Njoo, Unifuate
Julai 29–Agosti 4. Matendo ya Mitume 22–28: ‘Mtumishi na Shahidi’


“Julai 29–Agosti 4. Matendo ya Mitume 22–28: ‘Mtumishi na Shahidi’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Julai 29–Agosti 4. Matendo ya Mitume 22–28,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Picha
Paulo gerezani

Julai 29–Agosti 4

Matendo ya Mitume 22–28

“Mtumishi na Shahidi”

Mawazo kutoka kwa Roho Mtakatifu mara nyingi ni tulivu na mara nyingine ni ya muda mfupi tu. Kuandika mawazo yako hukuruhusu kuyatafakari kwa kina zaidi. Unaposoma Matendo ya Mitume 22–28, andika mawazo na hisia zinazokuijia na chukua muda kuyatafakari.

Andika Misukumo Yako

“Tunapokuwa katika kazi ya Bwana,” Rais Thomas S. Monson aliahidi, “tunakuwa wenye kustahili msaada wa Bwana”“Kujifunza, Kutenda, Kuwa,” Ensign au Liahona, Nov. 2008, 62). Hatuna haki, hata hivyo, barabara nzuri na kijito kinachobubujika mafanikio yasiyo na mwisho. Kwa ushahidi wa hili, hatuhitaji kuangalia mbali zaidi ya Paulo Mtume. Kazi yake kutoka kwa Mwokozi ilikuwa “kulichukua jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli” (Matendo ya Mitume 9:15). Katika sura 22–28 za Matendo ya Mitume, tunaona Paulo akitimiza kazi hii na kupata upinzani mkubwa—minyororo, kufungwa jela, mateso ya kimwili, kuvunjika kwa merikebu, na hata kuvamiwa na nyoka. Lakini pia tunaona kwamba Yesu “alisimama karibu naye, na kusema, Uwe na moyo mkuu, Paulo” (Matendo ya Mitume 23:11). Uzoefu wa Paulo ni ukumbusho wa mwongozo wa kiungu kwamba watumishi wa Bwana hukubali wito Wake wa “enendeni … na kuwafundisha mataifa yote,” Yeye atatimiza ahadi Yake kwao: “Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari” (Mathayo 28:19–20).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Matendo ya Mitume 22:1–21; 26:1–29

Wafuasi wa Yesu Kristo hutoa shuhuda zao kwa ujasiri.

Wakati Paulo alipotoa shuhuda zake zenye nguvu zilizoandikwa katika Matendo ya Mitume 22 na 26, alikuwa akishikiliwa kama mfungwa na wanajeshi wa Kirumi. Watu alioongea nao walikuwa na uwezo wa kumpa hukumu ya kifo. Lakini bado yeye alichagua kwa ujasiri kutoa ushahidi juu ya Yesu Kristo na “ono la mbinguni” (Matendo ya Mitume 26:19) alilokuwa amepokea. Je, ni kitu gani kinakupa mwongozo wa kiungu kuhusu maneno yake? Fikiria nafasi ulizonazo za kutoa ushuhuda wako. Kwa mfano, ni lini ilikuwa mara yako ya mwisho kuwaambia familia yako au wengine kuhusu ni kwa jinsi gani ulipata ushuhuda wako wa injili?

Matendo ya Mitume 22:1–21; 26:9–20

Kwa nini kuna tofauti kati ya hadithi hizi tatu za ono la Paulo juu ya Yesu Kristo?

Kitabu cha Matendo ya Mitume kina hadithi tatu za ono la kimiujiza la Paulo akiwa njiani kwenda Dameski (ona Matendo ya Mitume 9:3–20; 22:1–21; 26:9–20). Kila moja ya hadithi hizi ni tofauti kidogo na nyingine, na baadhi hutoa maelezo mengi kuliko nyingine. Kwa sababu hadithi zilisemwa kwa hadhira tofauti kwa madhumuni tofauti, inakubalika kwamba Paulo alichagua kusisitiza sehemu tofauti ya tukio kwa kila hadhira.

Hali kadhalika, Joseph Smith aliandika hadithi kadhaa za Ono lake la Kwanza (ona “Hadithi ya Ono la Kwanza,” Ono la Kwanza, topics.lds.org). Hadithi hizi kadhaa zilitolewa kwa hadhira tofauti kwa madhumuni tofauti na kutoa utambuzi ambao usingeweza kuwepo kama tukio moja tu lingekuwepo.

Matendo ya Mitume 23:10–11; 27:13–25, 40–44

Mwokozi husimama karibu na wale wanaojitahidi kumtumikia.

Kama huduma ya Paulo inavyoonyesha wazi, magumu katika maisha yetu siyo ishara kwamba Mungu hakubaliani na kazi tunayofanya. Kwa kweli, wakati mwingine ni katika wakati wa magumu ambapo tunauona msaada Wake kwa nguvu sana. Inaweza kuwa ya kuvutia kurudia kile mlichosoma hivi karibuni kuhusu huduma ya Paulo na kuorodhesha baadhi ya mambo aliyovumilia (ona, kwa mfano, Matendo ya Mitume 14:19–20; 16:19–27; 21:31–34; 23:10–11; 27:13–25, 40–44). Ni kwa jinsi gani Bwana alikuwa naye, na hii inakufundisha nini kuhusu juhudi zako mwenyewe katika huduma ya Bwana?

Matendo ya Mitume 24:24–27; 26:1–3, 24–2927

Ninaweza kuchagua kukubali au kukataa maneno ya watumishi wa Mungu.

Katika huduma yake yote, Paulo alitoa ushuhuda wenye nguvu juu ya Yesu Kristo na injili Yake. Watu wengi walikubali ushahidi wake, lakini si kila mtu aliukubali. Unaposoma Matendo ya Mitume 24:24–27 and Matendo ya Mitume 26:1–3, 24–29, andika maneno na virai ambavyo huonyesha ni kwa jinsi gani watawala wafuatao wa Kirumi katika Yudea walipokea mafundisho ya Paulo:

Feliki

Festo

Mfalme Agripa

Wakati wakisafiri na merikebu kwenda Rumi kuhukumiwa na Kaisari, Paulo alitabiri kwamba “madhara na hasara nyingi” zingeipata merikebu na abiria wake (Matendo ya Mitume 27:10). Soma sura ya 27 kujua ni jinsi gani abiria wenzake na Paulo walivyopokea maonyo yake. Je, unapata funzo lolote kwa ajili yako katika uzoefu wao?

Je, umewahi kutoa jibu kama yeyote kati ya watu hawa wakati uliposikiliza mafundisho ya viongozi wa Kanisa? Je, ni nini baadhi ya matokeo ya kutoa jibu katika njia hizi? Je, unajifunza nini kutoka katika matukio haya kuhusu kusikiliza ushauri wa Bwana kupitia watumishi Wake?

Ona pia 2 Nefi 33:1–2; Joseph Smith—Historia ya 1:24–25; D. Todd Christofferson, “Sauti ya Onyo,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 108–11.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:

Matendo ya Mitume 24:16

Kabla ya uongofu wake, Paulo alikuwa na historia ndefu ya hatia dhidi ya Mungu. Lakini kwa sababu alikuwa radhi kutubu, aliweza kusema, “Nami ninajizoeza katika neno hili, niwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu” (ona pia M&M 135:4). Ni kwa jinsi gani tunaweza kuzuia dhamiri zetu zisiwe na hatia mbele za Mungu na mbele ya wengine?

Matendo ya Mitume 26:16–18

Katika mistari hii, Bwana alimuita Paulo kufanya nini? Ni nafasi zipi ambazo tunazo za kufanya mambo kama hayo?

Matendo ya Mitume 28:1–9

Je, kuna mtu katika familia yako anawapenda nyoka? Unaweza kumuuliza mtu huyo au mwanafamilia mwingine kusimulia hadithi zinazopatikana katika Matendo ya Mitume 28:1–9. Watoto wako wanaweza kufurahia kuchora picha ya hadithi hizi au kuziigiza. Ni mafunzo gani tunaweza kupata kutokana na hadithi hizi? Moja laweza kuwa kwamba Bwana hutimiza ahadi Zake kwa watumishi Wake. Kwa mfano, unaweza kulinganisha ahadi zilizofanywa katika Marko 16:18 na utimizwaji wake katika uzoefu wa Paulo. Unaweza pia kutafuta katika hotuba ya mkutano mkuu wa hivi karibuni ahadi iliyofanywa na mmoja wa watumishi wa Bwana—pengine moja ambayo ina maana kwa familia yako—na kuibandika nyumbani mwako. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha imani yetu kwamba ahadi hii itatimizwa?

Picha
nyoka

Mungu alimlinda Paulo wakati nyoka mwenye sumu alipomuuma.

Matendo ya Mitume 28:22–24

Kama Kanisa katika wakati wa Paulo (lilivyoitwa “dhehebu” katika mstari wa 22), Kanisa leo mara kwa mara “unenwa vibaya.” Watu walipompinga Mwokozi na Kanisa Lake, ni kwa jinsi gani Paulo alijibu? Je, tunaweza kujifunza nini kutokana na uzoefu wa Paulo?

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Zingatia kanuni ambazo zitabariki familia yako. Unapojifunza maandiko, jiulize, “Ni nini Ninachopata hapa ambacho kitakuwa cha muhimu hasa kwa familia yangu?” (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 17.)

Picha
Paulo mbele ya Mfalme Agripa

Jasiri katika Ushuhuda wa Kristo, na Daniel A. Lewis. Paulo mbele ya Mfalme Agripa.

Chapisha