Njoo, Unifuate
Oktoba 21–27. 1 na 2 Wathesalonike: ‘Msitikiswe Katika Mawazo Yenu, au Kuhuzunishwa’


“Oktoba 21–27. 1 na 2 Wathesalonike 2–7: ‘Msitikiswe Katika Mawazo Yenu, au Kuhuzunishwa” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Oktoba 21-27. 1 na 2 Wathesalonike 2–16,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Dada mmisionari akiongea na kijana mdogo wa kiume

Oktoba 21–27.

1 na 2 Wathesalonike

“Msitikiswe Katika Mawazo Yenu, au Kuhuzunishwa”

Alma alifundisha, “Na pia msimwamini yeyote kuwa mwalimu wenu wala mhubiri wenu, ila tu awe mtu wa Mungu, anayetembea katika njia zake na kutii amri zake” (Mosia 23:14). Andiko hili takatifu linapendekeza nini kuhusu jinsi unavyotakiwa kujiandaa kufundisha?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wape washiriki wa darasa dakika chache ili kwa haraka wapitie 1 na 2 Wathesalonike ili kupata mstari ambao unawavutia. Waalike washiriki mistari hiyo na mtu mwingine katika darasa, na kisha uliza baadhi yao kushiriki walichojifunza kutoka kwa kila mmoja wao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

11 Wathesalonike 1:5–8; 2:1–13

Wahudumu wa injili huubiri kwa dhati na kwa upendo.

  • Paulo alianza Waraka wake kwa Wathesalonike kwa kuwakumbusha Watakatifu namna ambayo yeye pamoja na wengine walishiriki injili kwao. Hii inaweza kuwa fursa nzuri kwa washiriki wa darasa kutathmini ni kwa kiasi gani wanafanya katika kufundisha na kujifunza kutoka kwa kila mmoja wao. Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma 1 Wathesalonike 1:5–8; 2:1–13 na kutambua kanuni zinazohusiana na kushiriki injili kikamilifu. Kisha wangeweza kuandika maswali kulingana na mistari hii ambayo itawasaidia wao kutathmini juhudi zao za kufundisha injili kwa wengine. Kwa mfano, swali moja lingeweza kuwa “Je, mimi ni mfano wa yale niyajuayo?” (ona 1 Wathesalonike 1:7). Ni kwa namna ipi ufuataji wa kanuni katika ukurasa huu hutusaidia kuhudumu vizuri zaidi kwa wale tunaowafundisha?

  • Kusoma 1 Wathesalonike 1:5–8; 2:1–13 kunaweza kuwakumbusha washiriki wa darasa juu ya walimu kwa mfano wa Kristo ambao walikuwa na ushawishi chanya kwao “kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe” (1 Wathesalonike 2:11). Waalike washiriki wa darasa kuchunguza vifungu hivi ili kupata sifa ya mhudumu wa dhati na kufikiria kuhusu mwalimu wanayemjua ambaye anaonyesha sifa hiyo. Unaweza kuwauliza washiriki wa darasa kuandiika barua au kutengeneza cheti cha kutunuku kwa ajili ya mwalimu wanayemfikiria. Wahimize kujumuisha katika barua au tuzo mstari kutoka 1 Wathesalonike na maelezo ya jinsi gani mwalimu anaonyesha mfano wa mstari huo. Wanaweza hata kupata mwongozo wa kiungu kumpa barua au tuzo mtu ambaye wamemuandika kuhusu.

11 Wathesalonike 3:9–13; 4:1–12

Tunapomfuata Yesu Kristo, tunaweza kuwa watakatifu.

  • Paulo aliwafundisha Wathesalonike watakatifu kwamba “Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso” (1 Wathesalonike 4:7). Kwa kuanza mjadala kuhusu utakatifu, darasa lako au mtu binafsi angeweza kuimba “More Holiness Give Me” (Wimbo, namba. 131). Waombe washiriki wa darasa kujadili sifa za utakatifu zilizoorodheshwa katika wimbo ambao umewapendeza. Andika ubaoni utakatifu zaidi, hunipa zaidi … , na alika washiriki wa darasa kuangalia maneno au virai kutoka 1 Wathesalonike 3:9–13; 4:1–12 ili kumalizia sentensi. Ni kwa namna gani tunaweza kujenga sifa hizi?

  • Kwa baadhi, wito wa kuwa watakatifu unaweza kuonekana mgumu. Ingeweza kusaidia kama washiriki wa darasa wangeelewa kwamba kujenga utakatifu ni mchakato wa taratibu ambao unatuhitaji sisi “kuongezeka zaidi na zaidi” kadiri ya muda (1 Wathesalonike 4:10). Ili kuonyesha mchakato huu, ungeweza kumwalika mshiriki wa darasa kuzungumza kuhusu kipawa au mafanikio ambayo yalichukua juhudi endelevu kwa muda, kama vile kutengeneza farishi au kucheza chombo cha muziki. Je, hii ni sawa kiasi gani na mchakato wa kuwa mtakatifu? Alika washiriki wa darasa kurejea 1 Wathesalonike 3:9–13; 4:1–12 na kushiriki umaizi wao kuhusu juhudi ambazo huitajika ili kuwa mtakatifu katika njia iliyoelezwa na Paulo. Nini kilitusaidia kukua kuelekea utakatifu?

1 Wathesalonike 4:11–12; 2 Wathesalonike 3:7–13

Lazima tufanye kazi ili tuweze kutimiza mahitaji yetu na ya wale wenye uhitaji.

  • Swali kama lifuatalo lingeweza kuhamasisha mjadala kuhusu ushauri wa Paulo kuhusu kazi: Ni nini madhara ya kutokuwa na shughuli yoyote? Unafikiri Paulo alimaanisha nini kwa maneno “kutulia” na “utulivu”? (1 Wathesalonike 4:11; 2 Wathesalonike 3:12). Ungetaka kuandika maswali kama haya kwenye ubao kwa ajili ya washiriki wa darasa kutafakari wakati wakisoma 1 Wathesalonike 4:11–12 na 2 Wathesalonike 3:7–13. Waalike kujadili maswali haya katika jozi, makundi madogo au kama darasa. Ni maandiko gani mengine hutusaidia kuelewa umuhimu wa kazi na majanga ya kutokuwa na shughuli? (ona mapendekezo “Nyenzo za Ziada.”)

2 Wathesalonike 2

Ukengeufu ulipaswa kutangulia ujio wa pili wa Yesu Kristo.

  • Kuuelewa Ukengeufu Mkuu kunaweza kuimarisha ushuhuda wa washiriki wako wa darasa kuhusu Urejesho wa injili ya Yesu Kristo. Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unajumuisha nyenzo kadhaa kuhusu Ukengeufu. Ungeweza kuwaalika washiriki wachache wa darasa waje wamejiandaa kushiriki umaizi wao kutoka kwenye kusoma kwao nyenzo hizi, au mngeweza kusoma na kujadiliana kwa pamoja kama darasa. Pia kuna baadhi ya video kuhusu ukengeufu katika “Nyenzo za Ziada” ambazo zingeweza kuongezea katika mjadala wenu.

  • Ingeweza kusaidia kama kujadili baadhi ya mifano manabii wameitumia kuelezea Ukengeufu, kama vile kuanguka (ona 2 Wathesalonike 2:3), njaa (ona Amosi 8:11–12), mbwa mwitu wakali wakiingia kwenye kundi (ona Matendo ya Mitume 20:28–30), na masikio ya utafiti (ona 2 Timotheo 4:3–4). Fikiria kugawanya darasa katika jozi na waombe kusoma moja au zaidi ya maandiko ( au mengine ambayo umechagua) na waelezee nini mistari inafundisha kuhusu Ukengeufu Mkuu. Manabii walifundisha nini kuhusu Ukengeufu na nini yangekuwa matokeo yake?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza zaidi kuhusu Ukengeufu Mkuu, waalike kufikiria kuwa wana rafiki ambaye haelewi umuhimu wa hitaji la urejesho wa injili. Tengeneza chati ya safu mbili kwenye ubao Visababishi vya Ukengeufu na Matokeo ya Ukengeufu. Waalike washiriki wa darasa kutafuta sehemu iliyo na kichwa cha habari “Ukengeufu Mkuu” katika Hubiri injili Yangu (ukurasa 35–36) wakiwa katika jozi au vikundi vidogo, wakitafuta visababishi na matokeo ya Ukengeufu ili kuandika ubaoni. Ni umaizi gani kutoka kwenye chati hii wangeweza kuutumia kuwasaidia marafiki zao kuelewa uhitaji wa Urejesho?

  • Je, washiriki wa darasa lako wangenufaika vipi kwa kujadili ni kwa jinsi gani tunaweza kujiweka katika “kutoanguka”? Ungeweza kuwaalika kuchunguza 2 Wathesalonike 2 na kuangalia ushauri ambao wangeweza kumpa rafiki ambao ungemsaidia kuepuka ukengeufu binafsi.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwapa msukumo washiriki wa darasa kusoma 1 na 2 Timotheo, Tito, na Filemoni wiki hii, waalike kuvuta taswira kwamba wamepokea barua binafsi kutoka kwa Mtume ikiwa na ushauri kuhusu namna ya kutekeleza miito yao Kanisani. Pendekeza kwamba wafikirie kuhusu miito yao wakati wakisoma barua hizi binafsi kutoka kwa Paulo kwenda kwa viongozi wa Kanisa la mwanzo.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

1 na 2 Wathesalonike

Maandiko kuhusu kazi na uzembe.

Video kuhusu ukengeufu kwenye LDS.org.

  • “Ukengeufu Mkuu”

  • “Ukengeufu—Jan”

  • “Ukengeufu na Urejesho—Urejesho unamaanisha nini kwangu”

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia njia mbali mbali. Inaweza kuwa rahisi kuridhika na aina fulani ya ufundishaji, lakini njia mbali mbali za ufundishaji huwafikia washiriki tofauti wa darasa. Tafuta njia za kubadilisha namna ya ufundishaji wako, kama vile kutumia video, michoro, muziki, au kutoa nafasi za kufundisha kwa washiriki wa darasa (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 22).

Chapisha