“Agosti 29–Septemba 4. Mithali 1–4; 15–16; 22; 31; Mhubiri 1–3; 11–12: ‘Kumcha Bwana ni Chanzo cha Hekima,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)
Agosti 29– Septemba 4. Mithali 1–4; 15–16; 22; 31; Mhubiri 1–3; 11–12,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022
Agosti 29– Septemba 4
Mithali 1–4; 15–16; 22; 31; Mhubiri 1–3; 11–12
“Kumcha Bwana ni Chanzo cha Hekima”
Ni kwa jinsi jumbe katika Mithali na Mhubiri zingeweza kubariki maisha ya wale unaowafundisha? Fuata minong’ono na misukumo unayopokea unapojifunza na kujiandaa kufundisha.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Kuna ujumbe mwingi mzuri na ulio na nguvu katika Mithali na Mhubiri. Kabla ya kujadili vifungu mahususi, kama vile vilivyopendekezwa hapo chini, waalike washiriki wa darasa kushiriki baadhi ya vifungu wavipendavyo kutoka katika kujifunza maandiko kwao binafsi au na familia wiki hii.
Fundisha Mafundisho
Mithali 1–4; 15– 31; Mhubiri 1–3; 11–12
“Tega sikio lako kusikia hekima.”
-
Mwaliko wa kutafuta hekima na uelewa umerudiwa kote katika Mithali. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki na familia zao kile walichojifunza darasani? Njia moja inaweza kuwa ni kuandika hekima ubaoni na kuwaalika washiriki wa darasa waongeze nambari za mistari au virai kutoka katika Mithali au Mhubiri ambavyo wanahisi vinatoa umaizi kuhusu hekima. (Kama ingeweza kuwa msaada, unaweza kupendekeza kwamba washiriki wa darasa wapekue Mithali 1–4; 15– 31; Mhubiri 1–3; 11–12.) Tunajifunza nini kuhusu hekima kutoka kwenye maandiko haya? Ni kwa jinsi gani tunabarikiwa tunapotafuta hekima kutoka kwa Mungu?
Mithali 1:7; 2:5; 3:7; 8:13; 15:33; 16:6; 31:30; Mhubiri 12:13
“Usiwe mwenye hekima machoni pako; mche Bwana.”
-
Mada ingine inayopatikana kote katika Mithali na Mhubiri ni “kumcha Bwana” (Mithali 1:7; ona pia Mithali 2:5; 3:7; 8:13; 15:33; 16:6; 31:30; Mhubiri 12:13). Pengine washiriki wa darasa wangeweza kusoma baadhi ya mistari hii na kushiriki kile wanachohisi inamaanisha kumcha Bwana. Je, Ni kwa jinsi gani kumcha Bwana ni tofauti na aina nyingine za hofu? Unaweza kushiriki umaizi kutoka katika maelezo ya Mzee David A. Bednar yanayopatikana katika “Nyenzo za Ziada.”
“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote.”
-
Washiriki wa darasa wanaweza kufurahia somo la kielelezo ambalo linawasaidia kuelewa kile inachomaanisha “kumtumaini Bwana” na “wasizitegemee akili [zao] wenyewe” (Mithali 3:5). Kwa mfano, unaweza kumwalika mshiriki wa darasa aegemee kitu fulani imara na thabiti, kama vile ukuta. Kisha yule mtu ajaribu kuegemea kitu fulani ambacho si imara, kama vile ufagio. Ni kwa jinsi gani onyesho hili linatusaidia kuelewa Mithali 3:5? Je, Mithali 3: 5–7 inafundisha nini kuhusu kumtumaini Bwana? Kwa nini si busara kutegemea uelewa wetu wenyewe? Ni kwa jinsi gani Bwana huongoza mapito yetu tunapomtumaini Yeye?
Mithali 15:1–2, 4, 18,28; 16:24–32
“Jawabu la upole hugeuza hasira.”
-
Kuwasaidia washiriki wa darasa kujadili jinsi wanavyoweza kuwa na amani zaidi na kutokuwa na ubishi katika maisha yao, unaweza kuwaalika wasome Mithali 15:1–2.18; 16:32. Kisha wangeweza kushiriki uzoefu ambao wamekuwa nao ambao unaonyesha ukweli katika mistari hii. Kwa mfano, ni lini kutumia “jawabu la upole” lilisaidia “kugeuza hasira”? (Mithali 15:1). Au wanaweza kufikiria nyakati ambapo Mwokozi alitoa mfano wa kile kinachofundishwa katika mistari hii (ona Yohana 8:1–11; 18:1–11). Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano Wake tunapotangamana na wengine?
-
Hali waandishi wa Mithali hawakujua kuhusu mikondo mingi ya mawasiliano ambayo ipo katika siku yetu, ushauri katika Mithali 15 na16 unaweza kutumika katika aina zote za mawasiliano. Kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa hili, unaweza kumwalika kila mtu kuchagua mojawapo ya maandiko yafuatayo ili asome: Mithali 15:1–2, 4, 18,28; 16:24, 27–30. Washiriki wa darasa kisha wanaweza kuzisema upya mithali zao katika aina ya ushauri kuhusu kutangamana na wengine kwenye mitandao ya kijamii, kwa njia ya kutuma ujumbe, au kimtandao. Wanaweza kupata ushauri wa ziada wenye msaada katika “Lugha” katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, (2011), 21– 21.
Nyenzo za Ziada
“Kumcha Mungu ni kumpenda na kumtumaini Yeye.”
Mzee David A. Bednar alielezea:
“Hivyo, hofu ya Mungu inakua nje ya uelewa sahihi wa asili ya kiungu na misheni ya Bwana Yesu Kristo, utayari wa mapenzi yetu kumezwa na mapenzi Yake, na uelewa kwamba kila mwanaume na mwanamke atawajibika kwa dhambi zake mwenyewe Siku ya Hukumu.…
“Kumcha Mungu ni kumpenda na kumtumaini Yeye. Tunapomcha Mungu zaidi kabisa, tunampenda Yeye kwa ukamilifu zaidi. Na ‘upendo ulio kamili hutupa nje hofu’ (Moroni 8:16). Ninaahidi mwanga angavu wa kumcha Mungu utafukuzia mbali vivuli vyeusi vya woga wa maisha ya mauti (ona Mafundisho na Maagano 50:25) tunapomtegemea Mwokozi, tunajenga juu Yake kama msingi wetu, na kusonga mbele juu ya njia yake ya agano pamoja na ahadi iliyotukuka” (“Kwa Hiyo Walizima Uoga Wao,” Liahona, Mei 2015, 48–49).