“Oktoba 17–23. Yeremia 30–33; 36; Maombolezo 1; 3: ‘Nitageuza Masikitiko Yao kuwa Furaha,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)
“Oktoba 17–23. Yeremia 30–33; 36; Maombolezo 1; 3,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022w
Oktoba 17–23
Yeremia 30–33; 36; Maombolezo 1; 3
“Nitageuza Masikitiko Yao kuwa Furaha”
Tafakari misukumo uliyopokea wakati wa kujifunza kwako binafsi Yeremia na Maombolezo. Ni vifungu gani kutoka katika sura hizi unahisi vitakuwa vya muhimu zaidi kwa wale unaowafundisha?
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki kile ambacho wamejifunza kutokana na kujifunza kwao maandiko, unaweza kuandika ubaoni virai kama Nimejifunza kwamba…, Nina ushuhuda wa…, au Nimepata uzoefu wa… Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki kitu fulani kutoka katika Yeremia au Maombolezo ili kukamilisha sentensi hizi.
Fundisha Mafundisho
Yeremia 30–31; 33; Maombolezo 1:1–7; 3:1–5
Bwana atawatoa Israeli kutoka utumwani na kuwakusanya.
-
Uumbe wa matumaini katika unabii wa Yeremia unaweza kuwapa washiriki wa darasa matumaini katika hali zao wenyewe. Labda darasa lako linaweza kujadili hali ambazo zinaweza kuwafanya watu katika siku yetu kuhisi kukosa matumaini kama vile katika nyakati za Yeremia walivyohisi (ona Yeremia 30:5; 31:15; Maombolezo 1:1–7; 3:1–5; na nukuu katika “Nyenzo za Zaida”). Unaweza kisha kugawa washiriki wa darasa katika vikundi vitatu na kualika kila kundi kupitia Yeremia 30; 31; na 33 kwa ajili ya ujumbe ambao unaweza kuleta matumaini kwa watu leo. Je, ni kwa jinsi gani Bwana ametusaidia kuvumilia majaribu?
“Nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.”
-
Kupitia tena Yeremia 31:31–34; 32:37–42 kunaweza kulisaidia darasa lako kutafakari maagano ambayo wamefanya. Njia moja ya kuhimiza mjadala kuhusu hii mistari ni kuwapa washiriki wa darasa dakika chache za kusoma mistari hiyo na kisha kuandika kwenye kipande cha karatasi swali ambalo wangependa kuuliza darasa kuhusu kile ambacho wamesoma. Kwa mfano, wanaweza kutaka kujadili kile inachomaanisha kuwa na sheria za Mungu zimeandikwa katika mioyo yetu (ona Yeremia 31:33) au jinsi maagano yanavyotusaidia kuja kumjua Bwana (ona Yeremia 31:34). Unaweza kisha kukusanya maswali na kuchagua machache ya kujadili pamoja. Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii ambacho kinatupa mwongozo wa kuwa hodari katika kushika maagano yetu?
Maandiko yana nguvu za kutugeuza sisi kutoka kwenye uovu.
-
Washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa wamepata umaizi kuhusu maandiko walipokuwa wanajifunza Yeremia 36 nyumbani. Waalike kushiriki kile walichojifunza. Unaweza pia kuwapa washiriki wa darasa jina la mtu katika sura hii na uwaalike wasome kuhusu kile ambacho mtu huyu alifanya na neno la Mungu. Washiriki wa darasa wanaweza kujifunza maneno na matendo ya Bwana (ona mstari wa 1–3, 27–31); Yeremia (ona mstari wa 4–7,32); Baruki (ona mstari wa 4, 8–10, 14–18); Yehudi na Mfalme Yehoyakimu (ona mstari wa 20–26); na Elnathani, Delaya, na Gemaria (ona mstari wa 25). Je, maneno na vitendo vinaonyeshaje jinsi tunavyohisi kuhusu maandiko?
Nyenzo za Ziada
Unaweza kuwa na matumaini daima.
Rais M. Russell Ballard alitaja baadhi ya hali ambazo zinaweza kusababisha wengine wapoteze matumaini, na akatoa ushauri kuhusu mahali pa kupata matumaini.
“Baadhi yetu tunaweza kuona maisha yetu yamejaa kukata tamaa, masikitiko, na huzuni. Wengi wanahisi kukosa matumaini kukabiliana na vurugu ambayo inaonekana kukithiri ulimwenguni. Wengine wanafadhaika juu ya wanafamilia ambao wamesombwa katika mkondo mkali, unaotanda wa maadili yaliyodorora na kushuka kwa viwango vya maadili. … Wengi hata wamejiuzulu wenyewe na kukubali uovu na ukatili wa ulimwengu usioweza kurekebishika. Wamekosa matumaini.…
“… Wengine miongoni mwetu wamepoteza matumaini yote kwa sababu ya dhambi na uvunjaji wa sheria. Mtu anaweza kuwa amejiingiza sana katika njia za ulimwengu kiasi kwamba yeye haoni njia ya kuponyokea na kupoteza matumaini yote. Maombi yangu kwa wote ambao wametumbukia katika huu mtego wa adui ni kamwe wasikate tamaa! Bila kujali jinsi mambo yanavyokatisha tamaa au jinsi yanavyoelekea kuwa mabaya, tafadhali niamini, unaweza daima kuwa na matumaini. Daima” (“Shangwe ya Tumaini Inatimizwa,” Ensign, Nov. 1992, 31–32).
“Kwa urahisi, tumaini letu moja kwa ajili ya usalama wa kiroho nyakati hizi za msukosuko ni kugeuza akili zetu na mioyo yetu kwa Yesu Kristo. … Imani katika Mungu na katika Mwanawe, Yesu Kristo, ni muhimu kabisa kwetu ili kudumisha msimamo sambamba kupitia nyakati za majaribu na dhiki” (“Shangwe ya Tumaini Inatimizwa,”32).