“Septemba 5–11. Isaya 1–12: ‘Mungu Ndiye Wokovu Wangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)
“Septemba 5–11. Isaya 1–12,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022
Septemba 5–11
Isaya 1–12
“Mungu Ndiye Wokovu Wangu”
Fikiria njia za kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki misukumo na uelewa waliopokea wakati wa kujifunza kwao binafsi na kama familia wiki hii?
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unatoa mawazo kwa ajili ya kuelewa maandiko ya Isaya. Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki jinsi mojawapo ya mawazo haya, au kitu kingine, kilivyowasaidia kujifunza kutoka katika Isaya 1–12.
Fundisha Mafundisho
Maneno ya Isaya yote yatatimizwa.
-
Akiongea juu ya Isaya, Mwokozi alifundisha kwamba “vitu vyote ambavyo alizungumza vimekuwa na vitakuwa, hata kulingana na maneno ambayo alisema (3 Nefi 23:3). Unaweza kuanza kwa kujadili kuhusu Isaya kwa kushiriki andiko hili na kauli katika “Nyenzo za Ziada.” Unaweza kisha kuandika ubaoni siku ya Isaya, Huduma ya Mwokozi duniani na Siku za Mwisho. Washiriki wa darasa wanaweza kutafuta vifungu katika Isaya 1–12 ambavyo vinaweza kulingana na kirai kimoja au zaidi vilivyo ubaoni (kwa mfano, Isaya 2:1–5; 7:1–7; 7:10–14; 9:2–7; 10:20; 11:10; 12:1). Kwa nini ni baraka kuwa unabii huu unapatikana kwetu leo?
“Acheni kutenda mabaya.”
-
Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki kitu walichojifunza kutoka katika kujifunza kwao binafsi na kama familia katika Isaya1, 3,5 kuhusu hali za kiroho za Ufalme wa Yuda katika siku za Isaya. Labda wangeweza kupitia tena sura hizi na kutengeneza orodha ya mistari na hali wanazoelezea. Ni ujumbe gani wa matumaini tunapata katika sura hizi? (Kama inahitajika, unaweza kuwarudisha washiriki wa darasa kwenye Isaya 1:16–20, 25–27; 3:10.) Kama Yuda ya kale ilikuwa na ujumbe kwa ajili yetu, ungekuwa upi?
-
Washiriki wa darasa wanaweza kujifanya kwamba walikuwa wanaishi katika Yerusalemu wakati Isaya alipotoa unabii. Unaweza kuwahoji wachache kati yao, ukiwauliza Isaya alisema nini na wao walijisikiaje. Kwa mfano, unaweza kuwauliza washiriki wa darasa kuongea kuhusu maneno ya Isaya yanayopatikana katika Isaya 1:16–20; 3:16–26; 5:20–23. Je, Isaya alisema nini ambacho kinatuhamasisha sisi kutubu?
Mungu atafanya kazi kuu katika siku za mwisho.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari jinsi unabii wa Isaya kuhusu siku za mwisho unavyotimizwa, unaweza kuchagua baadhi ya mistari kutoka katika Isaya 2; 4; 11–12 (kama vile Isaya 2:2–3; 4:5–6). Waalike washiriki wa darasa kutafuta vitenzi vya njeo ya wakati ujao katika hii mistari (kama vile “takuwa” au “taenda”). Waalike wao wabadilishe baadhi na mahali pake waweke vitenzi vya wakati uliopo (kama vile “imekuwa” au nimeenda”). Je, unabii huu unatimizwaje katika maisha yetu? Kwa nini ni muhimu kujua kuhusu unabii huu?
-
Unaweza kusema kwamba wakati Moroni alipomtembelea Joseph Smith katika mwaka wa 1823, alinukuu Isaya 11 na kusema kwamba ulikuwa karibu kutimia (ona Joseph Smith—Historia 1:40; ona pia Mafundisho na Maagano 113:1–6). Washiriki wa darasa wanaweza kusoma mistari michache kutoka katika Isaya 11 (kama vile mstari wa 6–12) na kufanya muhtasari kwa maneno yao wenyewe kwa kile ambacho Isaya alitabiri. Je, nafasi yetu sisi ni ipi katika kutimizwa kwa unabii huu?
Isaya alitoa unabii juu ya Yesu Kristo.
-
Unaweza kuwauliza washiriki wa darasa kitu walichojifunza kuhusu Yesu Kristo kutoka kwenye vifungu kama vile Isaya 7:14; 8:13–14; 9:2, 6–7. Kwa mfano, kwa nini Imanueli ni jina zuri kwa Mwokozi? (ona Mathayo 1:23). Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo amekuwa “Mshauri” au “Mfalme wa Amani” kwetu sisi? Washiriki wa darasa pia wanaweza kushiriki vifungu vingine walivyovipata katika Isaya 1–12 ambavyo vinawakumbusha juu ya Yesu Kristo. Je, vifungu hivi vinatufundisha nini kumhusu Yeye?
-
Kabla ya darasa, waalike washiriki wa darasa kuleta picha ya Kristo ambayo wanahisi inawakilisha mojawapo ya maelezo ya Mwokozi yanayopatikana katika Isaya 7–9. Wakati wa darasa, wape muda kuonyesha picha waliyoleta na kuelezea jinsi inavyolingana na maneno ya Isaya.
Nyenzo za Ziada
Unabii wa Isaya unaweza kuwa na utimizwaji mwingi.
Rais Dallin H. Oaks alifundisha: “Kitabu cha Isaya kina unabii mwingi ambao unaonekana kuwa na utimizwaji mwingi. Mmoja unaonekana kuhusisha watu wa siku ya Isaya au hali za kizazi kinachofuata. Maana nyingine, mara nyingi kiishara, unaonekana kurejelea matukio katika wakati wa meridiani, wakati Yerusalemu ilipoangamizwa na watu wake kutawanywa baada ya kusulubiwa kwa Mwana wa Mungu. Bado maana nyingine ya utimizwaji wa unabii huo huo unaonekana kuhusika na matukio yatanguliayo Ujio wa Pili wa Mwokozi. Ukweli kwamba wingi wa unabii huu unaweza kuwa na maana nyingi inadhihirisha umuhimu wa haja yetu ya ufunuo kutoka kwa Roho Mtakatifu hili kutusaidia kuutafsiri (“Scripture Reading and Revelation,” Ensign, Jan. 1995, 1995,8).