Agano Jipya 2023
Julai 3–9. Matendo ya Mitume 1–5: “Mtakuwa Mashahidi juu Yangu”


“Julai 3–9. Matendo ya Mitume 1–5: ‘Mtakuwa Mashahidi Juu Yangu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022.)

“Julai 3–9. Matendo ya Mitume 1–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
umati wa watu kando ya mto na wanabatizwa mtoni

Siku ya Pentekoste, na Sidney King

Julai 3–9

Matendo ya Mitume 1–5

“Mtakuwa Mashahidi Juu Yangu”

Kama utasoma Matendo ya Mitume 1–5 na kutafuta mwongozo wa Roho, utapokea mwongozo wa kiungu kuhusu kweli zilizopo kwenye sura hizi ambazo zitawasaidia washiriki wa darasa lako kutegemea kikamilifu zaidi juu ya Roho Mtakatifu na kuwa mashahidi waaminifu wa Bwana Yesu Kristo.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kuna vifungu vingi na kanuni nyingi muhimu katika Matendo ya Mitume 1–5. Njia kuu mojawapo ya kugundua ni vipi vya thamani na vyenye kuhusiana na washiriki wa darasa lako ni kwa kuwaacha wao wakuambie ni kitu gani cha kipekee walichokipata wakati wa kujifunza kwao. Je, ni kwa namna gani unaweza kualika namna hii ya kushiriki? Ingeweza kuwa rahisi kama vile kuwapa dakika chache kutafuta na kuelezea mstari kutoka Matendo ya Mitume 1–5 ambapo walihisi sauti ya Bwana ikizungumza nao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho Rasmi

Matendo ya Mitume 1:1–8; 2:37–39; 4:1–13, 31–33

Yesu Kristo huliongoza Kanisa Lake kupitia Roho Mtakatifu.

  • Kusoma kuhusu uzoefu wa Mitume kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuona jinsi gani wanaweza kupokea nguvu na mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu katika miito yao na kazi za Kanisani. Njia mojawapo ya kurejelea uzoefu katika Matendo ya Mitume 1–5 ingekuwa kuandika ubaoni Roho Mtakatifu aliwasaidia Mitume kuliongoza Kanisa kwa: na kisha waalike washiriki wa darasa kutafuta kutoka Matendo ya Mitume 1:1–8; 2:37–39; na 4:1– 13, 31–33, wakiangalia njia za kumalizia sentensi hiyo. Washiriki wa darasa pia wangeweza kushiriki uzoefu wao ambapo Roho Mtakatifu aliwasaidia katika njia hizi. Kwa nini Mitume walimhitaji Roho Mtakatifu—na kwa nini sisi tunamhitaji Yeye?

Matendo ya Mitume 1:15–26

Mitume wa Yesu Kristo wanaitwa na Mungu kupitia ufunuo.

  • Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kuelezea jinsi gani makampuni ya kibiashara hupitia mchakato wa kumchagua mtu kujaza nafasi ya mtendaji. Je, ni sifa gani wangeweza kuziangalia? Waombe washiriki wa darasa kutofautisha na jinsi Mtume Mathiya alivyoitwa (ona Matendo ya Mitume 1:15–26; ona pia 1 Samweli 16:1–13) na pamoja na maneno ya Rais Gordon B. Hinckley katika “Nyenzo za Ziada” akielezea jinsi Mitume wanavyoitwa leo. Ni kwa namna gani mbinu ya Mungu ya kuwachagua viongozi inagusa imani yetu kwa viongozi Anaowaita? Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki ni kwa namna gani wao wamepata ushahidi kwamba mitume na manabii wanaitwa na Yeye.

Matendo ya Mitume 2:37–47

Roho Mtakatifu hutushawishi kutendea kazi yale tunayojifunza.

  • Wakati washiriki wa darasa wanapojifunza maandiko nyumbani na kwa pamoja katika darasa kila wiki wanaweza kila mara kuhisi “kuchomwa mioyoni mwao” (Matendo ya Mitume 2:37). Unaweza kusikia mwongozo wa kiungu ili kuwasaidia kwenda hatua moja mbele kwa kuwauliza, “Je, tunapaswa kufanya nini?” Matendo ya Mitume 2:37). Someni Matendo ya Mitume 2:37–47 kwa pamoja, waalike washiriki wa darasa kutafuta mambo ambayo kundi hili la watu 3,000 lilifanya kama matokeo ya mwaliko wa Petro. Labda wangeweza pia kuelezea njia ambazo wao wamefanyia kazi kutokana na mwongozo wa kiungu waliopata kutokana na usomaji wao wa neno la Mungu. Kisha ungeweza kubakiza muda wakati wa darasa kuisha kwa kila mtu kujiuliza swali “Je, mimi nitafanya nini?” na kuandika misukumo yao.

Picha
Petro akitabasamu na kuhubiri huku uso wake ukiwa na majeraha

Licha ya kufungwa gerezani na kupigwa, Petro kwa uthabiti alihubiri injili.

Matendo ya Mitume 3; 4:1–21; 5:12–42

Tunapokuwa tumejawa na Roho Mtakatifu, tunaweza kufundisha injili kwa ujasiri.

  • Washiriki wa darasa wangeweza kurejelea Matendo ya Mitume 3; 4:1–21; 5:12–42, wakitafuta mifano ya Petro akishuhudia kwa ujasiri. Au wangeweza kutazama moja ya video zifuatazo: “Peter Preaches and Is Arrested,” “Peter and John Are Judged,” au “Peter and John Continue Preaching the Gospel” (ChurchofJesusChrist.org). Je, inamaanisha nini kuzungumza “neno la Mungu kwa ujasiri”? Matendo ya Mitume 4:31). Je, Roho Mtakatifu anatusaidiaje kushiriki injili kwa ujasiri? Ni jinsi gani aina hii ya ujasiri ni tofauti na kuwa mbishi? Washiriki wa darasa yawezekana pia wakawa na uzoefu wa kusimulia ambapo wao, au mtu mwingine wanayemjua, kwa ujasiri alitetea au alishuhudia juu ya injili.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Wito wa mshiriki wa wale Kumi na Wawili

Gordon B. Hinckley alielezea utambuzi ufuatao kuhusu mchakato wa kuitwa kwa Mtume mpya: “utaratibu ni wa kipekee kwa kanisa la Bwana. Hakuna kutafuta ofisi, hakuna kushindania nafasi, hakuna kampeni ya kunadi wema wa mtu. Njia ya Bwana ni tofauti na njia ya ulimwengu. Njia ya Bwana ni tulivu, ni njia ya amani, haina mshindo wa nderemo wala gharama za kifedha. Haina kujikweza wala malengo yasiyo na maana. Chini ya mpango wa Bwana, wale wenye majukumu ya kuchagua maofisa wanaongozwa na swali moja la muhimu: ‘Ni yupi Bwana angemtaka?’ Kuna ukimya na kushauriana kwa kina. Na kuna sala nyingi ili kupokea uthibitisho wa Roho Mtakatifu kwamba chaguo ni sahihi” (“God Is at the Helm,” Ensign, Mei 1994,53).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Waalike Wanafunzi Kutenda. Roho Mtakatifu mara kwa mara anatushawishi kufanyia kazi kitu tunachojifunza (ona Matendo ya Mitume 2:37). Wakati hili lilipotokea kwa watu ambao Petro alikuwa akiwafundisha, alitoa mwaliko kwao (ona Mtaendo ya Mitume 2:38). Fikiria jinsi unavyoweza kufuata mfano wa Petro.

Chapisha