“Septemba 2–8. 1 Wakorintho 14–16: ‘Mungu si Mungu wa Machafuko, bali wa Amani’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)
“Septemba 2–8. 1 Wakorintho 14–16,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019
Septemba 2–8
1 Wakorintho 14–16
“Mungu si Mungu wa Machafuko, bali wa Amani”
Kabla ya kurejea muhtasari huu, soma 1 Wakorintho 14–16. Andika misukumo yako ya awali kuhusu kweli zipi zitawasaidia washiriki wa darasa lako, na endelea kutafuta mwongozo wa nyongeza kutoka kwa Roho Mtakatifu katika kipindi cha wiki.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Toa dakika chache kwa ajili ya washiriki wa darasa kurejea 1 Wakorintho 14–16 na kutafuta mstari wanaohisi una maana hususan kwao. Waalike kutafuta mtu fulani katika darasa ambaye wanaweza kushiriki naye mstari huo na kuelezea kwa nini waliuchagua.
Fundisha Mafundisho
Wakati Watakatifu wanapokusanyika pamoja, wanapaswa kutafuta kujengana.
-
Fikiria kutumia mafundisho ya Paulo katika 1 Wakorintho 14 kuwakumbusha washiriki wa darasa kwamba tunaweza kujengana—au kusaidiana na kuinuana—katika kanisa. Njia rahisi ya kufanya marejeo ya sura hii ingeweza kuwa kwa kuandika swali kwenye ubao, kama vile Nini linapaswa kuwa lengo letu pale tunapokusanyika pamoja? Alika washiriki wa darasa kutafuta majibu katika 1 Wakorintho 14. Mawazo mengine yanaweza kupatikana katika Moroni 6:4–5 na Mafundisho na Maagano 50:17–23. Wakati washiriki wa darasa wakishiriki kile walichopata, fikiria kuwauliza ni jinsi gani wanahisi darasa lenu linaendelea katika kutimiza malengo haya. Wangeweza pia kuelezea uzoefu wao pale walipohisi kurekebishwa na kitu ambacho mshiriki wa darasa alishiriki nao.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa ushauri wa Paulo kwamba waumini watafute kutoa unabii, fikiria kuwauliza kupendekeza maana ya neno toa unabii. Wewe au washiriki wa darasa lako mngeweza kuandika kila maana kwenye ubao na kurejea kwa pamoja maana ya neno toa unabii katika Mwongozo wa Maandiko na ushauri wa Paulo katika 1 Wakorintho 14:3, 31, 39–40. Ni nini tunaweza kuongeza katika maana zetu kutoka kwenye nyenzo hizi? Ona pia Ufunuo 19:10.) Ni nini tunashawishika kufanya kanisani na nyumbani kama matokeo ya ushauri wa Paulo?
Kwa sababu Kristo alifufuka, sisi sote tutafufuka.
-
Je, unawezaje kutumia ushauri wa Paulo katika 1 Wakorintho 15 ili kuimarisha ushuhuda wa washiriki wa darasa lako kuhusu ufufuko? Njia mojawapo ingeweza kuwa kwa kugawanya darasa katika makundi mawili na kuliomba kundi moja kutafuta kutoka 1 Wakorintho 15 matokeo ambayo tungeyapata kama Yesu Kristo asingefufuka. Kundi lingine lingeweza kutafuta baraka ambazo tunapokea kutokana na Ufufuko Wake. Kisha kila kundi lingeweza kuandika kwenye ubao kile walichojifunza. Ni nini wangeweza kuongeza kwenye orodha yao ya awali baada ya kusoma maelezo kutoka kwa Mzee Elder D. Todd Christofferson katika “Nyenzo za Ziada”? Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuhisi Roho katika mjadala huu, fikiria kuonyesha picha ya Mwokozi aliyefufuka (ona Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Nifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia).
-
Kwa sababu Paulo alikuwa akiwajibu watu ambao walikuwa hawaamini katika ufufuko, washiriki wa darasa lako wanaweza kunufaika kupitia kuigiza hali kama hii. Kwa mfano, ni kwa namna gani wangeweza kuimarisha imani ya mpendwa wao kuhusu Ufufuko? Ni nini washiriki wa darasa wamekipata katika 1 Wakorintho 15 ambacho kingewasaidia kuelezea umuhimu na uthibitisho wa ufufuko wa Yesu Kristo? Ni maandiko gani mengine wangeweza kuyatumia? (Ona, kwa mfano, Luka 24:1–12, 36–46; Alma 11:42–45.)
-
Paulo anataja fahari tatu za utukufu wa ufufuko mara kadhaa katika waraka wake (ona 1 Wakorintho 15:40–42 na 2 Wakorintho 12:1–2). Ili kulisaidia darasa lako kugundua jinsi gani ufunuo wa siku za mwisho unatoa ufafanuzi wa mafundisho ya Paulo, ungeweza kuligawa darasa katika makundi matatu na kulipa kila kundi kipande cha karatasi kilichokatwa kama jua (M&M 76:50–70), mwezi (M&M 76:71–80), au nyota (M&M 76:81–89). Waalike kusoma maandiko yaliyohusishwa kutoka Mafundisho na Maagano 76 na kuelezea kile tunachohitajika kufanya ili kupokea fahari tofauti za utukufu alizoelezea Paulo. Ona pia Mafundisho na Maagano 131:1–4; 137:7–10.
-
1 Wakorintho 15 ni moja ya kati ya sehemu chache kwenye maandiko ambapo ubatizo kwa niaba ya wafu umetajwa (ona mstari 29; ona pia M&M 128:18). Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao waliupata wakati walipofanya ubatizo au ibada zingine kwa niaba ya wafu. Fikiria kuelezea uzoefu wa Wilford Woodruff katika “Nyenzo za Ziada” kama sehemu ya mjadala. Kwa nini Paulo aitumia ubatizo kwa niaba ya wafu kama uthibitisho wa ufufuko? Kama itasaidia kujadili kwa nini ubatizo kwa niaba ya wafu ni muhimu, ona “Ubatizo kwa niaba ya wafu,” Mada za Injili, topics.lds.org. video “Habari Njema: Historia ya Ubatizo kwa niaba ya Wafu” (LDS.org) inaelezea jinsi gani ibada hii ilirejeshwa katika siku zetu.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waombe washiriki wa darasa kufikiria kuhusu majaribu wanayokabiliana nayo au udhaifu waliyonao. Waambie wasome 2 Wakorintho, watajifunza kile kilichomsaidia Paulo kustahimili majaribu na jinsi gani alivyoyachukulia udhaifu wake.
Nyenzo za Ziada
Umuhimu wa Ufufuko
Mzee D. Todd Christofferson alishuhudia:
Fikiria kwa muda umuhimu wa Ufufuko katika kuamua mara moja na daima utambulisho wa kweli wa Yesu wa Nazareti na mashindano makubwa ya kifalsafa na maswali ya maisha. Kama kweli Yesu alifufuka kiuhalisia, basi ni muhimu ikafuata kuwa Yeye ni kiumbe kiuungu. Hakuna kiumbe chenye mwili wenye kufa kilicho na nguvu ndani yake ya kurudia uhai tena baada ya kufa. Kwa sababu Yeye alifufuka, Yesu hawezi kuwa alikuwa tu fundi seremala, mwalimu, rabi, au nabii. Kwa sababu Yeye alifufuka, Yesu lazima alikuwa Mungu, hata Mwana wa Pekee wa Baba.
“Kwa hivyo, kile Alichofundisha ni kweli; Mungu hawezi kudanganya.
“Kwa hivyo, Yeye alikuwa Muumbaji wa dunia, kama Yeye alivyosema.
“Kwa hivyo, mbingu na jehanamu ni hakika, kama alivyofundisha.
“Kwa hivyo, kuna ulimwengu wa roho, ambao Yeye aliutembelea baada ya kifo Chake.
“Kwa hivyo, Atakuja tena, kama malaika walivyosema, na kutawala mwenyewe juu ya dunia.’
“Kwa hivyo, kuna ufufuko na hukumu ya mwisho kwa wote” (“Ufufuko wa Yesu Kristo,” Ensign au Liahona, Mei 2014, 113).
Ibada kwa niaba ya wafu: “Mwale wa mwanga kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu.”
Mzee Wilford Woodruff alisema kwamba wakati alipojifunza kuwa waumini wa Kanisa walio hai wanaweza kupokea ibada za kuokoa kwa niaba ya mababu zao ambao wamekwishafariki, “Ilikuwa kama mwale wa mwanga toka kwenye kiti cha enzi cha Mungu kuja kwenye mioyo yetu. Ilifungua uwanda mpana kama umilele katika akili zetu.” Pia alidokeza: “Ilionekana kwangu kwamba Mungu aliyeifunua kanuni hii kwa mwanadamu alikuwa mwenye busara, haki na mkweli, akimiliki vyote sifa njema sana na uelewa mzuri na maarifa. Nilihisi alikuwa na uendelevu katika upendo, rehema, haki na hukumu, na nilijihisi kumpenda Bwana zaidi kuliko hapo awali katika maisha yangu. … Nilihisi kusema haleluya wakati ufunuo huu ulipokuja ukitufunulia juu ya ubatizo kwa niaba ya wafu. …”
“Kitu cha kwanza kilichoingia akili mwangu,” alisema, “ni kwamba nilikuwa na mama katika ulimwengu wa roho. Alikufa nikiwa na miezi 14. …” Baadaye, alizungumzia kuhusu wakati alipopata nafasi ya mama yake kuunganishwa na baba yake: “Atakuwa na nafasi katika ufufuko wa kwanza; na hili pekee lingenilipa kwa kazi yote maishani mwangu” (Teachings of Presidents of the Church: Wilford Woodruff, [2011], 185–86).