Agano Jipya 2023
Julai 10–16. Matendo ya Mitume 6–9: “Ungetaka Nifanye Nini?”


“Julai 10–16. Matendo ya Mitume 6–9: ‘Ungetaka Nifanye Nini’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Julai 10–16. Matendo ya Mitume 6–9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Paulo ameanguka chini ardhini

Uongofu katika Njia ya kwenda Dameski, na Michelangelo Merisi da Caravaggio

Julai 10–16

Matendo ya Mitume 6–9

“Ungetaka Nifanye Nini?”

Jifunze Matendo ya Mitume 6–9 na uandike misukumo yako. Hii itakusaidia kupokea ufunuo juu ya jinsi ya kuwasaidia washiriki wa darasa lako kumsogelea Kristo kupitia kujifunza kwao sura hizi.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ubaoni, andika majina ya watu waliotajwa katika Matendo ya Mitume 6–9, kama vile Stefano, Sauli, Filipo, Anania, Petro, na Tabitha au Dorkasi. Waliike washiriki wachache wa darasa kuelezea kitu walichojifunza kutoka kwa mmoja wa watu hawa katika kujifunza kwao wiki hii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Matendo ya Mitume 7

Kumpinga Roho Mtakatifu kunaweza kusababisha kumkataa Mwokozi na watumishi Wake.

  • Unaweza kuanzisha mjadala kuhusu tukio la Stefano kwa kuwaalika washiriki wa darasa kurejelea maneno ya Stefano katika Matendo ya Mitume 7:37–53. Ni maonyo gani maneno yake yanaweza kuwa nayo kwa ajili yetu leo? Unaweza kuzingatia maelezo ya Stefano katika Matendo ya Mitume 7:51. Je, ina maana gani “kumpinga Roho Mtakatifu? Ili kuelewa maneno haya kwa kina, washiriki wa darasa wangeweza kujadili kifungu kimoja au zaidi ya vifungu hivi: 2 Nefi 28:3–6; 33:1–2; Mosia 2:36–37; Alma 10:5–6; na Alma 34:37–38. Je, ni kwa nini sisi wakati mwingine “tunampinga Roho Mtakatifu”? Tunaweza kufanya nini ili kuweza kutambua zaidi na kufuata ushawishi wa Roho Mtakatifu?

Matendo ya Mitume 8:9–24

Mioyo yetu inatakiwa kuwa “minyoofu mbele za Mungu.”

  • Ili kusoma hadithi ya Simioni kama darasa, ungeweza kuandika ubaoni maswali haya Je, Simoni alikuwa nani? Alitaka nini? na Jinsi gani alijaribu kukipata? Mpangie kila mshiriki wa darasa kusoma Matendo ya Mitume 8:9–24, akitafuta majibu ya maswali haya. Ni kweli zipi ambazo Simoni alikuwa hajazielewa? Tunajifunza nini kutokana na uzoefu wa Simoni? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuhakikisha mioyo yetu ni “minyoofu mbele za Mungu”? (mstari 21).

  • Wakati wa kujifunza kwao binafsi, baadhi ya washiriki wa darasa yawezekana kuwa wamegundua sifa ambazo Stefano na Paulo walikuwa nazo ambazo Simoni hakuwa nazo (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia). Kama ndivyo, waalike kushiriki walichopata. Washiriki wa darasa wangeweza pia kushiriki mifano mingine kutoka Matendo ya Mitume 6–9 ya watu ambao mioyo yao ilikuwa minyoofu mbele za Mungu, kama vile Filipo na yule mtu wa kutoka Ethiopia (ona Matendo ya Mitume 8:26–40), Sauli (ona Matendo ya Mitume 9:1–22), na Tabitha (ona Matendo ya Mitume 9:36–39).

    Picha
    Petro akimfufua Tabitha kutoka wafu

    Tabitha Ondoka, na Sandy Freckleton Gagon

Matendo ya Mitume 8:26–39

Roho Mtakatifu atatusaidia kuwaongoza wengine kwa Yesu Kristo.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa ni kwa namna gani wanaweza kuwaongoza wengine kwa Yesu Kristo (ona Matendo ya Mitume 8:31), ungeweza kuwaalika washiriki wawili wa darasa kukaa wakitazamana na kusoma majibizano kati ya Filipo na mtu yule wa kutoka Ethiopia katika Matendo ya Mitume 8:26–39. Mshiriki wa tatu wa darasa angeweza kusoma sehemu ambazo si za majibizano. Tunajifunza nini kutokana na mfano wa Filipo kuhusu kufundisha injili kwa wengine?

  • Ili kufafanua mifano ya sasa ya hadithi katika Matendo ya Mitume 8:26–39, washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu waliokuwa nao katika kushiriki injili au kujiunga kwao na Kanisa. Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu aliwasaidia? Ni kwa namna gani mtu alitumika kama mwongozaji kwao? Waalike washiriki wa darasa kutafakari nani wanaweza kumwongoza kwenye injili.

Matendo ya Mitume 9

Tunapokubali mapenzi ya Bwana, tunaweza kuwa vyombo katika mikono yake.

  • Washiriki wa darasa wanaweza kujifunza kweli zenye nguvu kuhusu uongofu wao kwa kujifunza kutokana na uzoefu wa Sauli, ikijumuisha ukweli kwamba kila mtu anaweza kutubu na kubadilika kama watakuwa tayari. Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kulinganisha tukio la Sauli na lile la Alma (ona Mosia 17:1–4;18; 26:15–21) na Wapinga Nefi–Lehi (ona Alma 24: 7–12). Je, Bwana alifanya nini ili kuwasidia watu hawa kuwa wenye kuongoka? Je ni kwa namna gani walionyesha utayari wao wa kubadilika? Ni jumbe gani tunazipata kwa ajili ya maisha yetu wenyewe kutokana na hadithi hizi?

  • Ili kuchochea mjadala kuhusu tukio la Sauli, ungeweza kuwaalika washiriki wachache kuja wakiwa wamejiandaa kuelezea kile wanachojifunza kutoka kila sehemu ya ujumbe wa Rais DieterF. Uchtdorf “Kusubiri katika Barabara iendayo Dameski” (Liahona, Mei 2011, 70–77). Ni kwa namna gani wakati mwingine tunasubiri katika njia yetu wenyewe ya kwenda Dameski? Kulingana na Rais Uchtdorf, nini kinaweza kutusaidia kuisikia vyema zaidi sauti ya Mungu? Unaweza pia kufikiria kuangalia video “The Road to Dameski” (ChurchofJesusChrist.org). Labda washiriki wa darasa wangeelezea uzoefu wao wa kutafuta katika kufuata mapenzi ya Mungu.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Shuhudia juu ya Yesu Kristo. Kama mwalimu, unaweza kuwaongoza wale unaowafundisha kupitia maandiko, kama vile tu Filipo alivyomwongoza Muethiopia kwa kumfundisha kutoka Isaya (ona Matendo ya Mitume ya Mitume 8:26–37). Ili kufanya hili, ni lazima uwe na uzoefu wako wewe mwenyewe wa kujenga imani katika maandiko. Ushahidi unaoutoa unaweza kuwa nguvu kubwa katika kuwasaidia washiriki wa darasa kuimarisha shuhuda zao juu ya Yesu Kristo.

Chapisha