“Desemba 26–Januari 1. Tunawajibika kwa Kujifunza Kwetu Wenyewe,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022.)
“Desemba 26–Januari 1. Tunawajibikia kwa Kujifunza Kwetu Wenyewe.” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Desemba 26–Januari 1
Tunawajibika kwa Kujifunza Kwetu Wenyewe
Unaposoma na kutafakari vifungu vya maandiko katika muhtasari huu, andika misukumo ya kiroho unayopokea. Hii itamwalika Roho katika maandalizi yako. Njoo Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia na mawazo yafuatayo yanaweza kukusaidia kuwapa mwongozo watu katika darasa lako kujifunza Agano Jipya mwaka huu.
Alika Kushiriki
Mojawapo ya malengo yako kama mwalimu ni kuwahimiza washiriki wa darasa kujifunza kutoka katika maandiko wao wenyewe pamoja na familia zao. Kusikiliza uzoefu wa wengine kunaweza kuwahamasisha watu kutafuta uzoefu wao wenyewe. Kwa hiyo, mwanzoni mwa kila darasa, waombe washiriki wa darasa kushiriki maandiko kutokana na kujifunza kwao ambayo yaliwapa mwongozo au yaliwavutia.
Fundisha Mafundisho
Kujifunza kunahitaji kutenda kwa imani.
-
Ni kwa jinsi gani unaweza kushawishi washiriki wa darasa lako kuchukua nafasi za kujishughulisha zaidi katika kujifunza kwao, kuliko kumwachia jukumu hilo mwalimu pekee? Hapa kuna wazo. Rusha kitu kwa mshiriki wa darasa, ambaye ulimpanga mapema ukimwomba asifanye jitihada yoyote ya kukidaka. Tumia shughuli hii kuanzisha majadiliano kuhusu wajibu wa wanafunzi na walimu katika kujifunza injili. Kama wanafunzi, “tunadakaje” kile kinachofundishwa madarasani mwetu? Maelezo yanayopatikana katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza kusaidia katika mjadala huu.
-
Washiriki wote wa darasa wana wajibu wa kumwalika Roho katika darasa. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa hili, waambie wasome Alma 1:26 na Mafundisho na Maagano 50:13–22; 88:122–23 na kushiriki kile walimu na wanafunzi wanaweza kufanya ili kumwalika Roho. Inaweza kusaidia kuandika majibu yao ubaoni chini ya vichwa vya habari kama hivi: Nini mwalimu anaweza kufanya na Nini wanafunzi wanaweza kufanya. Washiriki wa darasa wangeweza kutengeneza bango lenye majibu yao ambalo lingeweza kuonyeshwa kwa wiki chache zitakazofuata?
Tunahitaji kuujua ukweli sisi wenyewe.
-
Vifungu vingi katika Agano Jipya vinafundisha kanuni ambazo zinaweza kuongoza uchunguzi wetu wa ukweli. Mifano inajumuisha Luka 11:9–13; Yohana 5:39; 7:14–17; na 1 Wakorintho 2:9–11. Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa lako wanaosoma vifungu hivi katika kujifunza kwao binafsi kushiriki kile walichojifunza. Au mnaweza kusoma vifungu hivi kama darasa na kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki jinsi walivyopata shuhuda zao.
-
Matendo ya Mitume 17:10–12 inaelezea kwamba Watakatifu walipekua maandiko na kupata ushahidi wa ukweli wao wenyewe. Kuwahimiza washiriki wa darasa kufuata mfano wao, someni aya hizi pamoja na waalike washiriki wa darasa kushiriki vifungu vya maandiko ambavyo vimeimarisha shuhuda zao juu ya injili.
Tunawezaje kufanya kujifunza kwetu maandiko kuwa na maana zaidi?
-
Kujenga tabia ya kujifunza maandiko inaweza kuwa changamoto kwa washiriki wa darasa wanaohisi kwamba hawana muda unaohitajika, uelewa au ujuzi. Unaweza kufanya nini ili kuwasaidia waweze kufanikiwa? Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupata kujiamini kujifunza maandiko, unaweza kushiriki taarifa kutoka “Mawazo ya Kuboresha Kujifunza kwako Binafsi Maandiko” katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia. Labda wewe au washiriki wengine wa darasa mngeshiriki uzoefu wa kutumia baadhi ya mawazo haya au uzoefu mwingine wa maana wa kujifunza maandiko. Mnaweza pia kuchagua sura katika Agano Jipya na kujaribu kujifunza kama darasa mkitumia baadhi ya mawazo haya.
Nyenzo za Ziada
Kudai maarifa ya kiroho kwa ajili yetu wenyewe.
Nabii Joseph Smith alifundisha: “Mambo ya Mungu ni yenye umuhimu mkubwa na muda, na uzoefu, na mawazo ya uangalifu na tafakuri na unyenyekevu ndivyo pekee vinaweza kuyagundua. Akili yako, Ewe mwanadamu! Kama utapenda itaiongoza nafsi kwenye wokovu, lazima itanuke na kufika mbali kama ziliko mbingu, na kupekua ndani na kutafakari kilindi chenye kiza kuu na anga pana la umilele—lazima uongee na Mungu. Ni matukufu na ya kipekee zaidi kiasi gani mawazo ya Mungu, kuliko ndoto tupu za moyo wa mwanadamu!” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007],267).
Mzee David A. Bednar alielezea: Kama wote ninyi au mimi tunajua kuhusu Yesu Kristo na injili Yake ya urejesho ndicho watu wengine wanachofundisha au wanachotuambia, basi msingi wa ushuhuda wetu juu Yake na kazi Yake tukufu ya siku za mwisho imejengwa juu ya mchanga. Hatuwezi tukategemea pekee juu ya au kuazima nuru ya injili na maarifa kutoka kwa watu wengine—hata wale tunaowapenda na kuwatumaini” (“Kuandaliwa Kupata Kila Kitu Kinachohitajika,” Liahona, Mei 2019, 102).