Agano la Kale 2022
Agosti 22–28. Zaburi 102–103; 110; 116–119; 127–128; 135–139; 146–150: “Kila Mwenye Pumzi na Amsifu Bwana”


“Agosti 22–28. Zaburi 102–103; 110; 116–119; 127–128; 135–139; 146–150: ‘Kila Mwenye Pumzi na Amsifu Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Agosti 22–28. Zaburi 102 102;-103; 116-119; 127-128; 135-139; 146-150,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
Kristo katika joho jekundu akiwa amezungukwa na watu waliopiga magoti

Kila Goti Litapigwa, na J. Kirk Richards

Agosti 22–28.

Zaburi 102–103; 110; 116–119; 127–128; 135–139; 146–150

“Kila Mwenye Pumzi na Amsifu Bwana.”

Je, ni mafundisho gani katika Zaburi unahisi yatakuwa ya msaada zaidi kwa washiriki wa darasa lako? Unapojifunza wiki hii, tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata maana katika maneno ya zaburi hizi.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wape washiriki wa darasa dakika chache kupitia upya zaburi walizosoma wiki hii, na waalike wachache kushiriki kifungu wanachopenda. Wahimize kushiriki kile walichofundishwa na Roho. Je, Zaburi zimeongezaje ufanyaji wetu binafsi wa ibada kwa Bwana?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Zaburi 102-3116

Bwana anaweza kutufariji katika mateso yetu.

  • Je, washiriki wa darasa lako wamejisikia kama mwandishi wa Zaburi 102 alivyojisikia? Je, tunawezaje kumgeukia Bwana tunapojisikia kuvunjika moyo au kufadhaika? Walipojifunza Zaburi 102, 103, na 116 nyumbani wiki hii, washiriki wa darasa yawezekana kuwa waliona vifungu vya maneno ambavyo vinawahamasisha kumgeukia Bwana katika majaribu yao. Wahimize kuelezea kile walichokipata, au watafute vifungu vya maneno vyenye mwongozo wa kiungu kwa pamoja kama darasa. Washiriki wa darasa pia wanaweza kuzungumza kuhusu jinsi Bwana alivyowasaidia nyakati za shida.

  • Washiriki wa darasa lako wanaweza kufurahia kuandika zaburi yao wenyewe kuhusu jinsi Bwana alivyowasaidia nyakati za majaribu. Hizi hazihitaji kuwa zaburi ndefu au ngumu—maneno rahisi tu yenye kuelezea imani, shukrani, na sifa. Washiriki wa darasa wanaweza kufanya kazi kila mtu peke yake au wawili wawili, na wanaweza kurejelea Zaburi 102, 103, na 116 kwa ajili ya kupata mawazo. Waalike watu wachache kushiriki zaburi zao, kama wanapenda. Mnaweza pia kuimba nyimbo pamoja kuhusu jinsi Bwana anavyotufariji, kama vile “Where Can I Turn for Peace?” (Nyimbo za Kanisa, na. 129).

    Picha
    Yesu akiponya

    Uponyaji, na J. Kirk Richards

Zaburi 119

Neno la Mungu litatuweka katika njia Yake.

  • Ili kuanza majadiliano kuhusu Zaburi 119, unaweza kualika washiriki wa darasa kuzungumza juu ya wakati ambapo walifuata njia ya kufikia waendako (inaweza kusaidia kuwasiliana na mtu mapema na kumwomba awe tayari kuzungumza juu ya hili). Ni jambo gani lililofanya iwe vigumu kukaa kwenye njia hiyo? Ni nini kiliwasaidia kukaa juu yake? Kisha unaweza kuchora njia ubaoni na uwaalike washiriki wa darasa kuandika vifungu vya maneno kutoka Zaburi 119 ambavyo vinaelezea kile Bwana alichofanya ili kutusaidia kubaki kwenye njia Yake ya agano. Fikiria kushiriki nukuu za Rais Russell M. Nelson katika “Nyenzo za Ziada” kama sehemu ya mjadala wako.

  • Washiriki wa darasa lako wanaweza kufaidika kwa kulinganisha kile Zaburi 119 inafundisha kuhusu kubaki kwenye njia ya Bwana na maandiko mengine ambayo yanafundisha ukweli kama huo. Fikiria kuligawa darasa katika makundi na kulitaka kila kundi kupitia vifungu vya maandiko kama haya: Zaburi 119:33–40, 105; Mithali 4:11–19; 1 Nefi 8:20–28; 11:25; 2 Nefi 31:17–21; Alma 7:9, 19–20. Alika kila kikundi kuelezea kile walichojifunza. Wape washiriki muda wa kutafakari nini wameshawishika kufanya kulingana na kile walichojifunza.

Zaburi 139

Bwana anaijua mioyo yetu.

  • Kuelewa kuwa Bwana anatujua—mawazo na matendo yetu, uimara na udhaifu—na kwamba Yeye anatupenda kunaweza kuwa na ushawishi mkubwa juu ya uchaguzi ambao tunafanya. Unaweza kualika darasa kutafuta vifungu vya maneno katika Zaburi 139 ambavyo vinafundisha ukweli huu muhimu. Je, maisha yetu yanaguswaje na kujua ukweli huu? Washiriki wa darasa pia wanaweza kujadili njia ambazo tunaweza kumwalika Bwana “uchunguze, Ee Mungu, na uujue moyo wangu” (mstari 23).

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Njia nyembamba iliyosonga.

Rais Russell M. Nelson alisema:

“Ikiwa safari yetu maishani inatakiwa kuwa yenye mafanikio, tunahitaji kufuata maelekezo ya kiungu. Bwana alisema, ‘Nitegemeeni katika kila wazo; msitie shaka, msiogope’ [Mafundisho na Maagano 6:36] Na mtunga Zaburi aliandika, ‘Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu’ [Zaburi 119:105]. …

“Katika safari yako ya maisha, unakutana na vizuizi vingi na hufanya makosa. Mwongozo wa kimaandiko hukusaidia kutambua makosa na kufanya masahihisho muhimu. Unaacha kwenda katika mwelekeo mbaya. Unasoma kwa uangalifu ramani ya barabara ya kimaandiko. Halafu unaendelea na toba na kurejesha vinavyohitajika kurejeshwa ili kuingia kwenye ‘njia nyembamba iliyosonga inayoongoza kwenye uzima wa milele’ [2 Nefi 31:18]” (“Living by Scriptural Guidance,” Ensign, Nov. 2000, 17).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wajumuishe wale wote wanaosumbuka. Wakati mwingine washiriki wa darasa wanaosumbuka wanahitaji tu kujumuishwa ili wajisikie kupendwa. Fikiria kuwaomba wao kuchukua nafasi katika somo lijalo ukiwaalika kuja darasani, au kuhakikisha wanapata usafiri wa kuwaleta kanisani. Usikate tamaa kama watashindwa kuitikia jitihada zako kwa mara ya kwanza. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 8-9.)

Chapisha