“Agosti 14–20. Warumi 7–16 ‘Shinda Uovu kwa Wema’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022.)
“Agosti 14–20. Warumi 7–16” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Agosti 14–20
Warumi 7–16
“Shinda Uovu kwa Wema”
Soma Warumi 7–16, na andika misukumo unayopokea kuhusu jinsi ya kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kutoka kwenye maandiko. Unapotafakari misukumo yako, inaweza kukuongoza kwenye shughuli za maana za kujifunza.
Alika Kushiriki
Fikiria kusoma Warumi 10:17 na 15:4 na kuwaomba kushiriki maandiko kutoka Warumi 7–16 ambayo yanajenga imani yao katika Yesu Kristo au kuwapa tumaini.
Fundisha Mafundisho
Tunaweza kuwa warithi pamoja na Kristo”
-
Kama Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunaamini kuwa virai kama “warithi wa Mungu” na “warithi pamoja na Kristo” vinamaanisha kwamba kwa msaada wa Yesu Kristo, tunaweza kuwa kama Baba wa Mbinguni na kupokea vyote Yeye alivyo navyo (Warumi 8:17; ona pia Mafundisho na Maagano 132:20–21). Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuona jinsi gani mafundisho haya yanafundishwa kote katika maandiko, ungeweza kuwaalika kuwa wawili wawili au vikundi vidogo vidogo na kujifunza baadhi ya maandiko yaliyoorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada.” Kisha washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile walichopata na kujadili kwa nini mafundisho haya ni muhimu sana.
-
Analojia iliyotolewa na Rais Dallin H. Oaks katika “Nyenzo za Ziada” ingeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kujadili ni kwa namna gani tunaweza kujiandaa kuwa “Warithi wa Mungu” (Warumi 8:17). Ni zipi baadhi ya “sheria na kanuni” Rais Oaks anazungumzia? Ni tofauti gani inaweza kutokea kwenye maisha yetu kama tukijua kuwa sisi tunaweza kuwa “warithi wa Mungu” na “warithi pamoja na Kristo”? (Warumi 8:17).
“Ni nani atakayetutenganisha na upendo wa Kristo?”
-
Kujadili Warumi 8 kwa pamoja kungeweza kuleta fursa ya kuwasaidia washiriki wa darasa kujionea upendo wa Mwokozi. Fikiria kuonyesha picha ya Yesu Kristo (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia) wakati mnasoma Warumi 8:18, 28, 31–39 kama darasa. Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki umaizi au hisia walizonazo baada ya kusoma mistari hii. Wengine wanaweza tayari kushiriki jinsi walivyojipatia shuhuda juu ya kweli wanazoziona katika mistari hii.
Amri zote za Mungu hutimizwa katika amri ya kupenda.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuona ni kwa jinsi gani amri zote kwa “kifupi zimejumuishwa katika” amri ya kumpenda jirani yako (Warumi 13:9), waalike kutengeneza orodha kwenye ubao ya amri zote ambazo wanaweza kufikiria. Someni kwa pamoja Warumi 13:8–10 na Mathayo 22:36–40, na jadilini kama darasa uhusiano uliopo kati ya kumpenda Mungu na majirani zetu na kutii kila amri iliyoorodheshwa kwenye ubao. Ni kwa namna gani ukweli huu unabadilisha namna tunavyofikiri kuhusu amri na utiifu? Kwa mfano, ukweli huu unapendekeza nini kuhusu madhumuni ya amri hizi?
“Acha tusizidi … kuhukumiana.”
-
Kutoa muktadha wa Warumi 14, ungeweza kuonyesha kuwa baadhi ya watakatifu wa Rumi walibishana wao kwa wao kuhusu desturi za kitamaduni, kama tabia za wakati wa kula, na maadhimisho ya sikukuu. Ni hali gani kama hiyo ambayo tunakabiliana nayo kwa leo? Labda washiriki wa darasa wangeweza kuchunguza Warumi 14 na kutoa ufupisho kwa sentensi moja kuhusu ushauri wa Paulo. Ni ushauri gani tunaweza kushiriki na wengine kuhusu namna ya kuepuka kuwa wenye kuhukumu? Pengine washiriki wa darasa wanaweza kupata mawazo katika ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf “Wenye Rehema Watapata Rehema” Liahona, Mei 2012, 70–77
Nyenzo za Ziada
Kupokea “yote ambayo Baba anayo” (Mafundisho na Maagano 84:38).
-
“Kuwa Kama Mungu” (Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org)
Rais Dallin H. Oaks alisimulia fumbo lifuatalo:
“Baba tajiri alijua kwamba kama angemrithisha utajiri mtoto wake ambaye alikuwa bado hajakuza vya kutosha busara na akili ilivyohitajika, urithi ule pengine ungetumika vibaya. Baba alimwambia mtoto wake:
“Vyote nilivyo navyo ninatamani kukupa—siyo tu utajiri wangu, lakini pia cheo changu na sifa yangu miongoni mwa watu. Kile ambacho ninacho ninaweza kukupa kiurahisi, lakini ule utu wangu lazima uupate wewe mwenyewe. Utastahili urithi wako kwa kujifunza kile nilichojifunza mimi na kwa kuishi kama mimi nilivyoishi. Nitakupa sheria na kanuni ambazo kwazo mimi nimepata busara yangu na akili. Fuata mfano wangu, pata ujuzi kama nilivyopata, na utakuwa kama nilivyo, na vyote nilivyonavyo vitakuwa vyako’” (“Changamoto ya Kuwa,” Ensign, Nov. 2000, 32).