Shukrani Ziwe kwa Mungu.
Ingekuwa bora jinsi gani kama sote tungetambua uwezo mtakatifu na upendo wa Mungu na kutoa shukrani Kwake.
Ndugu na kina dada wapendwa, asanteni kwa uhimili wenu wa kudumu na uaminifu wenu. Tunatoa shukrani zetu na upendo wetu kwa kila mmoja wenu.
Majuzi, Dada Nelson nami tulifurahia urembo wa samaki wa tropiki katika tangisamaki dogo la kibinafsi. Samaki wa rangi kali na maumbo na ukubwa tofauti tofauti warukaruka huku na kule. Nilimuuliza mhudumu aliyekuwa karibu, “Ni nani anayewapa chakula samaki hawa warembo?”
Alijibu, “Mimi”
Kisha nikauliza, “Je! Wamesha kushukuru?”
Akajibu, “Bado!”
Nikafikiria juu ya watu fulani ninaowajua ambao hawana habari kuhusu Muumba wao na “mkate wa maisha” yao halisi.” 1 Wanaishi siku baada ya siku bila kutambua Mungu na wema Wake kwao.
Ingekuwa bora jinsi gani kama sote tungetambua uwezo mtakatifu na upendo wa Mungu na kutoa shukrani Kwake. Amoni alifunza, “Wacha tulishukuru [Mungu] jina lake takatifu, kwani yeye hufanya kazi ya haki milele.” 2 Kiwango chetu cha shukrani ni kipimo cha upendo wetu Kwake.
Mungu ni Baba wa roho zetu. 3 Ana mwili mkamilifu wa nyama na mfupa uliotukuzwa. .4 Tuliishi na Yeye mbinguni kabla ya kuzaliwa. 5 Na wakati alituumba kimwili, tuliumbwa kwa mfano wa Mungu, kila mmoja akiwa na mwili binafsi.6
Fikiria juu ya chakula cha kimwili. Kwa kweli vyatoka mbinguni. Haja ya hewa, chakula, na maji vyote vinakuja kama zawadi kutoka kwa Baba wa Mbinguni wenye upendo. Ulimwengu uliumbwa kwa ajili ya makaazi yetu mafupi ya maisha ya muda. 7 Tulizaliwa na uwezo wa kukua, kupenda, kuoa, na kujenga familia.
Ndoa na familia zimetawazwa na Mungu. Familia ndio kitengo muhimu sana cha kijamii katika wakati na katika milele. Chini ya mpango mkuu wa Mungu, familia zinaweza kufunganishwa katika mahekalu na kutayarishwa kurudi kuishi katika uwepo Wake mtakatifu milele. Huo ndio uzima wa milele! Inatimiza hamu kuu ya nafsi ya mwanadamu---tamaa ya asili kwa uhusiano usio na mwisho na wanafamilia wapendwa katika familia ya mtu.
Sisi tu sehemu ya madhumuni Yake matakatifu: “Kazi yangu na utukufu wangu,” Yeye alisema, ni “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu.” 8 Ili kupata malengo hayo, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” 9 Hicho kitendo kilikuwa udhirihisho mtakatifu wa upendo wa Mungu. “Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”10
Kitovu cha mpango wa milele wa Mungu ni huduma ya Mwanawe, Yesu Kristo. 11 Yeye alikuja kukomboa watoto Wake. .12 Kwa sababu ya Upatanisho wa Bwana, ufufuo (au kutokufa) kukawa halisi. 13 Kwa sababu ya Upatanisho uzima wa milele ukawa unawezakupatika kwa wote ambao watahitimu. Yesu alielezea hivi:
“Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
“Naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.”14
Kwa Upatanisho wa Bwana na kipawa Chake cha ufufuo---kwa huu ujumbe mtukufu wa Pasaka---shukrani ziwe kwa Mungu!
Vipawa vya Kimwili
Baba yetu wa Mbinguni anawapenda watoto Wake. 15 Amewabariki kila mmoja na vipawa vya kimwili na kiroho. Acha niongee juu ya kila kimoja. Unapoimba “Mimi ni Mtoto wa Mungu,” fikiria juu ya kipawa Chake kwako cha mwili wako mwenyewe. Hizi sifa nyingi za ajabu za mwili hushuhudia utukufu wako mwenyewe wa asili.” 16
Kila sehemu ya mwili wako ni kipawa cha ajabu kutoka kwa Mungu. Kila jicho lina lensi inayolenga kiautomatiki. Mshipa na misuli uthibiti macho mawili kutengeneza picha moja ya kadiri tatu. Macho yameunganishwa na ubongo, ambao unarekodi madhari yanayoonekana.
Moyo wako ni pampu ya ajabu. 17 Ina vali nne laini ambazo zinathibiti mwelekeo wa mbubujiko wa damu. Hizi vali hufunga na kufungua zaidi ya mara 100,000 kila siku---mara milioni 36 kila mwaka. Hali, zisiposumbuliwa na ugonjwa, zinaweza kuvumilia shinikizo kama hilo pasipokukoma.
Fikiria juu ya kinga ya mwili. Ili kujikinga kutokana na madhara, husikia uchungu. Kijikinga maambukizi, hutengeneza kingamwili. Ngozi hutoa kinga. Hukutahadharisha dhidi kujeruhiwa ambako kunaweza kutoka na moto mwingi au bariki kali.
Mwili utengeneza upya seli zilizozeeka na kuthibiti kiwango cha viungo vyake muhimu. Mwili huponya kukatwa, kuchubuliwa, na mifipa iliyovunjika. Uwezo wa kuzaa ni kipawa kingine kitakatifu kutoka kwa Mungu.
Acha tukumbushe mwili kamili sio mahitaji ya mtu kupata kudura yake takatifu. Kwa kweli kati ya zile roho nzuri sana ziko ndani ya miili iliyodhoofika au miili isiyokamili. Uwezo mkuu wa kiroho mara nyingi hukuzwa na watu walio na changamoto za kimwili, kweli kwa sababu wana changamoto sana.
Mtu yeyote anayejifunza ufanyaji kazi wa mwili wa wanadamu kwa kweli “ameona Mungu akitembea katika ukuu wake na uwezo.” 18 Kwa sababu mwili unatawaliwa na sheria takatifu, uponyaji huja kwa utii wa sheria ambapo juu yake baraka hiyo hutoka. 19
Hali watu wengine kimakosa wanafikiria kwamba hizi sifa za ajabu zilitokea kwa bahati au matokeo ya “big bang” mahali fulani. Jiulize, “Kweli mlipuko katika duka ya uwanda wa kupiga chapa unaweza kutoa kamusi?” Uwezekano huu uko mbali sana.” Lakini kama ni kweli, hauwezi kuponya kurasa zilizoraruka au kutoa matoleo yake mapya!
Kama uwezo wa mwili kwa utendaji wa kawaida, kinga, urekebishaji, uthibiti, na ufanyaji upya ungeendelea bila kikomo, maisha yangeendelea katika udumishaji. Naam! Tungekwama hapa ulimwenguni! Kwa kuturehemu sisi, Muumba aliweka mfanyiko wa kuzeeka na ile mifanyiko ingine ambayo hatimaye italeta kifo chetu cha mwili. Kifo, kama vile kuzaliwa, ni sehemu ya maisha. Maandiko yanafundisha kwamba “Haikuwa ya kufaa kwamba mwanadamu arudishwe kutoka kwa kifo chake cha mwili, kwani hiyo ingeangamiza mpango mkuu wa furaha.” 20 Ili kurudi kwa Mungu kupitia lango tunaloita kifo ni shangwe kwa wale wanaompenda Yeye na wamejitayarisha kukutana na Yeye. 21 Hatimaye wakati utafika ambapo kila “Roho na …mwili vitaungwa tena katika hali yake ya ukamilifu; viungo vyote vitarudishwa katika sehemu zao kamili.” 22 kamwe havitategenishwa tena. Kwa hivi vipawa, shukrani ziwe kwa Mungu!
Vipawa vya Kiroho
Muhimu kama ulivyo mwili, hutumika kama tabenakulo la roho ya milele ya mtu. Roho zetu ziliishi katika maisha kabla ya hapa duniani23 na zitaendelea kuishi baada ya mwili kufa. 24 Roho hupatia mwili uhuisho na nafsi. 25 Katika maisha haya na katika yafuatayo, roho na mwili, vitakapounganishwa pamoja, na kuwa nafsi hai ya thamani ya kiungu.
Kwa sababu roho ya mtu ni muhimu sana, ukuaji wake una athira ya milele. Inaimarishwa tunapowasiliana kwa maombi ya unyenyekevu na Baba yetu wa Mbinguni mweye upendo. 26
Sifa ambazo kwazo tutahukumiwa siku moja zote ni za kiroho. 27 Hizo zinajumuisha upendo, wema, uaminifu, huruma, na huduma kwa wengine. 28 Roho yako, ikiunganishwa na kuwekwa ndani ya mwili wako, inaweza kukua na kujionyesha katika hizi sifa katika njia ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa wako wa milele. 29 Ukuaji wa kiroho hupatikana kupitia hatua za imani, toba, ubatizo, kipawa cha Roho Mtakatifu, na kuvumilia hadi mwisho, ikijumuisha maagizo ya endaumenti na kufunganishwa ya hekalu takatifu. 30
Kama vile mwili unavyohitaji chakula kila siku ili kudumu, roho inahitaji lishe pia. Roho hulishwa kwa kweli za milele. Mwaka uliopita tulisherekea adhimisho la miaka 400 ya tafsiri ya Biblia Takatifu ya King James. Na sisi tumekuwa na Kitabu cha Mormoni kwa karibu miaka 200. Kimetafsiriwa chote au kama sehemu katika lugha 107. Kwa sababu ya haya maandiko na mengine yenye thamani, tunajua kwamba Mungu ni Baba yetu wa Milele na kwamba Mwanawe, Yesu Kristo, ni Mwokozi wetu na Mkombozi wetu. Kwa hivi vipawa vya kiroho, shukrani na ziwe kwa Mungu!
Vipawa vya Injili
Tunajua kwamba manabii wa vipindi vingi, kama vile Adamu, Nuhu, Musa, na Ibrahimu, wote walifunza uungu wa Baba yetu wa Mbinguni na Yesu Kristo. Kipindi chetu cha sasa kilitambulishwa na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, walipomtokea Nabii Joseph Smith mnamo 1820. Kanisa liliasisiwa mnamo 1830. Sasa, miaka 182 baadaye, tunabaki chini ya agano la kupeleka injili “kila taifa, ukoo, ndimi na watu,” 31 Tanapofanya hivyo, wote wanatoa na wapokeaji watabariwa.
Letu ni jukumu la kufunza watoto Wake na kuwaamsha katika utambuzi wa Mungu. Miaka mingi iliyopita Mfalme Benyamini alisema:
“Mwamini Mungu; amini kwamba yupo, na kwamba aliumba vitu vyote, katika mbingu na katika ardhi, amini kwamba ana hekima yote, na uwezo wote, mbinguni na ardhini; …
“… Mwamini kwamba lazima mtubu dhambi zenu na kuziacha, na kujinyenyekeza mbele ya Mungu; na muombe kutoka moyo wa kweli ili awasamehe; na sasa, kama mnaamini hivi vitu vyote hakikisheni kwamba mnavitenda.32
Mungu ni yule yule jana, leo, na milele, lakini hatuko hivyo. Kila siku, yetu ni changamoto ya kupata uwezo wa Upatanisho, ili kwamba tubadilike kikweli, kuwa zaidi kama Kristo, na kuhitimu kipawa cha kuinuliwa na kuishi milele na Mungu, Yesu Kristo na familia zetu. 33 Kwa huu uwezo, nafasi, na vipawa vya injili, shukrani na ziwe kwa Mungu!
Nashuhudia kwamba Yeye yu hai, kwamba Yesu ndiye Kristo, na kwamba hili ni Kanisa Lake, lililorejeshwa katika hizi siku za mwisho ili kutimiza kudura yake takatifu. Tunaongozwa na Rais Thomas S. Monson, ambaye tunampenda na kumkubali kwa mioyo yetu, pia tunawakubali washauri wake na Mitume Kumi na Wawili, kama manabii, waonaji, na wafunuaji. Nashuhudia hivyo katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.