Agano Jipya 2023
Agosti 14–20. Warumi 7–16: “Ushinde Ubaya kwa Wema”


“Agosti 14–20. Warumi 7–16: ‘Ushinde Ubaya kwa Wema,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Agosti 14–20. Warumi 7–16,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
magofu ya Rumi ya kale

Agosti 14–20

Warumi 7–16

“Ushinde Ubaya kwa Wema”

Ni kanuni chache tu za injili katika Warumi 7–16 zinaweza kujumuishwa kwenye muhtasari huu, kwa hiyo usijiwekee mipaka kwenye kile kilichoshughulikiwa hapa. Zingatia mwongozo wa kiungu unaopokea pale unapojifunza.

Andika Misukumo Yako

Alipofungua waraka wake kwa Warumi, Paulo aliwasalimu waumini wa Kanisa kwa kuwaita “wapendwao na Mungu” “walioitwa kuwa watakatifu.” Alisema kwamba “imani yao [ilikuwa] inahubiriwa katika dunia nzima” (Warumi 1:7–8). Japokuwa Paulo alitumia sehemu kubwa ya waraka wake kusahihisha mawazo ya uongo na tabia zenye dosari, inaonekana alitaka pia kuwahakikishia waongofu hawa wapya wa Kikristo kwamba wao kweli walikuwa Watakatifu wapendwao na Mungu. Ushauri wake nyororo hutubariki sisi wote ambao tunahangaika kuhisi upendo wa Mungu na kwa wale wanaokuwa Watakatifu wanaweza kuhisi kuwa hauwezi kufikika. Kwa unyenyekevu wa maono kwa ajili yao, Paulo alikiri kwamba amejihisi kama “maskini” wakati fulani (Warumi 7:24), lakini injili ya Yesu Kristo ilimpa nguvu ya kushinda dhambi (ona Tafsiri ya Joseph Smith, Warumi 7:22–27 [katika kiambatisho cha Biblia]). Kwa nguvu hizo, nguvu za kukomboa za Mwokozi, tunaweza “kuushinda ubaya”—wote ubaya katika ulimwengu na ubaya ndani yetu wenyewe—“kwa wema” (Warumi 12:21).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Warumi 7–8

Wale ambao wanamfuata Roho wanaweza kuwa “warithi pamoja na Kristo.”

Hata baada ya kuingia katika “upya wa uzima” kupitia ibada ya ubatizo (Warumi 6:4), pengine umehisi baadhi ya vita vya ndani Paulo alivyovielezea katika Warumi 7—“kupigana vita” kati ya mwanadamu wa tabia ya asili na matamanio yenu ya haki (Warumi 7:23). Lakini Paulo pia alizungumza juu ya matarajio katika Warumi 8:23–25. Ni sababu zipi za matarajio haya unazipata katika sura ya 8? Unaweza pia kutafuta baraka zinazokuja kutokana na “Roho wa Mungu kukaa ndani yako” (Warumi 8:9). Ni kwa jinsi gani unaweza kutafuta wenza wa Roho Mtakatifu kwa utimilifu zaidi katika maisha yako?

Warumi 8:16–39

Kipawa cha utukufu wa milele kinapita majaribu yangu duniani.

Miaka michache tu baada ya Paulo kuandika waraka huu, Watakatifu katika Rumi walipata mateso ya kutisha. Je, unapata nini katika Warumi 8:16–39 ambacho kiliweza kuwasaidia Watakatifu hawa wakati mateso yalipokuja? Ni kwa jinsi gani maneno haya yanaweza kutumika kwako na majaribu unayokabiliwa nayo sasa?

Tafuta uhusiano kati ya mistari hii na ushauri huu kutoka kwa Dada Linda S. Reeves: “Sijui ni kwa nini tuna majaribu haya mengi tuliyonayo, lakini ni hisia yangu binafsi kwamba thawabu ni kubwa sana, ambayo ni ya milele na ya kudumu milele, ya furaha na ya kupita uelewa wetu kwamba katika siku ile ya thawabu, tuweze kujisikia kusema kwa Baba yetu mpendwa, mwenye rehema, ‘Je, hayo ndiyo yote yaliyohitajika? Ninaamini kwamba kama kila siku tutakumbuka na kutambua kina cha upendo ule Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu walio nao kwetu, tutakuwa radhi kufanya chochote ili kurudi katika uwepo Wao tena, tukizungukwa na upendo Wao milele. Hatutajali … kile tulichoteseka hapa kama, mwishoni, majaribu hayo ndicho kitu hasa kinachotupasisha sisi kwa ajili ya uzima wa milele na kuinuliwa katika ufalme wa Mungu tukiwa na Baba yetu na Mwokozi wetu?” (“Kustahili Baraka Zetu Tulizoahidiwa,” Liahona, Nov. 2015, 11). Amua nini utafanya “kila siku ili kukumbuka na kutambua” upendo wa Mungu kwako.

Warumi 8:29–30; 9–11

Je, Paulo alimaanisha nini kwa “chaguliwa tangu asili,” “chaguliwa,” na “jua tangu asili”?

Paulo alitumia maneno “chaguliwa tangu asili,” “chaguliwa,” na “jua tangu asili” ili kufundisha kwamba kabla ya maisha haya, Mungu aliwachagua baadhi ya watoto Wake kuwa sehemu ya Israeli, watu Wake wa agano. Hii ilimaanisha wangepokea baraka na majukumu maalumu ili kwamba waweze kubariki mataifa yote ya ulimwengu (ona Mwongozo wa Maandiko, “Uchaguzi,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Hata hivyo, Paulo alisisitiza katika Warumi 9–11 kwamba watoto wote wa Mungu wanaweza kuwa watu Wake wa agano, na watapokea uzima wa milele kwa njia hiyo hiyo—kupitia imani katika Yesu Kristo na utiifu kwa amri Zake.

Ona pia Waefeso 1:3–4; 1 Petro 1:2; Alma 13:1–5; Mada za Injili, “Kuchaguliwa Tangu Mwanzo,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

Warumi 12–16

Paulo ananialika kuwa Mtakatifu na mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo.

Sura tano za mwisho za Warumi zina idadi kubwa ya maelekezo mahususi kuhusu kuishi kama Watakatifu. Njia mojawapo ya kujifunza maelekezo haya ni kutafuta mada ambazo zinajirudia rudia. Ni kwa jinsi gani ungeweza kufanyia muhtasari ushauri wa Paulo?

Hautaweza kutumia ushauri huu wote kwa mara moja, lakini Roho anaweza kukusaidia kupata kanuni moja au mbili ambazo ungeweza kuanza kuzifanyia kazi leo. Shiriki matamanio yako kwa Baba yako wa Mbinguni katika sala, na omba msaada Wake.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Warumi 8:31–39.Tunapata nini katika Warumi 8:31–39 ambacho kinafundisha kuhusu jinsi Baba wa Mbinguni na Yesu wanavyohisi kutuhusu sisi? Ni lini tulihisi upendo wa Mungu?

Ili kuelezea mstari 38–39, wanafamilia wangeweza kutafuta mifano ya vitu ambavyo, kama vile sisi na upendo wa Mungu, haviwezi kutenganishwa.

Picha
baba na binti wakicheza densi

Mzee Wilford W. Andersen alifundisha, “Muziki wa injili ni hisia ya furaha ya kiroho.”

Warumi 9:31–32.Ujumbe wa Mzee Wilford W. Andersen “Muziki wa Injili” (Liahona, Mei 2015, 54–56; ona pia video kwenye ChurchofJesusChrist.org) unaweza kusaidia kuelezea kile Paulo anachofundisha kuhusu sheria, matendo, na imani. Baada ya kujadili hotuba yake, familia yako inaweza kujaribu kucheza densi pakiwepo na muziki au bila muziki kuwepo. Ni kwa jinsi gani imani inaweza kutusaidia kupata shangwe ya injili?

Warumi 10:17.Wekea alama glasi kadhaa za maji kwa vyanzo vya neno la Mungu (kama maandiko, ufunuo binafsi, na mkutano mkuu). Jadili ni kwa jinsi gani neno la Mungu linaongeza imani yetu unapomimina kila glasi katika chombo chenye kitambulisho “Imani.”

Warumi 12.Inamaanisha nini kujitoa sisi wenyewe kuwa “dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu”? (mstari wa 1).

Warumi 14:13–21.Familia yako ingeweza kunufaika kwa kujifunza ushauri wa Paulo kuhusu kuhukumu na kubishana juu ya mapendeleo binafsi? Pengine mnaweza kujadili njia sahihi za kujibu wakati watu wengine, ikijumuisha wanafamilia, wanapofanya chaguzi ambazo zinatofautiana na zenu. Ni kwa jinsi gani tunaweza “kufuata mambo yaletayo amani”? (mstari wa 19).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “I Feel My Savior’s Love,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Waruhusu watoto waoneshe ubunifu wao. Wakati unapowaalika watoto kubuni kitu kinachohusiana na kanuni ya injili, unawasaidia kuelewa vyema kanuni hiyo. … Waruhusu kujenga, kuchora, kupaka rangi, kuandika, na kubuni” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

Picha
Kristo akiwa amenyoosha mikono

Kaa Nami, na Del Parson

Chapisha