Njoo, Unifuate
Agosti 26–Septemba 1. 1 Wakorintho 8–13: ‘Ninyi Ni Mwili wa Kristo’


“Agosti 26–Septemba 1. 1 Wakorintho 8–13: ‘Ninyi Ni Mwili wa Kristo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Agosti 26–Septemba 1. 1 Wakorintho 8–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
mkutano wa sakramenti

Agosti 26–Septemba 1

1 Wakorintho 8–13

“Ninyi ni Mwili wa Kristo”

Mzee Richard G. Scott alifundisha kwamba tunaweza “kuacha mwongozo binafsi wa thamani sana, wa Roho kutosikika” kama tutashindwa kuandika na kuitikia “mwongozo wa kwanza unaokuja [kwetu]” (“To Acquire Spiritual Guidance,” Ensign au Liahona, Nov. 2009, 8).

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Paulo alitumia analojia na taswira katika 1 Wakorintho 8–13, kama vile mkimbiaji katika mbio, mwili wa mwanadamu, na “shaba iliayo” (1 Wakorintho 13:1). Je, ni umaizi gani washiriki wa darasa wanao kuhusu taswira hii? Ni kwa namna gani iliwasaidia kuelewa ukweli wa injili?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

1 Wakorintho 10:1–13

Wote tunakabiliwa na majaribu, lakini Mungu huandaa njia ya kutokea.

  • Unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua kweli zenye nguvu katika 1 Wakorintho 10:13? Wazo moja ni kuugawa kifungu katika virai, toa kila kimoja kwa mshiriki tofauti wa darasa, na waombe washiriki wa darasa kusema tena virai kwa maneno yao wenyewe. Kwa mfano, ni njia ipi nyingine ya kusema “Mungu ni mwaminifu” au “kujaribiwa zaidi ya vile mnavyoweza kustahimili”? Kisha ungeweza kuweka baadhi ya kauli za washiriki wa darasa pamoja na kuangalia matumizi yake zaidi kwenye maisha yetu. Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki uzoefu ambapo waligundua ahadi katika kifungu hiki kuwa za kweli. Ni umaizi gani wa ziada tunaoweza kuupata kutoka kwenye mistari hii kutoka katika Alma 13:27–28?

  • Badala ya kuzingatia katika majaribu mahususi ya mtu fulani, ungeweza kuzingatia mjadala wako wa 1 Wakorintho 10:13 juu ya majaribu ambayo, kwa maneno ya Paulo “ni kawaida ya mwanadamu.” Washiriki wa darasa wangeweza kuanza kwa kutambua majaribu ambayo Paulo alionya juu yake katika mstari 1–12. Wanaweza pia kupendekeza mifano ya majaribu ya siku hizi ambayo ni ya kawaida, kama majaribu ya kutokuwa mwaminifu, kusengenya, au kuhukumu wengine. Ni kwa namna gani mtu, kwa msaada wa Mungu, anaweza “kuyaepuka” majaribu haya? Unaweza kutaka kuigiza baadhi ya hali.

  • Inaweza kuwa ya thamani kufikiria 1 Wakorintho 10:13 katika muktadha wa Paulo wa kutafuta kwa bidii umoja miongoni mwa Watakatifu. Je, tunaweza kufanya nini ili tuweze kusaidiana “kuepuka” na “kuyastahimili” majaribu ambayo tunaweza kupata? Ni kwa namna gani umoja unatusaidia kuyashinda majaribu?

1 Wakorintho 10:16–17; 11:23–30

Sakramenti hutuunganisha kama waumini wa Kanisa la Kristo.

  • Mistari hii ingeweza kuchochea mjadala kuhusu namna gani sakramenti inaweza kuunganisha kata yenu katika juhudi zenu za kuwa kama Mwokozi. Ungeweza kuanza kwa kusoma 1 Wakorintho 10:16–17 na kuchunguza neno ushirika lingeweza kumaanisha nini katika muktadha huu (mwingine angeweza kuangalia maana katika kamusi). Ni kwa namna gani kushiriki sakramenti pamoja kunatusaidia kujiona kuwa na umoja zaidi? Tunaweza kufanya nini ili kuendeleza umoja wakati wa mkutano wa sakramenti? Je, ni kwa namna gani ushauri wa Paulo “lakini mtu ajihoji mwenyewe” unahusiana na lengo hili? (1 Wakorintho 11:28).

1 Wakorintho 12

Yatupasa tutafute vipawa vya Roho kwa ajili ya manufaa ya watoto wote wa Baba wa Mbinguni.

  • Je, ni kwa namna gani unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kurejea vipawa vya kiroho vilivyoelezwa na Paulo na kutambua tofauti kubwa ya vipawa vya kiroho? Ungeweza kuwapa dakika moja kuandika orodha ya vipawa vya Roho kadiri wawezavyo. Wakishamaliza, alika washiriki wa darasa kushiriki kile walichoandika mpaka kila kipawa walichoorodhesha kimetajwa. Kisha washiriki wa darasa wangeweza kutafuta vipawa vingine ili kuongezea kwenye orodha yao kwa kutafuta kwenye 1 Wakorintho 12 na kutoka katika orodha ya Mzee Marvin J. Ashton katika “Nyenzo za Ziada.” Je, ni vipawa vipi kati ya hivi washiriki wa darasa wameviona kwa watu wanaowajua? Je, ni kwa namna gani kukuza vipawa hivi hutusaidia kuwa kama Yesu Kristo?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuona mifano ya jinsi gani kukuza vipawa vyao vya kiroho husaidia kuliinua Kanisa, fikiria kuwaalika kutafakari kuhusu vipawa vya kiroho watu katika maandiko walivyokuwa navyo. Kwa mawazo juu ya hilo, ungeweza kuwapa majukumu ya kutafuta moja kati ya marejeo ya maandiko katika “Nyenzo za Ziada” na kuelezea vipawa vya kiroho wanavyodhani mtu huyo alikuwa navyo. Je, ni kwa namna gani vipawa hivi vya kiroho vya watu viliwabariki wao wenyewe na wengine? Tunawezaje kutumia vipawa vyetu vya kiroho ili kuwabariki wengine na kuujenga mwili wa Kristo au Kanisa? (ona 1 Wakorintho 12:12–31; ona pia 1 Wakorintho 14:12).

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa jinsi ya kukuza vipawa vya kiroho, waalike kusoma 1 Wakorintho 12:27–31; Moroni 7:48; 10:23, 30; Mafundisho na Maagano 46:8; na nukuu kutoka kwa Rais George Q. Cannon katika “Nyenzo za Ziada.” Nyenzo hizi zinatufundisha nini sisi juu ya kupata vipawa vya kiroho? Ni kwa jinsi gani kukuza vipawa vyetu vya kiroho hutufanya kuwa kama Mwokozi? Alika washiriki wa darasa kuchagua kipawa ambacho wangetaka kupata na kutafuta msaada wa Bwana katika kukipata.

1 Wakorintho 13

Hisani ni kipawa cha kiroho kikuu zaidi.

  • Baadhi ya watu hudhani hisani ni kama kutoa michango kwa ajili ya masikini au ukarimu kwa wengine. Wakati vitu hivi hakika vinaweza kuonyesha hisani, maelezo ya Paulo ni mapana zaidi. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuchanganua hili, ungeweza kuwaomba watafakari kimya kimya 1 Wakorintho 13 na kumfikiria mtu wanayemjua ambaye ni mfano mzuri wa jambo moja au zaidi la hisani aliyoisema Paulo. Baadhi ya washiriki wa darasa wangeweza kumwelezea mtu waliyemfikiria na tukio ambapo mtu huyu alionyesha mfano mzuri wa hisani. Ungeweza pia kuorodhesha sehemu ya maelezo ya Paulo kwenye ubao na kuwaalika washiriki wa darasa kutoa mawazo yao kuhusu kinachomaanishwa kwa “huvumilia” au “[hau]hesabu mabaya” (1 Wakorintho 13:4–5). Je, ni kwa namna gani Mwokozi alionyesha mfano wa tabia hizi za hisani? Tunakuzaje hisani? (Ona Moroni 7:46-48).

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Je, washiriki wako wa darasa wanajua kwamba mafundisho ya ubatizo kwa niaba ya wafu na falme tatu za utukufu yametajwa katika Biblia? Waambie kwamba watakuwa wakijifunza kuhusu kweli hizi wanaposoma 1 Wakorintho 14–16 wiki hii.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

1 Wakorintho 8–13

Vipawa vya kiroho ambavyo hukuwahi kuvifikiria.

Mzee Marvin J. Ashton alishiriki mifano ya vile alivyoviita “vipawa ambavyo havionekani sana” vya Roho: “Karama ya kuuliza; karama ya kusikiliza; karama ya kusikia na kutumia sauti tulivu, ndogo; karama ya kuweza kulia; karama ya kuepuka ubishi; karama ya kuweza kuelewana; karama ya kuepuka kupayuka payuka; karama ya kutafuta yale ambayo ni ya haki; karama ya kutohukumu; karama ya kumtegemea Mungu kwa ajili ya mwongozo; karama ya kuwa mfuasi; karama ya kuwajali wengine; karama ya kuwa na uwezo wa kutafakari; karama ya kutoa sala; karama ya kutoa ushuhuda wenye nguvu; na karama ya kupokea Roho Mtakatifu” (There Are Many Gifts Ensign, Nov. 1987, 20).

Mifano ya Maandiko kuhusu vipawa vya kiroho.

Tafuta vipawa vya kiroho.

Rais George Q. Cannon (1827–1901) wa urais wa kwanza alisema kwamba ni jukumu letu “kuomba kwa Mungu atupatie [sisi] vipawa ambavyo vitasahihisha mapungufu [yetu]. … Vimekusudiwa kwa lengo hili. Mtu yeyote hapaswi kusema, ‘Oh, siwezi kujizuia; ni asili yangu.’ Hawezi kuhalalishwa kwa hilo, kwa sababu Mungu ameahidi kutoa nguvu ili kusahihisha mambo haya, na kutoa vipawa ambavyo vitayaondoa. Kama mtu hana busara, ni wajibu wake kumwomba Mungu ampe busara. Ni sawa kwa kitu chochote kingine” (Millennial Star, Apr. 23, 1894, 260).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ishi kanuni unazofundisha. Kuishi kanuni unazofundisha kutakusaidia kuzitolea ushuhuda wenye nguvu zaidi. Paulo alifundisha, “Na hivyo Bwana ameamuru kwamba wale waihubirio injili wapate riziki kwa hiyo injili” (1 Wakorintho 9:14).

Chapisha