Imani, Ushupavu, Ukamilisho: Ujumbe kwa Wazazi Wasio na Wenzi
Mnajitahidi kuwalea watoto wenu katika hako na kweli, mkijua kwamba ingawa hamwezi kubadilisha yaliyopita, mnapochonga siku za usoni.
Ujumbe wangu ni kwa wazazi pekee Kanisani, wengi wao ambao ni kina mama wasio na wenzi---ninyi ni wanawake hodari ambao, kupitia katika hali tofauti za maisha, mlijipata mkilea watoto na kusimamia nyumba wenyewe. Labda mmefelewa na mke au mume au mmetalakiwa. Mnaweza kuwa mnakabiliana na changamoto za uzazi wa peke kama matokeo ya kupiga kona mbaya katika ndoa lakini sasa mnaishi ndani ya mipaka ya injili, baada ya kubadilisha maisha yenu. Na mbarikiwe kwa kuepuka aina ya urafiki ambao ungekuja badala ya nemsi na uanafunzi. Hiyo ingekuwa gharama kuu sana kulipia.
Hata hivyo wakati wengine mnaweza kuuliza, kwa nini mimi? Ni kupitia ugumu wa maisha ambapo tunakua kuelekea uungu kama vile silka yetu inavyochongwa katika kalibu ya mateso, vile matukio ya maisha yanavyotokea Mungu anapoheshimu wakala wa mtu. Kama Mzee Neal A. Maxwell alivyosema, hatuwezi kufanya hesabu zote au kujumlisha yote kwa sababu “hatuna namba zote.” 1
Hata ikiwa hali zenu au sababu zake zikiwa zipi, ninyi ni wa ajabu.. Siku baada ya siku mnakumbana na shida za maisha, mkifanya kazi ile daima inahitaji watu wawili lakini mkiifanya peke yenu. Mnakuwa kina baba vile vile kina mama. Mnaendesha nyumba zenu, mnatunza familia, wakati mwingine mnataabika kutosheleza mahitaji, na kimiujiza hata mnapata nafasi za kuhudumu katika Kanisa kwa njia ya ajabu sana. Mnawalea watoto wenu. Mnalia na kuomba pamoja na wao na kuwaombea. Mnawatakia mema lakini mna wasiwasi kila usiku kwamba juhudi zenu bora hazitaweza kuwa za kutosheleza.
Ingawaje nasita kuwa mbinafsi sana, mimi ni tunda la nyumba kama hiyo. Katika miaka mingi ya utotoni mwangu na ujana wangu, mama yangu alitulea katika hali ya umaskini. Hela zilibaniwa sana. Alikumbwa na upweke wa ndani, nyakati za dhiki ya uhimili na uenzi. Hali licha ya haya yote, kulikuwa na staha kuhusu mama yangu, chanzo cha azimio kuu na silka ya kiskoti.
Vyema, miaka yake ya baadaye ilikuwa imebarikiwa kuliko ya mwanzoni. Aliolewa na mwongofu mpya, mjane mwanaume, walifunganishwa katika Hekalu la London England na baadaye kuhudumu huko kwa muda mfupi kama wafanya maagizo. Walikuwa pamoja kwa karibu robo karne---wenye furaha, wametosheka, na kukamilika mpaka mkono wa mauti ulipowachukua.
Kuna wengi wenu wanawake wema katika Kanisa ulimwenguni kote ambao mnakabiliana na hali kama hizi na ambao mnaonyesha uthabiti huo huo mwaka baada ya mwaka.
Hivi sivyo vile mlikuwa mmetumainia au mmepangia, mmeombea au mmetarajia, mlipoanza miaka iliyopita. Safari yenu katika maisha ina matuta, mikato, manyombo na kona, sana sana kama matokeo ya maisha katika ulimwengu ulioanguka ambao unatakiwa kuwa mahali pa kuthibitishwa na kujaribiwa.
Hata hivyo mnajitahidi kulea watoto wenu katika haki na kweli, mkijua kwamba kuwa hamwezi kubadilisha yaliyopita, mnaweza kuchonga maisha ya usoni. Njiani mtapata baraka za malipo, hata kama si wazi kwa sasa.
Kwa msaada wa Mungu, hamfai kuogopa siku za usoni. Watoto wenu watakua na kuwaita wabarikiwa na kila mmoja kwa mafanikio mengi yatakayosimama kama sifa za shukrani kwenu.
Tafadhali msihisi kamwe kwamba mmekuwa katika daraja la pili, jamii ya chini katika ushiriki wa Kanisa, vyovyote vile kuwa hamna haki ya baraka za Bwana kuliko wengine. Katika ufalme wa Mungu hamna raia wa daraja la pili.
Tunatumaini kwamba mnapohudhuria mikutano na mkionekana kama familia kamili na yenye furaha au mnasikia mtu akizungumza juu ya sifa nzuri za familia, mtahisi vyema kuwa sehemu ya Kanisa ambalo linalenga familia na linafunza umuhimu wake katika mpango wa Baba wa Mbinguni kwa furaha ya watoto wake; kwamba katika janga la ulimwengu na kuoza kwa maadili, tuna kanuni, mamlaka, na maagano yale yanayotoa matumaini bora kwa ulimwengu, ikijumuisha furaha ya watoto wao ya siku za usoni na familia ambazo wataanzisha.
Katika mkutano wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama mkuu wa septemba 2006, Rais Gordon B. Hinckley alielezea uzoefu ulioshirikishwa na mama peke wa watoto saba aliyetalakiwa wakati huu wakiwa umri wa miaka 7 hadi 16. Alikuwa ameenda mtaa wa upande mwingine kupeleka kitu kwa jirani. Alisema:
“Nilipogeuka kurudi nyumbani, niliweza kuona taa zimewaka nyumbani kwangu. Niliweza kusikia miangi ya watoto wangu nilipotoka nje ya mlango dakika chache mapema. Walikuwa wanasema: ‘Mama, tutakula nini jioni hii?’ ‘Unaweza kunipeleka kwenye maktaba?’ ‘Ningependa kupata karatasi ya bango jioni hii.’ Nimechoka na mchovu sana, nilitazama ile nyumba na kuona mwangaza katika kila chumba. Nilifikiria wale watoto wote ambao walikuwa nyumbani wakiningoja mimi nije na kukidhi mahitaji yao. Mizigo yangu ilionekana kuwa mizito kuliko vile ningeweza kubeba.
“Nakumbuka nikitazama mbinguni kupitia majonzi yangu, na kusema ‘Baba Mpendwa, siwezi kutenda lolote jioni hii. Mimi nimechoka. Siwezi kukabiliana na haya. Siwezi kwenda nyumbani na kuwatunza watoto hawa peke yangu. Naweza kuja Kwako na kuishi Nawe kwa usiku mmoja tu? …’
“Sikusikia maneno ya jibu kihalisi, lakini niliyasikia kwenye akili yangu. Jibu lilikuwa: ‘La, mdogo wee, huwezi kuja kwangu sasa. …. Lakini mimi nitakuja kwako.’” 2
Asanteni, kina dada, kwa yale yote mnayofanya kulea familia zenu na kudumisha nyumba yenye upendo ambapo kuna wema, amani, na nafasi.
Ingawaje mnaweza kuhisi wapweke, kwa kweli kamwe hupo peke yakokabisa. Mnaposonga mbele kwa subira na katika imani, Majaliwa yataandamana na ninyi; mbingu zitamwaga baraka zinazohitajika.
Mtazamo wenu na twasira ya maisha itabadilika wakati, badala ya kutazama chini mtazama juu.
Wengi wenu tayari mmeshagundua kweli kuu za kubadilisha ambayo mnaishi kuinua mizigo ya wengine, mizigo yenu itakuwa nyepesi. Ingawaje hali zinaweza kuwa zisibadilike, mtazamo wenu utabadilika. Mnaweza kukabiliana na majaribu yenu kwa kuyakubali sana, moyo unao uelewa, na shukrani kuu kwa kile ulichonacho, badala ya kutamani kile unachokosa.
Mmegundua kwamba mnapotoa muamana wa matumaini kwa wale ambao akaunti zao za maisha ni tupu, hazina zetu za faraja zitarutubishwa na kujazwa; kikombe chetu kweli “kinafurika” (Zaburi 23:5).
Kutokana na kuishi vyema, ninyi na watoto wenu siku moja mtaweza kupokea baraka za kuwa sehemu ya familia kamili ya milele.
Washiriki na viongozi, kuna chochote ambacho mnaweza kufanya kuwahimili familia za mzazi peke bila kuhukumu au kuwaalumu? Na muwe wanasihi kwa vijana katika familia hizi, hasa kuwapatia vijana mifano ya kile watu wema wanaweza kufanya na jinsi watu wema wanaishi? Kukosekana kwa baba, ninyi mnatoa mifano ya kustahili kuigwa?
Sasa zipo hapa, familia zingine za mzazi peke ambapo baba ndiye mzazi peke. Ndugu, pia tunawaombea ninyi na kuwasifia ninyi. Ujumbe huu pia ni wenu.
Wazazi peke, nashuhudia kwamba mnapofanya vyema mnavyoweza katika changamoto ngumu sana za mwanadamu, mbingu zitatabasamu juu yenu. Kweli hampo peke yenu. Acha ukombozi, uwezo wa upendo wa Yesu Kristo huangaze maisha yetu sasa na kutujaza kwa matumaini ya ahadi za milele. Muwe jasiri. Muwe na imani na matumaini. Tazama sasa kwa ushupavu na tazama siku za usoni kwa imani. Katika jina la Yesu Kristo, amina.