Agano Jipya 2023
Desemba 4–10. Ufunuo 1–5: “Utukufu, na Ukuu, Una … Mwana Kondoo Milele”


“Desemba 4–10. Ufunuo 1–5: ‘Utukufu, na Ukuu, Una … Mwana Kondoo Milele’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2021)

“Desemba 4–10. Ufunuo 1–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Mwanakondoo amekalia nyasi

Desemba 4–10

Ufunuo 1–5

“Utukufu, na Ukuu, Una … Mwana Kondoo Milele”

Kupokea misukumo ya kiroho hukusaidia wewe kutambua kwamba Roho Mtakatifu anataka kukufundisha. Kuandika na kufuata misukumo hiyo kunaonyesha kwamba wewe unathamini na unatamani kupokea zaidi.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Unapoanza mjadala, inaweza kusaidia kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki baadhi ya jumbe walizozipata katika kitabu cha Ufunuo wakati wa kujifunza kwao binafsi au kama familia. Kwa mfano, walijifunza nini kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni wa kuwaokoa watoto Wake? Walijifunza nini kuhusu Mwokozi na nafasi Yake katika mpango huu? Wahimize washiriki wa darasa kuendelea kutafuta jumbe muhimu kuhusu Yesu Kristo na mpango huu wa wokovu wanapoendelea kusoma Ufunuo huko nyumbani. Wapatie nafasi katika darasa lijalo kushiriki kile walichopata.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Ufunuo 1

Yesu Kristo ni Mwana Aliye Hai wa Mungu Aliye Hai.

  • Picha na alama katika Ufunuo 1 kwa uwazi zinashuhudia kwamba Yesu Kristo yu hai na kwamba anaongoza Kanisa Lake. Labda washiriki wa darasa wangeandika kwenye ubao vifungu kadhaa vya maneno kutoka Ufunuo 1 ambavyo vinajumuisha taswira au alama na kushiriki kila kifungu cha maneno hayo kinawafundisha nini kuhusu Yesu Kristo. Kwa mfano, tunajifunza nini kutokana na alama hizi kuhusu namna ambavyo Kristo analiongoza Kanisa Lake leo? Ni kwa namna gani maelezo ya Yohana kuhusu Mwokozi yanalingana na yale katika Mafundisho na Maagano 110:1–4?

Ufunuo 2–3

Yesu Kristo anatujua sisi binafsi na atatusaidia kushinda changamoto zetu.

  • Kusoma jumbe za Bwana kwa matawi mbalimbali ya Kanisa katika Ufunuo 2–3 kungeweza kusaidia kuwahakikishia washiriki wa darasa kwamba Mwokozi anawatambua. Pengine ungeweza kuwaalika kuzichanganua sura hizi ili kupata ushahidi kwamba Yesu Kristo alijua majaribu na nguvu ya kila tawi. Wangeweza pia kuelezea matukio ambayo walihisi kwamba Mwokozi alikuwa akijua hali zao za kipekee. Je, ni ushauri gani Mwokozi aliutoa kwa Watakatifu hao ambao unaweza pia kutusaidia sisi kushinda mahangaiko yetu?

  • Katika sura hizi Bwana alitoa ahadi zenye mwongozo wa kiungu kwa wale wanaoshinda. Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kufanya kazi watu wawili wawili ya kupekua Ufunuo 2–3 ili kupata ahadi za Bwana. Labda pia wangechora picha ubaoni kuwakilisha baadhi ya ahadi hizi, kisha walielezee darasa kile walichopata. Je, ni kwa namna gani ahadi hizi zinatutia hamasa sisi kuendelea kujitahidi kushinda majaribu na udhaifu wetu?

Ufunuo 5

Ni Yesu Kristo pekee ambaye angeweza kufanya mpango wa Baba wa Mbinguni uwezekane.

  • Je, somo la vitendo lingeweza kulisaidia darasa lako kuelewa lugha ya alama katika Ufunuo 5 kuhusu Mwokozi kufungua kitabu kilichofungwa? Unaweza kuleta zawadi ikiwa imefungwa katika chombo kwa ajili ya kushiriki na darasa. Kabla ya darasa, kwa siri mpe mtu mmoja ufunguo wa kufuli. Elezea darasa ni kitu gani kilichomo ndani ya chombo, na waruhusu washiriki kadhaa wa darasa wajaribu kukifungua chombo kabla ya mtu mwenye funguo hajakifungua. Kisha washiriki wa darasa wangeweza kulinganisha hili somo la vitendo na Ufunuo 5. Maswali kama haya yangeweza kusaidia: Ni kwa namna gani ukombozi wa watoto wa Baba wa Mbinguni ni kama chombo kilichofungwa au kitabu kilichofungwa? Kwa nini Yesu Kristo alikuwa ndiye Mtu pekee ambaye angeweza kufungua mihuri hiyo? (Ona nukuu katika “Nyenzo za Ziada”).

  • Kama watu wenye shangwe waliosemwa katika Ufunuo 5, leo pia tunaweza kupaza sauti zetu kumsifu Mwokozi kama Mtu ambaye anastahiki kutupatia wokovu. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kuimba pamoja wimbo wa Kanisa waupendao wa sifa kuhusu Mwokozi, kama vile “Glory to God on High” (Nyimbo za Kanisa, na. 67). Washiriki wa darasa wangeweza kuzitambua kweli ambazo wimbo huu unafundisha kuhusu Yesu Kristo. Je, ni mifanano gani tunayoiona kati ya ujumbe wa nyimbo zetu za kusifu na tamko katika Ufunuo 5:9–14?

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Ni Yesu Kristo pekee ndiye angeweza kulipia dhambi zetu sisi.

Akielezea matukio katika maisha kabla ya maisha ya duniani, Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

“Kristo alijitolea kuheshimu maadili ya haki ya kujiamulia ya wanadamu wote hata wakati Yeye akilipia dhambi zao. Katika mchakato huo, Yeye angerudisha utukufu wote kwa Baba kwa upendo huo wenye kukomboa.

“Upatanisho huu usio na mwisho wa Kristo uliwezekana kwa sababu (1) Yeye alikuwa ni mtu pekee asiye na dhambi aliyewahi kuishi katika dunia hii na hivyo hakuwa chini ya kifo cha kiroho kitokanacho na dhambi, (2) Yeye alikuwa ni Mwana Pekee wa Baba na hivyo kumiliki sifa za kiungu ambazo zilimpa Yeye nguvu juu ya kifo cha kimwili, na (3) Yeye ni wazi alikuwa mtu mnyenyekevu vya kutosha na aliye kuwa tayari katika baraza la kule mbinguni kutawazwa kwenye huduma hiyo ” (“Upatanisho wa Yesu Kristo,” Liahona, Machi. 2008, 35).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho. “Bwana ametuamuru ‘kufundishana mafundisho ya ufalme’ [Mafundisho na Maagano 88:77] na kutumia maandiko ‘kufundisha kanuni za injili [Yake]’ [Mafundisho na Maagano 42:12]. Maandiko na maneno ya manabii na mitume wa siku za mwisho ndivyo chanzo cha ukweli tunaofundisha” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi21).

Chapisha