Agano la Kale 2022
Septemba 26–Oktoba 2. Isaya 50–57; “Ameyachukua Masikitiko Yetu, na Amejitwika Huzuni Zetu”


Septemba 26–Oktoba 2. Isaya 50–57; “Ameyachukua Masikitiko Yetu, na Amejitwika Huzuni Zetu”,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

Septemba 26–Oktoba2. Isaya 50–57,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Famila: 2022

Kristo amevaa taji la miiba na akidhihakiwa na askari

Dhihaka za Kristo, na Carl Heinrich Bloch

Septemba 26–Oktoba 2

Isaya 50–57

“Ameyachukua Masikitiko Yetu, na Amejitwika Huzuni Zetu,’”

Tafakari maono kutoka Isaya 50–57 ambayo yanakusaidia kukuleta karibu na Mwokozi. Andika misukumo unayopokea.

Andika Misukumo Yako

Kote katika huduma yake yote, Isaya alizungumzia mkombozi hodari (ona, kwa mfano, Isaya 9:3–7). Unabii huu ungekuwa wa maana sana kwa Waisraeli karne nyingi baadaye wakati wakiwa utumwani Babeli. Mtu ambaye angeangusha kuta za Babeli angekuwa mshindi hodari kweli. Lakini huyo sio aina ya Masiya ambaye Isaya alimwelezea katika sura ya 52–53: “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao. … Tulimdhania kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu, na kuteswa” (Isaya 53:3–4). Kwa kumtuma mkombozi asiyetarajiwa kama huyo, Mungu alitufundisha juu ya ukombozi wa kweli. Ili kutuokoa kutokana na uonevu na mateso, Mungu alimtuma Yule ambaye Yeye mwenyewe alionewa na … kuteswa.” Ambapo wengine walitarajia simba, Alituma mwana-kondoo (ona Isaya 53:7). Hakika, njia za Mungu sio njia zetu (ona Isaya 55:8–9). Yesu Kristo anatuweka huru sio kwa kufungua gereza tu bali kwa kuchukua nafasi yetu huko. Yeye hutuondolea minyororo yetu ya masikitiko na huzuni kwa kuubeba Yeye mwenyewe (ona Isaya 53:4–5, 12). Hatuokoi tukiwa mbali. Anateseka pamoja nasi, kwa tendo la “fadhili za milele” ambazo “hazitaondolewa kwako” (Isaya 54:8, 10).

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Isaya 50–52

Wakati ujao unang’a kwa ajili ya watu wa Bwana.

Ingawa Waisraeli walikaa miaka mingi utumwani—na ingawa utekaji huo ulikuwa matokeo ya uchaguzi wao mbaya—Bwana aliwataka watazame wakati ujao kwa tumaini. Je! Unapata jumbe gani zenye matumaini katika Isaya 50–52? Je! Bwana anatufundisha nini kumhusu Yeye mwenyewe katika sura hizi, na kwa nini hii inakupa tumaini? (ona, kwa mfano, Isaya 50:2, 5–9; 51:3–8, 15–16; 52:3, 9–10).

Unaweza pia kuorodhesha kila kitu katika sura ya 51–52 ambacho Bwana anaialika Israeli kufanya ili kufanya siku zijazo za matumaini kuwa kweli. Je, unahisi Bwana anakualika kufanya nini kupitia maneno haya? Kwa mfano, unafikiri nini maana ya “amka” na “jivike nguvu”? Isaya 51:9; ona pia Isaya 52:1; Mafundisho na Maagano 113:7–10). Kwa nini unafikiri mwaliko wa “kusikiliza” (au “kusikiliza kwa nia ya kutii”) unarudiwa mara nyingi? (Russell M. Nelson, “Msikilize Yeye,” Liahona, Mei 2020,89).

Ona pia Mosia 12:20–24; 15:13–18; 3 Nefi 20:29–46.

sanamu ya Kristo akibeba msalaba

Kwa Sababu ya Upendo, na mchongaji Angela Johnson

Isaya53

Yesu Kristo alijichukulia juu Yake dhambi zangu na huzuni.

Sura chache katika maandiko zinaelezea ujumbe wa ukombozi wa Yesu Kristo kwa uzuri zaidi kuliko Isaya 53. Chukua muda kutafakari maneno haya. Kwa kila mstari, pumzika kutafakari kile Mwokozi alichoteseka—“huzuni,” “masikitiko,” na “makosa” aliyoyabeba—kwa watu wote na hasa kwako. Unaweza kubadlisha maneno kama “sisi” na “yetu” na “mimi” na “yangu” unaposoma. Je! Ni hisia au mawazo gani mistari hii inakutia moyo ndani yako? Fikiria kuyaandika chini.

Unaweza kutaka kupitia Mosia 14; 15:1–13 kuona jinsi nabii Abinadi alivyotumia maneno ya Isaya kufundisha kuhusu Mwokozi.

Isaya 54; 57:15–19

Yesu Kristo ananitaka nirudi Kwake.

Sisi sote tuna nyakati ambapo tunahisi tuko mbali na Bwana kwa sababu ya dhambi zetu au udhaifu. Wengine hata wamekata tumaa kwamba atawasamehe milele. Isaya 54 na57 ni sura nzuri za kusoma kwa uhakikisho na kutiwa moyo nyakati kama hizo. Hasa katika Isaya 54:4–10; 57:15–19, unajifunza nini juu ya rehema ya Mwokozi na hisia Zake juu yako? Kuna tofauti gani katika maisha yako kujua vitu hivi vinavyomhusu Yeye?

Ni jinsi gani baraka zilizoelezewa katika Isaya 54:11–17 zinafanyakazi kwako?

Isaya 55–56

Bwana anawaalika wote “kushika agano langu.”

Kwa vizazi vingi, Israeli ilitambuliwa kama watu wa agano la Mungu. Walakini, mpango wa Mungu umejumuisha zaidi ya taifa moja tu, kwani “kila aonaye kiu” amealikwa “njoni … majini” (Isaya 55:1). Weka hili akilini mwako unaposoma Isaya 55 na56, na tafakari inamaanisha nini kuwa watu wa Mungu. Je! Ni ujumbe gani wa Mungu kwa wale ambao wanahisi “wametengwa kabisa” kutoka Kwake? (Isaya 56:3). Fikiria kuweka alama mistari inayoelezea mitazamo na matendo ya wale ambao “wanashikilia agano langu” (ona Isaya 56:4–7).

ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Isaya 51–52.Unapojadili mialiko ya Bwana katika sura hizi, unaweza kuwaalika wanafamilia kuigiza. Kwa mfano, inaonekanaje “inueni macho yenu mbinguni,” “amka, simama,” au “jikung’ute mavumbi”? (Isaya 51:6,17; 52:2). Ni nini virai hivi vinatufundisha kuhusu kumfuata Yesu Kristo?

Isaya 52:9.Baada ya kusoma mstari huu, familia yako inaweza “kuimba pamoja” wimbo au wimbo wa watoto ambao huwaletea furaha. Ni ahadi gani katika Isaya 52 ambazo zinatusababisha “kujawa na furaha”?

Isaya 52:11; 55:7.Hii mistari inaweza kuelekeza majadiliano kuhusu kile kirai “Kuweni wasafi” kinaweza kumaanisha. Kama sehemu ya majadiliano haya, unaweza kupitia mada katika Kwa Ajili ya Nguvu za Vijana (kijitabu, 2011) au soma maandiko kuhusu baraka za kuwa safi kiroho (ona 3 Nefi 12:8; Mafundisho na Maagano 121:45–46)).

Isaya 53.Kutambulisha maelezo ya Isaya ya Mwokozi, familia yako inaweza kuzungumza juu ya jinsi hadithi, sinema, na mitandao mingine mara nyingi inaonyesha mashujaa wanaowaokoa watu. Unaweza kulinganisha picha hizo na maelezo ya Mwokozi uliyosoma katika Isaya 53. Ungeweza pia kuangalia video “My Kingdom Is Not of This World” (ChurchofJesusChrist.org) na kuzungumza kuhusu jinsi unabii katika Isaya 53 ulivyotimizwa. Ni baadhi ya huzuni na masikitiko gani ambayo Mwokozi aliyabeba kwa ajili yetu?

Isaya 55:8–9.Je, ni kwa namna gani vitu huonekana tofauti unapokuwa juu ya ardhi? Inamaanisha nini kwako kwamba njia na akili za Mungu zipo juu zaidi yetu?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “I Stand All Amazed,” Nyimbo za Kanisa, na.193.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Tumia muziki. Nyimbo za Kanisa hufundisha kanuni za injili kwa nguvu. Fikiria kusikiliza au kusoma nyimbo za sakramenti ili kukusaidia kuelewa ukweli kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo unaofundishwa katika Isaya 53. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 22.)

mchoro wa Kristo

Nuru Yake, na Michael T. Malm