Ono la Manabii kuhusu Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama: Imani, Familia, Usaidizi
Imani, familia, na usaidizi---haya maneno rahisi yamekuja kuonyesha ono la manabii kwa kina dada katika Kanisa.
Katika miaka ya majuzi nimepata msukumo kila mara niongee kuhusu Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama---madhumuni yake na sifa zake,1 thamani ya a historia yake,2 kazi zake, na ushirika wake na maaskofu na jamii za Ukuhani wa Melkizediki.3 Inaonekana muhimu sasa kulenga nathari katika ono la manabii kuhusu Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama.4
Kama vile manabii wa Bwana wameendelea kuwafunza wazee na makuhani wakuu wajibu na kazi zao, wameshiriki ono lao kwa kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Kutoka kwa ushauri wao, ni wazi kwamba madhumuni ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ni kuongeza imani na wema wa kibinafsi, kuimarisha familia na nyumba, kuwatafuta na kuwasaidia wenye mahitaji. Imani, familia, na usaidizi —haya maneno matatu yamekuja kuonyesha ono la manabii kwa kina dada wa Kanisa.
Tangu siku za mwanzoni za urejesho, manabii wameshiriki ono lao la wanawake imara, waaminifu, wenye majukumu, ambao wanaofahamu thamani na madhumuni ya milele. Wakati Joseph Smith alipoanzisha Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alielekeza urais wake wa kwanza “kusimamia hiki kikundi, katika kutunza maskini---kuhudumia mahitaji yao, na kushughulikia mambo mengi ya shirika hili.”5Aliona hili shirika kama “kikundi teule, kilichotengwa kutokana na uovu wa dunia.” 6
Brigham Young, Rais wa pili wa Kanisa, aliwaelekeza washauri wake na Jamii ya Mitume Kumi na Wawili kuwaelekeza maaskofu “kuwaacha [kina dada] kutengeneza Vikundi vya Usaidizi vya Kike katika kata tofauti.” Aliongezea, “Wanaweza kusema hiki ni kitu cha mzaa, lakini sivyo.” 7
Baadaye, Rais Joseph F. Smith alisema kwamba katika kulinganisha na vikundi vya duniani, ambavyo “vimeundwa na waaume, au vimeundwa na wanawake,” Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama “ kimeundwa kiungu, kimeidhinishwa kiungu, kimeasisiwa kiungu, kimetawazwa kiungu na Mungu. 8 Rais Joseph Fielding Smith aliwaambia kina dada kwamba “walikuwa wamepatiwa uwezo na mamlaka kufanya mambo mengi makuu.”9 Alisema, “Ninyi ni washiriki wa shirika kuu la wanawake katika dunia, shirika ambalo ni sehemu muhimu ya ufalme wa Mungu ulimwenguni na ambalo limeundwa na kuendeshwa kwamba lisaidie washiriki wake waaminifu kupata uzima wa milele katika ufalme wa Baba yetu.”10
Eneo Pana la Mamlaka
Kila mwaka, mamia ya maelfu wa kina dada wapya huwa sehemu ya hili kundi linalopanuka daima la kina dada.” 11 Baadaye, popote dada anapoishi na popote anapohudumu, anakuwa na ushiriki na uhusiano na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama.12 Kwa sababu ya umuhimu wa madhumuni ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama,, Urais wa Kwanza wameonyesha hamu yao kwamba wasichana huanza matayarisho yao kwa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kabla ya hawajafika miaka 18 .13
Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama sio mradi. Ni sehemu rasmi ya Kanisa la Bwana ambayo “imetawazwa kiuungu na Mungu” kufunza, kuimarisha, na kuhamasisha kina dada katika madhumuni yao juu ya imani, familia, na usaidizi. Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ni njia ya maisha ya wanawake Watakatifu wa Siku za Mwisho, na ushawishi wake daima umeenea zaidi ya madarasa ya Jumapili au kusanyiko la kijamii. Hufuatia mpangilio wa wanawake wafuasi ambao wanahudumu pamoja na Bwana Yesu Kristo na Mitume Wake katika Kanisa Lake la kale.14 Tumefunzwa kwamba “ni wajibu wa mwanamke kuleta katika maisha yake maadili ambayo yanayoendelezwa na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kama ilivyo wajibu wa wanaume kujenga katika maisha yao mpangilio wa silka za kuendeleza ukuhani.”15
Wakati Nabii Joseph Smith alipoanzisha Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alifunza kina dada kwamba “watapatia maskini afueni” na “kuokoa nafsi.”16 Katika jukumu lao la “kuokoa nafsi” kina dada wana mamlaka ya kuanzisha na kushiriki katika eneo pana la mamlaka. Rais wa kwanza wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama alitengwa ili kufafanua maandiko, na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama bado una majukumu haya muhimu ya kufundisha katika Kanisa la Bwana. Wakati Joseph Smith alipowaambia kina dada kwamba kundi la Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama litawatayarisha wao kwa “nafasi, baraka na vipawa vya ukuhani,”17 kazi ya Bwana ya wokovu ilifunguliwa kwao. Kuokoa nafsi kunajumuisha kushiriki injili na kushiriki katika kazi ya umisionari. Ikijumuisha kujishughulisha na kazi ya hekalu na historia ya familia. Ikijumuisha kufanya kila kitu kinachowezekana kuwa wa kujitegemea kiroho na kimwili.
Mzee John A. Widtsoe alitamka kwamba Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama unatoa afueni kwa umaskini, afueni kwa magonjwa; afueni ya shaka, afueni ya ujinga---afueni ya yale yote yanayozuia shangwe na maendeleo ya wanamke. Ni agizo kuu namna gani!”18
Rais Boyd K. Packer alifananisha Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama na “ukuta wa ulinzi.”19 Majukumu ya kuwalinda kina dada na familia zao huongezea umuhimu wa utunzaji na uhudumiaji wa ualimu tembelezi, na ni onyesho la upendeleo wetu wa kukumbuka maagano yetu na Bwana, Kama “wahudumu wa wenye mahitaji na walioathiriwa,” tunafanya kazi kwa uwiano na maaskofu kutunza mahitaji ya kimwili na kiroho ya Watakatifu.20
Rais Spencer W. Kimball alisema: “Kuna kina dada wengi ambao wanaishi na matambara---matambara ya kiroho. Wana haki ya majoho mazuri sana, majoho ya kiroho. … Ni nafasi yenu kwenda katika nyumba na kubadilisha majoho kwa matambara.”21 Rais Harold B. Lee alishiriki hili ono. Alisema: “Hamwezi kuona kwa nini Bwana ameweka juu ya … Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kutembelea hizi nyumba? Kwa sababu, karibu na Bwana mwenyewe, hamna yeyote katika Kanisa ambaye ana ushawishi mzuri sana, uelewa kamili sana wa mioyo na maisha ya hawa watu.”22
Rais Joseph F. Smith aliwaonya kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama na viongozi wao, akisema kwamba hangetaka “kuona wakati ambapo Miungano ya Usaidizi wa Kina Mama ikifuata, au ikichanganika na makundi ambayo yameundwa na wanawake.” Aliwatarajia kina dada “kuongoza ulimwengu na … hasa wanawake wa ulimwengu, katika kila kitu kinachostahili sifa njema, kila kitu ambacho kinalingana na Mungu, kila kitu ambacho kinainua na kile kinachotakasa kwa watoto wa watu.”23 Ushauri wake unasisitiza haja ya kuondoa kutoka kwa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama desturi zozote, mada, tabia ambazo haziambatani na madhumuni ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama.
Viongozi ambao Wanatafuta ufunuo na kuhakikisha kila mkutano, somo, darasa, shughuli, juhudi za Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama utimiza madhumuni kwa kile ulitengezewa. Ujamii, urafiki, na umoja tunaotamani si madhumuni ya ushirika; bali, ni matokeo mazuri ya kuhudumu pamoja na Bwana katika kazi Yake.
Kutimiza Ono la Manabii
Rais Thomas S. Monson na washauri wake majuzi walishuhudia “kwamba Bwana amerejesha utimilivu wa injili kupitia Nabii Joseph Smith na kwamba Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ni sehemu muhimu ya huo urejesho.” Kama ushuhuda wa hamu yao kwamba “urithi mtukufu” wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama unaweza kuhifadhiwa, Urais wa Kwanza majuzi ulichapisha na kusambaza ulimwenguni kote Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society. Katika kurasa za kitabu hiki, tunaweza kuona mpangilio na mifano ya kina dada na ndugu wakifanya kazi pamoja kwa ushirika katika familia na Kanisa, na tunaweza kujifunza kanuni juu ya sisi ni kina nani, kile tunachoamini, na kile tunafaa kulinda. Tumetiwa moyo na Urais wa Kwanza kujifunza hiki kitabu muhimu na “kukubali kweli zake za milele na mifano ya mema ya kushawishi maisha [yetu] .”24
Kina dada wanapokuwa na uwiano na madhumuni ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, maono ya manabii yatatimizwa. Rais Kimball alisema, “Kuna uwezo katika hili kundi la [Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama] ambao bado haujatumizwa kikamilifu katika kuimarisha nyumba za Sayuni na kujenga Ufalme wa Mungu---wala hautafanyika mpaka wote kina dada na ukuhani watakaposhika ono la Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama.”25 Yeye alitoa unabii kwamba “wingi wa ukuaji mkuu ambao unakuja katika Kanisa katika siku za mwisho utakuja kwa sababu wingi wa wanawake wema wa duniani (ambao kwao kuna hisia ya kiroho) watavutwa Kanisani kwa idadi kubwa. Hii itatokea kwa kiwango ambacho wanawake wa Kanisa … wanaonekana wazi na tofauti---katika njia za furaha---kutoka kwa wanawake wa ulimwengu.”26
Nina shukrani kwa ono la manabii kuhusu Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Mimi, kama vile Rais Gordon B. Hinckley, “nimeshawishika kuwa hapana kundi lolote linaloweza kulinganishwa na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wa Kanisa hili.”27 Ni jukumu letu sasa kujiwianisha na ono la manabii kuhusu Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama tunapotafuta kuongeza imani, tunapoimarisha families, na kutoa usaidizi.
Nafunga kwa maneno ya Rais Lorenzo Snow: “Kudura ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama umejawa na ahadi. Kanisa linapokua, uwanda wake wa ufanisi utalingana na upanukaji wake, na litakuwa na nguvu sana kwa wema kuliko vile ilivyokuwa hapo mapema.”28 Kwa kina dada ambao husaidia kuendeleza ufalme wa Mungu, alisema, “Mnaposhiriki kazi hizi, vivyo hivyo mtashiriki katika ushindi wa kazi na katika kuinuliwa na utukufu ambao Bwana atawapatia watoto Wake waaminifu.”29 Kwa hili ono mimi pia nashuhudia katika jina la Yesu Kristo, amina.