Agano la Kale 2022
Juni 13–19. 1 Samweli 8–10; 13; 15–18: “Vita Ni vya Bwana”


“June 13–19. 1 Samweli 8–10; 13; 15–18: ‘Vita Ni vya Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Juni 13–19. 1 Samweli 8–10; 13; 15–18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
kijana Daudi na kombeo

Daudi na Goliathi, na Steve Nethercott

Juni 13–19

1 Samweli 8–10; 13; 15–18

“Vita Ni vya Bwana”

Unapojiandaa kufundisha, kumbuka kwamba washiriki wa darasa wanaweza kuwa na uzoefu wenye tija kwa kusoma maandiko nyumbani. Je, unaweza kufanya nini ili kujenga juu ya uzoefu huo?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kuhimiza washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza wiki hii, wape muda wa kufikiria juu ya hisia zozote walizokuwa nazo kuhusu 1 Samweli 8–10; 13; 15–18 Kisha waombe washiriki mstari ambao ulichochea hisia.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

1 Samweli 9:15–17; 10:1–12; 16:1–13

Mungu huwaita watu kwa unabii kutumikia katika ufalme Wake.

  • Hadithi ya Mungu akiwachagua Sauli na Daudi kwa njia ya unabii na ufunuo yaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa jinsi watu wanavyochaguliwa kuhudumu katika Kanisa leo. Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma 1 Samweli 9:15–17; 10:1–12; na 16:1–13, wakiangalia vifungu ambavyo vinaweza kuwasaidia kuelewa ina maana gani “kuitwa na Mungu” (Makala ya Imani 1:5). Je, inaleta tofauti gani, kwa watu walioitwa na kwa wale wanaowakubali, kujua kwamba Mungu huchagua watu kuhudumu katika Kanisa Lake?

    Picha
    Samweli akimpaka mafuta Sauli

    Kielelezo cha Samweli akimpaka mafuta Sauli, © Lifeway Collection/licensed kutoka goodsalt.com

1 Samweli 13:5–14; 15

“Kutii ni bora kuliko dhabihu.”

  • Ili kujadili kwa nini ni muhimu kumtii Bwana, unaweza kualika darasa kupitia upya 1 Samweli 13:5–14 na kutafuta mitazamo na tabia ambazo zilisababisha anguko la Sauli. Je, tunaweza kujifunza nini kutokana na makosa ya Sauli?

  • Wakati hatujui sababu zote za Sauli kuamriwa kuwaua Waamaleki wote na wanyama wao, kuna masomo ya kujifunza kutokana na majibu yake kwa amri hiyo. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutambua masomo haya, unaweza kuandika kwenye ubao Kutii ni bora kuliko … na waalike washiriki wa darasa kutafakari kifungu hiki wakati mnapitia upya pamoja matukio kutoka 1 Samweli 15. Je, ni baadhi ya mambo gani mazuri tunayofanya katika maisha yetu ambayo wakati mwingine sisi huchagua badala ya kumtii Mungu? Kwa nini utii kwa Mungu ni bora kuliko vile vitu vingine vizuri?

1 Samweli 16:6–7

“Bwana huutazama moyo.”

  • Baada ya kusoma 1 Samweli 16:6–7, washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mawazo yao kuhusu nini maana ya kutazama “moyoni” (mstari wa 7). Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuona kwa njia anazoona Bwana? Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao uliwafundisha umuhimu wa kuangalia moyoni badala ya muonekano wa nje.

1 Samweli 17

Bwana anaweza kutusaidia kushinda changamoto yoyote.

  • Katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia washiriki wa darasa wametafakari maneno ya watu mbali mbali yanayopatikana katika 1 Samweli 17. Fikiria kuliomba darasa kushiriki kile walichojifunza kutokana na shughuli hii. Hasa, walijifunza nini kuhusu Daudi?

  • Washiriki wengine wa darasa lako labda wanakabiliwa na changamoto ambazo zinaweza kuonekana kuwa za kutisha kama vile Goliathi alivyofanya kwa Sauli na jeshi lake. Je, unawezaje kutumia hadithi ya Daudi na Goliathi ili kuwasaidia washiriki wa darasa kukabiliana na changamoto zao na imani katika Bwana? Labda unaweza kuonyesha picha ya Daudi na Goliathi (kama mojawapo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Washiriki wa darasa wanaweza kuorodhesha ubaoni baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kuwa “Goliathi” katika maisha yetu. Kisha wanaweza kutafuta mistari katika 1 Samweli 17 ambayo inaonyesha imani ya Daudi, ambayo ilimwezesha kumshinda Goliathi (ona pia taarifa katika “Nyenzo za Ziada”). Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao waliuhisi Bwana aliposaidia kupigana vita vyao.

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Kuwashinda Akina Goliathi wetu.

Rais Gordon B. Hinckley alifundisha:

“Kuna akina Goliathi wanaokuzunguka, wakubwa wanene wenye nia mbaya ya kukuangamiza. Hawa sio wanaume wenye urefu wa futi tisa, lakini ni wanaume na taasisi zinazodhibiti mambo ya kuvutia japo ni mabaya ambayo yanaweza kukupa changamoto na kukudhoofisha na kukuangamiza. …

“… Lakini hauhitaji kuogopa ikiwa una kombeo la ukweli mikononi mwako. … Una mawe ya wema na heshima na uadilifu wa kutumia dhidi ya maadui hawa ambao wangependa kukushinda. Kwa kadiri unavyohusika, unaweza kuwapiga ‘katikati ya macho,’ nikisema kwa mfano. Mnaweza kuwashinda kwa kuwa na nidhamu ninyi wenyewe ili kuwaepuka. Unaweza kusema kwa wengi wao kama vile Daudi alivyomwambia Goliathi, “Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana’ [1 Samweli 17:45]” (“Overpowering the Goliaths in Our Lives,” Ensign, Mei 1983, 46, 51).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wito wako ni una mwongozo wa kiungu. Kama mwalimu, umeitwa na Mungu ili kubariki watoto Wake. Kadiri unavyoishi ukiwa mwenye ustahiki wa msaada Wake, Yeye atakupa ufunuo unaoutafuta. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 5.)

Chapisha