Agano Jipya 2023
Desemba 11–17. Ufunuo 6–14: “Wameshinda … kwa Damu ya Mwanakondoo”


“Desemba 11–17. Ufunuo 6–14: ‘Wameshinda … kwa Damu ya Mwanakondoo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2021)

“Desemba 11–17. Ufunuo 6–14,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Yesu amesimama katikati ya nyota

Sanaa Mchanganyiko na Eric Johnson: Baraza Kuu Mbinguni, na Robert T. Barrett; kwa heshima ya star cluster ya European Space Agency

Desemba 11–17

Ufunuo 6–14

“Wameshinda … kwa Damu ya Mwana kondoo”

Joseph Smith alisema kwamba kitabu cha Ufunuo “ni moja ya vitabu vilivyo wazi zaidi ambavyo Mungu amesababisha kuandikwa” (katika Shajara, Desemba 1842–Juni 1844; Kitabu cha 2, 10 Machi 1843–14 Julai 1843, 98, JosephSmithPapers.org). Unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua kweli za wazi katika sura hizi?

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kurejelea baadhi ya utambuzi waliokuwa nao wakati wakijifunza Ufunuo 6–14, andika nambari 6 hadi 14 ubaoni. Washiriki wa darasa wanaweza kuandika pembeni ya nambari hiyo utambuzi wowote walioupata katika sura inayohusika ambao unahusiana na mtu anayeishi katika siku hizi za mwisho.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Ufunuo 6

Yesu Kristo anafungua lakiri ya kitabu.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuvuta taswira ya kitabu chenye lakiri saba (ona Ufunuo 5:1), ungeweza kuelezea kwamba hati ndefu za kizamani mara nyingi zilitiwa lakiri kwa udongo wa mfinyanzi kidogo au nta. Pete au muhuri ungegandamizwa kwenye huo udongo wa mfinyanzi au nta kabla haijakuwa ngumu, ikionyesha saini ya mamlaka ya mtu aliyefunga hati hiyo ndefu na ikimkataza mtu asiye na mamlaka kuifungua. Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki mawazo yoyote au misukumo waliyopata wakati wakisoma kuhusu kitabu hiki katika Ufunuo 6; Mafundisho na Maagano 77:6–7; na muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia. Kwa nini unafikiri ni muhimu kujua maana ya alama katika kitabu hiki? Kwa nini unadhani kwamba ni muhimu kujua kwamba Mwokozi ndiye mwenye kufungua kila moja ya lakiri za kitabu hiki? (ona Ufunuo 5:1–9).

Ufunuo 7–11

“Falme za ulimwengu huu zimekuwa falme za Bwana wetu,”

  • Ufunuo 7–11 unaweza kuwa mgumu kueleweka. Moja ya baraka ya darasa la Shule ya Jumapili ni kwamba washiriki wanaweza kusaidiana kuyaelewa maandiko. Unaweza kutengeneza orodha ya maswali ambayo washiriki wa darasa wanayo kuhusu sura hizi na waalike washiriki utambuzi na kila mmoja. Wahimize washiriki wote wa darasa—wale wanaojiona kuwa na uelewa zaidi na wale wanaojiona hawajui sana—kushiriki utambuzi kuhusu sura hizi.

  • Unaweza kuanzisha mjadala kwa kuwauliza washiriki wa darasa ni dhima gani inayojitokeza mara kwa mara waliyoipata katika Ufunuo 7–11. Wanaweza kushiriki mistari ambamo dhima hizi zinapatikana na waelezee ni kwa nini dhama hizi ni za kipekee. Kama wanahitaji msaada, ungeweza kupendekeza kwamba wasome Ufunuo 11:15–17. Ni dhima gani unazipata katika mistari hii, na ni jinsi gani dhima hii imeelezwa katika mistari mingine katika Ufunuo 7–11? Ingawa dhima hizi zinaelezea kuhusu vita na mabaa, tunapata nini ambacho kinatupatia sisi matumaini na kujiamini katika Yesu Kristo?

Ufunuo wa Yohana 12–14

Tulimshinda Shetani “kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda [wetu].”

  • Kujifunza kuhusu Vita vya Mbinguni kunaweza kutusaidia kuelewa vizuri zaidi maisha ya hapa duniani. Washiriki wa darasa wangeweza kusoma Tafsiri ya Joseph Smith, Ufunuo 12:7–11 (katika kiambatisho cha Biblia) na kubaini jinsi tulivyomshinda Shetani na jeshi lake. Ni umaizi gani mwingine tunaoupata kutoka kwenye maingizo juu ya Vita huko Mbinguni katika Kamusi ya Biblia au Mada za Injili? (topics.ChurchofJesusChrist.org). Je, tunajifunza nini ambacho kinaweza kutusaidia kumshinda adui?

  • Vita kati ya mema na mabaya inaelezwa katika Ufunuo 13–14. Je, sura ya 13 inatufundisha nini kuhusu jinsi joka anavyopigana vita hii? Kulingana na sura ya 14, je, ni kwa namna gani Mwana kondoo anapigana vita hiyo? Inaweza kuvutia kutengeneza orodha ya njia ambazo kila upande unapigana vita hii kulingana na sura hizi mbili. Je, ni mifanano na tofauti zipi unazoziona?

  • Je, inamaanisha nini kwamba Mwana kondoo “alichinjwa tangu kuwekwa kwa msingi wa dunia”? (Ufunuo 13:8; ona pia Ufunuo 5:6). Fikiria kuwasaidia washiriki wa darasa lako kupata majibu ya swali hili kwa kusoma Mosia 3:13 na Musa 7:47 kama darasa. Inamaanisha nini kumshinda Shetani “kwa damu ya Mwana kondoo”? (Ufunuo 12:11).

Ufunuo 14:6–7

“Nikamwona malaika mwingine … akiwa na injili isiyo na mwisho.”

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kujifunza kuhusu malaika wa aina nyingi ambao wamerejesha injili isiyo na mwisho kwa … wao wakaao duniani” (Ufunuo 14:12). Waalike washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza. Je, Mafundisho na Maagano 133:36–40 inatufundisha nini kuhusu Ufunuo 14:6–7? Je, ni kwa jinsi gani sisi tunashiriki katika kazi iliyotajwa na malaika katika Ufunuo 14:6–7. Ungeweza pia kuonyesha video ya “The Work of These Last Days” (ChurchofJesusChrist.org).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ni SAHIHI kusema “Sijui.” “Wakati ni kawaida kutaka kujibu kila swali, wakati mwingine ni vyema tu kusema, ‘sijui. Acha tujifunze swali hilo sisi wenyewe wiki hii, na tunaweza kulijadili wakati ujao’” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 24). Kisha waombe washiriki wa darasa kupekua maandiko na nyenzo nyingine za Kanisa kwa ajili ya kupata majibu.

Chapisha