Njoo, Unifuate
Oktoba 14–20. Wafilipi; Wakolosai: ‘Nayaweza Mambo Yote katika Kristo Anitiaye Nguvu’


Oktoba 14–20. Wafilipi; Wakolosai: ‘Nayaweza Mambo Yote katika Kristo Anitiaye Nguvu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

Oktoba 14–20. Wafilipi; Wakolosai,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Paulo akitoa imla ya barua akiwa gerezani

Oktoba 14–20.

Wafilipi; Wakolosai

“Nayaweza Mambo Yote katika Kristo Anitiaye Nguvu”

Anza kwa kusoma Wafilipi na Wakolosai, na kwa sala tafakari kuhusu mafundisho ambayo Bwana anataka wewe ufundishe. Acha Roho akuongoze unapofikiria maswali na nyenzo ambazo ungeweza kutumia katika kufundisha mafundisho haya.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Alika washiriki wa darasa kuandika ubaoni neno moja au kirai ambacho kinafupisha kile walichojifunza kutoka Wafilipi na Wakolosai na kisha waelezee chaguo lao. Wahimize kutoa mistari kutoka maandiko kama sehemu ya maelezo yao.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Wafilipi 2:1–5, 14–18; 4:1–9; Wakolosai 3:1–17

Wafuasi wa Kristo huwa “wapya” pale walipoishi injili Yake.

  • Ungeweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuvuta taswira ya nini humaanisha “kuuvua utu wa kale” na “kuvaa utu upya” kupitia Yesu Kristo (Wakolosai 3:9–10). Ili kufanya hivi, ungeweza kuonyesha kitu cha zamani na kitu kipya ( kama vile tunda lililoiva sana na tunda ambalo bado ni bichi au nguo mpya na nguo nzee). Washiriki wa darasa wangeweza kujadili ni kwa namna gani tunakuwa “wapya” kupitia imani katika Yesu Kristo na utayari wetu wa kuishi injili yake. Kama sehemu ya mjadala ungeweza kuwaomba nusu ya darasa kujifunza Wafilipi 2:1–5, 14–18; 4:1–9 na nusu nyingine wajifunze Wakolosai 3:1–17, wakionyesha tabia za “utu wa kale” na “utu upya.” Ungeweza pia kuwaalika washiriki wachache wa darasa kuelezea ni kwa namna gani imani katika Yesu Kristo na kuishi injili Yake kumewasaidia wao kuwa watu wapya. Maandiko mengine ambayo mngeweza kuyachunguza kwa pamoja ni pamoja na Warumi 6:3–7; Mosia 3:19; na Alma 5:14, 26.

Wafilipi 4:1–13

Tunaweza kupata shangwe katika Kristo, bila kujali hali zetu.

  • Ingawa hali zetu ni tofauti na za Paulo, bado tunaweza kujifunza kutokana na utayari wake wa kuridhika na kufurahia katika hali zote za maisha yake. Ili kuanza mjadala juu ya mada hii, ungeweza kurejea baadhi ya majaribu aliyoyapitia Paulo (ona, kwa mfano, 2 Wakorintho 11:23–28). Halafu ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa kurejea Wafilipi 4:1–13 ili kupata ushauri Paulo aliotoa ambao unaweza kutusaidia sisi kufurahia, hata katika nyakati za majaribu.

    Kama ungependa kuchunguza mada hii kwa undani, ungeweza kumuomba mshiriki wa darasa kushiriki tukio la kuhamasisha au kauli kutoka ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Shangwe na Kudumu Kiroho” (Ensign au Liahona, Nov. 2016, 81–84), au darasa lingeweza kuangalia video “Jaribu la Dhiki” (LDS.org). Ni kwa namna gani watu katika ujumbe wa Rais Nelson au mwanamke katika video wanapata furaha, licha ya hali zao ngumu?

  • Labda washiriki wa darasa wangeweza kupata ushauri kutoka Wafilipi 4 ambao unaweza kuwasaidia wakati wanapopitia majaribu. Ungeweza kumpa kila mshiriki wa darasa kadi ndogo ya kuandika ili waandike kile wanachopata. Waombe waweke kadi hiyo mahali ambapo wataweza kuiona wakati wanapoihitaji.

  • Wakati mwingine wimbo unaweza kuboresha uelewa wetu wa maandiko. Kwa mfano, baada ya kusoma Wafilipi 4:7, 13, mngeweza kuimba kwa pamoja “Wapi Ninaweza Kupata Amani?” au ubeti wa kwanza wa “Bwana Nitakufuata” (wimbo, namba. 129, 220). Ni muunganiko upi washiriki wa darasa wanauona katika maneno ya nyimbo hizi na Wafilipi 4:7, 13? Labda wangeweza kuelezea matukio ambapo walihisi “amani ya Bwana, ipitayo uelewa wote” au wakati walipohisi kuimarishwa “kupitia Kristo” ili kutimiza jambo ambalo wasingeweza kulifanya kwa namna nyingine. Uzoefu wa Mzee Jay E. Jensen unaopatikana katika “Nyenzo za Ziada” ungeweza kusaidia kuhamasisha mjadala kuhusu mistari hii.

  • Kwa sababu uovu unaongezeka katika dunia ya leo, washiriki wa darasa lako watanufaika kutokana na ushauri wa Paulo wa kutafakari juu ya mambo ambayo ni safi, yenye kupendeza, yenye sifa njema, yenye staha au wema (Wafilipi 4:8). Labda ungeweza kumpa jukumu kila mshiriki wa darasa (au kundi dogo la washiriki wa darasa) moja kati ya sifa zilizoorodheshwa katika Wafilipi 4:8 au Makala ya Imani 1:13. Kila mmoja angeweza kutumia Mwongozo wa Maandiko kupata maandiko kuhusu jukumu lao walilopewa na kushiriki na wengine darasani kile walichopata. Wangeweza pia kuelezea mifano ya sifa hizo katika maisha ya watu. “Tunayatafakari vipi mambo hayo”?

Wakolosai 1:12–23; 2:3–8

Wakati imani yetu “ina shina” katika Yesu Kristo, tunaimarishwa dhidi ya ushawishi wa kidunia.

  • Ushuhuda wa Paulo juu ya Mwokozi katika Wakolosai 1:12–23; 2:3–8 unatoa fursa nzuri kwa washiriki wa darasa kutafakari na kuimarisha imani zao. Washiriki wa darasa wangeweza kuchunguza mistari hii ili kupata vitu ambavyo vinaimarisha imani yao katika Yesu Kristo. Inamaanisha nini kuwa “wenye shina na kujengwa katika [Yesu Kristo]”? (Wakolosai 2:7). Picha ya mti katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia na video “Tufani za Kiroho” (LDS.org) inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kujadili mstari huu. (Ona pia Neil L. Andersen, “ vimbunga vya Kiroho,” Ensign au Liahona, Mei 2014, 18-21.) Nini kinaweza kuimarisha au kudhoofisha mizizi ya mti? Ni kwa namna gani kuwa “wenye shina na kujengwa katika [Yesu Kristo]” kunatuimarisha dhidi ya vishawishi vya kidunia? (Ona Wakolosai 2:7–8; ona pia Helamani 5:12; Etheri 12:4).

  • Washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa na ufahamu wa falsafa na tamaduni za watu ambazo zinaweza “kuharibu” imani ya mtu katika Kristo kwa sababu zinapingana na ukweli wa injili na kufanya kuishi injili kuwa vigumu. (Wakolosai 2:8). Labda washiriki wa darasa wangeweza kuorodhesha baadhi ya haya (mawazo yaliyopendekezwa na Mzee Dallin H. Oaks, yapatikanayo katika “Nyenzo za Ziada,” ingesaidia). Kisha mngeweza kujadiliana ni kwa namna gani kuwa na shina katika mafundisho ya Yesu Kristo hutusaidia kufuata ushauri wa Paulo: “Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye” (Wakolosai 2:6). Ni kwa namna gani tunaweza kusaidiana katika jitihada zetu za kumfuata Mwokozi na si tamaduni za uongo za kidunia?

ikoni ya a kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Je, washiriki wa darasa lako wamewahi kuteswa kwa sababu wanaamini katika injili? Waambie kwamba 1 na 2 Wathesalonike kuna ushauri ambao Paulo alitoa kwa Watakatifu walioishi katikati ya mateso makali na wakabaki waaminifu.

ikoni ya  nyenzo

Nyenzo za Ziada

Wafilipi; Wakolosai

Amani ipitayo akili zote.

Wakati akihudumu kama mshiriki wa wale Wasabini, Mzee Jay E. Jensen alielezea uzoefu huu:

Mjukuu wetu wa kiume Quinton alizaliwa akiwa na kasoro nyingi na aliishi mwaka kasoro wiki tatu, kipindi chote ambacho alikuwa ndani au nje ya hospitali. Dada Jensen pamoja na mimi kipindi hicho tulikuwa tukiishi Ajentina. Kwa kweli tulitaka kuwa pamoja na watoto wetu ili kuwafariji na pia kufarijiwa na wao. Huyu alikuwa ni mjukuu wetu ambaye tulimpenda na kutaka kuwa karibu nae. Tungeweza tu kusali, na tulifanya hivyo kwa dhati!

Dada Jensen pamoja na mimi tulikuwa katika matembezi ya kutembelea misheni ambapo tulipokea ujumbe kuwa Quinton amefariki. Tulisismama kwenye ukumbi wa nyumba ya mkutano na kukumbatiana na kufarijiana. Ninashuhudia kwenu kwamba uhakikisho ulitujia kutoka kwa Roho Mtakatifu, amani ipitayo akili zote na iendeleayo mpaka leo (ona Wafilipi 4:7). Pia tulishuhudia zawadi isiyoelezeka ya Roho Mtakatifu katika maisha ya wakwe zetu na watoto wao, ambao mpaka sasa huzungumzia kuhusu wakati ule kwa imani, amani, na faraja” (“Roho Mtakatifu na Ufunuo,” Ensign au Liahona, Nov. 2010, 78).

Kanuni za injili na tamaduni za wanadamu.

Mzee Dallin H. Oaks alionyesha baadhi ya tamaduni za kidunia ambazo zinapingana na kweli za injili (ona “Toba na Badiliko,” Ensign au Liahona, Nov. 2003, 37–40).

  • Kutothamini sheria ya usafi wa kimwili

  • Uhudhuriaji wa kutoshiriki kikamilifu na usio wa kila mara kanisani

  • Kutoishi neno la hekima

  • Udanganyifu

  • Kutamani “madaraka” katika nafasi za Kanisa

  • Utamaduni wa utegemezi badala ya uwajibikaji binafsi

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia muziki. Muziki mtakatifu hukaribisha ushawishi wa Roho Mtakatifu. Unaweza kutengeneza mazingira ya utulivu na kuhamasisha uwajibikaji na matendo. Fikiria jinsi “kufundishana na kuinuana katika zaburi na nyimbo” kunavyoweza kuwa sehemu ya darasa lako (Wakolosai 3:16; ona pia Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 22).