Agano Jipya 2023
Julai 31–Agosti 6. Matendo ya Mitume 22–28: “Mtumishi na Shahidi”


“Julai 31–Agosti 6. Matendo ya Mitume 22–28: ‘Mtumishi na Shahidi’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Julai 31–Agosti 6. Matendo ya Mitume 22-28,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Paulo akiwa gerezani

Julai 31–Agosti 6

Matendo ya Mitume 22–28

“Mtumishi na Shahidi”

Soma Matendo ya Mitume 22–28 kwa maombi moyoni mwako kwamba Roho Mtakatifu akupe mwongozo wa kiungu ili kujua kile unachotakiwa kuzingatia juu yake ambacho kitawasaidia washiriki wa darasa lako. Andika mawazo yoyote yanayokuja akilini; haya yanaweza kuwa mwanzo wa mpango wako wa kufundisha

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waombe washiriki wa darasa kuandika andiko la rejeo kutoka Matendo ya Mitume 22–28 ambalo limewavutia wiki hii. Kusanya majibu yao na usome baadhi ya mistari hiyo kwa pamoja. Alika washiriki kadhaa wa darasa kuelezea ni kwa nini mistari hii ni ya maana kwao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Matendo ya Mitume 22:1–21; 26:1–29

Ushuhuda ni tangazo juu ya ukweli kulingana na uelewa au imani ya mtu binafsi.

  • Ushuhuda wa Paulo kwa Festo na Mfalme Agripa unaweza kuwa ni fursa ya kujadili kile kutoa ushuhuda humaanisha nini. Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kurejelea Matendo ya Mitume 22:1–21 na 26:1–29. Tunajifunza nini kutokana na mfano wa Paulo kuhusu kutoa ushuhuda? Ni kanuni gani za ziada kuhusu kutoa ushuhuda tunazojifunza kutokana na maelezo ya Rais M. Russell Ballard katika “Nyenzo za Ziada”? Kuimba au kupiga wimbo “Ushuhuda” (Nyimbo za Kanisa, na.137) kunaweza kusaidia kumwalika Roho katika majadiliano yenu.

  • Ingawa Paulo hakuwa akitafuta ushahidi wa kiroho alioupokea akiwa njiani kwenda Dameski, alitumia maisha yake yote yaliyobakia akifanya kazi kuutunza na kuulinda ushuhuda wake (ona Matendo ya Mitume 22:10, 14–16; 26:19). Mfano wa Paulo unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa kwamba ushuhuda huhitaji matendo na dhabihu. Ili kuanza majadiliano kuhusu hili, pengine mshiriki wa darasa angeweza kuelezea jitihada zake katika kuwa mwanamuziki hodari, mwana sanaa au mwana riadha. Ni kwa namna gani kukuza ujuzi wa jinsi hii ni sawa na kupata na kuimarisha ushuhuda? Ni juhudi gani lazima tufanye ili kupata na kuimarisha ushuhuda? (ona pia Alma 5:46).

Matendo ya Mitume 26:9–23

Tunao wajibu wa kuwatumikia wengine.

  • Bwana alimwita Paulo kuwa “mtumishi” (Matendo ya Mitume 26:16), lakini neno hili linamaanisha nini? Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuchunguza ni kwa jinsi gani wanaweza kuwatumikia wengine, wawe na au bila wito maalumu, ungeweza kuandika kwenye ubao swali kama Kutumikia kunamaanisha nini? Alika washiriki wa darasa kutafuta majibu katika nyezo zifuatazo: Mathayo 20:25–28; Matendo ya Mitume 26:16–18; 3 Nefi 18:29–32; Jean B, Bingham “Kutumikia kama Mwokozi Anavyofanya,” Liahona, Mei 208, 104–7. Wakati wakielezea walichokipata, wahimize kujadili jinsi ambavyo sisi sote tunaweza kuwatumikia wengine, ikijumuisha katika miito yetu kanisani. Pia mnaweza kutazama video “The Miracle of the Roof” (ChurchofJesusChrist.org).

Matendo ya Mitume 27

Kama tutawatii manabii wa Bwana, Yeye atatuongoza na kutulinda dhidi ya uovu.

  • Waalike washiriki wa darasa kuzungumzia kuhusu jibu la yule akida wakati Paulo alipotoa unabii kuwa meli ingepata “madhara makubwa” na watu wangepotea” (ona Matendo ya Mitume 27: 10–11). Kwa nini yule akida alijibu hivyo? Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile ambacho wangesema kwa yule akida ili kumsaidia kuwa na imani katika unabii wa Paulo. Je, ni masomo gani mengine tunayojifunza kutoka Matendo ya Mitume 27 kuhusu kuwafuata watumishi wa Bwana? Yawezekana baadhi ya washiriki wa darasa lako wanao uzoefu wakati walipofuata maelekezo ya manabii hata wakati yalipopingana na maoni ya watu wanaowazunguka. Waalike washiriki wachache wa darasa kutoa uzoefu wao.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kutoa ushuhuda.

Rais M. Russell Ballard aliongelea kuhusu ushuhuda wa Paulo mbele ya Mfalme Agripa na kufundisha inamaanisha nini kwetu kutoa ushuhuda:

“Mikutano yetu ya kutoa ushuhuda inahitaji kujikita zaidi katika Mwokozi, mafundisho ya injili, baraka za Urejesho, na mafundisho ya maandiko. Tunahitaji kubadilisha hadithi, mambo ya safari, na mihadhara kwa kutoa shuhuda safi. Wale ambao wameaminiwa kuongea na kufundisha katika mikutano yetu wanahitaji kufanya hivyo kwa nguvu za mafundisho ambazo zitasikika na kugusa mioyo, wakiinua roho na kuwajenga watu wetu. …

“… Wakati daima ni vyema kuelezea upendo na shukrani, mitazamo hiyo haijumuishi aina ya ushuhuda ambao utawasha moto wa imani katika maisha ya wengine. Kutoa ushuhudia ni ‘kutoa ushahidi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu; kutoa tamko la dhati juu ya ukweli kulingana na uelewa binafsi au imani’ [Mwongozo wa Maandiko, “Shuhudia,” scriptures.ChurchofJesuChrist.org]. Tamko wazi la ukweli huleta tofauti katika maisha ya watu. Hiki ndicho kinachobadilisha mioyo. Hiki ndicho ambacho Roho Mtakatifu anaweza kukishuhudia katika mioyo ya watoto wa Mungu” (“Ushuhuda Safii,” Liahona, Liahona, Nov. 2004, 41).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jiandae Mapema. “Unapotafakari jinsi kanuni za injili unazofundisha zitakavyowabariki washiriki wa darasa lako, mawazo na misukumo itakuja katika maisha yako ya kila siku—unaposafiri kwenda kazini, unapofanya kazi za nyumbani au unapokuwa pamoja na familia na marafiki. Usifikirie maandalizi ya kiroho ni kama kitu ambacho unakitengea muda lakini kama kitu ambacho daima unakifanya” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi12).

Chapisha