2010–2019
Je! Bado ni Nzuri Sana Kwako?
Aprili 2015


10:13

Je! Bado ni Nzuri Sana Kwako?

Kushangaa maajabu ya injili ni ishara ya imani. Ni kuutambua mkono wa Bwana katika maisha yetu na kila kitu kinachotuzunguka

Mke wangu nami tulikuwa na furaha ya kuwalea watoto wetu watano karibu na mji mzuri wa Paris. Kipindi cha miaka hiyo tulitaka kuwapa nafasi ya kugundua vitu vingi vya ulimwengu huu. Kila msimu wa joto, familia yetu ilisafiri ili kutembelea majengo ya ukumbusho, maeneo ya kihistoria, na shani za asili za Ulaya. Mwisho, baada ya kukaa miaka 22 katika eneo la Paris, tulikuwa tunajiandaa kuhama. Bado ninakumbuka siku ambayo watoto wangu walikuja kwangu na kusema, “Baba, kweli ni aibu! Tumeishi hapa maisha yetu yote, na kamwe hatujawahi kufika kwenye Mnara wa Eiffel!”

Kuna maajabu mengi katika ulimwengu huu. Hata hivyo, wakati mwingine yanapokuwa karibu na macho yetu, sisi tunayaona kuwa ya kawaida. Tunaangalia, lakini hatuoni; tunasikia, lakini hatusikilizi.

Wakati wa huduma Yake duniani, aliwaambia wafuasi Wake:

“Heri wanaoona yale mnayoyaona ninyi:

“Kwani nawaambieni, manabii na wafalme walitamani kuona yale mnayoyaona ninyi, na hawakuyaona, na kusikia yale mnayoyasikia, na wasiyasikie.”1

Mara nyingi nimejiuliza ingekuaje kuishi wakati wa Mwokozi. Ungeweza kujisikiaje kukaa miguuni Mwake? Kupata kumbatio Lake? Kushuhudia kadiri alivyo watumikia wengine? Na hata hivyo wengi waliokutana Naye walishindwa kumgundua---“kumwona”---kwamba Mwana wa Mungu alikuwa akiishi pamoja nao.

Nasi pia tumebahatika kuishi katika wakati mzuri. Manabii wa kale waliiona kazi ya Urejesho kama “kazi ya ajabu… , ndio, kazi ya ajabu na ya kushangaza.”2 Hakuna kipindi cha nyuma kilichokuwa na wamisionari wengi walioitwa kutumikia kama sasa, mataifa mengi yalifunguliwa kwa ajili ya ujumbe wa injili na mahekalu mengi kujengwa ulimwenguni kote.

Kwetu sisi, kama Watakatifu wa Siku za Mwisho, maajabu pia yanatokea katika maisha yetu binafsi. Yanajumuisha uongofu wetu binafsi, majibu tunayoyapata kupitia sala zetu, na baraka za upendo wa Mungu anazotupa kila siku.

Kushangaa maajabu ya injili ni ishara ya imani. Ni kuutambua mkono wa Bwana katika maisha yetu na kila kitu kinachotuzunguka. Mshangao wetu pia huleta uimarisho wa kiroho. Unatupa nguvu ya kubaki imara katika imani yetu na kujihusisha wenyewe katika kazi ya wokovu.

Lakini acheni tuwe wangalifu. Uwezo wetu wa kushangaa ni dhaifu. Zaidi ya miaka mingi, vitu vya aina hii kama kutii amri kwa nadra, kutojali, au hata kwa kuchoka kunaweza kutufanya tusijali ishara na miujiza ya ajabu ya injili.

Kitabu cha Mormoni kinaelezea kipindi, ambacho ni sawa na chetu, ambacho kilitangulia kuja kwa Masiya kule Amerika. Ghafla ishara za kuzaliwa Kwake zikatokea mbinguni. Watu walishangazwa sana na kustaajabu kwamba wakajinyenyekeza wenyewe, na karibu wote wakaongoka. Hata hivyo, miaka minne baadaye, “watu wakaanza kusahau hizo ishara au maajabu kutoka mbinguni … na walianza kwa kutoamini yote ambayo walisikia na kuona.”3

Ndugu na dada zangu, je injili bado ni nzuri kwenu? Bado mnaweza kuona, kusikia, kuhisi, na kushangaa? Au hisia zako za kiroho zimeenda katika modi ya subiri? Bila kujali matatizo yetu, ninawaalika mfanye mambo matatu.

Kwanza, usichoke kuvumbua au kuvumbua tena kweli za injili. Mwandishi Marcel Proust alisema, “Safari ya kweli ya uvumbuzi haijumuishi katika kutafuta mandhari mapya, bali kwa kuwa na macho mapya.”4 Unakumbuka mara ya kwanza uliposoma mstari wa maandiko na kuhisi kama Bwana alikuwa akiongea nawe binafsi? Je! Unaweza kukumbuka mara ya kwanza ulipohisi ushawishi wa Roho Mtakatifu kuja kwako, pengine kabla hata hujagundua alikuwa ni Roho Mtakatifu? Je! Huu haukuwa wakati mtakatifu, wa kipekee?

Tunatakiwa kuwa na njaa na kiu kila siku kwa ajili ya elimu ya kiroho. Tabia ya aina hii inapatikana katika kujifunza, kutafakari, na maombi. Wakati mwingine tunaweza kujaribiwa kufikiri, “Sihitaji kujifunza maandiko leo; nimeshayasoma hapo awali” au “sihitaji kwenda kanisani leo; na hakuna kitu kipya kule.”

Lakini injili ni chemchemi ya elimu ambayo kamwe haikauki. Mara zote kuna kitu kipya cha kujifunza kila Jumapili, katika kila mkutano, na katika kila mstari wa maandiko. Katika imani tunasimama kwenye ahadi kwamba kama “tutafuta, …tutaona.”5

Pili, iweke imani yako katika kweli za wazi na rahisi za injili. Mshangao wetu uwe unalenga katika kanuni za imani yetu, katika usafi wa maagano na katika matendo ya kawaida ya kuabudu.

Dada mmisionari alisimulia hadithi ya watu watatu aliokutana nao wakati wa mkutano wa wilaya huko Afrika. Walitoka kijiji cha mbali msituni ambako Kanisa lilikuwa bado halijaanzishwa lakini kulikuwepo na waumini waaminifu 15 wa kanisa na karibu 20 wachunguzi. Zaidi ya wiki mbili watu hawa walitembea kwa miguu, wakitembea zaidi ya maili 300 (kilomita 480) kwenye njia zilizojaa tope wakati wa mvua, ili waweze kuhudhuria mkutano na kuleta zaka toka kwa waumini wa kundi lao. Walipanga kukaa wiki nzima ili waweze kufurahia nafasi ya kula sakramenti Jumapili iliyofuata na kisha walitegemea kufanya safari ya kurudi wakiwa wamebeba masanduku yaliyojaa nakala za Kitabu cha Mormoni vichwani mwao ili kuwapa watu katika kijiji chao.

Mmisionari alishuhudia alivyoguswa ilikuwa kwa njia ya ajabu ndugu hawa waliionyesha na kwa moyo wao wa dhabihu kupata vitu ambavyo kwake mara zote vilikuwa vipo karibu naye.

Alishangaa: Kama nitaamka Jumapili moja asubuhi huko Arizona na kukuta gari langu haifanyi kazi, je, naweza kutembea kwa miguu kwa umbali kidogo toka nyumbani kwangu? Au nitabaki nyumbani kwa sababu ya umbali au kwa sababu mvua ilikuwa inanyesha?”6 Haya ni maswali mazuri kwetu sisi wote kufikiria.

Mwisho, ninawaalika mtafute na mstawishe uusiano na Roho Mtakatifu. Zaidi ya maajabu na miujiza ya injili hatuwezi kuyaona kwa hali yetu ya asili. Ni vitu ambavyo “macho hayawezi kuona, wala kusikia, …. mambo ambayo Mungu ameyaandaa kwa ajili yao wampendao Yeye.”7

Tunapokuwa na Roho kuwa pamoja nasi, ufahamu wetu wa kiroho unanoleka na kumbukumbu yetu inachochewa hivyo hatuwezi kusahau miujiza na ishara tulizoziona. Hii ndiyo sababu, walipojua Yesu alikaribia kuwaacha, Wafuasi wake wa Kinefi waliomba kwa moyo “ili wapate kile ambacho walitaka zaidi; na walitaka kwamba Roho Mtakatifu apewe kwao.”8

Japokuwa walimwona Mwokozi kwa macho yao wenyewe na kugusa majeraha Yake kwa mikono yao wenyewe, walijua kwamba ushuhuda wao ungekoma bila ya kufanywa upya na uwezo wa Roho wa Mungu. Ndugu na dada zangu, msifanye chochote kuhatarisha kupotea kwa zawadi hii nzuri na ya ajabu---wenza wa Roho Mtakatifu. Ipate zawadi kwa maombi ya dhati na maisha mema.

Ninashuhudia kwamba kazi ambayo tunaifanya ni nzuri na ya ajabu.” Tunapomfuata Yesu Kristo, Mungu anatoa ushahidi kwetu, “kwa ishara na maajabu, na miujiza, na zawadi ya Roho Mtakatifu, kulingana na mapenzi yake.”9 Katika siku hii maalum, ninatoa ushuhuda kwamba maajabu na ajabu za injili zinatia nanga katika zawadi zote za Mungu---Upatanisho wa Mwokozi. Hii ni zawadi nzuri ya upendo ambao Baba na Mwana, waliungana katika malengo, na kuitoa kwa kila mmoja wetu. Pamoja nanyi “Ninasimama nikishangaa kwa upendo ambao Yesu amenionyesha. ….Eeh, ni ajabu, ni ajabu kwangu!”10

Kwamba daima tuwe na macho ya kuona, masikio ya kusikia, na mioyo ambayo inaona maajabu ya injili ya ajabu ni sala yangu katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Luke 10:23–24.

  2. 2 Nefi 27:26.

  3. 3 Nefi 2:1.

  4. “Marcel Proust,” Guardian, July 22, 2008, theguardian.com/books/2008/jun/11/marcelproust.

  5. Mathayo 7:7.

  6. Imetoholewa kutoka kwa Lorraine Bird Jameson, “The Giants of Kinkondja” (article on Africa Southeast Area website, 2009); web.archive.org/web/20101210013757/http:/www.lds.co.za/index.php/news-a-events/news/aseanews/91-the-giants-of-kinkondja.

  7. 1 Wakorintho 2:9.

  8. 3 Nefi 19:9.

  9. Waebrania 2:4.

  10. “I Stand All Amazed,” Hymns, no. 193.