Agano la Kale 2022
Septemba 26–Oktoba 2. Isaya 50–57: “Ameyachukua Masikitiko Yetu, Amejitwika Huzuni Zetu”


“Septemba 26–Oktoba 2. Isaya 50–57: ‘Ameyachukua Masikitiko Yetu, Amejitwika Huzuni Zetu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Septemba 26– Oktoba 2. Isaya 50–57,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
Kristo akiwa amevaa taji la miiba na askari anamkejeli

Kukejeliwa kwa Kristo, na Carl Heinrich Bloch

Septemba 26–Oktoba 2

Isaya 50–57

“Ameyachukua Masikitiko Yetu, Amejitwika Huzuni Zetu”

Njia muhimu zaidi ya kujiandaa kufundisha ni kusoma na kuyatafakari maandiko. Unahisi na kujifunza nini unaposoma Isaya 50–57?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwachochea washiriki wa darasa kushiriki uzoefu walioupata walipokuwa wanasoma Isaya 50–57, unaweza kuandika ubaoni sentensi kama hii Imani yangu katika Yesu Kristo iliimarishwa nilipokuwa nikisoma… Waalike washiriki wa darasa kushiriki jinsi ambavyo wangekamilisha sentensi hii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Isaya 50–52

Siku za usoni ni angavu kwa watu wa Bwana.

  • Sisi sote tunazo nyakati ambapo tunahisi kuwa dhahifu. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutegemea nguvu za Bwana, ungeweza kumpatia kila mmoja kazi ya kusoma 1 Isaya 51–52 na kushiriki kile ambacho wamepata kinachoweza kumuimarisha mtu fulani ambaye anahisi kuwa dhahifu au amevunjika moyo. Unaweza pia kusema kwamba Mwokozi aliyefufuka alirudia baadhi ya maneno kwa watu katika Amerika (ona 3 Nefi 20:32–45). Maneno ya Mwokozi katika 3 Nefi 20:30–34 yanaongeza nini kwenye uelewa wako wa lini unabii huu utatimizwa?

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kuorodhesha kila kitu ambacho Yeye aliwaalika watu Wake kufanya. Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile walichopata na kuongelea kuhusu kile mialiko hii inamaanisha kwao. Unaweza kutaka kufokasi kwenye mialiko katika Isaya 51:1–2, 6–8; 52:1–3, 9–11. Je, tunaweza kutenda nini juu ya mialiko hii? Unaweza kuonyesha kwamba Mafundisho na Maagano 113:7–10 hutoa maelezo yenye kuvutia kwa Isaya 52:1–2. Ni nini maneno haya yanaongeza kwenye uelewa wetu?

Picha
Sanaa ya uchongaji ya Kristo akibeba msalaba

Kwa Sababu ya Upendo, na mchongaji Angela Johnson

Isaya 52:13–15; 53

Yesu Kristo alijichukulia mwenyewe dhambi zetu na huzuni zetu.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupiga taswira kichwani maneno ya Isaya katika Isaya 53, unaweza kuonyesha picha kadhaa za matukio yanayozunguka Upatanisho wa Yesu Kristo (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 56–60). Kisha ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kutafuta virai katika Isaya 53 ambavyo vinaelezea matukio kwenye picha. Maneno ya Isaya yanafundisha nini kuhusu kuteseka kwa Mwokozi kwa ajili yetu? Yanapendekeza nini kuhusu kwa nini Yeye aliteseka kwa ajili yetu? Je, mafundisho haya yanatushawishi kufanya nini?

  • Ili kumwalika Roho Mtakatifu kushuhudia ukweli unaofundishwa katika Isaya 52:13–15; 53, unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kusoma mistari hii kimya kimya hali wewe unacheza wimbo kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo. Waalike washiriki wa darasa kutafuta maneno au virai katika maandiko ambavyo wanahisi ni muhimu hasa. Kisha waache washiriki kile ambacho wamepata na jinsi wanavyohisi kuhusu Mwokozi. Fikiria pia kuwaalika washiriki wa darasa kusoma Mosia 15:10–12, pale Abinadi alipoelezea ilimaanisha nini kwa kirai “mbegu yake.” Ni kwa jinsi gani hii inatusaidia kuelewa Isaya 53:10?

Isaya 54

Yesu Kristo anatutaka sisi turejee Kwake.

  • Kujifunza Isaya 54 kunaweza kuwashawishi washiriki wa darasa ambao wanajisikia kuvunjika moyo kwa sababu ya dhambi zao au udhaifu wao. Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kupekua sura ya 54 wakitafuta virai au mistari inayoonyesha jinsi gani Mwokozi anajisikia kuhusu sisi. Je, Yeye anataka sisi tujisikieje kuhusu dhambi zetu za zamani na udhaifu wetu? Je, Yeye hutaka sisi tuhisi vipi kuhusu Yeye? Wahimize washiriki wa darasa kushiriki chochote wanachojifunza kuhusu Yesu Kristo. Maelezo ya Rais Dieter F. Uchtdorf katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza kuongezea kwenye mjadala wako.

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Kwa Yesu Kristo tunaweza kuwa na matumaini.

Rais Dieter F. Uchtdorf alifundisha:

“Bila kujali ni kiasi gani maisha yetu yameharibiwa. Bila kujali dhambi zetu ni nyekundu kiasi gani, uchungu mkubwa kiasi gani, wapweke kiasi gani, kutelekezwa, au kuvunjika kwa mioyo yetu. Hata wale wasio na matumaini, waliokata tamaa, ambao walisaliti uaminifu, walio salimisha heshima zao, au kumkufuru Mungu wanaweza kujengwa upya.…

“Habari za furaha za injili ni hizi: kwa sababu ya mpango wa furaha wa milele uliotolewa na Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo na kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, hatuwezi tu kukombolewa kutoka kwenye anguko na kurejeshwa kwenye usafi, bali tunaweza pia kuvuka mawazo ya maisha ya kidunia na kuwa warithi wa uzima wa milele na washiriki wa utukufu wa Mungu” (“Atakubeba Mabegani Mwake na Kukupeleka Nyumbani,” Liahona, Mei 2016,102).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ishi kwa kustahili mwongozo wa Roho. Unapoishi injili kwa kustahili, unaishi ukiwa mwenye kustahili wenzi wa Roho ambaye ni mwalimu aliye bora. Unapotafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu, atakupa mawazo na ushawishi kuhusu jinsi ya kutosheleza mahitaji ya wale unaowafundisha. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 5.)

Chapisha