2010–2019
Mlima ya kupanda
Aprili 2012


Milima ya Kukwea

Kama tuna imani katika Yesu Kristo, nyakati ngumu vile vile nyakati rahisi katika maisha zinaweza kuwa baraka.

Nilimsikia Rais Spencer W. Kimball katika kikao cha mkutano mkuu akiuliza kwamba Mungu ampatie milima ya kukwea. Alisema: Kuna changamoto kubwa mbele yetu, nafasi kuu za kutimizwa. Nakaribisha hayo matazamio ya kusisimua na kuhisi kusema kwa Bwana kwa unyenyekevu, Nipe mlima huu,’ nipe changamoto hizi.”1

Moyo wangu ulikorogwa, kujua, kama nilivyojua, baadhi ya changamoto na dhiki alizokuwa amepata hapo mapema. Nilihisi hamu ya kuwa kama yeye, mtumishi shupavu wa Mungu. Basi usiku mmoja niliomba jaribio la kutathimini ujasiri wangu. Nakumbuka wazi kabisa. Jioni nilipiga magoti katika chumba changu cha kulala kwa imani ambayo ilionekana karibu kujaza moyo wangu hata upasuke.

Karibu siku au siku mbili maombi yangu yalijibiwa. Jaribio gumu sana maishani mwangu lilinishangaza na kuninyenyekeza. Lilinipatia somo la pembe mbili. Kwanza, nilikuwa na thibitisho kwamba Mungu alisikia na kujibu ombi langu. Na pili, nilianza somo ambalo bado linaendelea ili kujifunza kwa nini nilihisi kujiamini kama huko usiku ule baraka kuu ambayo ingetokana na dhiki ili kuwa zaidi ya fidia ya gharama yoyote.

Dhiki iliyonigonga katika siku hiyo ya zamani sasa inaonekana kuwa ndogo kulingana na kile kimenijia tangu wakati huo, kwangu na kwa wale ninaowapenda. Wengi wenu sasa mnapitia majaribu ya kimwili, kiakili, na kimhemko ambayo yanawafanya kulia kama alivyofanya mtumishi mkuu na mwaminifu wa Mungu niliyemjua vyema. Muuguzi wake alimsikia akisema kwa sauti kutoka kwa kitanda chake cha maumivu: “Nimejaribu katika maisha yangu yote kuwa mwema, kwa nini haya yatendeke kwangu?”

Mnajua jinsi Bwana alivyojibu swali hili kwa Nabii Joseph Smith katika chumba cha gereza:

“Na kama utatupwa ndani ya shimo, au katika mikono ya wauaji, na hukumu ya kifo ikapitishwa juu yako; kama utatupwa kilindini; kama mawimbi makali yatakula njama dhidi yako; kama upepo mkali utakuja kuwa adui yako; kama mbingu zitakusanya giza, na vitu vyote vya asili vikiungana ili kuzingira njia yako; na juu ya yote, kama mataya yale ya jahanamu yataachama kinywa wazi kwa ajili yako, fahamu wewe, mwanangu, kwamba mambo haya yote yatakupa wewe uzoefu, na yatakuwa kwa faida yako.

“Mwana wa Mtu amejishusha chini yao wote. Je, wewe u mkuu kuliko yeye?

“Kwa hiyo, shikilia njia yako, na ukuhani utabakia nawe; kwa kuwa mipaka yao imewekwa, hawawezi kuivuka. Siku zako zinafahamika, na miaka yako haitahesabika kuwa michache; kwa hiyo, usiogope mwanadamu awezacho kukutenda, kwani Mungu atakuwa pamoja nawe milele na milele.”2

Hakukuonekana kwangu jibu bora kwa swali la kwa nini majaribu huja na nini tutafanya zaidi ya maneno ya Bwana Mwenyewe, ambaye alipitia majaribu makali kwa sababu yetu kushinda vile tunaweze kufikiria.

Kumbuka maneno Yake aliposhauri kwamba tunafaa, kutokana na imani katika Yeye, tutubu:

“Kwa sababu hii ninakuamuru wewe kutubu—tubu, nisije nikakupiga kwa fimbo ya kinywa changu, na ghadhabu yangu, na kwa hasira yangu, na mateso yako kuwa machungu—machungu namna gani hujui, makali namna gani hujui, ndiyo, namna gani magumu kuyavumilia hujui.

“Kwani tazama, Mimi, Mungu nimeteseka mambo haya kwa ajili ya watu wote, ili kwamba wasiteseke kama watatubu;

“Lakini kama hawatatubu lazima wateseke hata kama Mimi;

“Mateso ambayo yalisababisha Mimi mwenyewe, hata Mungu, mkuu kuliko yote, kutetemeka kwa sababu ya maumivu, na kutoka damu kwenye kila kinyweleo, na kuteseka mwili na roho—na kutamani nisinywe kikombe kichungu, na kusita—

“Hata hivyo, utukufu na uwe kwa Baba, na Mimi nikachukua na kukamilisha maandalizi yangu kwa wanadamu. ‎”3

Wewe na mimi tuna imani kwamba njia ya kuinuka kupitia na kushinda majaribu ni kuamini kwamba kuna “mafuta katika Giliadi” 4 na kwamba Bwana ameahidi, “sitakupungukia … sitakuacha.” 5 Hivi ndio Rais Thomas S. Monson ametufunza sisi na wale tunaohudumu katika kile kinachoonekana kuwa upweke na majaribu makali. 6

Lakini Rais Monson amefunza pia kwa hekima kwamba msingi wa imani kihalisi ya zile ahadi huchukua muda kujengeka. Unaweza kuwa umeona haja ya huu msingi kama vile nimepata kuona kandoni mwa mtu aliye tayari kushindwa na vita ili kuvumilia hadi mwisho. Kama msingi wa imani haujapandwa katika mioyo yetu, uwezo wa kuvumilia utabomoka.

Madhumuni yangu leo ni kuelezea kile ninachojua kuhusu jinsi tunavyoweza kuweka ule msingi usiotikisika. Nafanya hivyo kwa unyenyekevu mkuu kwa sababu mbili. Kwanza, kile nitakachosema kinaweza kuwavunja moyo wengine wenu ambao mnapambana ndani ya dhiki kubwa na kuhisi misingi yao ya imani inabomoka. Na pili, najua kwamba yale majaribu makubwa sana yapo mbele yangu kabla mwisho wa maisha.Kwa hivyo dawa ninayowapa bado haijathibitishwa katika maisha yangu mwenyewe kupitia kuvumilivu hadi mwisho.

Kama kijana nilifanya kazi na kontrakta wa ujenzi wa vitako vya nyumba na msingi kwa nyumba mpya. Katika joto la majira ya joto ilikuwa vigumu kufanya kazi ya kutayarisha uwanda umbo ambalo tungemwagia simiti kwa kitako cha nyumba. Hapakuwa na mashini. Tulitumia sururu na mwiko. Kujenga msingi thabiti kwa majengo ilikuwa ni vigumu siku hizo.

Pia ilihitaji subira. Baada ya kumwaga kitako cha nyumba tulingojea kikauke. Hata kwamba tulitaka kuendeleza kazi mbele, tulingojea pia kumwagia msingi kabla ya kuondoa umbo.

Na kilichokuwa cha kustajabisha kwa mjenzi mgeni kilikuwa ni kile kilichoonekana kuwa kigumu na mfanyiko uliochukua muda mrefu wa kuweka vyuma ndani ya umbo ili kupatia msingi uliomalizika nguvu.

Kwa njia hio hio, uwanda lazima utayarishe vyema kwa msingi wetu wa imani ili ustahimili dhoruba ambazo zitakuja katika kila maisha. Sehemu thabiti muhimu kwa msingi wa imani ni uaminifu wa kibinafsi.

Kuchagua kwetu kwa kile kilicho sahihi kila mara wakati chaguzi zimeweka mbele yetu hujenga uwanda thabiti chini ya imani yetu. Inaweza kuanza utotoni kwa vile kila nafsi huzaliwa na kipawa cha bure cha Roho wa Kristo. Kwa yule Roho tunaweza kujua wakati tumefanya kile kilicho sahihi mbele za Mungu na wakati tumefanya kosa mbele Zake.

Hizo chaguzi, kwa mamia katika siku nyingi, hutayarisha uwanda thabiti ambao majumba yetu ya imani hujengwa. Vyuma ambavyo dutu ya imani yetu humwagwa ni injili ya Yesu Kristo, pamoja na maagano, maagizo, na kanuni zake zote.

Mojawapo ya funguo za imani zinazodumu ni kuhukumu vyema ule wakati wa kukauka unaohitajika. Hii ndio maana nilikuwa mpumbavu kuomba mapema sana katika maisha yangu nipate milima mirefu ya kukwea na majaribu makuu.

Huku kukauka hakutokezi kiotomatiki kupitia mpito wa masaa, bali uchukua muda. Kuzeeka peke yake hakutafaa. Ni katika kumtumikia Mungu na wengine daima kwa moyo na nafsi kujufu ambako ubadilisha ushuhuda kuwa nguvu za kiroho zisizovunjika.

Sasa, ningependa kuwatia moyo wale waliopo katikati ya majaribu makali, ambao wanahisi kuwa imani yao inafifia chini ya mashambulizi ya shida. Shida zenyewe zinaweza kuwa njia yako ya kuimarisha na hatimaye kupata imani isiyotingisika. Moroni, mwana wa Mormoni katika Kitabu cha Mormoni, alituambia jinsi baraka zinaweza kuja . Anafunza kweli rahisi na tamu kwa kutenda hata kwa kijitawi cha imani humpatia Mungu kuikuza:

“Na sasa, mimi, Moroni, nitazungumza machache kuhusu vitu hivi; ninataka kuonyesha ulimwengu kwamba imani ni vitu ambavyo vinatumainiwa na havionekani; kwa hivyo, msishindane kwa sababu hamwoni, kwani hamtapata ushahidi wowote mpaka baada ya majaribu ya imani yenu.

“Kwani ilikuwa kwa imani kwamba Kristo alijionyesha kwa babu zetu, baada ya kuamka kutoka kwa wafu; na hakujionyesha kwao mpaka walipokuwa na imani ndani yake; kwa hivyo, lazima iwe kwamba wengine walikuwa na imani ndani yake, kwani hakujionyesha kwa ulimwengu.

“Lakini kwa sababu ya imani ya watu amejionyesha kwa watu wa ulimwengu, na kulitukuza jina la Baba, na alitayarisha njia ambayo kwake wengine wangeshiriki kwa mwito wa zawadi ya mbinguni, kwamba wangetumainia vitu hivyo ambavyo hawajaviona.

“Kwa hivyo, mnaweza kuwa pia na tumaini, na muwe washiriki wa zawadi, ikiwa mtakuwa tu na imani.” 7

Ile chembe ya imani iliyo na thamani sana na ambayo unafaa kulinda na kuitumia kwa kiwango chochote uwezacho ni imani katika Bwana Yesu Kristo. Moroni alifunza uwezo wa imani hiyo kwa njia hii: “Na wala kwa muda wowote hakujawa na yeyote ambaye amefanya miujiza mpaka awe na imani; kwa hivyo waliamini kwanza katika Mwana wa Mungu.”8

Niliongea na mwanamke ambaye alipokea mwujiza wa nguvu za kutosha ili kuvumilia misiba isiyoweza kufikirika tu kwa uwezo wa kurudia maneno bila kikomo, “Najua kwamba Mkombozi wangu yu hai.” 9 Imani hiyo na maneno hayo bado yalikuwepo hapo katika ukungu bali hayakufuta kumbukumbu za utotoni wake.

Ninashangaa kuona mwanamke mwengine aliyemsamehe mtu aliyemkosea kwa miaka mingi, nilistajabu na kumuuliza kwa nini alichagua kumsamehe na kusahau miaka mingi sasa ya dhuluma.

Alisema kwa upole, “Kilikuwa kitu kigumu ambacho nimewahi kufanya, lakini nilijua nilifaa kukifanya, Kwa hivyo nilikifanya.” Imani yake kwamba Mwokozi atamsamehe kama yeye atawasamehe wengine ilimtayarisha kwa hisia ya amani na matumaini alipokabiliwa na kifo miezi tu baada ya kumsamehe adui wake asiyekuwa tayari kutubu.

Aliniuliza, “Nitakapofika huko, itakuwaje huko mbinguni?”

Na mimi nikasema, “Mimi najua tu kutokana na kile nimeshaona kuhusu uwezo wako wa kutumia imani na kusamehe kwamba itakuwa makaribisho ya ajabu kwako.”

Nina tumainisho lingine kwa wale sasa wanaoshangaa kama imani yao katika Yesu Kristo itatosha kwao kuvumilia vyema hadi mwisho. Nimebarikiwa kuwajua wengine wenu ambao mnasikiliza sasa mlipokuwa vijana, wachangamfu, mmezawadiwa kuliko wengi wenu wa karibu nanyi, hali mlichagua kufanya kile Mwokozi angependelea mfanye. Kutoka na wingi wenu mmepata njia za kuwasaidia na kuwatunza wale mnaweza kutowaangalia au kuwadharu kutokana na nafasi zenu katika maisha.

Majaribu yanapokuja, imani ya kuyavumilia vyema itakuwepo, iliyojengwa kama mnavyoweza kutambua bali hamkuweza wakati ambao mlitenda juu ya upendo halisi wa Kristo, mkihudumu na kuwasamehe kama vile Mwokozi angefanya. Mnajenga msingi wa imani kutoka kwa kupenda kama vile Mwokozi anavyopenda na kuhudumu kwa ajili Yake. Imani yenu katika Yeye iliwapeleka kwa vitendo vya hisani ambavyo vinaleta matumaini.

Bado hajachelewa sana kuimarisha msingi wa imani. Daima kuna wakati. Kwa imani katika Mwokozi, unaweza kutubu na kuomba msamaha. Kuna mtu unaweza kusamehe. Kuna mtu unaweza kushukuru. Kuna mtu unaweza kuhudumia. Unaweza kufanya hivyo popote ulipo na vyovyote unavyohisi mpweke na kutupwa.

Siwezi kuahidi kumalizika kwa dhiki yako katika maisha haya. Siwezi kuhakikisha kwamba majaribu yako kuwa yatakuwa ya muda. Mojawapo wa sifa bainifu za majaribu katika maisha ni kuwa yanaonekana kufanya saa kwenda pole pole na kisha karibu kusimama.

Kuna sababu za hivyo. Mkijua hizo sababu hazipatiani faraja, bali zinaweza kuwapatia hisia za subira. Hizo sababu zitatokana na jambo hili moja: katika upendo Wao kamili kwako, Baba wa Mbinguni na Mwokozi wanataka ninyi kuunganishwa Nao na kuishi katika familia milele. Ni wale tu watatakaswa kikamilifu kuwa wasafi kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo wanaweza kuwa.

Mama yangu alipigana na saratani kwa karibu miaka 10. Matibabu na upasuaji na mwishowe kulazwa kitandani kulikuwa ni kati ya majaribu yake.

Nakumbuka baba yangu akisema akimtazama akitweta pumzi zake za mwisho, “Msichana mdogo ameenda nyumbani kupumzika.”

Mmoja wa wanenaji katika mazishi yake alikuwa ni shemejiye na rafiki Rais Spencer  W. Kimball. Kati ya kusifia alikofanya, nakumbuka akisema kitu kilichokuwa kama hiki: “Wengine wenu mnaweza kufikiria kwamba Mildred aliteseka kwa muda mrefu na sana kwa sababu ya kitu alifanya makosa ambacho kilihitaji majaribu haya.” Kisha akasema, “La, ni kwamba Mungu alitaka kumkwatua kidogo zaidi.” Nakumbuka wakati huu nikifikiria, “Kama wanamke mwema hivi alihitaji kukwatuliwa zaidi, basi ni nini kilichokuwa kinaningoja mimi?

Kama tuna imani katika Yesu Kristo, nyakati zile ngumu na zile rahisi katika maisha zinaweza kuwa baraka. Katika hali zote, tunaweza kuchagua kilicho sahihi kwa mwongozo wa Roho. Tuna injili ya Yesu Kristo kuchonga na kuongoza maisha yetu kama tutachagua hivyo. Na manabii wakifunua kwetu nafasi zetu katika mpango wa wokovu tunaweza kuishi kwa matumaini kamili na hisia za amani. Hatutakuwa na haja ya kuhisi kwamba tu wapweke au hatupendwi katika huduma ya Bwana, kwa sababu sivyo kamwe. Tunaweza kuhisi upendo wa Mungu. Mwokozi ameahidi malaika kushoto kwetu na kulia kwetu, atatuhimili. 10 na Yeye hutimiza neno Lake.

Nashuhudia kwamba Mungu Baba yu hai na kwamba Mwanawe Mpendwa ni Mkombozi wetu. Roho Mtakatifu amethibitisha kweli katika mkutano huu na atafanya hivyo tena kama mtatafuta kama mnaposikiliza na mnaposoma hapo baadaye jumbe za watumishi wa Bwana wenye mamlaka ambao wako hapa. Rais Thomas S. Monson ni nabii wa Bwana kwa ulimwengu wote. Bwana anawalinda. Mungu Baba yu hai. Mwanawe Mpendwa, Yesu Kristo, ndiye Mkombozi wetu. Na upendo Wake upo daima. Nashuhudia hivi katika jina la Yesu Kristo, amina.