“Novemba 27–Desemba 3. 1–3 Yohana; Yuda: ‘Mungu ni Pendo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2021)
“Novemba 27–Desemba 3. 1–3 Yohana; Yuda,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Novemba 27–Desemba 3
1–3 Yohana; Yuda
“Mungu ni Pendo”
Ni dhima na kanuni gani ambazo kwako ni za kipekee unaposoma 1–3 Yohana na Yuda? Unawezaje kuvitumia ili uweze kuwasaidia washiriki wa darasa lako?
Alika Kushiriki
Alika washiriki kadhaa wa darasa kushiriki dhima au kweli maalum ambazo kwao ni za kipekee wakati wakisoma Nyaraka za Yohana na Yuda. Ni jumbe zipi kutoka nyaraka hizi zilizokuwa na maana kwao na kwa familia zao.
Fundisha Mafundisho
1 Yohana 1:5–10; 2:3–11; 3:1–3; 4:7–21; 5:1–3
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ni mifano kamili ya nuru na upendo.
-
Unawezaje kuwasaidia wale unaowafundisha kutambua nuru na upendo wa Mungu katika maisha yao? Ungeweza kuanza kwa kuandika nuru na upendo kwenye ubao. Waombe washiriki wa darasa kushiriki maneno mengine yanayokuja akilini wakati wanapofikiria juu ya maneno haya mawili. Kila mshiriki wa darasa angeweza kisha kujisomea moja ya vipengele vya maandiko yafuatayo, akitafuta kitu ambacho mistari hii inafundisha kuhusu nuru au upendo: 1 Yohana 1:5–10; 2:3–11; 3:1–3; 4:7–12; 4:16–21; 5:1–3. Waombe wachache wao kushiriki pamoja na darasa kile wanachokipata. Ungeweza pia kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki uzoefu wakati walipohisi nuru na upendo wa Mungu.
-
Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kuangalia mwangaza kwenye dari au mwangaza unaokuja kupitia dirishani na kushiriki kile wanachojua kuhusu mwanga wa kawaida. Ni kwa namna gani mwangaza wa kawaida ni kama mwangaza wa kiroho? Washiriki wa darasa wangeweza kujisomea yafuatayo ili kupata utambuzi wa ziada wa jinsi gani Mungu na Mwanaye wanavyotoa nuru katika maisha yetu: Zaburi 27:1; Yohana 1:4–5; 1 Yohana 1:5–7; 3 Nefi 11:11; Mafundisho na Maagano 88:6–13; na wimbo wa Kanisa kuhusu Nuru, kama vile “The Lord Is My Light” (Nyimbo za Kanisa, na. 89). Washiriki wa darasa wanaweza pia kushiriki uzoefu ambapo walitafuta na kupokea mwangaza wa kiroho katika maisha yao.
1 Yohana 2:18–28; 4:3; 2 Yohana 1:7–11; 3 Yohana 1:9–11; Yuda
Ni lazima sisi “[tukae] katika mafundisho ya Kristo.”
-
Mafundisho ya Yohana na Yuda kuhusu ukengeufu yanaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuzingatia jinsi ya kushika kwa nguvu imani yao kwa Yeu Kristo. Fikiria kuwaalika nusu ya darasa kupekua kwa ajili ya kupata maelezo juu ya mafundisho ya uongo au ukengeufu katika 1 Yohana 2:18–23, 26–28; 4:3; 2 Yohana 1:7–11; 3 Yohana 1:9–11 na nusu nyingine kupekua kwa ajili ya maelezo kama haya katika Yuda. Au wangeweza kutafuta majibu ya maswali kama haya: Ni kwa namna gani Yohana na Yuda wanamwelezea mpinga kristo? (Ona pia Mwongozo wa Maandiko, “Mpinga Kristo,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Je, kuna chochote katika mistari hii ambacho kinaonekana hasa kinahusika katika changamoto tunazokumbana nazo leo? Je, ina maanisha nini “[kukaa] katika mafundisho ya Kristo”? 2 Yohana 1:9.
-
Yuda anatumia taswira ya kupendeza kuelezea walimu wa uongo au wale ambao “huyatukana mambo wasiyoyajua” (Yuda 1:10). Ungeweza kuwaalika washiriki wachache kuchora ubaoni baadhi ya taswira zilizoelezewa katika Yuda 1:12–13 wakati washiriki wengine wa darasa wakikisia ni kirai gani mtu huyo anachora. Ni kwa namna gani taswira hizi huwakilisha walimu wa uongo na wapinga Kristo? Kwa mfano, ni kwa namna gani vitendo viovu hutengeneza “mawaa katika karamu [zetu] za hisani”? Tunaweza kufanya nini ili kujilinda dhidi ya “wanaotudhihaki”? (ona Yuda 1:18–21). Ni kwa nini Yuda alipendekeza kwamba “tuwe na huruma” (Yuda 1:22) kwa wale ambao wanaidhihaki injili?
Shangwe huja pale tunapowasaidia wengine “kwenda katika kweli.”
-
Kuna uwezekano kwamba kuna watu katika darasa lako ambao wanaweza kuhusisha kile ambacho Yohana alikuwa akihisi aliposema kwamba hajapata “furaha kuu” zaidi ya kusikia kwamba Gaisa (mmoja wa “watoto wake”) alikuwa akienenda katika kweli. Washiriki wa darasa wanaweza kunufaika kutokana na kusikia uzoefu wa kila mmoja wao. Labda mngeweza kuanza kwa kusoma kwa pamoja 3 Yohana 1:1–4 na maandiko katika “Nyenzo za Ziada.” Maandiko haya yanatufundisha nini kuhusu chanzo cha shangwe ya kweli? Washiriki wa darasa wangeweza kuongea kuhusu namna walivyohisi kama wazazi, wamisionari, viongozi wa Kanisa, au walimu walipojua kwamba watu waliokuwa wakiwafundisha walikuwa wakienenda katika kweli. Ungeweza kuwasiliana na washiriki wachache wa darasa kabla ya darasa na kuwaomba kuja na picha za watu ambao walisaidia kuwaleta kwa Kristo na kuzungumzia kuhusu uzoefu wao.