“Septemba 12–18. Isaya 13–14; 24–30; 35: “Kazi ya Ajabu na Mwujiza,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)
“Septemba 12–18. Isaya 13–14; 24–30; 35,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022
Septemba 12–18
Isaya 13–14; 24–30;35
“Kazi ya Ajabu na Mwujiza”
Kabla ya kuweza kuwasaidia wengine kugundua ukweli katika kitabu cha Isaya, unahitaji kugundua ukweli huo wewe mwenyewe. Unaposoma wiki hii, fikiria ni ukweli upi unahisi kuvutiwa kuzingatia darasani.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki kile wanachojifunza kutoka katika Isaya, unaweza kuwauliza jinsi ambavyo wangemjibu mtu ambaye anasema “Kitabu cha Isaya ni kigumu sana kukielewa.” Ni nini kinaweza kutusaidia kupata maana katika mafundisho ya Isaya? Ni vifungu vipi vimetusaidia kupata maana katika mafundisho ya Isaya?
Fundisha Mafundisho
Isaya 24:21– 23; 25:6–8; 26:19; 28:16
Maandishi ya Isaya yanatuelekeza kwa Yesu Kristo.
-
Kama Nefi, washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa walifurahia katika ushuhuda wa Isaya juu ya Yesu Kristo (ona 2 Nefi 11:2). Ungeweza kuwaomba wao kushiriki mistari yo yote waliyoipata katika usomaji wao wiki hii ambayo uliwafundisha kuhusu Mwokozi. Au unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki kile ambacho wao wamejifunza kuhusu Yesu Kristo kutoka katika Isaya 24:21–23; 25:6–8; 26:19; 28:16 au mistari mingine ambayo wewe uliipata katika kujifunza kwako. Kwa nini ukweli huo ni wa thamani kwetu?
Isaya 24:1–5; 28:1–8; 29:7–10; 30:8– 14
Ukengeufu maana yake ni kugeuka kutoka kwa Bwana na manabii Wake.
-
Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kutafakari baadhi ya sitiari ambazo Isaya alitumia kuelezea matokeo ya kugeuka kutoka kwa Bwana na kuwakataa manabii Wake. Waalike washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza. Au unaweza kuwaalika wao kila mmoja kurejelea mojawapo ya vifungu hivi: Isaya 24:1–5; 28:7–8; 29:7–10; 30:8–14. Kulingana na kile ambacho wamesoma, wanaweza kukamilisha sentensi hii: Kama tukigeuka kutoka kwa Bwana, sisi ni kama…” Je, tunaweza kufanya nini ili kubakia waaminifu kwa Bwana na kuepuka ukengeufu? (Ona “Nyenzo za Ziada” kwa ajili ya mapendekezo.) Je, ni kwa jinsi gani Bwana anawabariki wale wanaobakia waaminifu Kwake?
-
Ili kuanzisha mjadala kuhusu mitazamo na tabia ambazo zinaweza kutuelekeza kwenye ukengeufu, unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kupekua Isaya 24:1–5; 28:1–8; 29:7–10; 30:8–14. Waombe kutafuta vitu ambavyo watu katika nyakati za Isaya walikuwa wanafikiria na kufanya. Tengeneza nembo ya onyo ubaoni ambayo inasema Onyo: Mitazamo na tabia zifuatazo zinaweza kuongoza kwenye ukengeufu. Washiriki wa darasa wanaweza kuorodhesha ubaoni kile wanachopata katika mistari. Wape fursa kushiriki jinsi wanavyojikinga wenyewe au familia zao kutokana na ukengeufu.
Bwana anaweza kurejesha vitu ambavyo vimepotea au kuvunjika.
-
Hapa kuna swali unaloweza kuandika ubaoni ambalo litaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari Isaya 29: Je, maandishi ya Isaya yanahusiana vipi na Urejesho wa injili katika siku yetu? Wahimize kufikiria juu ya swali hili wanaposoma kimya kimya Isaya 29: 13–24. (Kama wanahitaji msaada, wanaweza kurejelea pia vifungu kama vile: 2 Nefi 27:6–26; Joseph Smith—Historia 1:17–19, 63–65. Baada ya kuzungumza kuhusu swali lililo ubaoni, wanaweza kujadili kwa nini “ajabu” na “mwujiza” (Isaya 29:14) ni maneno mazuri ya kuelezea Urejesho wa injili. Tunajifunza nini kuhusu Urejesho kutoka katika “Urejesho wa Utimilifu wa Injili ya Yesu Kristo: Tangazo kwa Ulimwengu la Maadhimisho ya Miaka Mia Mbili”? (ChurchofJesusChrist.org).
-
Sura ya 30 na35 ya Isaya ina vifungu kadhaa ambavyo vinaweza kukupa mwongozo wa imani kuu katika nguvu za Bwana za kuwabariki wale wanaomgeukia Yeye. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua vifungu hivi, unaweza kuwaalika wajifunze mojawapo ya Isaya 30:18–26 au Isaya 35. Waombe waelezee maneno au virai walivyovipata vinavyoweza kumsaidia mtu kumgeukia Bwana kwa ajili ya ukombozi.
Nyenzo za Ziada
Kubaki mwaminifu kwa Bwana na Kanisa Lake.
Rais M. Russell Ballard alitoa ushauri wa kutusaidia kubaki waaminifu kwa Bwana na kwa Kanisa Lake:
“Tunahitaji kupata uzoefu wa uongofu endelevu kwa kuongeza imani yetu katika Yesu Kristo na uaminifu wetu kwa injili Yake maishani mwetu mwote—siyo tu mara moja, bali kila mara [ona Alma 5:56].…
“… Maneno ya Bwana yanapatikana katika maandiko na mafundisho ya mitume na manabii. Yanatupatia ushauri na mwongozo ambao, unapofuatwa, utakuwa kama koti la kuokoa la kiroho na utatusaidia kujua jinsi ya kushikilia kwa mikono yote miwili.…
“Pamoja na kukuza desturi ya kujisomea maandiko kibinafsi, tunahitaji kuwa kama wana wa Mosia na tujitoe wenyewe ‘kwa kusali sana, na kufunga’ [Alma 17:3]” (“Kaa Chomboni na Ushikilie!” Liahona, Nov. 2014, 90–91).