“Agosti 7–13. Warumi 1–6: ‘Uweza wa Mungu Uletao Wokovu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)
“Agosti 7–13. Warumi 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Agosti 7–13
Warumi 1–6
“Uweza wa Mungu Uletao Wokovu”
Kwa maombi soma Warumi 1–6 ukiwa na washiriki wa darasa lako akilini mwako. Hii itakusaidia kuwa makini na ushawishi wa Roho unapojiandaa kufundisha.
Alika Kushiriki
Fikiria kuwapa washiriki wa darasa dakika chache kupekua Warumi 1–6 kwa ajili ya aya ambayo Roho Mtakatifu aliwasaidia wao kuuelewa vizuri zaidi. Kisha wanaweza kushiriki aya hiyo waliyoichagua na mtu ambaye wamekaa karibu naye.
Fundisha Mafundisho
“Siionei haya injili ya Kristo.”
-
Watu wengi wamekuwa na matukio ambapo walifanyiwa mzaha kwa sababu ya imani zao. Ili kuwasaidi washiriki wa darasa wanapokutwa na matukio ya jinsi hiyo, unaweza kuwaalika kusoma Warumi 1:16–17 na kufikiria juu ya mifano kutoka kitabu cha Matendo ya Mitume ambapo Paulo alionyesha kutoionea haya injili. Labda washiriki wa darasa wangeweza pia kushiriki sababu wanazohisi kutoionea aibu injili ya Yesu Kristo. Au wangeweza kuelezea matukio ambapo wao au watu wengine walionyesha kuwa hawaionei haya injili.
Ufuasi wa kweli unapatikana katika kujitolea kwetu kwa dhati kutoka ndani kabisa, si tu katika matendo yetu.
-
Ni kwa namna gani tunatathmini ufuasi wetu? Ushauri wa Paulo kwa Warumi unaweza kutusaidia sisi kukumbuka kufokasi zaidi juu ya “moyo [na] roho” (Warumi 2:29). Ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa ushauri wa Paulo, ungeweza kuandika ujumbe kutoka Warumi 2:28–29 kwenye ubao. Badilisha neno Myahudi kwa neno Mtakatifu wa Siku za Mwisho na neno tohara kwa neno agano. Badiliko hili linaongeza nini katika uelewa wetu kuhusu mafundisho ya Paulo? Ungeweza pia kujadili mifano ya mambo tunayofanya kama waumini wa Kanisa ambayo huwa ya maana na nguvu zaidi kama yakifanywa kwa “moyo, katika roho” (Warumi 2:29).
“Na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi.”
-
Je, unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa mafundisho ya Paulo kuhusu imani, matendo, na neema? Fikiria kushiriki matukio mawili yafuatayo ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kwamba hatupaswi kuona matendo yetu mema kama njia ya kuthibitisha ustahiki wetu, wala hatupaswi kuiona neema ya Kristo kama sababu ya kuhalalisha makosa na dhambi zetu. Washiriki wa darasa wangeweza kutafuta kweli kutoka Warumi 3:20–31; 5:1–2; 6:1–2, 21–23 ambazo zingeweza kuwasaidia Gloria na Justin. Ni kweli zipi zingine katika “Nyenzo za Ziada” zingeweza kuwasaidia kuelewa umuhimu wa vyote matendo mema na neema ya Kristo?
Nyenzo za Ziada
Imani, neema na matendo
Onyesho 1
-
J. Devn Cornish, “Je, Mimi ni Mzuri vya Kutosha? Je, Nitaweza?” Liahona, Nov. 2016, 32–34
-
Rais Dieter F. Uchtdorf alifundisha: “Wokovu hauwezi kununuliwa kwa sarafu ya utiifu; unanunuliwa kwa damu ya Mwana wa Mungu. … “Neema ni kipawa cha Mungu, na hamu yetu kuwa watiifu kwa kila amri ya Mungu ni njia ya kunyoosha mkono wetu kupokea kipawa hiki kitakatifu kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni” (“Kipawa cha Neema,” Liahona, Mei 2015, 109–10).
Mfano wa 2
-
D. Todd Christofferson, ““Kaeni katika Pendo Langu,” Liahona, Nov. 2016, 48.
-
Rais Uchtdorf alifundisha: “Kama neema ni kipawa cha Mungu, kwa nini basi utiifu kwa amri za Mungu ni muhimu sana? Kwa nini kusumbuka na amri za Mungu—au toba, kwa jambo hilo? … “Utii wetu kwa amri za Mungu unakuja kama matokeo ya asili ya upendo wetu usio na mwisho na shukrani kwa wema wa Mungu. Aina hii ya upendo wa kweli na shukrani kimiujiza utaunga matendo yetu na neema ya Mungu” (“Kipawa cha Neema,” 109).