Njoo, Unifuate
Agosti 5–11 Warumi 1–6: ‘Nguvu za Mungu katika Ukombozi’


Agosti 5–11 Warumi 1–6: ‘Nguvu za Mungu katika Ukombozi’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

Agosti 5–11 Warumi 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019: 2019

Picha
Paulo anaandika waraka

Agosti 5–11

Warumi 1–6

“Nguvu za Mungu katika Ukombozi”

Kwa maombi soma Warumi 1–6 ukiwa na washiriki wa darasa lako akilini mwako. Hii itakusaidia kuwa makini na ushawishi wa Roho unapojiandaa kufundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Fikiria kuwapa washiriki wa darasa dakika chache kutafuta mstari toka Warumi 1–6 ambao wanaupenda. Wanaweza kushiriki mstari waliouchagua na mtu ambaye wamekaa karibu naye.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Warumi 1:16–17

“Siionei haya injili ya Kristo.”

  • Je, washiriki wa darasa lako wamewahi kukumbwa na kejeli kwa sababu ya wanachokiamini? Waalike kusoma Warumi 1:16–17 na kufikiria juu ya mifano kutoka kitabu cha Matendo ya Mitume ambapo Paulo alionyesha kutoionea haya injili. Ni baadhi ya vitu gani ambavyo hutufanya sisi kutoona haya kuwa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho? Waalike washiriki wa darasa kuelezea matukio ambapo wao au watu wengine walionyesha kuwa hawaionei haya injili ya Yesu Kristo.

Warumi1:16–17; 2:28–29; 6:1–11

Ufuasi wa kweli unapatikana katika kujitolea kwetu kwa dhati, si tu katika matendo yetu.

  • Ni kwa namna gani tunatathmini ufuasi wetu? Ushauri wa Paulo kwa Warumi unaweza kutusaidia sisi kukumbuka kuzingatia si katika kukamilisha orodha ya shughuli bali katika “moyo [na] roho” (Warumi 2:29). Ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa ushauri wa Paulo, ungeweza kuandika ujumbe kutoka Warumi 2:28–29 kwenye ubao. Badilisha neno Myahudi kwa neno Mtakatifu wa Siku za Mwisho na neno tohara kwa neno agano. Badiliko hili linaongeza nini katika uelewa wetu kuhusu mafundisho ya Paulo? Ugeweza pia kujadili mifano ya mambo tunayofanya kama waumini wa Kanisa ambayo huwa ya maana na nguvu zaidi kama yakifanywa kwa “moyo, katika roho” (Warumi 2:29). Kwa mfano, ona ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland kuhusu mafundisho ya nyumbani, “Wajumbe wa Kanisa” (Ensign au Liahona, Nov. 2016, 61–67), au ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen kuhusu kazi ya umisionari, “Shahidi wa Mungu” (Ensign au Liahona, Nov. 2016, 35–38).

Warumi 3–6

“Pale dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi.”

  • Kunaweza kuwa na baadhi ya washiriki katika darasa lako wanaohitaji msaada kuelewa mafundisho ya Paulo katika sura hizi kuhusu imani, matendo na neema ( ona pia muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia na tafsiri ya Joseph Smith kwa ajili ya sura hizi katika tanbihi na kiambatisho cha Biblia). Unawezaje kuwasaidia kujifunza kutoka kwa kila mmoja wao? Fikiria kuwasilisha matukio mawili yafuatayo ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kwamba hatupaswi kuona matendo yetu mema kama njia ya kuthibitisha ustahiki wetu, wala hatupaswi kuiona neema ya Kristo kama sababu ya kuhalalisha makosa na dhambi zetu. Alika washiriki wa darasa kutafuta kweli kutoka Warumi 3:20–31; 5:1–2; 6:1–2, 21–23 ambazo zingeweza kuwasaidia Gloria na Justin. Ni kweli zipi zingine za mafundisho katika “Nyenzo za Ziada” zingeweza kuwasaidia kuelewa umuhimu wa kufanya matendo mema na kuamini katika neema ya Kristo? Ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa kuelezea walichopata katika maongezi ya maigizo.

Mfano 1

Una rafiki anaitwa Gloria ambaye anahisi kulemewa katika jitihada zake za kuwa mfuasi mwaminifu. Anajitahidi kwa bidii kufanya kila kitu anachohisi anatakiwa kufanya lakini kila mara ana wasiwasi kwamba jitihada zake hazitoshi “Je, mimi ni mzuri vya kutosha?” anajiuliza. “Je, Bwana atanikubali?”

Mfano 2

Una rafiki anayeitwa Justin ambaye hana wasiwasi sana kuhusu kufanya chaguzi sahihi. Anaamini katika Yesu Kristo, anahudhuria mikutano ya kanisa, ni baba mwenye upendo na jirani mzuri. Hata hivyo, ameamua kuishi kwa viwango ambavyo havingemruhusu kustahili kibali cha hekaluni. Wakati familia na marafiki wakijaribu kumpa hamasa kujiandaa kwa ajili ya hekalu, hujibu, “mimi ni mtu mzuri. Nina imani katika Kristo. Yeye amekwisha lipia deni la dhambi zangu, na sidhani kama hataniruhusu kwenye ufalme wa selestia kwa sababu ndogo kama hizo.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma Warumi 7–16, ungeweza kuwaambia kwamba Paulo alielezea vita ndani yake—na kwetu sote. Katika Warumi 7–16 tunapata kujua hiyo vita ni vita ipi na jinsi ya kuishinda.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Warumi 1–6

Imani, neema, na matendo

Wakati tunatakiwa kujitahidi kufuata amri, utiifu kwa sheria za Mungu pekee hautatuokoa (ona Warumi 3:27–31). Hata kwa jitihada zetu za dhati, “wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Kwa sababu hiyo, wote tunamhitaji Yesu Kristo, ambaye neema yake inaturuhusu kusamehewa dhambi zetu na kutuwezesha kuendelea kutenda matendo mema. Kama Paulo alivyofundisha, “Pale dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi” (Warumi 5:20).

Rais David O. McKay alielezea analojia moja kuhusu mvulana ambaye alianza kuzama wakati akiogelea pamoja na rafiki zake: “Kwa bahati nzuri, mtu mmoja ambaye alikuwa na akili na mwepesi wa kutenda, alishikiza fimbo ndefu kutoka kwenye uzio wenye nyavu yenye matundu na kuelekeza mwisho mwingine wa fimbo hiyo kwa yule kijana aliyekuwa akizama [ambaye] aliikamata, na kuishikilia kwa nguvu na aliokolewa.

“Wavulana wote walitoa tamko kuwa kijana aliyefanyiwa jambo la kijasiri ana deni kwa mvulana aliyetengeneza njia ya kumuokoa.

“Huu ni ukweli usio na shaka; na licha ya njia iliyotengenezwa kwa ajili yake, kama kijana asingetumia fursa hiyo, kama asingeweka jitihada zake binafsi , angezama, bila kujali tendo la kishujaa la rafiki yake” (David O. McKay, “Injili ya Matendo,” Mwelekezaji, Jan. 1955, 1).

Akizungumzia kuhusu swali la kama tunaokolewa kwa imani au matendo, mwandishi wa Kikristo C. S. Lewis aliandika: “ina [onekana] kwangu ni kama vile kuuliza ni makali yapi katika mkasi ni muhimu zaidi” (Ukristo Tupu, 148).

Mfano 1

“Wokovu hauwezi kununuliwa kwa sarafu ya utii; unanunuliwa kwa damu ya Mwana wa Mungu [ona Matendo ya Mitume20:28]. …

“Neema ni kipawa cha Mungu, na hamu yetu kuwa watiifu kwa kila amri ya Mungu ni njia ya kunyoosha mkono wetu kupokea kipawa hiki kitakatifu kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni” (Dieter F. Uchtdorf, “Zawadi ya Neema,” Ensign au Liahona, Mei 2015, 109–10).

Mfano 2

“Kama neema ni kipawa cha Mungu, kwa nini basi utii kwa amri za Mungu ni muhimu sana? Kwa nini kusumbuka na amri za Mungu—au toba, kwa jambo hilo? …

“Utii wetu kwa amri za Mungu unakuja kama matokeo ya asili ya upendo wetu usio na mwisho na shukrani kwa wema wa Mungu. Desturi hii ya upendo wa kweli na shukrani kimiujiza itaunganisha matendo yetu na neema ya Mungu” (Dieter F. Uchtdorf, “Zawadi ya Neema,” Ensign au Liahona, Mei 2015, 109).

Hitaji letu endelevu la neema.

Kwa kuongezea kwenye kuhitaji neema kwa ajili ya wokovu wako wa juu, unahitaji nguvu hii yenye kuwezesha kila siku ya maisha yako. Unaposogea karibu na Baba yako wa Mbinguni katika juhudi, unyenyekevu, na upole Atakuinua na kukuimarisha kupitia neema Yake (ona Mithali 3:34; 1 Petro 5:5; MM 88:78; 106:7–8). Utegemezi katika neema Yake unakuwezesha kuendelea na kukua katika haki” (Kweli katika Imani, 78).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wito wako ni wa mwongozo wa kiungu. Kama mwalimu, umeitwa na Bwana kubariki watoto Wake. Bwana anataka ufanikiwe, kwa hivyo unapoishi kwa ustahiki wa msaada Wake, atakupa ufunuo unaoutafuta. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 5.)

Chapisha