Agano Jipya 2023
Januari 9–15. Mathayo 2: Luka 2: Tumekuja Kumwabudu


“Januari 9–15. Mathayo 2; Luka 2: Tumekuja Kumwabudu,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Januari 9–15. Mathayo 2; Luka 2,” Njoo,Unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Wanaume watatu wakisafiri juu ya ngamia

Na Tumsujudie, na Dana Mario Wood

Januari 9–15

Mathayo 2; Luka 2

Tumekuja Kumsujudia

Kabla hujasoma mawazo katika muhtasari huu, soma Mathayo 2 na Luka 2, na uandike misukumo yako ya kiroho. Hii itakusaidia kupokea ufunuo juu ya jinsi bora ya kukidhi mahitaji ya darasa lako.

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Unawezaje kuwahimiza washiriki wa darasa lako kushiriki utambuzi na uzoefu waliopata walipokuwa wanajifunza maandiko haya kibinafsi na pamoja na familia zao? Ingawa wanaifahamu hadithi ya kuzaliwa kwa Mwokozi iliyoko katika Mathayo 2 na Luka 2, daima wanaweza kujipatia utambuzi mpya wa kiroho Fikiria kuwaalika washiriki wachache wa darasa kushiriki ujumbe walioupata katika Luka 2 au Mathayo 2 ambao uliwavutia katika njia mpya.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 2:1–12; Luka 2:1–38

Kuna mashahidi wengi wa kuzaliwa kwa Kristo.

  • Maelezo ya waabuduo katika Mathayo 2:1– 12 na Luka 2:1– 38 yanaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kutafakari njia wanazoonyesha upendo wao kwa Mwokozi. Rejelea chati kuhusu mashahidi wa kuzaliwa kwa Kristo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Baadhi ya watu katika darasa lako wanaweza kuwa na utambuzi wa kushiriki kutoka katika shughuli hii, au mnaweza kufanya shughuli kama darasa. Kwa nini ni ya kipekee kwamba mashahidi hawa wa Kristo walikuja kutoka kada mbalimbali za maisha? Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mifano yao?

    mchungaji pamoja na kondoo

    Wachungaji walikuja kuwa sehemu ya mashahidi wa kwanza wa kuzaliwa kwa Mwokozi.

  • Kabla mashahidi hawa hawajamwabudu mtoto Kristo, kwanza walimtafuta. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kutoka mfano wao, unaweza kuandika ubaoni vichwa vya habari vifuatavyo: Wachungaji, Ana, Simioni, na Mamajusi. Kisha waalike washiriki wa darasa kupekua Luka 2 na Mathayo 2 na waandike ubaoni kitu ambacho watu hawa walichofanya ili kumtafuta Mwokozi. Hadithi hizi zinapendekeza nini kuhusu baadhi ya njia tunazoweza kumtafuta Kristo?

Mathayo 2:13–23

Wazazi wanaweza kupokea ufunuo ili kuzilinda familia zao.

  • Ili kuanza majadiliano kuhusu Baba wa Mbinguni kuwaongoza Yusufu na Mariamu katika nafasi zao kama wazazi wa Mwokozi, fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kuorodhesha ubaoni baadhi ya hatari tunazokabiliana nazo leo. Tunajifunza nini kutoka katika Mathayo 2:13–23 kuhusu jinsi ya kupata ulinzi kutokana na hatari hizi? Ni kwa jinsi gani ufunuo binafsi umetusaidia kulinda familia zetu au wapendwa wetu wengine kutokana na hatari? Ni ushauri gani manabii na mitume wametupatia ili kutusaidia kupata usalama wa kiroho?

Luka 2:40–52

Hata alipokuwa kijana, Yesu alizingatia kutenda mapenzi ya Baba Yake.

  • Hadithi ya Yesu akifundisha hekaluni wakati alipokuwa na umri wa miaka 12 tu inaweza kuwa yenye nguvu hususani kwa vijana ambao wanajiuliza kuhusu mchango wanaoweza kufanya kwenye kazi ya Mungu. Ungeweza kuligawa darasa katika jozi ili kusoma Luka 2:40–52 pamoja (ona utambuzi kutoka Tafsiri ya Joseph Smith inayopatikana katika Luka 2:46, tanbihi c ). Kila jozi inaweza kuchukua dakika chache kushiriki pamoja kile kinachowavutia kuhusu tukio hili. Ni fursa gani tulizo nazo za kushiriki kitu tunachojua kuhusu injili? Ni uzoefu gani tunaweza kuushiriki?

  • Ni kitu gani Luka 2:40–52 inatufundisha kuhusu Yesu alikuwa mtu wa aina gani alipokuwa bado kijana ? Mpangilio wa ukuaji binafsi uliopendekezwa katika Luka 2:52 unaweza kuchochea majadiliano juu ya sisi tunafanya nini ili kuwa zaidi kama Kristo. Unaweza kupendekeza kwamba washiriki wa darasa watafakari jinsi wanavyoongezeka katika hekima (kiakili), kimo (kimaumbile), kupendwa na Mungu (kiroho) na kupendwa na wengine (kijamii). Wanaweza hata kuweka malengo katika moja au zaidi ya maeneo haya. Kama ungependa kuendeleza majadiliano kuhusu kuwa zaidi kama Kristo katika maeneo haya , hususani kama wewe unafundisha vijana, zingatia kutumia kauli katika “Nyenzo za Ziada.”

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kuwasaidia watoto na vijana kukua “katika hekima na kimo, wakimpendeza Mungu na mwanadamu.”

Rais Steven J. Lund alielezea programu ya Watoto na Vijana, ambayo kwa sehemu imetokana na Luke 2:52, katika njia hii:

“Watoto na Vijana ni chombo cha kumsaidia kila mtoto wa Msingi na kijana kukua katika ufuasi na kupata maono yaliyojaa imani ya jinsi njia ya furaha ilivyo. Wanaweza kutarajia na kutamani vituo vya njiani na mabango ya alama kwenye njia ya agano, ambapo watabatizwa na kuthibitishwa kwa kipawa cha Roho Mtakatifu na punde kuwa sehemu ya akidi na madarasa ya Wasichana, ambako watahisi shangwe ya kuwasaidia wengine kupitia urithi wa matendo ya huduma kama ya Kristo. Watajiwekea malengo, makubwa na madogo, ambayo yataleta uwiano katika maisha yao kadiri wanavyokuja kuwa zaidi kama Mwokozi” (“Kupata Shangwe katika Kristo,” Liahona, Nov. 2020, 36–37).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wajumuishe wanafunzi ambao hawakujifunza maandiko nyumbani. Hata kama baadhi ya washiriki wa darasa hawakuweza kusoma Mathayo 2 na Luka 2 kabla ya darasa, wanaweza bado kushiriki utambuzi wa maana. Hakikisha kwamba washiriki wote wa darasa wana fursa ya kushiriki na kuchangia kwenye majadiliano.