Familia zilizo chini ya Agano
Hakuna chochote ambacho kimekuja au kitakuja katika familia yako kilicho muhimu kama baraka za ufunganisho.
Nafurahia kukutana nanyi hapa katika mkutano huu ambao wenye ukuhani wa Mungu wote katika ulimwengu wamealikwa. Tumebarikiwa kusimamiwa na Rais Thomas S. Monson. Kama Rais wa Kanisa, yeye ni mtu mmoja aliye hai ambaye ana majukumu ya funguo ambazo ufunganisha familia na maagizo yale yote ya ukuhani muhimu kwa kupokea uzima wa milele, kikuu cha vipawa vyote vya Mungu.
Kuna baba anayesikiliza leo ambaye amekuja kutoka katika kutoshiriki kikamilifu kwa sababu yeye anataka hakikisho la kipawa hicho kwa moyo wake wote. Yeye na mkewe wanapenda watoto wao wawili wadogo kijana na msichana. Kama vile wale wazazi wengine anaweza kutambua furaha ya mbinguni anaposoma maneno haya: “Na kwamba uhusiano huu huu uliopo miongoni mwetu hapa utakuwepo miongoni mwetu kule, isipokuwa utazidishiwa utukufu wa milele, utukufu ambao sasa hatuufaidi.” 1
Huyu baba anayesikiliza pamoja nasi jioni ya leo anajua mapito hadi ule mwisho mtukufu. Sio rahisi. Yeye anajua hivyo tayari. Ilihitaji imani katika Yesu Kristo, hakikisho la kina na mabadiliko ya moyo ambayo huja kwa askofu mkarimu akimsaidia yeye kuhisi upendo wa Bwana wa msamaha.
Mabadiliko ya ajabu yanaendelea jinsi anapoenda kwenye hekalu takatifu kwa endaumenti ambayo Bwana alielezea kwa wale aliwapatia uwezo katika hekalu la kwanza katika kipindi hiki. Ilikuwa katika Kirtland, Ohio. Bwana alisema kulihusu:
“Kwa hivyo, kwa sababu hii, niliwapa amri kuwa yawapasa kwenda mto Ohio; na huko nitawapa sheria yangu; na huko mtajaliwa uwezo kutoka juu;
“Na kutoka huko, …. kwani ninayo kazi kubwa inayosubiri, kwani Israeli ikombolewe, nami nitawaongoza kokote nitokako, na hakuna mamlaka yatakayozuia mkono wangu.” 2
Kwa rafiki yangu ambaye majuzi alirudi katika ushiriki kamili na kwa wa ukuhani wote, kazi kuu mbele yetu ni kuongoza katika kuokoka sehemu ya Israeli ambayo kwayo tuna au tutakuwa na majukumu, familia yetu. Rafiki yangu na mke wake alijua kwamba hiyo ilihitaji kufunganishwa kwa uwezo wa Ukuhani wa Melkizedeki katika hekalu takatifu la Mungu.
Yeye aliniuliza mimi niwafunganishe. Yeye na mkewe walitaka ifanyika upesi iwezekanavyo. Kwa sababu ya shughuli nyingi za mkutano mkuu uliokuwa unakaribia. Niliwaachia hao wenzi, askofu wao na karani wangu kushughulika kutafuta siku iliyofaa.
Cha kushangaza na kufurahisha kwangu ilikuwa wakati huyu baba aliniambia siku ya kufunganishwa ni Aprili 3. Hiyo ndio siku mnamo 1836 wakati Eliya, nabii alyeuhishwa,alitumwa katika Hekalu la Kirtland kupeana uwezo wa kufunganisha kwa Joseph Smith na kwa Oliver Cowdery. Hizi funguo zipo katika Kanisa leo na zitaendelea hadi mwisho wa nyakati. 3
Ni mamlaka matakatifu yale yale yaliyopatianwa na Bwana kwa Petero kama Yeye aliyoahidi: “Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.”4
Kurudi kwa Eliya kulibariki wote ambao wanamiliki ukuhani. Mzee Harold B. Lee alisema wazi alipokuwa anaogea katika mkutano mkuu, akumnukuu Rais Joseph Fielding Smith. Sikilizeni kwa makini: “Mimi nina ukuhani; ninyi ndugu mlio hapa muna ukuhani; tumepokea Ukuhani wa Melkizedeki---ambao ndio ulikuwa na Eliya na wale manabii wengine na Petero, Yakobo, Yohana. Ilhali tuna mamlaka ya kubatiza, hali tuna mamlaka ya kuwekelea mikono kwa kipawa cha Roho Mtakatifu na kutawaza wengine na kufanya mambo yote haya, bila uwezo wa kufunganisha hatuwezi kufanya lolote, kwani hakutakuwa na uhalali wowote kwa yale tumefanya.”
Rais Smith aliendelea:
“Maagizo ya juu, baraka kuu, ambazo ni muhimu kwa kuinuliwa katika ufalme wa Mungu … na ambazo zinaweza kupatikana tu katika mahali fulani, …. hakuna mtu aliye na haki ya kutenda pasipo yeye kupokea mamlaka ya kufanya hivyo kutoka kwa mtu anayeshikilia funguo hizi …
Hakuna mtu katika uso wa ulimwengu huu ambaye ana haki kwenda na kuhudumu katika maagizo yoyote ya injili hii isipokuwa Rais wa Kanisa, ambaye ana funguo hizi, hutoa idhini. Yeye hutupatia sisi mamlaka; yeye uweka uwezo wa kufunganisha katika ukuhani wetu kwa sababu yeye anashikilia funguo hizo.” 5
Hakikisho hilo hilo lilikuja kutoka kwa Rais Boyd K. Packer alipoandika kuhusu uwezo wa kufunganisha. Kujua maneno haya ni kweli kunanipatia faraja, kama itakavyokuwa kwa ile familia nitakayofunganisha Aprili 3: “Petero alikuwa ashikilie funguo hizi. Petero alikuwa ashikilie uwezo wa kufunganisha,... wa kufunga au kufunganisha hapa ulimwenguni au kufunguanisha ulimwenguni na itakuwa hivyo mbinguni. Hizi funguo ni za Rais wa Kanisa---nabii, mwonaji, na mfunuaji. Uwezo mtakatifu wa kufunganisha upo katika Kanisa sasa. Hakuna kinachukuliwa kwa umakini mtakatifu sana na wale wanaoelewa umuhimu wa mamlaka haya. Hakuna kinachoshikiliwa sana. Kuna wanaume wachache ambao [wanashikilia] huu uwezo wa kufunganisha hapa ulimwenguni katika wakati fulani ---katika kila hekalu kuna ndugu ambao wamepatiwa uwezo wa kufunganisha. Hakuna anayeweza kuzipata pasipo kutoka kwa nabii, mwonaji, na mfunuaji na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.”6
Katika kuja kwa Eliya, sio tu uwezo ulipatianwa kwa ukuhani bali, pia mioyo iligeuzwa: “Roho, uwezo, na wito wa Eliya ni, kwamba una uwezo wa kushikilia funguo za ufunuo, maagizo, mausia, uwezo na endaumenti za ujalivu wa Ukuhani wa Melkizedeki na ufalme wa Mungu hapa ulimwenguni; na kupokea, kupata, na kutenda maagizo yote yanayohusika na ufalme wa Mungu, hata kugeuza mioyo ya baba kwa watoto, na mioyo ya watoto kwa baba, hata wale ambao walio mbinguni.”7
Hisia hiyo ya moyo wake kugeuka tayari imekuja kwa rafiki yangu na familia yake. Inaweza kuja kwako katika mkutano huu. Unaweza kuwa umeiona akilini mwako, kama mimi nilivyoona, uso wa baba au mama yako. Inaweza kuwa ilikuwa dada au kaka. Inawezakuwa ni binti au mwana.
Wanaweza kuwa katika ulimwengu wa roho au mabara ya mbali sana nawe. Lakini shangwe inayotokana na hisia ambayo inakuunganisha wa wao ni sahihi kwa sababu wewe umewezaau unaweza kufunganisha na wao kwa maagizo ya ukuhani ambayo Mungu ataheshimu.
Wenye Ukuhani wa Melkizedeki ambao ni kina baba katika familia zilizofunganishwa wamefundishwa kile sharti wafanye. Hakuna chochote kilichokuja au kitakachokuja katika familia yako kilicho muhimu kama baraka za ufunganisho. Hakuna kilicho muhimu zaidi kuliko kuheshimu maagano ya ndoa na familia uliyofanya au utakayofanya katika mahekalu ya Mungu.
Njia ya kufanya hivyo ni wazi. Roho Mtakatifu wa Ahadi, kupitia utii wetu na kujitolea kwetu, sharti tufunganishe maagano yetu ya hekalu ili tuweze kuyapata katika ulimwengu ujao. Rais Harold B. Lee alielezea kile kinachomaanisha kufunganishwa na Roho Mtakatifu wa Ahadi, katika kumnukuu Mzee Melvin J. Ballard: “Tunaweza kuwadanganya watu lakini hatuwezi kumdanganya Roho Mtakatifu, na baraka zetu hazitakuwa za milele zisipofunganishwa pia na Roho Mtakatifu wa Ahadi. Roho Mtakatifu ndiye anayesoma mawazo na mioyo ya binadamu na hutoa idhinisho lake kwa baraka zilizotajwa juu ya kichwa chao. Kisha zitafunganishwa, ni halali, na ni nguvu kamili.” 8
Wakati Dada Eyring nami tulifunganishwa katika Hekalu la Logan Utah, sikuelewa vyema umuhimu kamili wa ahadi hiyo. Bado ninajaribu kuelewa yote yanavyomaanisha, lakini mke wangu nami tuliamua mwanzoni wa karibu miaka 50 ya ndoa kualika Roho Mtakatifu jinsi tulivyoweza katika maisha yetu na katika familia yetu.
Kama baba kijana, aliyefunganishwa katika hekalu na kwa moyo uliogeuzwa kwa mke wangu na familia, nilikutana na Rais Joseph Fielding Smith kwa mara ya kwanza. Katika chumba cha baraza cha Urais wa Kwanza, ambako nilikuwa nimealikwa, ukaja ushahidi halisi kwangu kama Rais Harold B. Lee alinuliza, akiashiria Rais Smith, ambaye alikuwa ameketi karibu naye, “Je! Unaamini kwamba mtu huyu anaweza kuwa Nabii wa Mungu?”
Rais Smith alikuwa ameingia chumbani na alikuwa hajaongea neno bado. Ninashukrani milele kwamba niliweza kusema kwa sababu ya kile kilichotoka ndani ya moyo wangu, “Najua yeye ndiye” na nilijua kwa hakika kama ninavyojua jua lilikuwa linaangaza kwamba alikuwa anashikilia uwezo wa ukuhani wa kufunganisha kwa ulimwengu wote.
Uzoefu huu ulipatia maneno yake nguvu sana kwangu na mke wangu, katika mkutano mkuu wa Aprili 6,1972, Rais Joseph Fielding Smith alitoa ushauri ufuatao: “Ni mapenzi ya Bwana kuimarisha na kuhifadhi kitengo cha familia. Tunawasihi kina baba wachukue nafasi yao kamili kama vichwa vya nyumba. Tunawaomba kina mama kuwakubali na kuwahimili waume wao na kuwa nuru kwa watoto wao.”9
Acha nitoe ushauri wa mambo manne mnayoweza kufanya kama baba mwenye ukuhani kuinua na kuongoza familia yako tena kuwa na Baba wa Mbinguni na Mwokozi.
Kwanza, pata na uwe na ushahidi halisi kwamba funguo za ukuhani zipo kwetu na zinashikiliwa na Rais wa Kanisa. Ombea hivyo kila siku. Jibu litakuja kwa ongezeko katika azimio la kuongoza familia yako, katika hisia za matumaini, na kwa furaha kuu katika huduma yako. Utakuwa mwenye tabasamu na matumiani; baraka kuu kwa mke wako na familia.
Jambo la pili kuu ni kumpenda mke wako. Itachukua imani na unyenyekevu kuweka matakwa yake juu ya yako mwenyewe katika jitihada za maisha. Una majukumu ya kukidhi na kulea familia pamoja na yeye huku ukuhudumia wengine. Haya wakati mwengine yatatumia nguvu na uwezo ulionao. Uzee na ugonjwa unaweza kuongezea mahitaji ya mke wako. Kama unachagua hata kuweka mahitaji yake juu ya furaha yako mwenyewe, nakuahidi kwamba upendo wako kwake utaongezeka.
Tatu, uliza familia yote ipendane mmoja kwa mwengine. Rais Ezra Taft Benson alifunza:
Katika hali ya milele, wokovu ni jambo la familia. …
Juu ya yote, watoto wana haja ya kujua na kuhisi wanapendwa, wanatakikana, na wanatambuliwa. Wanataka kuhakikishiwa kila mara. Kwa kweli, huu ni wajibu wa wazazi wa kutenda hivi, na sana sana mama anaweza kufanya vizuri sana,”10
Lakini chanzo kingine muhimu cha hisia hii ya kupendwa ni upendo kutoka kwa watoto wengine katika familia. Utunzaji wa kila mara wa kaka na dada wa mmoja kwa mwengine utakuja tu kwa juhudi za kila mara za wazazi na usaidizi wa Mungu. Unajua kwamba hii ni kweli kutokana na uzoefu katika familia yako mwenyewe. Inathibitishwa kila mara unaposoma mizozo ya familia aliyowakumba watu wema Lehi na mkewe, Saria, katika Kitabu cha Mormoni imeandikwa.
Ufanisi waliopata unatupatia mwongozo. Walifunza injili ya Yesu Kristo vyema sana na kila mara hata kwamba watoto na hata uzao kizazi hata kizazi kililainisha mioyo yao kwa Mungu na mmoja kwa mwengine. Kwa mfano, Nefi na wengine waliandika na kuwatafuta wanafamilia ambao walikuwa wamekuwa adui zao. Roho wakati mwingine ulainisha mioyo na maelfu na kugeuza chuki kuwa upendo.
Njia moja unaweza kuleta ufanisi kama Baba Lehi ni kwa njia ya unavyoongoza maombi ya familia na wakati wa familia, kama vile jioni ya familia nyumbani. Wapatie watoto nafasi za kuomba wanapoweza kuwaombeana mmoja na mwengine katika duara ambao wanahitaji baraka. Tambua upesi vyanzo vya utata na tambua matendo ya huduma isiyo na choyo, hasa mmoja kwa mwengine. Wanapoombeana mmoja kwa mwengine na kuhudumiana, mioyo italainika na kugeuzwa kwa mmoja kwa mwengine na kwa wazazi wao.
Nafasi ya nne ni kuongoza familia yako katika njia ya Bwana huja wakati nidhamu inahitajika. Tunaweza kufikia majukumu yetu kwa kukosoa katika njia ya Bwana na kisha kuwaongoza watoto wetu hata maisha ya milele
Utakumbuka maneno, labda haujapata kuona uwezo wake kwa mwenye Ukuhani wa Melkizedeki akitayarisha familia yake katika hali ile ile ambayo watakayokuwa nayo katika ufalme wa selestia. Unakumbuka maneno haya. Yanafaamika sana:
“Hakuna nguvu au uwezo unaoweza au upaswao kudumishwa kwa njia ya ukuhani, isipokuwa tu kwa njia ya ushawishi, kwa uvumilivu, kwa upole na unyenyekevu, na kwa upendo usio unafiki;
“Kwa wema, na maarifa safi, ambayo yataikuza sana nafsi isiyo na unafiki, na isiyo na hila—
“Kukemea kwa ukali kwa wakati wake, utakapokuwa umeongozwa na Roho Mtakatifu; na halafu baadaye kuonyesha ongezeko la upendo kwa yule uliyemkemea, asije akakudhania wewe kuwa ni adui yake;
“Ili apate kujua kwamba uaminifu wako ni imara zaidi kuliko kamba za mauti.”11
Na baadaye ahadi inatokea ya thamani kuu kwetu sisi kama kina baba katika Sayuni: “Roho Mtakatifu atakuwa mwenzi wako daima, na fimbo yako ya kifalme fimbo isiyobadilika ya haki na ukweli; na utawala wako utakuwa utawala usio na mwisho, na usio wa njia ya kulazimisha utatiririka kwako milele na milele.”12
Hicho ni kiwango cha juu kwetu, lakini tunapokuwa na imani ikidhibiti hasira zetu na kuzima kiburi chetu, Roho Mtakatifu hutoa idhinisho Lake, na ahadi takatifu na maagano yanakuwa halisi.
Utafanikiwa kupitia imani yako kwamba Bwana alituma tena funguo za ukuhani ambapo zipo kwetu--- kwa kanda halisi za upendo kwa mke wako, kwa usaidizi wa Bwana katika kugeuza mioyo ya watoto wako kwa kila mmoja na kwa wazazi wao, na kwa upendo ukikuelekeza kukosoa na kusihi katika njia ya kualika Roho.
Najua kwamba Yesu ndiye Kristo na ni Mwokozi wetu, Nashuhudia kwamba Rais Thomas S. Monson, anashikilia na kutumia funguo zote za ukuhani ulimwenguni leo. Nampenda na kumbubali yeye. Nawapenda na kuwaombea. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.