Bwana ni Nuru Yangu
Uwezo wetu wa kusimama imara na wakweli na kumfuata Mwokozi licha ya mabadiliko ya maisha unaimarishwa na familia njema na umoja ambao kitovu chake ni Kristo katika kata zetu na matawi yetu.
Katika kipindi cha Pasaka tunatafakari na kufurahia ukombozi uliotolewa na Mwokozi, Yesu Kristo.1
Kelele zinazojirudia duniani kote kwa ajili ya uovu zinaleta hisia za ghasia. Tukiwa na mawasiliano ya kisasa madhara ya uovu, kukosa usawa, na udhalimu huleta hisia nyingi kwamba maisha hayako sawa. Bila kujali majaribu haya, hayatakiwi yatuvuruge katika kufurahi na kusherehekea utukufu wa Kristo kwa niaba yetu. Mwokozi hakika “alishinda kifo.” Kwa neema na huruma alijichukulia Mwenyewe maovu na dhambi zetu, hivyo kutukomboa na kutimiza mahitaji ya haki kwa wote watakaotubu na kuamini katika jina Lake.2
DhabihuYake kubwa ya upatanisho ni muhimu zaidi ya tunavyoweza kufikiria. Kitendo hiki cha neema kinaleta amani ambayo inapita uelewa wetu.3
Ni jinsi gani tunaweza kupambana na hali ya kikatili inayotuzunguka?
Mke wangu, Mary, mara yote amekuwa akipenda alizeti. Anaifurahia wakati akiiona katika sehemu tulivu, kando kando ya barabara. Tulipoanza kupita katika njia hiyo, Mary mara nyingi aliuliza, “Je, unafikiri tutaziona zile alizeti nzuri leo? Tulishangazwa kwamba alizeti inastawi katika udongo ambao umeathirika kwa vifaa vya kusafishia theruji na takataka nyingine ambazo haziwezi kufikiriwa kuwa udongo mzuri wa kustawisha maua pori.
Moja ya tabia za ajabu za maua pori machanga, katika nyongeza ya kukua kwenye udongo ambao ni mzuri, ni jinsi ua changa linavyochanua likifuata jua angani. Kwa kufanya hivyo, linapokea nguvu za kustawi kabla ya kuchanua na kutoa rangi tukufu ya njano.
Kama vile ua changa, tunapomfuata Mwokozi wa ulimwengu, Mwana wa Mungu, tunapendeza na kuwa watukufu bila kujali hali mbaya ambayo inatuzunguka sisi. Hakika Yeye ni nuru na uzima.
Katika fumbo la ngano na magugu, Mwokozi aliwaambia wafuasi wake kwamba wale wanaokosea na kutenda maovu watakusanyika nje ya ufalme Wake.4 Lakini akiwaongelea watiifu, Alisema, “Kisha wale wema watang’ara kama jua katika ufalme wa Baba yao.”5 Kama wafuasi wa Kristo, tuishio katika ulimwengu wenye uadui ambao ni vurugu tupu, tunaweza kukua na kuimarika tukiwa na upendo wa Mwokozi na kwa unyenyekevu tukifuata mafundisho Yake .
Uwezo wetu wa kusimama imara katika imani na kumfuata Mwokozi bila kujali mabadiliko ya maisha kunaimarishwa na familia zenye wema na umoja uliojengwa kwa Mwokozi katika kata na matawi yetu.6
Muda Sahihi Nyumbani
Jukumu la familia katika mpango wa Mungu ni “kutupa furaha, kutusaidia kujifunza kanuni sahihi kwa njia ya upendo, na kutuandaa kwa ajili ya uzima wa milele.”7 Tabia nzuri za kidini nyumbani inahitaji kupandikizwa kwenye mioyo ya watoto wetu.
Mjomba wangu Vaughn Roberts Kimball alikuwa mwanafunzi mzuri, mtunzi mzuri, na mchezaji wa mpira wa BYU. Desemba 8, 1941, siku moja baada ya mashamhulizi ya Pearly Harbor, alijumuishwa kwenye jeshi la wanamaji la Marekani. Akiwa kwenye mafunzo huko Albany, New York, aliandika makala kwenye Reader’s Digest. Jarida likamlipa $200 na wakachapisha makala yake iliyokuwa na kichwa cha habari “Muda Sahihi Nyumbani,” kwenye toleo la Mei 1944.
Mchango wake kwenye Reader’s Digest, ambapo alijitaja yeye kama mwanamaji, inasomeka hivi:
“Muda Sahihi Nyumbani:
“Jioni moja huko Albany, New York, nilimwuliza mwanamaji ilikuwa saa ngapi. Alitoa toka mfukoni saa kubwa na akajibu, “Ni saa 1:20.” Nilijua muda umepita. ‘Saa yako itakuwa ilisimama, ni kweli?’ Nikauliza.
‘“Hapana,’ alisema, ‘Bado nipo kwenye Mountain Standard Time. Mimi natoka Utah ya Kusini. Nilipojiunga na Jeshi la Maji, baba alinipa hii saa. Alisema ingenisaidia nikumbuke nyumbani.
“‘Wakati saa yangu inaposoma saa 11 asubuhi. Ninajua Baba anakwenda kukamua ng’ombe. Na usiku wowote inaposema saa 1:30 ninajua familia yote imekaa mezani, na Baba akimshukuru Mungu kwa chakula kilichopo mezani na kumwomba Mungu anilinde,’ … alihitimisha. ‘Ninaweza kujua ni muda gani popote nitakapo kuwepo kwa urahisi. Ninachotaka kujua ni muda gani sasa Utah.”’8
Mara baada ya kuwasilisha makala, Vaughn alipangwa kikazi huko Pacific. Mnamo Mei 11, 1945, akiwa anatumikia kwenye meli ya USS Bunker Hill karibu na Okinawa, meli ililipuliwa na ndege mbili za kujitoa mhanga.9 Takribani mabaharia 400 walikufa akiwemo mjomba wangu Vaughn.
Mzee Spencer W. Kimball alitoa rambirambi za moyo wake wote kwa babaye Vaughn, akitilia mkazo ustahiki wa Vaughn na hakikisho la Bwana kwamba “wale wanakufa ndani yangu hawatahoja kifo, kwani itakuwa vyema kwao.”10 Babaye Vaughn kwa ukujufu alisema Vaugh alizikwa baharini, mkono wa Bwana utamchukua Vaughn hadi kwenye nyumba yake ya milele nyumbani.11
Miaka ishirini na nane baadaye, Rais Spencer W. Kimball alimwongelea Vaughn kwenye mkutano mkuu. Alisema machache: “Niliijua hii familia vizuri sana. … niliomba kwa sala ya dhati pamoja [nao]. … Mafundisho ya nyumbani yamesaidia baraka za milele katika familia hii kubwa.” Rais Kimball alipatia kila familia changamoto ya “kupiga magoti … kuwaombea wana na mabinti zao mara mbili kila siku.”12
Akina kaka na kina dada, kama sisi tutakuwa na maombi ya familia, mafunzo ya maandiko, jioni ya familia nyumbani, baraka za ukuhani, na kuitukuza siku ya Sabato watoto wetu watajua ni saa gani nyumbani. Watajiandaa kwa ajili ya nyumba ya milele huko mbinguni bila kujali kitakacho-- watokea katika ulimwengu wa matatizo. Ni muhimu kwamba watoto wetu wajue wanapendwa na wako salama nyumbani.
Waume na wake ni wenza walio sawa.13 Wana majukumu tofauti yanayofanya kazi pamoja. Mke aweza kuzaa watoto, tendo linaloleta baraka kwa familia yote. Mume aweza kupokea ukuhani, ambao utabariki familia nzima. Lakini kwenye kikao cha familia wake na waume, ni wenza walio sawa, wanaofanya maamuzi muhimu. Wanaamua jinsi watakavyowafundisha watoto na kuwatia nidhamu, jinsi ya kutumia pesa, wataishi wapi, na maamuzi mengine mengi ya kifamilia. Haya yanafanywa kwa pamoja baada ya kuomba mwongozo toka kwa Bwana. Lengo likiwa ni familia ya milele.
Nuru ya Kristo hupanda asili ya milele ya familia katika mioyo ya watoto Wake wote. Mmoja wa waandishi niwapendao, siyo wa dhehebu letu, alisema hivi; “Kuna mengi katika maisha yasiyo muhimu, [lakini] … familia ni kitu muhimu, ni kitu cha msingi, kitu cha milele; kitu cha kuangalia na kutunza na kuwa waaminifu kwacho.” 14
Kanisa linatusaidia Sisi kufokasi kwa Mwokozi kama Familia moja
Baada ya familia, majukumu ya Kanisa pia ni muhimu. “Kanisa linatoa mpangilio na njia ya kufundisha injili ya Yesu Kristo kwa watoto wote wa Mungu. Linaleta mamlaka ya ukuhani ili kusimamia ibada za wokovu na kuinuliwa kwa wale wote wenye kustahili na walio tayari kuzipokea.”15
Katika ulimwengu kumeenea ugomvi, uovu, na msisitizo mkubwa wa tamaduni zilizoachana na zisizo sawa. Katika Kanisa, isipokuwa mkusanyiko wa lugha moja, kata na matawi yetu yapo kijiografia. Hatutenganishwi kwa hadhi au cheo.16 Tunafurahi kwa sababu matabaka na tamaduni vimechanganyika pamoja katika mkusanyiko mwema. Familia yetu ya kata ni muhimu katika kuendelea, furaha, na juhudi binafsi za kuwa kama Kristo.
Tamaduni mara nyingi huwagawa watu na wakati mwingine ni chanzo cha fujo na ubaguzi.17 Katika Kitabu cha Mormoni baadhi ya lugha mbaya zinatumika kuelezea tamaduni za baba waovu zilizosababisha fujo, vita, matendo mabaya, uovu, na hata kuangamia kwa watu na mataifa.18
Hakuna sehemu nzuri ya kuanzia kusoma maandiko zaidi ya 4 Nefi kwa ajili ya kuelezea utamaduni wa Kanisa ambao ni muhimu kwa ajili yetu sote. Katika mstari wa 2 unasomeka, “Watu wote walimgeukia Bwana, nchini kote, wote Wanefi na Walamani, na hakukuweko na mabishano na ugomvi miongoni mwao, na kila mtu alimtendea mwingine haki.” Katika mstari wa 16 tunasoma, “Na kwa kweli hakujakuwa na furaha zaidi miongoni mwa watu watu wote ambao waliumbwa na mkono wa Mungu.” Na ikawa kwamba hakukuwa na ubishi katika nchi, kwa sababu ya mapenzi ya Mungu ambayo yaliishi katika mioyo ya watu.”19Huu ndio utamaduni tunaouhitaji.
Faida kubwa ya utamaduni na imani unakwenda kwenye kiini cha kuwa sisi ni akina nani. Tamaduni za dhabihu, shukrani, imani na wema zinapaswa kuenziwa na kutunzwa. Familia lazima zifurahie na kutunza tamaduni zinazokuza imani.20
Moja ya sifa muhimu za utamaduni wowote ni lugha yake. Katika eneo la San Francisco, California, ambapo nilihishi kulikuwa na makusanyiko ya vitengo vya lugha. Mafundisho yetu yanayoheshimu lugha yapo katika sehemu ya 90, mstari wa 11katika Mafundisho na Maagano: “Kwani itakuja kutokea katika siku ile, kwamba kila mtu atasikia utimilifu wa injili katika kabila lake, na katika lugha yake mwenyewe.”
Wakati watoto wa Mungu wanapoomba Kwake katika lugha zao za asili, hiyo ndiyo lugha ya moyoni mwao. Ni wazi kwamba lugha ya moyo ni tunu kwa watu wote.
Kaka yangu mkubwa, Joseph, ni daktari na amekuwa akifanyakazi kwa miaka mingi huko San Francisco. Muumini wa Kanisa mzee wa Kisamoa, aliyekuwa mgonjwa mpya, alikuja ofisini kwake. Alikuwa katika hali ya maumivu makali. Iligundulika kwamba alikuwa na jiwe katika figo na taratibu sahihi za tiba zilichukuliwa. Muumini huyu mwaminifu alieleza kwamba lengo lake la awali lilikuwa ni kujua tatizo ili aweze kuomba kwa Kisamoa kwa Baba yake wa Mbinguni juu ya tatizo lake la kiafya.
Ni muhimu kwa waumini kuielewa injili katika lugha ya mioyo yao ili waweze kuomba na kutenda kulingana na kanuni za injili.21
Hata pamoja na lugha mbalimbali na tamaduni zinazoimarisha, lazima tuwe na mioyo ya umoja na upendo.22 Bwana amesema kwa msisitizo: “Na kila mtu ampende ndugu yake kama vile ajipendavyo yeye mwenyewe. ... muwe na umoja; na kama hamna umoja ninyi siyo wangu.”23 Huku tukisifia utamaduni mzuri wa sehemu mbali mbali, lengo letu ni kuungana katika tamaduni, mila na desturi za injili ya Yesu Kristo katika kila njia.
Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho halijawahi kuwa imara kama sasa
Tunatambua kwamba baadhi ya waumini wana maswali na wasiwasi wanapojaribu kukuza imani na ushuhuda wao. Lazima tuwe waangalifu kutokuwa na hali ya kukosoa au kuhukumu wale wenye shida---iwe kubwa au ndogo. Wakati huo---huo, wale wenye shida wanatakiwa kufanya kila wawezalo kujenga imani na ushuhuda wao wenyewe. Wakijifunza kwa uvumilivu na unyenyekevu, wakitafakari, kuomba, kutii kanuni za injili, na kushauriana na viongozi sahihi ni njia sahihi ya kujibu na kutatua matatizo.
Baadhi wametamka kwamba waumini wengi wanaondoka Kanisani siku hizi, hivyo kuna wasiwasi zaidi na kutoamini kuliko hapo kale. Hii siyo kweli. Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho halijawahi kuwa imara kama lilivyo sasa. Idadi ya waumini wanaoondoa majina yao toka kwenye kumbukumbu za Kanisa imekuwa ndogo na imepungua sana katika miaka ya hivi karibuni kuliko hapa kale.24 Kuongezeka katika maeneo yanayoweza kuonekana wazi, kama vile waumini wenye kibali cha hekalu, watu wazima wanaolipa zaka kamili, na wale wanaotumikia misheni, imeongezeka. Acha niseme tena, Kanisa halijawahi kuwa imara kama ilivyo sasa. Lakini “kumbuka thamani ya nafsi ni kubwa machoni pa Mungu.”25 Tunamfikia kila mtu.
Kama matatizo mnayokabiliana nayo sasa yanaonekana kuwa kiza na mazito na hayabebeki, kumbuka kwamba hata kama nafsi zetu zitapambana na giza la Gethsemane na mateso na maumivu mazito ya Kalvari, Mwokozi alikamilisha Upatanisho, ambao unaondoa mzigo mzito uliokuwepo katika maisha haya. Alifanya hivyo kwa-ajili yako, na kwa-ajili yangu. Alifanya hivyo kwa sababu anatupenda na kwa sababu anamtii na kumpenda Baba Yake. Tutaokolewa na kifo---hata toka katika kina cha bahari.
Ulinzi wetu katika maisha haya na ya milele utakuwa katika wema wa kibinafsi na kifamilia na ibada za kanisa na kumfuata Mwokozi. Hili ndio kimbilio letu dhidi ya kimbunga. Kwa wale wanaojisikia kuwa wapweke, unaweza kusimama katika wema mkijua kwamba Upatanisho utawalinda na kuwabariki kupita uwezo wenu wa kuelewa.
Tunatakiwa tumkumbuke Mwokozi, kushika maagano, na kumfuata Mwana wa Mungu kama ua la alizeti changa linavyoufuata mwangaza wa jua. Tukifuata nuru na mfano Wake kutatuletea furaha, na amani. Kama vile Zaburi 27 na wimbo unaopendwa vyote vikisema, “Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu.”26
Katika wikiendi hii ya Pasaka, kama mmoja wa Mitume wa Mwokozi, ninatoa ushahidi mtakatifu wa Ufufuko wa Yesu Kristo. Ninajua Anaishi. Ninaijua sauti Yake. Ninashuhudia uungu wake na ukweli wa Upatanisho katika jina la Yesu Kristo, amina.