Agano la Kale 2022
Aprili 11–17. Pasaka: “Atameza Mauti hata Milele”


“Aprili 11–17. Pasaka: ‘Atameza Mauti hata Milele,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Aprili 11–17. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
kaburi pamoja na jiwe likiwa limeviringishwa mbali kutoka kaburini

Kielelezo cha kaburi tupu na maryna Kriuchenko

Aprili 11–17

Pasaka

“Atameza Mauti hata Milele”

Unapojiandaa kufundisha siku ya Jumapili ya Pasaka, fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata shukrani za kina kwa ajili ya, na ushuhuda wa dhabihu ya upatanisho wa Yesu Kristo na Ufufuko.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Pengine ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki kile wao au familia zao walichofanya kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo na Upatanisho wake wakati wa majira ya Pasaka.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Kwa sababu Mwokozi alishinda kifo, sisi vilevile tutaishi tena.

  • Kwa vile leo ni Jumapili ya Pasaka, fikiria kurejea upya maelezo ya maandiko ya Pasaka ya kwanza—Kufufuka kwa Yesu Kristo (ona Yohana 20:1–17). Ungeweza kumtaka mshiriki wa darasa kueleza hadithi katika maneno yake mwenyewe. Ungeweza pia kuonesha video “He has Risen” (ChurchofJesusChrist.org). Washiriki wa darasa wanaweza pia kufurahia kuimba nyimbo kuhusu Mwokozi na kusoma maandiko yanayohusiana (marejeleo yameorodheshwa chini ya kila wimbo katika Nyimbo za Kanisa). Washiriki wa darasa kisha wangeshiriki vifungu wanavyovipenda kutoka kwenye nyimbo na hisia zao kuhusu Mwokozi.

  • Kusaidia darasa lako kuwa na shukrani juu ya jinsi Agano la Kale linavyoshuhudia juu ya Yesu Kristo, ungeweza kuwaomba kurejea upya maandiko kwenye jedwali kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, vilevile vifungu katika Kitabu cha Mormoni ambavyo vinafuatana na jedwali. Tunajifunza nini kuhusu Mwokozi na misheni yake kutoka katika vifungu hivi? Kwa nini ni muhimu kujua kuhusu utabiri huu?

Tunaweza kupata amani na furaha kupitia Upatanisho wa Mwokozi.

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unajumuisha orodha ya maandiko yanayoelezea amani na furaha inayokuja kupitia Yesu Kristo. Kama washiriki wa darasa walisoma maandiko haya nyumbani, watie moyo kushiriki mawazo yao na hisia kuyahusu. Au mngeweza kusoma maandiko machache kama darasa na kuzungumza kuhusu amani na furaha tunayohisi kwa sababu ya mwokozi na Upatanisho Wake. Jinsi gani tunaweza kushiriki baraka hizi na watu ambao wanaweza kuwa wanapambana kupata amani na furaha katika maisha yao? Ungeweza pia kumwomba mshiriki wa darasa kusoma ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Joy and Spiritual Survival” (Liahona, Nov. 2016, 81–84) wakati wa wiki iliyotangulia darasa na kuja darasani akiwa amejiandaa kushiriki nini ujumbe huu unafundisha kuhusu kupata furaha kwa Mwokozi.

  • Unaweza kujisikia kutiwa moyo kuongoza majadiliano kuhusu jinsi ya kuwasaidia wengine kupata amani na furaha katika Kristo. Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kufikiria kuhusu mtu fulani wanayemjua—pengine mtu fulani wanayemhudumia—ambae pengine anahitaji msaada wao, huduma, au hata kusikia tu ushuhuda wao wa Kristo na Upatanisho Wake. Watie moyo washiriki wa darasa warejelee kwenye maandiko (kama vile yale katika “Nyenzo za Ziada”) wanapofikiria huduma wanayoweza kutoa au shuhuda wanazoweza kushiriki ili kuwaimarisha wale wanaowazunguka. Waombe washiriki wachache wa darasa kushiriki mawazo yao kuhusu kuhudumu kama Yesu alivyofanya.

Picha
Kristo msalabani

Grey Day Golgotha, na J. Kirk Richards

Kupitia Upatanisho Wake, Yesu Kristo ana nguvu ya kutusaidia kushinda dhambi, kifo, majaribu na udhaifu.

  • Njia mojawapo ya kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari baraka zinazokuja kupitia Upatanisho wa Mwokozi ingeweza kuwa kuandika vichwa vya habari ubaoni Dhambi, Kifo, Majaribu, na Udhaifu. Kila mshiriki wa darasa angeweza kusoma mojawapo ya maandiko yaliyoorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada” na kutakafari jinsi Mwokozi anavyotusaidia kushinda vitu vilivyoandikwa ubaoni. Washiriki wa darasa wanaweza kuandika marejeleo ya maandiko yao chini ya moja au zaidi ya vichwa vya habari ubaoni na kushiriki ushuhuda wao wa Mwokozi na Upatanisho Wake.

  • Hadithi na anolojia zinaweza kutusaidia kuelewa Upatanisho wa Kristo. Kwa mfano, ungeweza kumwomba mshiriki wa darasa kushiriki moja ya hadithi au analojia katika ujumbe wa Mzee Walter F. González “The Savior’s Touch” (Liahona, Nov. 2019, 90–92) au ujumbe wa Dada Neill F. Marriott “Abiding in God and Repairing the Breach” (Liahona, Nov. 2017, 10–12). Ni nini hadithi hizi na analojia zinatufundisha kuhusu Upatanisho wa Kristo? Waombe washiri wa darasa kufanya kazi katika jozi kufikiria juu ya hadithi au analojia zao wenyewe.

  • Tunajifunza nini kutoka mistari ifuatayo kuhusu gharama ambayo Yesu Kristo alilipa kwa ajili ya wokovu wetu: Isaya 53:3–5; Mosia 3:7; Mafundisho na Maagano 19:16–19? Ni gharama gani Baba yetu wa Mbinguni alilipa? (Ona Yohana 3:16).

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Maandiko kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Washukuru wanafunzi wako. “Usizame sana kwenye somo kiasi cha kusahau kuwashukuru wanafunzi kwa michango yao. Wanahitaji kujua ya kwamba unathamini utayari wao wa kushiriki umaizi na shuhuda zao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 33).

Chapisha