“Januari 23–29. Mathayo 3; Marko 1; Luka 3; ‘Itengenezeni Njia ya Bwana’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)
“Januari 23–29. Mathayo 3; Marko 1; Luka 3,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Januari 23–29
Mathayo 3; Marko 1; Luka 3
“Itengenezeni Njia ya Bwana”
Unaposoma na kutafakari Mathayo 3; Marko 1; na Luka 3, andika misukumo unayopokea. Hii itamwalika Roho katika maandalizi yako ya kufundisha. Kwa kuongezea katika mawazo ya kufundisha katika muhtasari huu, mawazo ya kujifunza katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia yanaweza kutumiwa katika darasa lako.
Alika Kushiriki
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki jinsi kujifunza kutoka kwenye Agano Jipya kunavyobariki maisha yao, unaweza kuandika swali lifuatalo ubaoni: Ni kitu gani ulifanya kwa sababu ya kile ulichokisoma katika Agano Jipya wiki hii? Waombe washiriki wa darasa kushiriki majibu yao.
Fundisha Mafundisho
Wafuasi wanajiandaa wao wenyewe pamoja na wengine kumpokea Yesu Kristo.
-
Tunajiandaa vipi kwa ziara ya mgeni mashuhuri? Swali kama hili linaweza kukusaidia kutambulisha majadiliano kuhusu jinsi Yohana Mbatizaji alivyowaandaa watu kumpokea Yesu Kristo. Ungeweza halafu kuligawa darasa katika makundi matatu. Kila kundi lingeweza kusoma ama Mathayo 3:1–6; Mathayo 3:7–12; au Luka 3:10–15, wakitafuta jinsi Yohana Mbatizaji alivyowaandaa watu kumpokea Yesu Kristo katika maisha yao. Acha kila kikundi kichukue zamu kushiriki kile walichopata.
Tunahitaji kuleta kwake “matunda yapatanayo na toba.”
-
Katika Luka 3:8, Yohana Mbatizaji aliwafundisha watu kwamba kabla hawajabatizwa, walihitaji kuonyesha “matunda,” au ushahidi, wa toba yao. Unawezaje kuwasidia washiriki wa darasa kutambua ushahidi wa toba yao wenyewe? Unaweza kuwaomba wapekue Luka 3:8–14 na kutafuta kile Yohana alichofikiria kuwa ni “matunda” ya toba. Wanaweza pia kurejelea Moroni 6:1–3 na Mafundisho na Maagano 20:37. Unaweza kuchora mti wa matunda ubaoni na waalike washiriki wa darasa kutoa jina kwenye tunda la mti kwa “matunda” ya toba wanayoyapata. Huu unaweza pia kuwa muda mzuri wa kuzungumza kuhusu inamaanisha nini kutubu kikweli kweli.
Tunamfuata Yesu Kristo wakati tunapobatizwa na kumpokea Roho Mtakatifu.
-
Ili kurejelea hadithi ya ubatizo wa Yesu Kristo, jaribu wazo hili: Waulize washiriki wa darasa jinsi watakavyotumia Mathayo 3:13–17 kumfundisha mtu, kama vile mtoto au mtu mwingine wa imani nyingine, kuhusu ubatizo. (Wanaweza pia kutumia picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Ni vipengele gani muhimu vya ubatizo watakavyotilia mkazo? Wanaweza kufanya mazoezi ya mawazo yao kwa kufundishana wao kwa wao.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kukumbuka umuhimu wa kuishi maagano yao ya ubatizo, ungeweza kumwaalika mtu kusoma maelezo ya Mzee Bednar kwenye “Nyenzo za Ziada.” Washiriki wa darasa wanaweza kufurahia kushiriki hisia zao kuhusu ubatizo wao wenyewe na maagano yao ya ubatizo. Wangeweza pia kuimba wimbo wa Kanisa kuhusu kumfuata Mwokozi, kama vile “Come, Follow Me” (Nyimbo za Kanisa, na. 116).
-
Yohana Mbatizaji alifundisha kwamba Mwokozi angebatiza “kwa Roho Mtakatifu, na kwa moto” (Mathayo 3:11). Ubatizo wa moto unatokea wakati tunapothibitishwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa nini lazima tuwe na kipawa cha Roho Mtakatifu ili kuendelea katika ufalme wa Mungu? Je, ubatizo wa moto na Roho Mtakatifu unayo tija gani juu yetu sisi? (ona Alma 5:14). Video ya “Baptism of the Holy Ghost” (ChurchofJesusChrist.org) ingeweza kusaidia katika mjadala huu.
Nyenzo za Ziada
Maagano ya ubatizo wetu.
Mzee David A. Bednar alifundisha: “Agano la ubatizo linajumuisha masharti muhimu matatu: (1)Kuwa radhi kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo, (2) na daima kumkumbuka na (3) kushika amri Zake. Baraka zilizoahidiwa kwa kuheshimu agano hili ni ‘ili daima Roho Wake apate kuwa pamoja nasi.”[Mafundisho na Maagano 20:77]. Hivyo, ubatizo ni matayarisho muhimu ya kupokea fursa iliyoidhinishwa ya wenza wa daima wa mshiriki wa tatu wa Uungu” (“Daima Linda Msamaha wa Dhambi Zako,” Liahona, Mei 2016, 60).
Kwa ajili ya mfano wa mvulana mdogo anayeshika maagano yake ya ubatizo, ona hadithi mwanzoni mwa ujumbe wa Dada Carole M. Stephen “Tunayo Sababu Kuu ya Kushangilia” (Liahona, Nov. 2013, 115–17).