2010–2019
Ilikuwa yenye Thamani?
Aprili 2012


Ilikuwa Inastahili?

Kazi ya kushiriki injili vifaavyo na kawaida na wale tunaojali na kupenda itakuwa kazi na furaha ya maisha yetu.

Katika mkutano huu na katika mikutano mingine ya hivi juzi,1 wengi wetu wameshangaa, naweza kufanya nini ili kusaidia kujenga Kanisa la Bwana na kuona ukuaji halisi ninakoishi?

Katika hii na kazi nyingine muhimu, kazi yetu muhimu sana kila mara zimo ndani ya nyumba zetu na familia.2 Ni katika familia ambapo Kanisa limejengwa na ndipo ukuaji halisi unafanyika.3 Tunapaswa kuwafundisha watoto wetu kanuni na mafundisho ya injili. Tunapaswa kuwasaidia kuwa na imani katika Yesu Kristo na kuwatayarisha kwa ubatizo wanapotimu miaka minane.4 Lazima tuwe waaminifu sisi wenyewe ili waweze kuona mfano wetu wa upendo kwa Bwana na Kanisa Lake. Hii inasaidia watoto wetu kuhisi furaha katika kutii sheria, furaha katika familia, na shukrani katika huduma kwa wengine. Ndani ya nyumba zetu tunapaswa kufuata utaratibu uliopeanwa na Nefi aliposema:

“Tunajitahidi … kuwashawishi watoto wetu … kumwamini Kristo, na kupatanishwa na Mungu. …

“… Tunazungumza kuhusu Kristo, tunafurahia katika Kristo, tunahubiri kuhusu Kristo, tunatoa unabii kumhusu Kristo, na tunaandika kulingana na unabii wetu, ili watoto wetu, wajue asili ya kutegemea msamaha wa dhambi zao.”5

Tunajitahidi kuleta baraka hizi kwa watoto wetu kwa kuhudhuria kanisa pamoja nao, kufanya mkutano wa jioni ya familia, na kusoma maandiko pamoja. Tunaomba kila siku pamoja na familia yetu, kukubali miito, kutembelea wagonjwa na wapweke, na kufanya mambo mengine yanayowezesha watoto wetu kujua kuwa tunawapenda na kuwa tunapenda Baba yetu wa Mbinguni, Mwanawe, na Kanisa Lao.

Tunazungumza na kutoa unabii wa Kristo tunapopeana somo la jioni ya familia nyumbani ama kuketi pamoja na mtoto na kueleza juu ya upendo wetu kwa mtoto na ushuhuda wetu wa injili uliorejeshwa.

Tunaweza kuandika juu ya Kristo kwa kuandika barua kwa wale walio mbali. Wamisionari, wana na mabinti katika jeshi, na wale tunaowapenda wote wanabarikiwa kwa barua tunazoandika. Barua kutoka nyumbani sio tu barua pepe ya haraka. Barua halisi hupeana kitu kinachoweza kukamatwa, kufikiriwa, na kuthaminiwa.

Tunasaidia watoto wetu kutegemea Upatanisho wa Mwokozi na kujua msamaha wa Baba wa Mbinguni mwenye upendo kwa kuonyesha upendo na msamaha katika njia yetu ya ulezi. Upendo wetu na msamaha sio eti unawanaleta watoto wetu kwetu pekee bali pia unajenga imani katika kujua kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda na kuwa atawasamehe wanapojitahidi kutubu na kutenda vyema na kuwa bora. Wanaamini ukweli huu kwa sababu wamezoea hivyo kutoka kwa wazazi wao wa duniani

Kuongezea kwa kazi ambayo tutafanya ndani ya familia yetu wenyewe, Nefi alifundisha kwamba “tunajitahidi … kuwashawishi … ndugu zetu, kumwamini Kristo, na kupatanishwa na Mungu.”6 Kama washiriki wa Kanisa La Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, kila mmoja wetu ana baraka na jukumu la kushiriki injili. Wengine wale wanaohitaji injili maishani mwao bado sio washiriki wa Kanisa. Wengine wao walikuwa miongoni mwetu bali wanahitaji tena kuhisi furaha waliohisi walipokubali injili mara ya kwanza maishani mwao. Bwana anawapenda wote wale ambao hawajasikia injili vile vile wale wanaomrudia Kwake.7 Kwake na kwetu, haijalishi. Yote ni kazi moja. Ni thamani ya nafsi, pasipokujali hali yao, ambayo ni kuu kwa Baba yetu wa Mbinguni, Mwanawe, na kwetu.8 Kazi ya Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe ni “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu”9 kwa watoto wake wote, bila kujali hali zao za sasa. Baraka yetu ni kusaidia katika kazi hii kubwa.

Rais Thomas S. Monson alielezea jinsi tunavyoweza kusaidia aliposema: “Uzoefu wetu wa umisionari lazima uwe wa kisasa. Haitoshelezi kuketi chini na kutafakari uzoefu wa zamani. Ili kuridhika, lazima uendelee kushiriki injili vifaavyo na kawaida.”10

Kazi ya kushiriki injili vifaavyo na kawaida na wale tunaojali na kupenda itakuwa kazi na furaha ya maisha yetu. Acha niwaambieni kuhusu muwili ya uzoefu huo.

Dave Orchard aliishi Mjini, ambako wengi wa marafiki zake walikuwa washiriki wa Kanisa. Walikuwa wenye ushawishi mkubwa kwake. Kuongezea, viongozi wa Kanisa wa ujirani wake walimwalika kila mara kwa tamasha. Rafiki zake walifanya hivyo hivyo. Ingawa hakuwa amejiunga na Kanisa wakati huo, miaka yake ya ukuaji ilibarikiwa kwa marafiki wema wa WSM na tamasha zilizofadhiliwa na Kanisa. Baada ya kuingia chuoni, alihama kutoka nyumbani kwao, na wengi wa marafiki zake wakaondoka kwenda misheni. Alikosa ushawishi wao maishani mwake.

Mmoja wa marafiki wa shule ya upili wa Dave alikuwa bado nyumbani. Huyu rafiki alikuwa akikutana kila wiki na askofu wake kwa juhudi ya kuyaweka maisha yake vifaavyo na kuweza kuhudumu kama mmisionari. Yeye na Dave wakawa wakazi wenza na, kama ifaavyo na kawaida, wangeongea kuhusu kwa nini hakuwa akihudumu kama mmisionari wakati huo na kwa nini alikutana kila mara na askofu. Rafiki alidhihirisha shukrani yake na heshima kwa askofu wake na fursa ya kutubu na kuhudumu. Kisha akamuuliza Dave ikiwa angependa kuja katika mahojiano yaliyofuata. Ni mwaliko ulioje! Bali kwa muktadha wa urafiki na hali yao, ilikuwa inafaa na kawaida.

Dave alikubali na mara tu alikutana na askofu mwenyewe. Hii iliongoza wazo la Dave la kukutana na wanamisionari. Alipata ushuhuda kwamba injili ni ya kweli, na tarehe ya ubatizo wake ikawekwa. Dave alibatizwa na askofu wake, na baada ya mwaka Dave Orchard na Katherine Evans wakaona hekaluni. Wana watoto watano warembo. Katherine ni dada yangu mdogo. Nitakuwa na shukrani milele kwa rafiki huyu mwema ambaye, pamoja na askofu mwema, alimleta Dave katika Kanisa.

Dave alivyokuwa akiongea kuhusu uongofu wake na kutoa ushuhuda wake juu ya mambo haya, aliuliza swali, “Kwa hivyo, Ilikuwa Inastahili? Je, juhudi zote za marafiki na viongozi wa vijana na askofu wangu, miaka hiyo yote, ilifaa juhudi ya kuwezesha mvulana mmoja tu kubatizwa?” akiwaelekezea kidole Katherine na watoto wake watano, alisema, “Vema, angalahu kwa mke wangu na watoto wetu watano, jibu ni ndio.”

Wakati wowote injili imeshirikishwa, haijawahi kamwe kuwa “mvulana mmoja tu.” Wakati wowote uongofu unapofanyika ama mtu kumrudia Bwana, ni familia ndiyo imeokolewa. Kama vile watoto wa Dave na Katherine walivyokua, wote wamekubali injili. Binti mmoja na wana wawili wamehudumu kama wamisionari na mmoja karibuni alipokea mwito wake kuhudumu katika misheni ya Alpine-wasemao kijerumani. Wawili wakubwa wameoana katika hekalu, na yule mdogo sasa yumo katika shule ya upili, waaminifu katika kila njia. Ilikuwa Inastahili? Aha ndio, Ilikuwa Inastahili?

Dada Eileen Waite alihudhuria mkutano moja wa kigingi ambako Dave Orchard alielezea kuhusu matukio ya uongofu wake. Kwote kwenye mkutano, yote ambayo angeweza kufikiria ilikuwa ni familia yake mwenyewe na haswa dadake, Michelle, ambaye alikuwa mbali na Kanisa kwa muda mrefu. Michelle alitalikiwa na alikuwa akijaribu kulea watoto wanne. Eileen alihisi kuvutiwa kumtumia nakala ya kitabu cha Mzee M. Russell Ballard Our Search for Happiness, pamoja na ushuhuda wake, ambayo alifanya. Wiki hiyo ifuatayo rafiki mwengine alimwambia Eileen kwamba yeye pia alihisi kwamba amtafute Michelle. Huyu rafiki pia alimwandikia Michelle barua akishiriki ushuhuda wake na kuthihirisha upendo wake. Inastajabisha jinsi Roho anavyotenda kwa watu kadha ili kusaidia aliye na mahitaji?

Muda ulipita. Michelle alimpigia simu Eileen na kumshukuru kwa kile kitabu. Alisema kwamba alianza kutambua upweke wa kiroho maishani mwake. Eileen alimwambia kuwa alijua kwamba amani aliyotaka ingepatikana katika injili. Alimwambia kuwa alimpenda na alimtaka awe na furaha. Michelle alianza kufanya mabadiliko maishani mwake. Mara tu akampata mwanamume wa ajabu aliyeshiriki kikamilifu Kanisani. Walioana na baada ya mwaka walifunganishwa katika Hekalu la Ogden Utah. Juzi mwanawe wa miaka 24 alibatizwa.

Kwa wengine katika familia ya Michelle na wengine wote ambao bado hawajui kwamba hili Kanisa ni la kweli. Nawaalika kwa maombi tafakari kama Kanisa ni la Kweli. Kubalini familia zenu na marafiki na wamisionari wasaidie. Utakapojua kwamba ni kweli, na ndiyo, njoo ujiunge pamoja nasi kwa kuchukua hatua hio hio katika maisha yako.

Mwisho wa hadithi hii bado haujaandikwa, lakini baraka zimepewa mwanamke huyu wa ajabu pamoja na familia yake kwa vile wale waliompenda walitenda juu ya ushawishi na katika njia halisi na kawaida kwa kushiriki ushuhuda wao na kumwalika yeye kurudi.

Nimefikiria sana juu ya matukio haya mawili. Kijana mmoja aliyejitahidi kuweka maisha yake vifaavyo alimsaidia kijana mwengine aliyekuwa akitafuta ukweli. Mwanamke mmoja alishiriki ushuhuda na imani yake na dada yake aliyekuwa mbali na Kanisa kwa miaka 20. Ikiwa tutasali na kuomba Baba wa Mbinguni yule tutakayemsaidia na kuahidi kutenda kulingana na vishawishi anavotupatia kutuwezesha kujua jinsi tunavyoweza kusaidia, Yeye atajibu maombi yetu na tutakuwa vyombo mikononi Mwake vya kufanya kazi Yake. Kutenda kwa upendo kulingana na vishawishi vipeanavyo na Roho huwa kichocheo cha mabadiliko. 11

Kama vile umesikiliza matukio haya ya kushiriki injili vifaavyo na kawaida na wale mnaowajali, wengi wenu wamekuwa na uzoefu kama huo ambao Eileen Waite alikuwa nao. Umefikiria mtu ambaye unapaswa kumfikia na ama kuwaalika kurudi au kushiriki nao hisia zako kuhusu injili ya Yesu Kristo. Mwaliko wangu ni kutenda, bila kusita, kwa mwongozo huo. Ongea na rafiki yako ama mshiriki wa familia. Ufanye hivyo kwa njia ifaayo na kawaida. Acha wajue kuhusu upendo wako kwao na kwa Bwana. Wamisionari wanaweza kusaidia. Ushauri wangu ni sawa na ule Rais Monson amepeana mara nyingi kutoka kwa jukwa hili; “Usiwahi kuchelewesha mwongozo.”12 Unapotenda kulingana na mwongozo na kutenda kwa upendo, tazama vile Baba yetu wa Mbinguni anatumia utayari wako wa kutenda ili kuleta muujiza maishani mwako na katika maisha ya yule unayemjali. 13

Wapendwa ndugu na dada zangu, tunaweza kujenga Kanisa Lake kuona ukuaji halisi tunapofanya kazi kuleta baraka za injili kwa familia zetu na kwa wale tunaowapenda. Hii ndio kazi ya Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe. Najua kwamba wanaishi na kuwa wanajibu maombi. Tunapotenda kwa maongozi haya, tukiwa na imani katika uwezo Wao wa kuleta muujiza, miujiza itafanyika na maisha yatabadilika. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona Worldwide Leadership Training Meeting, Feb. 11, 2012, LDS.org.

  2. Ona Teachings of Presidents of the Church: Harold B. Lee (2000), 134.

  3. Ona Boyd K. Packer, “Priesthood Power in the Home,” Worldwide Leadership Training Meeting, Feb. 11, 2012, LDS.org.

  4. Ona Mafundisho na Maagano 68:25–28.

  5. 2 Nefi 25:23, 26.

  6. 2 Nefi 25:23.

  7. Ona Luka 15:4–7.

  8. Ona Mafundisho na Maagano 18:10.

  9. Musa 1:39.

  10. “Status Report on Missionary Work: A Conversation with Elder Thomas S. Monson, Chairman of the Missionary Committee of the Council of the Twelve,” Ensign, Oct. 1977, 14.

  11. Ona Thomas S. Monson, “Anxiously Engaged,” Liahona and Ensign, Nov. 2004, 56–59; “To the Rescue,” Liahona, July 2001, 57–60; Ensign, May 2001, 48–50; “The Doorway of Love,” Liahona and Ensign, Oct. 1996, 2–7.

  12. Ona Ann M. Dibb, “My Father Is a Prophet” (Brigham Young University–Idaho devotional, Feb. 19, 2008), byui.edu/devotionalsandspeeches; Thomas S. Monson, “Stand in Your Appointed Place,” Liahona and Ensign, May 2003, 54–57; “Peace, Be Still,” Liahona and Ensign, Nov. 2002, 53–56; “Priesthood Power,” Liahona, Jan. 2000, 58–61; Ensign, Nov. 1999, 49–51; “The Spirit Giveth Life,” Ensign, May 1985, 68–70.

  13. Kwa ziada, Rais Thomas S. Monson, na manabii wengine wamefunza kanuni hii hii. Kwa mfano, Rais Spencer W. Kimball alifunza umuhimu wa kutanda juu ya vishawishi vinavyokuja kupitia Roho aliposema: “Mungu hutuona sisi, na hututunza sisi. Lakini kwa kawaida ni kupitia mtu mwingine ambapo mahitaji yetu ukidhiwa. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba tuhudumiane katika ufalme” (Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball [2006], 82).