Agano la Kale 2022
Oktoba 10–16. Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20: “Kabla Sijakuumba katika Tumbo Nalikujua”


“Oktoba 10–16. Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20: ‘Kabla Sijakuumba katika Tumbo Nalikujua,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Oktoba 10–16. Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20:” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
nabii akizungumza na wanaume

Yeremia, na Walter Rane

Oktoba 10–16

Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20

“Kabla Sijakuumba katika Tumbo Nalikujua”

Mnapojifunza, fikiria kuhusu washiriki wa darasa lako, tafuta mwongozo wa Roho ili kujua ni ujumbe gani unaweza kuwa muhimu sana kwao.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Njia moja unayoweza kuhimiza kushiriki ni kuwaalika washiriki wa darasa kuandika kwenye kipande cha karatasi ukweli wa injili waliojifunza wakati wa kujifunza kwao Yeremia wiki hii. Unaweza kisha kuchukua vipande hivyo vya karatasi na chagua vichache vya kuvijadili kama darasa. Je, ni kwa jinsi gani maandishi ya Yeremia hutusaidia kuelewa ukweli huu.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Yeremia 1:4–19

Manabii huitwa kunena neno la Bwana.

  • Unaweza kuanza mjadala kuhusu wito wa Yeremia kama nabii kwa kuonyesha picha ya nabii aliye hai na kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki jinsi ambavyo wamekuja kujua kwamba yeye ameitwa na Mungu. Ungeweza pia kuwaomba kushiriki jinsi wamewasaidia wengine kujua ukweli huu muhimu. Je, ni kwa namna gani maarifa haya yanabariki maisha yetu? Washiriki wa darasa wanaweza kuorodhesha ubaoni vitu ambavyo wamejifunza kuhusu nabii kutoka katika Yeremia 1:4–19. Manabii katika siku yetu “wanang’oa” au “wanabomoa” nini? Ni nini wanajenga” na “kupanda”? (mstari wa 10).

  • Waalike washiriki wa darasa kushiriki kile Yeremia alichojifunza kuhusu yeye mwenyewe katika Yeremia 1:5. Ni kwa jinsi gani maarifa haya yaliboresha huduma yake? Washiriki wa darasa wanaweza pia kusoma maelezo katika “Nyenzo za Ziada” na maandiko yafuatayo yanayounga mkono ukweli huu: Alma 13:1–4; Mafundisho na Maagano 138:53–56; Ibrahimu 3:22–23. Ni kwa jinsi gani ukweli huu kuhusu maisha yetu kabla ya kuzaliwa unaathiri jinsi tunavyoishi maisha yetu ya duniani?

Picha
mtu akisimama kwenye tangi la maji la kale

Watu katika Israeli ya kale walitumia matangi kuhifadhi maji ya thamani.

Yeremia 2; 7

“Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima.

  • Ili kuchochea mjadala kuhusu Yeremia 2:13, unaweza kuchora ubaoni tangi la maji (bwawa kubwa chini ya ardhi) na chemichemi (kama chemichemi ya asili). Washiriki wa darasa wanaweza kisha kusoma Yeremia 2:13 na kuzungumza kuhusu kwa nini ni bora kupata maji kutoka kwenye chemichemi kuliko kuchimba tangi la maji. Ni nini kinaweza kuwa kisawe cha kiroho cha kujenga matangi yaliyobomoka? Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma mistari kutoka katika Yeremia 2 na7 na kushiriki baadhi ya njia Waisraeli walizoacha “chemichemi ya maji ya uzima” (ona kwa mfano Yeremia 2:26–28; 7:2–11). Kwa nini “maji ya uzima” ni ishara nzuri ya kile ambacho Mwokozi hutupatia?

Yeremia 3:14–18; 16:14–15

Bwana atawakusanya watu Wake.

  • Kwa sababu Yeremia alilinganisha kukusanyika kwa Israeli kwa siku za mwisho na kukombolewa kwa Israeli kutoka Msiri kupitia Musa, unaweza kuonyesha picha ya Kutoka (ona muhtasari wa Aprili 4– 10 katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waalike washiriki wa darasa kujadili jinsi umuhimu wa Kutoka ulivyokuwa kwa Waisraeli kwa vizazi vingi. Washiriki wa darasa kisha wasome Yeremia 16:14–15 na kuzungumza kuhusu jinsi gani kukusanyika kwa Israeli katika siku za mwisho kutakavyo kuwa muhimu zaidi kwa watu wa Mungu (ona pia Yeremia 3:14–18). Washiriki wa darasa ambao walirejelea “Tumaini la Israeli” kama sehemu ya kijifunza kwao binafsi wanaweza kushiriki kile walichojifunza kuhusu umuhimu wa kukusanyika kwa Israeli (ona Russell M. Nelson na Wendy W. Nelson, “Tumaini la Israeli” [worldwide youth devotional, Juni 3, 2018], nyongeza kwenye New Era na Ensign, Agosti 2018, 2–17, ChurchofJesusChrist.org). Au mnaweza kupitia tena sehemu za ujumbe huo kama darasa. Je, Israeli inakusanywaje katika eneo letu?

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Baba wa Mbinguni anawajua ninyi.

Rais Russell M. Nelson alifundisha:

Roho yako ni chombo cha milele. Na Bwana akamwambia nabii Wake Ibrahimu: ‘Wewe ulichaguliwa kabla hujazaliwa’ (Ibrahimu 3:23]. Bwana alisema kitu kama hicho kuhusu Yeremia [ona Yeremia 1:5] na wengine wengi [ona Alma 13:2–3]. Yeye hata alisema hivyo kuhusu wewe [ona Mafundisho na Maagano 138:55–56].

“Baba yako wa Mbinguni amekujua wewe kwa muda mrefu sana. Wewe, kama mwana au binti Yake, ulichaguliwa na Yeye kuja duniani katika wakati mahususi, kuwa kiongozi katika kazi Yake kuu duniani. Wewe ulichaguliwa sio kwa sababu ya sifa zako za kimwili bali kwa sifa zako za kiroho, kama vile ushupavu, ujasiri, uaminifu wa moyo, kiu ya ukweli, njaa ya hekima, na shauku ya kuwahudumia wengine.

“Ulikuza baadhi ya sifa hizi kabla ya kuzaliwa. Nyingine unaweza kuzikuza hapa duniani kwa mwendelezo unapoendelea kuzitafuta” (“Maamuzi kwa Ajili ya Milele,” Ensign au Liahona, Nov. 2013,107).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ishi injili kwa moyo wako wote. Wewe utakuja kuwa mwalimu kama Kristo unapoikumbatia injili na kuiishi kila siku ya maisha yako. Ufundishaji kama Kristo hauhitaji wewe kuwa mkamilifu—jaribu tu na endelea kujaribu. Unapofanya bidii kadiri uwezavyo na kutafuta msamaha unapokosea, unaweza kuwa mwanafunzi wa Kristo ambaye Yeye anakuhitaji wewe uwe. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 13–14.)

Chapisha