Agano Jipya 2023
Agosti 21–27. 1 Wakorintho 1–7: “Muunganishwe Pamoja kwa Ukamilifu”


“Agosti 21–27. 1 Wakorintho 1–7: ‘Muunganishe Pamoja kwa Ukamilifu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Agosti 21–27. 1 Wakorintho 1–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Korintho ya zamani

Korintho, Kusini mwa Ugiriki, Baraza na Kituo cha Kisiasa, picha na Balage Balogh/www.ArchaeologyIllustrated.com

Agosti 21–27

1 Wakorintho 1–7

“Muunganishwe Pamoja kwa Ukamilifu”

Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha kwamba watu wengi “huja [Kanisani] wakitafuta tukio la kiroho” (“Mwalimu Hutoka kwa Mungu,” Ensign, Mei 1998, 26). Unaposoma 1 Wakorintho 1–7, kwa maombi fikiria unachoweza kufanya ili uweze kusaidia kutengeneza matukio ya kiroho katika darasa lako.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kuandika ni kwa namna gani wamefanyia kazi kile wanachojifunza kutoka kwenye maandiko. Waombe washiriki wachache wa darasa kuelezea walichoandika.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

1 Wakorintho 1:10–173

Waumini wa Kanisa la Kristo wanajitahidi kuwa na umoja.

  • Kujadili sura chache za mwanzo za 1 Wakorintho kunaweza kuwa ni fursa ya kujenga umoja mkubwa zaidi miongoni mwa waumini katika kata. Unaweza kuanza kwa kuwauliza washiriki wa darasa kuongelea kuhusu klabu, kikundi, timu au ushirika mwingine waliowahi kujiunga nao ambao ulikuwa na umoja mkubwa. Kwa nini kundi hili lilihisi kuwa na umoja sana? Kisha ungeweza kuchunguza baadhi ya mafundisho ya Paulo kuhusu umoja katika 1 Wakorintho 1:10–13; 3:1–11. Je, mistari hii, pamoja na uzoefu wetu, hufundisha nini kuhusu kile kinachosaidia kutengeneza umoja na kitu gani hutishia umoja huo? Ni dhabihu gani tunahitaji kufanya ili kufanikisha umoja? Ni baraka gani huja kwa wale walio na umoja? Ona pia analojia ya Dada Sharon Eubank katika “Nyenzo za Ziada.”

  • Paulo anatumia taswira ya jengo ili kuhimiza umoja katika 1 Wakorintho 3:9–17. Ni kwa namna gani analojia hii italisaidia darasa lako kuelewa vyema zaidi kuhusu umoja? Kwa mfano, baada ya kusoma mistari hii pamoja, ungeweza kumpa kila mshiriki wa darasa kitofali na acha wafanye kazi kwa pamoja ili kujenga kitu fulani. Ni kwa namna gani sisi ni “jengo la Mungu”? (1 Wakorintho 3:9). Ni kwa namna gani Mungu anamjenga kila mtu kibinafsi? Ni kitu gani sisi tunakijenga pamoja kama Watakatifu? Ni kitu gani sisi tunaweza kufanya kama kata yenye umoja ambacho tusingeweza kufanya kila mtu kibinafsi?

1 Wakorintho 1:17–31; 2; 3:18–20

Ili kutimiza kazi ya Mungu, tunahitaji busara ya Mungu.

  • Hapa kuna wazo la kulisaidia darasa lako kumtegemea Mungu: Gawa washiriki wa darasa lako katika makundi na waombe kuchunguza 1 Wakorintho 1:17–31; 2; au 3:18–20 wakitafuta maneno kama busara na upumbavu. Kisha wangeweza kushiriki katika makundi yao mistari hii inafundisha nini kuhusu kuwa na busara katika kazi ya Bwana. Ni mambo gani kuhusu injili yanaweza kuonekana ya kipumbavu kwa baadhi ya watu? Ni kwa namna gani mambo haya yanaonyesha busara ya Mungu? Labda washiriki wa darasa wangeweza pia kushiriki uzoefu ambapo walitegemea hekima ya Mungu, kuliko yao wenyewe, ili kutimiza kazi Yake.

1 Wakorintho 6:9–20

Miili yetu ni mitakatifu.

  • Kwa kuanza majadiliano juu ya mistari hii, ungeweza kuandika kwenye ubao maswali kama yafuatayo: Je, Bwana anatutaka sisi tuiangalieje miili yetu? Ni kwa namna gani hii ni tofauti na vile Shetani anavyotutaka sisi tuifikirie miili yetu? Inamaanisha nini kwamba miili yetu ni mahekalu ya Roho Mtakatifu? Waalike washiriki wa darasa kutafuta majibu ya maswali haya katika 1 Wakorintho 6:9–20 (ona pia Mafundisho na Maagano 88:15; Musa 6:8–9).

  • Mjadala wenu kuhusu utakatifu wa miili yetu ungeweza kujumuisha maongezi kuhusu sheria ya usafi wa kimwili. Labda ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa lako wanajifunza nini kutoka kwa Paulo—pia kutoka kwenye nyenzo zingine za Kanisa—ambazo zingeweza kuwasaidia kuelezea kwa wengine kwa nini usafi wa kimwili ni muhimu. Baadhi ya nyenzo hizi zinaweza kujumuisha zile zilizoorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada.”

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

“Tofauti zinaweza kugeuzwa kuwa faida.”

Dada Sharon Eubank alielezea jinsi timu za mashindano ya wapiga makasia wanavyojipatia umoja:

Wapiga makasia lazima watawale kwa ari katika uhuru na wakati huo huo kushikilia kiukweli uwezo wao binafsi. Ushindi wa mbio haupatikani kwa viumbe wasio halisi. Makundi mazuri yanafanya kazi kwa ushirikiano—mtu wa kuongoza, mtu wa kushikilia akiba, mtu wa kupigana vita, mtu wa kupatanisha. Hakuna mpiga kasia aliye na thamani kubwa kuliko mwingine, wote ni rasilimali kwenye boti, lakini ili wapige makasia vizuri, lazima kila mmoja azingatie mahitaji na uwezo wa wengine—mtu mwenye mkono mfupi anaongeza juhudi kidogo, mwenye mkono mrefu anavuta zaidi kidogo.

“Tofauti zinaweza kugeuzwa kuwa faida badala ya hasara” (“Kwa Umoja wa Hisia Tunapata Nguvu kwa Mungu,” Liahona, Nov. 2020, 56; ona Daniel James Brown, The Boys in the Boat: Nine Americans and Their Epic Quest for Gold at the 1936 Berlin Olympics [2013], 161, 179).

Baraka za usafi wa kijinsia.

Jeffrey R. Holland, “Usafi Binafsi,” Ensign, Nov. 1998, 76.

David A. Bednar, “Tunaamini katika Kuwa Wasafi Kimwili,” Liahona, Mei 2013, 42.

(Video)“Chastity: What Are the Limits?,” “I Choose to Be Pure”, ChurchofJesusChrist.org

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Shuhudia juu ya Yesu Kristo. Paulo “hakuja akiwa na ufasaha wa maneno, wala wa hekima, akitangaza … ushuhuda juu ya Mungu” (1 Corinthians 2:1). Ushuhuda wako rahisi juu ya Mwokozi unaweza kuwa na ushawishi kwa kiasi kikubwa sana.

Chapisha