Agano la Kale 2022
Mei 30–Juni 5. Waamuzi 2–4; 6–8; 13–16: “Bwana Akawainulia Mwokozi”


“Mei 30–Juni 5. Waamuzi 6–4; 6–8; 13–16: ‘Bwana Akawainulia Mwokozi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Mei 30–Juni 5. Waamuzi 2–4; 6–8; 13–16,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Debora na majeshi

Kielelezo cha Debora akiyaongoza majeshi ya Israeli, © Providence Collection/licensed kutoka goodsalt.com

Mei 30–Juni 5

Waamuzi 2–4; 6–8; 13–16

“Bwana Akawainulia Mwokozi”

Kumbuka kwamba mwalimu muhimu zaidi ni Roho Mtakatifu. Unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kufundishwa na Roho Mtakatifu ukiwa unajadili kweli kutoka kwenye kitabu cha Waamuzi?

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Andika ubaoni majina ya baadhi ya waamuzi wanaopatikana katika Waamuzi 2–4; 6–8; 13–16 (kama vile Debora, Baraka, Gideoni, na Samson). Wape washiriki wa darasa dakika chache kurejelea sura hizi na kuandika chini ya jina moja ubaoni ukweli waliojifunza kutokana na uzoefu wa mtu huyo.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Waamuzi 2:11–19; 3:5–12; 4:1–16

Bwana hutoa ukombozi tunapopotoka.

  • Kuchunguza mzunguko wa Israeli wa uasi, huzuni, toba, na ukombozi kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutambua nguvu ya Mungu ya ukombozi katika maisha yao wenyewe. Washiriki wa darasa wangeweza kufanya kazi katika vikundi vidogo ili kutafuta mzunguko ulioelezewa katika Waamuzi 2:11–19; 3:5–12. Je, wana wa Israeli waliokolewaje kutoka kwenye mzunguko wao wa dhambi na mateso? Tunajifunza nini kutokana na kitabu cha Waamuzi kuhusu jinsi tunavyoweza kuepuka dhambi na mateso? Ni zipi baadhi ya njia ambazo kwazo Mungu hutukomboa sisi? Pia unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kutafuta na kushiriki maandiko ambayo yanamshuhudia Bwana kama Mwokozi na Mkombozi wetu (kwa mfano, 2 Samueli 22:1–3; Zaburi 40:16–17; 1 Nefi 1:19–20; Mosia 23:21–23; Mafundisho na Maagano 138:23).

  • Waamuzi 2:19 inarekodi kwamba Waisraeli mara kwa mara walimwacha Mungu na kugeukia sanamu. Labda washiriki wa darasa wangeweza kufupisha mstari huu kwa njia ya onyo kwao. Ni katika njia zipi sisi wakati mwingine “tunasujudu” kwa “miungu wengine”? Ni kwa jinsi gani Mungu anaweza kutusaidia kubadili “njia yetu ya ukaidi”?

  • Ili kuanza majadiliano juu ya jinsi Debora na Baraka walivyoikomboa Israeli kutoka kwa Wakanaani, unaweza kumuuliza mshiriki wa darasa kufupisha hadithi kwa darasa (inaweza kusaidia kuwasiliana na mshiriki huyo wa darasa siku chache kabla ili aweze kujiandaa). Darasa linaweza kuongelea kuhusu sifa alizokuwa nazo Debora ambazo zinawavutia. Je, ni jinsi gani Debora aliwashawishi wana wa Israeli kumfuata Bwana? Labda unaweza kusoma pamoja Waamuzi 4:14 na kujadili maana ya tamko la uaminifu la Debora: “Je, Bwana hakutoka atangulie mbele yako?” Je, ni namna gani Bwana huenda mbele yetu? (Ona pia Mafundisho na Maagano 84:87–88).

Waamuzi 6-8

Bwana anaweza kufanya miujiza tunapoamini katika njia Zake.

  • Kujifunza wito wa Gideoni wa kuhudumu kunaweza kuwahamasisha washiriki wa darasa katika huduma yao wenyewe. Unaweza kuwaomba kusoma na kujadili Waamuzi 6:11–16. Tunajifunza nini kutoka kwenye uzoefu huu? Ili kuwasaidia kujifunza kutoka Waamuzi 7, unaweza kualika mshiriki mmoja au zaidi wa darasa kujifanya kuwa wanajeshi wa Gideoni na kusimulia hadithi kutokana na mtazamo wa wanajeshi hao. Washiriki wengine wa darasa wanaweza kuwauliza maswali kuhusu uzoefu wa wanajeshi hawa. Je, ni mifanano gani tunaiona kati ya hadithi hii na kile kinachotokea katika maisha yetu? Je, tunajifunza nini kuhusu Bwana kutoka kwenye hadithi hii?

Waamuzi 13–16

Nguvu huja kutokana na uaminifu kwa maagano yetu na Mungu.

  • Utawasaidia vipi washiriki wa darasa kugundua vyote ukweli wenye kutia moyo na maonyo muhimu kutoka katika hadithi ya Samsoni? Njia mojawapo inaweza kuwa kuwaalika nusu ya darasa kupitia Waamuzi 14–16 wakitafuta mistari inayoonyesha kuwa Bwana alikuwa na Samsoni. Nusu nyingine inaweza kutafuta mistari inayoonyesha kwamba Samsoni hakuwa na msimamo mkamilifu kwa Bwana. Waombe washiriki wa darasa kuelezea kile walichokipata. Maisha ya Samson yanatufundisha nini sisi kuhusu kutii maagano tunayofanya na Mungu? Maelezo na Dada Ann M. Dibb katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza kusaidia.

    Samson akisukuma nguzo

    Samson Anaangusha Nguzo Chini na James Tissot na wengine

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Somo kutokana na maisha ya Samson.

Dada Ann M. Dibb alifundisha: “Samsoni alizaliwa na uwezekano mkubwa wa kuwa mtu muhimu. Mama yake aliahidiwa, ‘Yeye ataanza kuwakomboa Israeli kutoka katika mikono ya Wafilisti’ [Waamuzi 13:5]. Lakini Samsoni alipokua, aliangalia zaidi majaribu ya ulimwengu kuliko mwelekeo wa Mungu. Alifanya chaguzi kwa sababu ‘zilimpendeza [yeye] vizuri’ [Waamuzi 14:3] badala ya kwamba chaguzi hizo zilikuwa sahihi. Kwa kujirudia, maandiko hutumia kifungu cha maneno kisemacho ‘basi akateremka’ [Waamuzi 14:7] wanaposimulia safari, matendo, na chaguzi za Samsoni. Badala ya kuinuka na kung’aa ili kutimiza uwezekano wake wa kuwa mtu muhimu, Samsoni alishindwa na ulimwengu, akapoteza nguvu aliyopewa na Mungu, na akafa kifo cha kutisha, kifo cha mapema” (“Arise and Shine Forth,” Liahona, Mei 2012, 118).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tenga muda kwa ajili ya wanafunzi kushiriki. “Wakati wanafunzi wanapoelezea kile wanachojifunza, hawahisi tu Roho na kuimarisha shuhuda zao pekee, bali pia wanawahimiza washiriki wengine wa darasa kugundua ukweli wao wenyewe. … Tenga muda kwa ajili ya wanafunzi kushiriki katika kila somo.” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 30.)