Agano la Kale 2022
Agosti 1–7. Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42: “Bado Nitamtumaini Yeye”


“Agosti 1–7. Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42: ‘Bado Nitamtumaini Yeye,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Agosti 1–7. Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
Watu watatu wakiongea na mtu akiwa chini

Hukumu za Ayubu,, na Joseph Brickey

Agosti 1–7

Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–4042

“Bado Nitamtumaini Yeye”

Ni ukweli gani ambao Roho Mtakatifu alikusaidia kujifunza wakati uliposoma kitabu cha Ayubu? Unataka kushiriki nini pamoja na darasa lako?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa ambao walisoma Ayubu wiki hii wanaweza kuwa wamegundua ukweli ambao ulikuwa na maana kwao. Ili kuwachochea washiriki, unaweza kuandika kwenye ubao Nimejifunza kutoka kwa Ayubu … na waulize washiriki wa darasa jinsi gani wangekamilisha sentensi hii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Ayubu 1–2; 12–13; 19:23–27

Uaminifu wetu kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo unaweza kutusaidia kubaki waaminifu katika hali zote.

  • Sura mbili za kwanza za Ayubu, ambazo zinaelezea Shetani akihoji sababu za uaminifu wa Ayubu, zinaweza kusaidia washiriki wa darasa kutathmini sababu zao za kuwa waaminifu kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Washiriki wa darasa wanaweza kuanza kwa kuorodhesha sababu kadhaa ambazo mtu anaweza kuchagua kutii amri za Mungu. Kisha wanaweza kupekua Ayubu 1:6–12; 2:1–6 ili kujua kile Shetani alichosema kuhusu uaminifu wa Ayubu. Kwa nini itakuwa hatari kumtii Bwana kwa sababu tu alizopendekeza Shetani? Jibu la Ayubu katika Ayubu 1:20–22; 2:9–10 linafunua nini kuhusu Ayubu? Washiriki wa darasa wangeweza kuzungumza kuhusu kwa nini wao walichagua kubaki waaminifu kwa Mungu.

    Picha
    mwanaume akitazama juu

    Ayubu, na Gary L. Kapp

  • Wakati Ayubu alipokuwa na muda wakati alipokuwa akihangaika na mashaka na kukata tamaa, mwishowe matumaini yake katika Bwana yalimsaidia katika mateso yake. Ili kujifunza kutokana na mfano wa Ayubu, washiriki wa darasa wangeweza kutafuta baadhi ya mistari ifuatayo ili kubaini majibu kadhaa mazuri ya Ayubu kwa majaribu yake: Ayubu 1:21; 2:10; 12:9–10, 16; 13:15–16; 19:23–27. Je, tunaweza kujifunza nini kutokana na majibu haya ambayo yanaweza kutusaidia kuwa na nguvu kiroho wakati tunapokabiliwa na majaribu? Kwa nini ni hatari kudhani kuwa majaribu ni adhabu ya dhambi?

  • Tamko la Ayubu katika Ayubu 19:23–27 linaweza kuhamasisha washiriki wa darasa kutafakari na kushiriki kusadiki kwao wenyewe kwamba Mkombozi, Yesu Kristo, anaishi. Unaweza kuanza kwa kuwaalika washiriki wa darasa kutafakari kimya kimya maneno ya Ayubu katika mistari hii. Wangeweza kujadili maswali kama haya: Kwa nini ushuhuda wa Mkombozi wetu ni muhimu sana wakati wa majaribu kama yale Ayubu aliyoteseka? Ushuhuda wetu umetuimarishaje katika majaribu yetu? Kuimba au kusoma maneno ya wimbo kuhusu Yesu Kristo, kama vile “Najua Mkombozi Wangu Anaishi” (Nyimbo za Kanisa, na.136), inaweza kuongeza ufahamu na nguvu ya kiroho kwenye majadiliano yako.

Ayubu 38

Mtazamo wa Mungu ni mkubwa kuliko wetu sisi.

  • Sehemu kubwa ya kitabu cha Ayubu (sura ya 3–37) inajumuisha Ayubu na marafiki zake wakipambana na swali “Kwa nini mambo mabaya huwatokea watu wema?” Wakati Bwana hajibu swali hili kabisa katika kitabu cha Ayubu, Yeye anatoa ujumbe muhimu. Unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua ujumbe huu kwa kuwaalika wasome maswali ambayo Bwana alimuuliza Ayubu katika Ayubu 38:1–7, 18–24. Tunajifunza nini kutoka katika maswali haya?

  • Injili iliyorejeshwa ya Yesu Kristo inatoa nuru zaidi ambayo inaweza kutusaidia kuelewa sababu zingine za kuteseka ulimwenguni. Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kweli wanazojua kwa sababu ya Urejesho wa injili ambazo zimewapa mtazamo mkubwa na uelewa juu ya mateso. Wangeweza kupata baadhi ya kweli hizi katika maandiko na maelezo yanayopatikana katika “Nyenzo za Ziada.”

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Utambuzi wa siku za mwisho juu ya malengo ya mateso.

Maandiko yafuatayo yanatoa utambuzi kuhusu malengo ya mateso:

Spencer W. Kimball alifundisha:

“Tukiangalia maisha ya duniani kama ndiyo maisha yote, basi maumivu, huzuni, kushindwa, na maisha mafupi yatakuwa msiba. Lakini kama tukiangalia maisha kama kitu cha milele kilichoanzia maisha yaliyopita kabla ya kuzaliwa na kisha maisha ya duniani na kuendelea hadi maisha ya milele yajayo baada ya kifo, ndipo matukio yote yanaweza kuwekwa katika mtazamo ulio sahihi.

Je, hakuna hekima katika [Mungu] ya kutupatia sisi majaribu ili tuweze kuyashinda, majukumu ili tupate kuyafikia, kazi ili tufanye misuli yetu iwe migumu, huzuni ili kuzijaribu nafsi zetu? Je, hatujaachwa kukabilina na majaribu ili kupima uwezo wetu, magonjwa ili tujifunze uvumilivu, kifo ili tuweze kuwa na maisha ya milele na walio tukuka? …

Kama shangwe na amani na thawabu zingepewa mtenda mema papo hapo, hakungekuwa na uovu—wote wangefanya mema lakini sivyo kwa sababu ya haki ya kutenda mema. Kusingekuwa na mtihani wa nguvu, hakuna ukuaji wa tabia, hakuna ukuaji wa nguvu, hakuna uhuru wa haki ya kuchagua” (Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball [2006], 15).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Mfuate Roho. Huwezi kutabiri jinsi kila somo litakavyokwenda, lakini ushawishi wa Roho utakuongoza. Iwapo mmejiandaa kiroho, Bwana atawapatia “katika saa ile ile, kile mtakachosema” (Mafundisho na Maagano 100:6), na inaweza kuwa kile tu washiriki wa darasa wanahitaji kusikia. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 10.)

Chapisha