Agano Jipya 2023
Desemba 25–31. Ufunuo 15–22: “Yeye Ashindaye Atayarithi Haya”


“Desemba 25–31. Ufunuo 15–22: ‘Yeye Ashindaye Atayarithi Haya’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2021.)

“Desemba 25–31. Ufunuo 15–22,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Yesu Kristo akiwasalimia watu katika Ujio Wake wa Pili

Mji wa Milele, na Keith Larson

Desemba 25–31

Ufunuo 15–22

“Yeye Ashindaye Atayarithi Haya”

Je, vita kati ya wema na uovu vilivyoelezwa katika Ufunuo vinakufundisha nini kuhusu umuhimu wa kumfuata Kristo hapa duniani? Baada ya kutafakari kanuni hii, fikiria mahitaji ya washiriki wa darasa lako. Je, ni ukweli gani kutoka katika Ufunuo unaweza kuwasaidia kufanya chaguzi sahihi?

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wakati washiriki wa darasa lako wanapofika mwisho wa kujifunza Agano Jipya, wahimizie kushiriki mawazo yao kuhusu Agano Jipya. Waalike kushiriki jinsi kujifunza kwao maandiko kulivyowasaidia wao kumjua vyema zaidi Yesu Kristo na kuwa zaidi kama Yeye.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Ufunuo 17–18

Lazima tujitenge na uovu wa ulimwengu.

  • Haivutii hasa kusoma kuhusu uovu na kuanguka kwa Babeli Ufunuo 17–18, lakini hii inatufundisha kwa sababu Babeli inaweza kuwa ishara ya ulimwengu ulio mwovu ambamo tunaishi leo hii. Labda ungeweza kugawanya sura hizi kwa miongoni mwa washiriki wa darasa na waombe kutafuta majibu ya maswali kama haya: Ni kwa nini watu wanavutiwa na Babilonia , au mambo ya kiulimwengu? Je, ni kwa nini Babeli ni hatari? Je, kitaitokea nini kwa Babeli? Je, ni maonyo gani Yohana anatoa ili kutusadia sisi kuiepuka hatma ya Babeli?

  • Baada ya kusoma Ufunuo 18:4, washiriki wa darasa wangetaka kujadili ni kwa namna gani wanaweza “kutoka nje ya” Babeli na “kutokuwa washiriki wa dhambi zake.” Wangeweza kushiriki maandiko au ujumbe kutoka kwa viongozi wa Kanisa ambao umewasaidia wao kushinda majaribu ya Babeli au ulimwengu. Fikiria kuangalia video ya “Dare to Stand Alone” (ChurchofJesusChrist.org) au kusoma maelezo ya Mzee Quentin L Cook katika “Nyenzo za Ziada.” Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki mawazo kuhusu jinsi ya kutumia kanuni mbili alizotaja Mzee Cook. Ni katika namna gani sisi “tunatoka nje ya Babeli? (ona, kwa mfano, Isaya 52:11; Mafundisho na Maagano 25:10). Tunaweza kufanya nini ili kuwahamasisha wengine kufanya vivyo hivyo?

Ufunuo 19–20

Tunaweza kujiandaa kwa Ujio wa Pili wa Bwana na Siku ya Hukumu.

  • Ujio wa Pili wa Yesu Kristo mara nyingi huitwa “siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo” (Yoeli 2:31), na kulingana na Ufunuo 19–20, hii inaonekana kuwa na maelezo mazuri. Fikiria kuandika ubaoni baadhi ya matukio yaliyoelezwa katika Ufunuo 19:5–20:15. Waalike washiriki wa darasa kutafuta mistari ambayo inaelezea matukio haya. Je, ni kwa nini matukio haya yaliitwa makuu na yatishayo? Je, tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu Mwokozi na wale wanaomfuata? Je, tunaweza kufanya nini sasa ili kuwa miongoni mwa watakaoshangilia wakati wa Ujio Wake?

  • Ili kuleta hamasa katika mjadala kuhusu kitabu cha uzima na hukumu ya mwisho waalike washiriki wa darasa kutengeneza kitabu kwa kukunja vipande vya karatasi katika sehemu nne. Kisha wanaweza kusoma Ufunuo 20:12–15; 2 Nefi9:14; 29:11 na kutafakari kitu ambacho wao wangetaka kiandikwe kuhusu wao katika hicho kitabu cha uzima. Waalike waandike mambo hayo katika vitabu vyao, na waalike washiriki wachache kushiriki kitu walichoandika. Ni chaguzi gani tunazoweza kufanya sasa ili kwamba baadhi ya mambo haya yaandikwe katika kitabu cha uzima. Ili kukusaidia washiriki wa darasa wasihisi kukatishwa tamaa kuhusu maendeleo yao ya kiroho, fikiria kushiriki ushauri kutoka ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland “Iweni Wakamilifu—Hatimaye” (Liahona, Nov. 2017, 40–42).

Yesu pamoja na watu katika nuru kwenye mkono wake wa kulia na watu wakiwa gizani mkono wake wa kushoto

Hukumu ya Mwisho, na John Scott

Ufunuo 21:1–22:5

Kama tukiwa waaminifu, tutabarikiwa kwa kupata utukufu wa selestia.

  • Ingawa siku za mwisho zinatolewa unabii wa kujawa na uovu na majanga, thawabu ambayo Yohana aliiona kwa walio waaminifu inaipita kwa mbali sana taabu ambayo wamepata mwanzoni. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuchunguza hitimisho hili zuri la Ufunuo, ungeweza kuwaalika kurejelea Ufunuo 21:1–22:5, wakitafuta virai ambavyo vinawapa mwongozo wa kiungu wa kuhangaikia utukufu wa selestia. Je, ni ahadi gani zimetolewa kwa walio waaminifu? Je, ni kwa namna gani ufafanuzi huu unatusaidia kukabiliana na changamoto na majaribu yetu ya sasa?

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kuchagua haki badala ya uovu wa Babeli.

Mzee Quentin L. Cook alifundisha:

“Hatuwezi kuepuka ulimwengu. Maisha ya kujifungia sio suluhisho. Katika njia chanya, mchango wetu katika ulimwengu ni sehemu ya changamoto yetu na ni muhimu kama tutataka kukuza vipaji vyetu. …

… Waumini wa Kanisa wanahitajika kujihusisha katika ulimwengu katika njia zilizo chanya. Je, ni kwa namna gani basi tunaweka katika usawa hitaji la kuchangia kwa njia chanya katika ulimwengu na kutoshawishika na dhambi za ulimwengu? [Ona Mafundisho na Maagano 25:10; 59:9.] Kanuni mbili zitaleta tofauti ya kipekee.

  1. Acha watu wajue kwamba wewe hakika ni Mtakatifu wa Siku za Mwisho. …

  2. Kuwa jasiri kuhusu na kuishi kile unachokiamini” (“Masomo kutoka Agano la Kale: Ulimwenguni lakini Siyo wa Kiulimwengu.” Ensign, Feb. 2006, 54–55).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Heshimu haki yao ya kujiamulia. “Kuna uwezekano mkubwa wa watu kufanya mabadiliko ya maana katika maisha yao wakati mabadiliko hayo yanatokana na kutumia kwao wenyewe haki yao ya kujiamulia. Wakati unapotoa mialiko ya kutenda, hakikisha unaheshimu haki ya kujiamulia ya wale unaowafundisha” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi35).