2010–2019
Wenye Rehema Watapata Rehema
Aprili 2012


Mwenye Rehema Hupokea Rehema

Wakati mioyo yetu anapojazwa na upendo wa Mungu, tunakuwa “wakarimu mmoja kwa mwengine, wenye moyo laini, wenye kusamehe.”

Ndugu na dada zangu wapendwa, si kitambo sana tangu nilipokee barua kutoka kwa mama aliyekuwa na tatizo akinisihi nitoe hotuba katika mkutano mkuu juu ya mada ambayo hasa itawanufaisha watoto wake wawili. Mzozo ulitokea kati yao, na walikuwa wameacha kuongeleshana. Huyo mama alikuwa amehuzunika. Katika barua yake alinihakikishia kwamba ujumbe wa mkutano mkuu juu ya mada hii ungeweza kuwapatanisha watoto wake, na mambo yote yangekuwa sawa.

Haya maombi ya uaminifu na kutoka moyoni mwa huyu dada mwema yalikuwa tu mojawapo wa shawishi kadha ambazo niliopokea katika hii miezi iliyopita kwamba nafaa kusema maneno machache leo juu ya mada ambayo ni tatizo linaloendelea kukua---si tu kwa mama mwenye hofu bali kwa wengi katika Kanisa na, hasa, duniani.

Nimependezwa na imani ya huyu mama mwenye upendo kwamba hotuba ya mkutano mkuu inaweza kusaidia kuponya uhusiano kati ya watoto wake. Nina hakika kwamba imani yake haikuwa sana kwenye uwezo wa wanenaji bali katika “wema wa neno la Mungu” ambalo lina “matokeo ya nguvu zaidi kwa akili za watu kuliko .... kitu chochote kingine.”1 Dada mpendwa, naomba kwamba Roho aiguse mioyo ya watoto wako.

Wakati Uhusiano Unakuwa Mbaya

Uhusiano mbaya na uliyovunjika ni kitu cha zamani kama vile wanadamu wenyewe. Kaini wa kale alikuwa wa kwanza aliyekubali saratani ya uchungu na kijicho kuharibu moyo wake. Alipalilia uwanda wa nafsi yake kwa wivu na chuki na kukubali hisia hizi kuiva hata akafanya yasiyoweza kufikirika---kumuua ndugu yake mwenyewe na kuwa, katika njia hiyo baba wa uongo wa Shetani.2

Tangu siku hizo za kwanza roho ya wivu na chuki imepelekea hadithi za huzuni mkubwa katika historia. Ilimgonganisha Saul dhidi ya Daudi, wana wa Yakobo dhidi ya kaka yao Yusufu, Lamani na Lemueli dhidi ya Nefi, na Amalikia dhidi ya Moroni.

Fikiria kwamba kila mtu katika ulimwengu ameathiriwa katika njia fulani na roho angamizi ya ubishi, chuki, na kisasi. Labda kuna nyakati pia tunapotambua hii roho wenyewe. Tunapohisi kuumizwa, hasira au wivu, ni rahisi sana kuhukumu wengine, kila mara kuwa na sababu chafu za matendo yetu ili kuhalalisha hisia zetu za chuki wenyewe.

Mafundisho

Ndio, tunajua hili ni kosa. Mafundisho ni wazi. Sote tunategemea Mwokozi; hakuna kati yetu anayeweza kuokolewa pasipo Yeye. Upatanisho wa Kristo hauna mwisho na ni wa milele. Msamaha wa dhambi zetu huja na masharti. Sharti tutubu, na sharti tuwe tayari kuwasamehe wengine. Yesu alifunza: ”Mnapaswa kusameheana ninyi kwa ninyi; kwani yule asiyemsamehe ... [husimama] na hatia mbele za Bwana; kwa kuwa ndani yake imebaki dhambi kubwa.” 3 na “Heri wenye rehema; maana hao watapata rehema.” 4

Ndio, haya maneno yanaonekana kuwa na maana kamilifu---yanapotumiwa kwa mtu mwingine. Tunaweza kuona wazi na kwa urahisi matokeo ambayo huja wakati tunapowahukumu wengine na kuwa na kinyongo. Na kwa kweli hatupendi wakati tunahukumiwa na wengine.

Lakini inapokuja kwa madai na malalamiko yetu, mara nyingi sana tunahalalisha ghadhabu yetu kama haki na hukumu yetu kama kutegemewa na inayofaa. Ingawa hatuwezi kuona moyo wa mtu mwengine, tunadhani tunajua nia mbaya au hata mtu mbaya tunapoona mtu. Tunafanya ubaguzi inapofikia uchungu wetu wenyewe kwa sababu tunahisi, ni katika hali yetu, tuna taarifa zote tunazohitaji tunapombeza mtu mwengine.

Mtume Paulo, katika barua yake kwa Warumi, alisema kwamba wale wanaowahukumu wengine “hawana msamaha.” Tunapomhukumu mtu mwingine, alielzea, tunajihukumu wenyewe, kwani hamna asiye na dhambi.5 Kukataa kusamehe ni dhambi kuu---ambayo Mwokozi alionya dhidi yake. Wafuasi wa Yesu Mwenyewe “walitafuta makosa kati yao na wala hawakusameheana katika mioyo yao; na kwa uovu huu walipata mateso na kuadhibiwa vikali.” 6

Mwokozi wetu amenena kwa uwazi sana juu ya hili swala kwamba kuna nafasi ndogo sana ya ufafanuzi wa kibinafsi. “Mimi, Bwana, nitamsamehe yule nitakaye kumsamehe,” basi kisha Yeye alisema,“ ….ninyi mnatakiwakuwasamehe watuwote.” 7

Naweza kuongeza tanbihi hapa? Bwana anapohitaji kwamba sisi tuwasamehe watu wote, hiyo inajumuisha kujisamehe wenyewe. Wakati mwingine, kati ya watu wote duniani, yule ambaye aliye mgumu kusamehe---pamoja na labda yule aliye na haja ya msamaha wetu---ni huyu mtu anayetutazama sisi kwenye kioo.

Jambo Muhimu

Hii mada ya kuhukumu wengine hasa inaweza kufunzwa kwa mahubiri ya maneno mawili. Inapofikia kuchukia, udaku, dharau, dhihaka, kuwa na kinyongo, au kutaka kuleta madhara, tafadhali tumia yafuatayo:

Sitisha!

Ni rahisi hivyo. Tunafaa kuacha kuhukumu wengine na kubadilisha mawazo ya hukumu na hisia za moyo uliojaa upendo wa Mungu na watoto Wake. Mungu ni Baba yetu. Sisi ni watoto Wake. Sisi sote ni ndugu na dada. Sijui hasa jinsi ninaweza kuelezea vyema hili jambo la kutowahukumu wengine kwa ufasaha wa lugha vya kutosha, hamu, na ushawishi wa kulifanya lishike. Naweza kudondoa maandiko, naweza kujaribu kufafanua mafundisho, na hata kudondoa kibandiko cha gari nilichokiona majuzi. Kilikuwa kimeandikwa nyuma ya gari ambalo dreva wake alionekana kama mjeuri kidogo, lakini maneno katika kibandiko yanafunza somo la kumakinisha. Kilisoma hivi, “Usinihukumu mimi kwa sababu ninatenda dhambi tofauti na wewe.”

Ni sharti tutambue kwamba sisi sote si wakamilifu---kwamba sisi ni waombaji mbele za Mungu. Si sisi sote, wakati mmoja au mwingine, tushaendea mbele ya kiti ya rehema na kuomba neema? Si sisi tushatamani kwa nguvu zetu zote za nafsi zetu rehema---tupatiwe kwa sababu ya makosa ambayo tumefanya na dhambi tulizotenda?

Kwa sababu sote tunategemea rehema za Mungu, tunawezaje kuwanyima wengine kipimo chochote cha neema tunachotamani kwa hamu sana kwetu wenyewe? Ndugu na dada wapendwa, si tunafaa kusamehe jinsi tunavyotamani kusamehewa?

Upendo wa Mungu

Je! Hivi ni vigumu kutenda?

Ndio, kweli.

Kujisamehe wenyewe na wengine si rahisi. Hasa, kwa wengi wetu inahitaji mabadiliko makuu katika mtazamo wetu na kwa njia ya kufikiria---hata mabadiliko ya moyo. Lakini kuna habari njema. Haya “mabadiliko makuu”8 ya moyo ndio hasa kile injili ya Yesu Kristo imetengenezwa kuzalisha katika maisha yetu.

Inafanyika vipi? Kupitia upendo wa Mungu.

Mioyo yetu inajazwa na upendo wa Mungu, kitu chema na halisi utendeka kwetu. Sisi “tunaziweka amri zake: na amri zake si kali. Kwani yeyote anayezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu.”9

Vile tunvyokubali upendo wa Mungu kutawala akili zetu na mihemko yetu---ndivyo tunavyokubali upendo wetu kwa Baba yetu wa Mbinguni kuvimba ndani ya mioyo yetu---inakuwa rahisi kuwapenda wengine kwa upendo halisi wa Kristo. Tunapofungua mioyo yetu kwa macheo ya joto ya upendo wa Mungu, giza na baridi ya uhasama na kijicho hatimaye hufifia.

Kama ilivyo kawaida, Kristo ni mfano wetu. Katika mafundisho Yake kama ilivyo katika maisha Yake, Yeye alituonyesha njia. Yeye aliwasamehe waovu, wenye lugha chafu, na wale waliotafuta kumuumiza na wanamuumiza.

Yesu alisema ni rahisi kwa kuwapenda wale wanaotupenda: hata waovu wanaweza kufanya hivyo. Lakini Yesu alifunza sheria kuu. Maneno Yake yanapiga mwangwi katika karne nyingi na yanakusudiwa sisi leo. Yanakusudiwa kwa wote ambao wanatamani kuwa wafuasi Wake. Yanakusudiwa wewe na mimi: “Wapendeni adui zenu, wabariki wale wa wanaowalaani ninyi, watendeeni mema wale wanaochukia, waombeeni wanaowaudhi, na kuwatesa.” 10

Mioyo yetu inapojazwa na upendo wa Mungu, tunakuwa “wakarimu ninyi kwa ninyi, wenye mioyo mikijufu, tukisameheana [kila mmoja], hata kama vile Mungu kwa ajili ya Kristo [alitusamehe].”11

Upendo halisi wa Kristo unaweza kuondoa magamba ya chuki na ghadhabu kutoka kwa macho yenu, kutuwezesha sisi kuona wengine kwa njia Baba yetu wa Mbinguni anavyotuona: kama watu wenye dosari na wasio kamili walio na uwezo na ustahiki wa juu sana kuliko uwezo wetu wa kufikiria. Kwa sababu Mungu anatupenda sana, sisi pia sharti tumpende na kusamehana.

Njia ya Ufuasi

Ndugu na dada wapendwa, fikirieni juu ya maswali kama jaribio la kibinafsi:

Je! Una kinyongo dhidi ya mtu yeyote?

Je! Unasengenyana, hata kama unachosema ni kweli?

Je! Unawabagua, kuwatenga au kuwaadhibu wengine kwa sababu ya kitu walifanya?

Je! Unaonea mtu kijicho kisiri?

Je! Una nia ya kumuumiza mtu yeyote?

Kama umejibu ndio kwa lolote kati ya maswali haya, unaweza kutaka kutumia mahubiri ya neno moja la mapema: Sitisha!

Katika ulimwengu wa tuhuma na uadui, ni rahisi kukusanya na kutupa mawe. Lakini kabla hujafanya hivyo, wacha tukumbuke maneno ya Mmoja ambaye ni Bwana wetu na mfano wetu: “Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.”12

Ndugu na dada, na tuweke mawe yetu chini.

Na tuwe wakarimu.

Na tusamehe.

Na tuongee amani na mmoja na mwingine.

Na upendo wa Mungu ujaze mioyo yetu.

“Na tufanye mema kwa watu wote.” 13

Mwokozi aliahidi: “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika … Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.”14

Je! Si hii taarifa inafaa kututia motisha ya kutosha kuwa kila mara tunalenga juhudi zetu kwenye matendo ya ukarimu, msamaha, na hisani badala ya tabia zozote mbaya?

Na, sisi kama wafuasi wa Yesu Kristo, turudishe mema kwa ubaya.15 Na tusitafute kulipiza au tusikubali ghadhabu kutushinda.

“Maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.

“Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe. …

“Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.” 16

Kumbukeni: hatimaye, Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. 17

Kama washiriki wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, popote tulipo, na tujulikane kama watu ambao “walio na upendo ninyi kwa ninyi.”18

Pendaneni Mmoja kwa Mwengine

Ndugu na dada, kuna usumbufu na huzuni wa kutosha katika maisha haya bila ya sisi kuongezea kupitia ukaidi wetu wenyewe usio na mwelekeo, uchungu, na chuki.

Sisi si kamili.

Watu wa karibu nasi si kamili.19 Watu hufanya mambo ya kuchukiza, ya kuhudhi, na kukasirisha. Katika maisha haya ya muda daima itakuwa hivyo.

Hata hivyo, ni sharti tuaachane na lawama zetu. Sehemu ya madhumuni ya maisha ya muda ni kujifunza jinsi ya kuachilia mambo kama hayo. Hiyo ndio njia ya Bwana.

Kumbukeni, mbinguni kumejaa wale ambao walio nayo kama kawaida: Watasamehewa. Na wanasamehe.

Wekeni mizigo yenu mbele za Mwokozi. Achaneni na kuhukumu. Acheni Upatanisho wa Kristo ubadilishe na kuponya moyo wenu. Pendaneni ninyi kwa ninyi. Samehaneni ninyi kwa ninyi.

Wenye rehema watapata rehema.

Kwa haya nashuhudia katika jina la Mmoja ambaye alikuwa na upendo sana na kikamlifu kwamba Yeye akautoa uzima Wake kwa ajili yetu---marafiki Zake, katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.