Agano la Kale 2022
Aprili 18–24. Kutoka 18–20: “Yote Ambayo Bwana Ameyasema Tutayafanya”


“Aprili 18–24. Kutoka 18–20: ‘Yote Ambayo Bwana Ameyasema Tutayafanya,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Aprili 18–24. Kutoka 18–20,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
mlima

Mlima ndani ya Misri kimapokeo uliaminika kuwa Mlima Sinai.

Aprili 18–24

Kutoka 18–20

“Yote Ambayo Bwana Ameyasema Tutayafanya”

Soma Kutoka 18–20, na andika misukumo unayopata kuhusu jinsi ya kuwasaidia washiriki wa darasa lako kujifunza kutoka kwenye sura hizi. Hata misukumo midogo inaweza kukuongoza kwenye uzoefu wa kujifunza wenye maana.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki kile ambacho walijifunza, ungeweza kuandika ubaoni 18, 19 na 20—sura walizosoma katika Kutoka wiki hii. Waombe washiriki wa darasa kuandika, karibu na kila nambari ya sura namba za mistari ambayo wangependa kuijadili kutoka katika sura ile. Wakati washiriki wa darasa wanashiriki umaizi wao, waulize washiriki wengine wa darasa kama walikuwa na umaizi kuhusu vifungu sawa na hivyo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Kutoka 18:13–26

Tunaweza kusaidia “kubeba mzigo” wa kufanya kazi ya Mungu.

  • Ungeweza kuwatia moyo darasa lako kujadili ushauri Yethro aliompa Musa (ona Kutoka 18:13–26) kwa kuwataka kufikiria kwamba wana mazungumzo na mtu fulani anayehisi kwamba miito yake ya Kanisani, wajibu wa familia, au majukumu mengine ni “mazito mno” na kwamba yeye “atadhoofika” (Kutoka 18:18). Jinsi gani ushauri katika Kutoka 18:13–26 utasaidia? Ni ushauri gani wa ziada tungeweza kushiriki kutokana na uzoefu wetu binafsi?

  • Kuzungumza kuhusu Kutoka 18:13–26 kunaweza kutoa fursa ya kujadili jinsi kuhudumia kunavyoweza kutusaidia “kubeba mzigo pamoja na” viongozi wetu katika kazi ya Bwana (Kutoka 18:22). Ni sifa gani ambazo Yethro alipendekeza kwa Musa kuzitafuta kwa hao ambao wangehudumu kama “watawala” wa watu? (Ona Kutoka 18:21). Kwa nini sifa hizo ni muhimu katika juhudi zetu za kuhudumiana? Jinsi gani kuhudumia wanafamilia, waumuni wa Kanisa, na wengine kunasaidia “kubeba mzigo” wa viongozi wetu wa Kanisa? Kama sehemu ya majadiliano yenu, ungeweza kuonesha moja ya video zinazohusiana zinazopatikana kwenye Ministering.Churchof JesusChrist.org.

    Picha
    mwanamume akisalimiana na mwanamke kwa mkono

    Kuhudumia wengine ni moja ya njia tunayoweza kushiriki katika kazi ya Bwana.

Kutoka 20:2–11.

Tunapaswa kumweka Bwana kwanza katika maisha yetu.

  • Unaweza kufikiria juu ya kazi ambayo inaenda vyema wakati tunapokamilisha hatua za muhimu kwanza? (Mifano inaweza kujumuisha kufumbua mlinganyo wa hesabu au kufuata maelezo ya upishi). Shiriki na darasa baadhi ya mifano unayoifahamu, na watake kufikiria yao wenyewe. Jinsi gani kukamilisha hatua muhimu kwanza kuna uhusiano na amri katika Kutoka 20:2–11? Ni nini amri zinatufundisha kuhusu kumweka Mungu kwanza katika maisha yetu? Ni vitu gani ambavyo tunaweza kujaribiwa kuviweka mbele Yake? (Kwa baadhi ya mifano, ona maelezo katika “Nyenzo za Ziada.”) Kurejea upya Kutoka 20:2–11 kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kufikiria juu ya msimamo wao wa kumweka Mungu kwanza.

Kutoka 20:2–17.

Mungu ni mwenye rehema.

  • Jinsi gani utaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa umuhimu wa Amri Kumi katika wakati wetu? Ungeweza kuligawa darasa katika jozi na waombe kusoma Kutoka 20:2–17 na kisha mjadiliane jinsi kutii kila amri kunavyowabariki, familia zao, na watu wanaowazunguka. Pia ungeweza kuonesha video “Obedience of the Ten Commendments” (ChurchofJesusChrist.org). Ni baraka gani Baba wa Mbinguni anatuahidi kwa kutii amri Zake? (Ona kwa mfano, Mosia 2:41). Jinsi gani amri hizi zinaonesha upendo wa Mungu kwetu?

Picha
additional resources icon

Nyenzo za Ziada

Hakuna miungu wengine.

Rais Spencer W. Kimball alifundisha kwamba kuna mliganisho kati ya kuabudu kwa kale kwa sanamu zilizochongwa na tabia za watu wa leo. Alisema:

“Kuabudu sanamu ni miongoni mwa dhambi mbaya mno. …

“Sanamu za kisasa au miungu ya uongo inaweza kuwa kwa mfano kama vile nguo, nyumba, biashara, mashine, magari, boti za starehe, na vifaa vingine vingi ambavyo hutupotosha kutoka kwenye njia ya uungu. …

“Vitu visivyoshikika vinafanya kama miungu iliyo tayari. Shahada na barua na vyeo vinaweza kuwa sanamu. …

“Watu wengi wanajenga na kuweka samani nyumbani na kununua magari kwanza—na kisha wanaona ‘hawawezi’ kulipa zaka. Wanamwabudu nani? Kwa hakika sio Bwana wa mbingu na dunia. …

“Wengi huabudu uwindaji, safari ya uvuvi, likizo, pikiniki za mwisho wa wiki na matembezi. Wengine wanazo kama sanamu zao michezo, baseball, soka, vita ya mafahali, au gofu. …

“Bado sanamu nyingine ambayo watu huabudu ni ile ya nguvu na ufahari.… Miungu hawa wa uwezo, utajiri, na wenye mahitaji mno na ni halisi hasa kama ndama wa dhahabu wa wana wa Israeli nyikani” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Spencer W. Kimball [2006], 146–47).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Lenga kwenye kanuni chache. “Kuna mengi ya kujadili katika kila somo, lakini siyo lazima kushughulikia kila kitu katika kipindi kimoja cha darasa ili kugusa moyo wa mtu—mara nyingi kipengele kimoja au viwili muhimu huwa vinatosha” (Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi, 7).

Chapisha