Kuzingatia moyoni mwetu na Kuweza kujitegemea Kiroho: Sakramenti, Hekalu, na Kujitolea katika Huduma
Tunaweza kuongoka na kuwa wa kujitegemea kiroho tunapoishi maagano yetu kwa maombi.
Mwokozi aliwaambia wanafunzi Wake kuhusu mwana aliyemwacha baba yake tajiri, kuelekea nchi ya mbali, na kuharibu urithi wake. Wakati njaa ilipotokea, kijana mdogo alichukua kazi ya hali ya chini ya kulisha nguruwe. Alikuwa na njaa sana kiasi kwamba alitaka kula maganda yaliyotengewa wanyama.
Mbali na nyumbani, mbali na mahali alikotaka kuwa, na katika hali ya umasikini, kitu cha umuhimu wa milele kilitokea katika maisha ya kijana huyu. Katika maneno ya Mwokozi, “alizingatia moyoni mwake.”1 Alikumbuka alikuwa mtu aina gani, kutambua kile alichokuwa akikosa, na kuanza kutamani baraka zilizopatikana bure katika nyumba ya baba yake.
Kote maishani mwetu, kama katika nyakati za giza, changamoto, huzuni, ama dhambi, tunaweza kuhisi Roho Mtakatifu akitukumbusha kwamba sisi ni wana na mabinti halisi wa Baba wa Mbinguni anayejali, anayetupenda, na kutamani baraka takatifu ambayo yeye pekee anaweza kupeana. Katika nyakati hizi tunapaswa kujitahidi kuzingatia moyoni mwetu na kurudi katika nuru ya upendo wa Mwokozi wetu.
Baraka hizi kwa haki ni za watoto wote wa Baba wa Mbinguni. Kutamani baraka hizi, ikiwemo maisha ya shangwe na furaha, ni sehemu muhimu ya mpango wa Baba wa Mbinguni kwa kila mmoja wetu. Nabii Alma alifunza, “Hata ikiwa hamwezi ila kutamani kuamini, acha hamu hii ifanye kazi ndani yenu.”2
Kama vile tamaa yetu ya kiroho inavyoongezeka, tunakuwa wakujitegemea kiroho. Basi, ni kivipi tunaweza kujisaidia wenyewe pamoja na familia zetu kuongeza tamaa yetu ya kumfuata Mwokozi na kuishi Injili Yake? Tunawezaje kuimarisha mapenzi yetu ya kutubu, kuwa wakustahili, na kuvumilia hadi mwisho? Tunawezaje kusaidia vijana wetu na watu wazima vijana kuruhusu tamaa hizi kuishi nao hadi waongoke na kuwa “watakatifu kupitia upatanisho wa Kristo”?3
Tunakuwa waongofu na kujitegemea kiroho tunapoishi maagano yetu kwa maombi.—kwa kushiriki sakramenti kwa maisha yanayostahili, kustahili kumiliki sifu ya hekalu, na kujitolea kuhudumia wengine.
Ili kushiriki sakramenti kwa maisha yanayostahili, tunakumbuka kwamba tunaweka upya agano tulioweka wakati wa ubatizo. Ili sakramenti kuwa ya kusafisha kiroho kila wiki, tunahitaji kujitayarisha kabla ya kuja kwa mkutano wa sakramenti. Tunafanya hivyo kwa kuacha nyuma makusudi kazi yetu ya kila siku na burudani na kuruhusu mawazo ya kidunia na wasiwasi kuondoka. Tunapofanya, tunaweka nafasi akilini mwetu na mioyo kwa ajili ya Roho Mtakatifu.
Kisha tunakuwa tayari kutafakari juu ya Upatanisho. Zaidi ya kufikiri tu kuhusu taarifa za kuteseka kwa Mwokozi na kifo, tafakari yetu unatusaidia kutambua kwamba kupitia kwa kujitolea kwa Mwokozi, tunayo matumaini, fursa, na nguvu za kufanya mabadiliko halisi na kweli katika maisha yetu.
Tunapoimba wimbo wa sakramenti kushiriki katika maombi ya sakramenti, na kushiriki ishara za mwili Wake na damu, kwa maombi tunatafuta msamaha wa dhambi zetu na upungufu. Tunafikiria kuhusu ahadi tulizoweka na kutii wiki iliyopita na kuweka ahadi za kibinafsi ili kufuata Mwokozi katika wiki ijayo.
Wazazi na viongozi, mnaweza kuwasaidia vijana kupata baraka za ajabu za sakramenti kwa kupeana fursa maalum kwao kujifunza, kujadiliana, na kugundua umuhimu wa Upatanisho katika Maisha yao. Waacheni wasome maandiko wenyewe na kujifunza mmoja kwa mwengine kutoka kwa uzoefu wao binafsi..
Kina baba, viongozi wa ukuhani, na marais wa jamii wana jukumu maalum la kusaidia wamiliki wa Ukuhani wa Haruni ili kujitayarisha vilivyo kuweza kutimiza majukumu yao matakatifu. Matayarisho haya yanafanywa wiki nzima kwa kuishi kanuni za injili. Wakati vijana wadogo wanapotayarisha, kubariki, na kupitisha sakramenti kwa ustahilivu na heshima, ama kweli wanafuata mfano wa Mwokozi wakati wa Chakula cha Mwisho 4 na kuwa kama Yeye.
Nashuhudia kwamba sakramenti inatupatia fursa ya } kuzingatia moyoni mwetu na kuona “mabadiliko makuu” moyoni 5—ili kukumbuka uhalisi wetu na yale tunayopenda sana. Tunapoweka upya agano la kutii sheria, tunapokea urafiki wa Roho Mtakatifu ili kutuongoza kurudi kwa uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni. Si ajabu tumeamriwa “kukutana pamoja mara kwa mara kushiriki kwa mkate na [maji]” 6na kushiriki sakramenti kwa ajili nafsi zetu.7
Kuongezea kwa sakramenti, hamu yetu ya kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni inaongezeka tunapokuwa wastahiki kupokea sifu ya hekalu. Tunakuwa wastahiki kwa kutii sheria kila wakati. Utiifu huu huanzia utotoni na kuendelea kupitia uzoefu katika Ukuhani wa Haruni na Usichana. Kisha, kwa matarajio, makuhani na wasichana huweka malengo na kujitayarisha vilivyo kubarikiwa na kufunganishwa hekaluni.
Ni nini viwango kwa wamiliki wa sifu? Mtunga Zaburi anatukumbusha:
“Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ama ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?
“Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe.”8
Kustahili kumiliki sifu ya hekalu kunatupatia nguvu za kuweka maagano yetu ya hekalu. Tunapataje nguvu hizo kibinafsi? Tunajitahidi kupata ushuhuda wa Baba yetu wa Mbinguni, Yesu Kristo, Roho Mtakatifu, uhalisi wa Upatanisho, na ukweli wa Nabii Joseph Smith na Urejesho. Tunaidhinisha viongozi wetu, kutendea familia yetu wema, kusimama kama mashahidi wa Kanisa la kweli la Bwana,tunahudhuria mikutano za Kanisa yetu, heshimu maagano yetu, kutimiza majukumu za uzazi, na kuishi maisha adilifu. Unaweza kusema kwamba hayo yanasikika kama kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho aliye mwaminifu! Ni kweli. Kiwango kwa wamiliki wa sifu ya hekalu sio juu sana kutushinda kutimiza. Ni kwa urahisi kuishi injili kwa uaminifu na kufuata manabii.
Kisha, kama wamiliki wa sifu ya hekalu, tunaunda taratibu za kuishi Kikristo. Haya yanajumuisha utiifu, kujitolea ili kutii sheria, kupendana mmoja na mwengine, kuwa wasafi katika mawazo na matendo, na kujitolea kujenga ufalme wa Mungu. Kupitia kwa Upatanisho wa Mwokozi na kwa kufuata taratibu hizi za kawaida za uaminifu, tunapokea “uwezo utokao juu” 9 ili kukabiliana na changamoto za maisha. Tunahitaji uwezo huu mtakatifu leo zaidi ya yote. Ni uwezo tunaopata tu kupitia maagizo ya hekalu. Nashuhudia kwamba jinsi tunavyojitolea ili kupokea maagizo ya hekalu yanastahili kila juhudi tunayofanya.
Hamu yetu ya kujifunza na kuishi injili inavyoongezeka, kwa kawaida tunajaribu kusaidia mmoja kwa mwengine. Mwokozi alimwambia Petro, “Utakapoongoka waimarishe ndugu zako.” 10 Nafurahia kwamba vijana siku hizi wana hamu kuu ya kuhudumu na kuwabariki wengine—ili kuleta mabadiliko katika ulimwengu huu. Pia wanatamani furaha inayoletwa na huduma yao.
Inagawa, ni vigumu kwa vijana kuelewa jinsi matendo yao ya sasa yatawatayarisha kwa au kuwazuia kutokana na fursa za huduma za siku zijazo. Sisi sote tuna “kazi muhimu” 11 ya kusaidia vijana wetu katika kujitayarisha kwa huduma ya maisha yote kwa kuwasaidia kujitegemea wenyewe. Kuongezea kwa kujitegemea kiroho ambako tumekuwa tukijadili, kuna kujitegemea kimaisha, kunakojumuhisha kupata elimu zaidi ya shule ya sekondari ama mafunzo ya ufundi, kujifunza kufanya kazi, na kuishi kulingana na uwezo wetu. Kwa kuepukana na deni na kuhifadhi pesa sasa, tunajitayarisha kwa huduma ya muda wote wa Kanisa katika miaka ijayo. Dhamira ya kujitegemea kimaisha na kiroho ni kujiweka katika sehemu panda ili kuweza kuinua wengine wenye mahitaji.
Kama tu vijana au wazee, kile tunachofanya leo kinabainisha huduma tutakayoweza kutoa na kufurahia kesho. Kama vile mshahiri unavyotukumbusha, “Kwa maneno yote yenye huzuni ya ulimi ama kalamu, ya kuhuzunisha zaidi ni haya: ‘Pengine ingekuwa!’” 12 Acha tusiishi maisha yetu kwa kujuta kile tuliofanya ama kutofanya!
Wapendwa ndugu na dada, kijana mdogo aliyeongelewa na Mwokozi, yule tunayemtambua kama mwana mpotevu, aliweza kurudi nyumbani. Baba yake hakuweza kumsahau; baba yake alikuwa akigojea. Na “alipokuwa [mwana] angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio, … akambusu sana.” 13 Kwa heshima ya kurudi kwa mwanaye, aliitisha vazi bora, pete, na sherehe kwa ndama 14 aliyenona—ukumbusho kwamba hakuna baraka tutakayo nyimwa ikiwa tutavumilia kwa uaaminifu katika kutembea njiani kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni.
Kwa upendo wake na upendo wa Mwanawe moyoni mwangu, Natoa changamoto kwa kila mmoja wetu kufuata mapenzi yetu ya kiroho na kuzingatia moyoni mwetu. Jiongeleshe mwenyewe kwenye kioo na jiulize, “Nasimamia wapi kwa kuishi maagano yangu?” Tuko kwenye njia sahihi tunapoweza kusema, “Nashiriki sakramenti kitakatifu kila wiki, nastahili kumiliki sifu ya hekalu, na najitolea kuhudumia na kwa bariki wengine.”
Nashiriki ushuhuda wangu kwamba Mungu anampenda kila mmoja wetu “hata akamtoa Mwanawe pekee” 15 ili alipie dhambi zetu. Anatujua na anatugojea, hata tukiwa mbali na Yeye. Tunapotenda kulingana na hamu yetu na kuzingatia moyoni mwetu, “tutazingirwa milele katika mikono ya upendo wake” 16na kukaribishwa nyumbani. Hivyo nashuhudia katika jina takatifu la Mwokozi wetu, Yesu Kristo, amina.