“Desemba 18–24. Krismasi: ‘Habari Njema ya Shangwe Kuu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2021)
“Desemba 18–24. Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Desemba 18–24
Krismasi
“Habari Njema ya Shangwe Kuu”
Majadiliano ya injili yanakuwa na nguvu za kiroho yanapokuwa na kiini katika Yesu Kristo. Unaposoma kuzaliwa na misheni ya Yesu Kristo wiki hii, tafuta mwongozo wa kiungu kutoka kwa Roho Mtakatifu ili kujua jinsi gani unaweza kuweka kiini cha mjadala wa darasa lako kuwa juu ya Mwokozi.
Alika Kushiriki
Waalike washiriki wa darasa kuelezea kile wanachofanya au wamefanya hapo awali kibinafsi au kama familia ili kusherehekea kuzaliwa kwa Mwokozi katika njia ambayo inawasogeza karibu Naye.
Fundisha Mafundisho
Mathayo 1:18–25; Luka 1:26–38; 2:1–20
Yesu Kristo alijishusha ili kuzaliwa duniani.
-
Krismasi ni muda mzuri wa kutafakari na kusheherekea kujishusha kwa Kristo–utayari Wake kuacha “enzi ya Baba yake mbinguni, kuishi pamoja na binadamu, kufa kwa ajili ya binadamu” (“Again We Meet around the Board,” Nyimbo za Kanisa, na.186). Ili kuupa mwongozo wa kiungu mjadala juu ya mada hii, ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa walijifunza nini katika kujifunza kwao binafsi au kama familia wiki hii kuhusu Yesu Kristo alikuwa nani kabla Yeye hajazaliwa (ona Yohana 17:5; Mosia 7:27; Mafundisho na Maagano 76:12–14, 20–24; Musa 4:2). Kisha ungeweza kuonyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia wakati washiriki wa darasa wakisoma kuhusu kuzaliwa kwa Mwokozi (ona Mathayo 1:18–25; Luka 1:26–38; 2:1–20). Wahimize kushiriki mawazo na hisia zao wakati wanapolinganisha utukufu wa Mwokozi kabla ya maisha ya duniani na hali duni ya kuzaliwa Kwake.
-
Swali moja kama lile Nefi aliloulizwa na malaika katika 1 Nefi 11:16 lingeweza kuwa njia nzuri ya kuanza mjadala, ingawa ungeweza kuliuliza kwa maneno mengine. Labda ungeweza kuandika kwenye ubao Ufadhili wa Mungu ni nini? Na waombe washiriki wa darasa kutafakari swali hili wakati wakisoma 1 Nefi 11:17–33. Waombe washiriki mawazo yoyote kuhusu Mwokozi ambayo yanaelezwa na mistari hii. Je, ni picha zipi ungeweza kuonyesha kwa darasa ambazo zinaelezea matukio kutoka kwenye maisha ya Mwokozi yaliyoelezwa na Nefi? Washiriki wa darasa wangeweza pia kufikiria ufadhili wa Mwokozi wakati wakiangalia video kuhusu kuzaliwa Kwake kama “A Gift to the World,” “The Nativity,” au “He Is the Gift” (ChurchofJesusChrist.org).
-
Muziki ni njia nzuri ya kumwalika Roho katika darasa lako. Mwalike mtu kuimba wimbo wa Krismasi, au kusoma au kuimba nyimbo chache kwa pamoja kama darasa (ona Nyimbo za Kanisa, na. 201–14). Washiriki wa darasa wangeweza kutafuta virai katika nyimbo hizi na maandiko yaliyoorodheshwa na nyimbo ambayo yanaongeza shukrani zao kwa Mwokozi na utayari Wake wa kuja duniani.
Yesu Kristo alikamilisha misheni Yake, ambayo ilifanya iwezekana kwetu sisi kuurithi uzima wa milele.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujadili sababu za Yesu Kristo kuzaliwa, ungeweza kuwaalika kutafuta na kushiriki maandiko ambayo yanatoa muhtasari wa misheni Yake (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa ajili ya mifano). Labda washiriki wa darasa wangeweza kutafuta na kusoma mistari katika jozi au vikundi vidogo. Wanajifunza nini kuhusu misheni ya Mwokozi kwenye mistari waliyoipata? Je, tunajifunza nini kuhusu misheni Yake kutokana na baadhi ya majina Aliyopewa katika maandiko? (Ona Kamusi ya Biblia, “Kristo, majina ya”).
-
Washiriki wa darasa wangeweza kujifunza kuhusu misheni ya Mwokozi kwa kusoma “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume” (ChurchofJesusChrist.org) na kushirikiana maelezo wanayoyapata ambayo yanaeleza ni kwa nini Yeye alikuja duniani. Wape washiriki wa darasa muda wa kutafakari juu ya shuhuda zao juu ya Yesu Kristo na misheni Yake. Wangeweza kuelezea uzoefu binafsi au hadithi kutoka katika maisha ya Mwokozi ambazo zimeongeza imani yao Kwake au upendo wao Kwake. Je, ni kwa namna gani kujifunza Agano Jipya mwaka huu kumechangia kuufanya msimu huu wa Krismasi kuwa wa maana zaidi? Ili kurejea baadhi ya hadithi za Agano Jipya ambazo washiriki wa darasa wamejifunza mwaka huu, ungeweza kuonyesha video “For God So Loved the World” or “To This End Was I Born” (ChurchofJesusChrist.org).