuongoza familia yako katika mambo ya kiroho kama unavyoongozwa na Roho Mtakatifu (ona M&M 20:44; 46:2; 107:12).
Nimewauliza Vijana wengi, “Kwa nini mpo hapa?”
Hadi hapa, hakuna hata mmoja aliyejibu, “Kujifunza kuwa Baba, ili kwamba niweze kujitayarisha na kustahili kupokea vitu vyote ambavyo Baba wa Mbinguni anavyo.”
Na tuchanganue wajibu wenu wa Ukuhani wa Haruni kama ulivyoelezwa katika sehemu ya 20ya Mafundisho na Maagano. Uwe mwepesi wa kuhisi kwa kile wewe unahisi ninapotimiza wajibu huu kwa huduma yako katika familia yako.
“Wakaribishe wote [wa familia yako] kuja kwa Kristo” (mstari wa 59).
“Kuwaangalia [wao] siku zote, na kuwa nao na kuwaimarisha” (mstari wa 53).
“Kuhubiri, kufundisha, kuelezea, kushawishi na kubatiza” wanafamilia yako (mstari wa 46).
“Kuwashawishi kusali kwa sauti na kwa siri na kushughulikia kazi zote za familia” (mstari wa 47).
“Kuona kwamba hakuna uovu katika [familia yako],wala kuzozana baina yao,wala kudanganya, kusengenyana, wala kusemana mabaya” (mstari wa 54).
“Ona kwamba [familia yako inakutana ] pamoja mara kwa mara” (mstari wa 55).
Msaidie Baba yako katika wajibu wake kama baba mkuu. Msaidie mama yako kwa nguvu za ukuhani wakati Baba hayupo mstari 52, 56).
Wakati unapoombwa, “tawaza makuhani wengine, waalimu, na mashemasi” katika familia yako (mstari wa 48).
Je! hii halionekani kama kazi na wajibu wa baba?
Kutekeleza wajibu wako wa ukuhani wa Haruni ni kuwatayarisha nyie wavulana wadogo kwa ubaba Nyenzo ya Wajibu kwa Mungu inaweza kukusaidia kujifunza kuhusu na kufanya mipango maalumu kutekeleza kazi zako. Inaweza kutumika kama mwongozo na msaada wakati unatafuta mapenzi ya Baba wa Mbinguni na kuweka malengo kuyakamilisha.
Baba wa Mbinguni amekuleta wewe hapa wakati huu maalumu kwa kazi maalum na kusudi la milele. Anakutaka wewe uone kwa uwazi na kuelewa kusudi lile ni nini. Ni baba yako, na unaweza wakati wote umgeukie kwa mwongozo.
Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni anajishughulisha kuhusu kila mmoja wetu binafsi na ana mpango binafsi kwa ajili yetu tuweze kutimiza majaliwa yetu ya milele. Alimtuma mwanawe pekee, Yesu Kristo, kutuasidia kishinda kutokamilika kwetu kupitia upatanisho. Ametubariki na Roho Mtakatifu awe shahidi, mwenza, na mwongozo kwenda kwenye hatima yetu ya milele kama tutamtegemea Yeye. Natuweze wote kufurahia wingi wa baraka za Baba katika maisha haya na ukamilifu wa kazi Yake na utukufu Wake kwa kuwa mababa milele (ona Musa 1:39). Katika jina la Yesu Kristo, amina.