Agano la Kale 2022
Septemba 26–Oktoba2. Isaya 50–57: “Ameyachukua Masikitiko Yetu na Amejitwika Huzuni Zetu”


“Septemba 26–Oktoba2. Isaya 50–57: ‘Ameyachukua Masikitiko Yetu na Amejitwika Huzuni Zetu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Septemba 26–Oktoba2. Isaya 50–57,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Kristo akiwa amevaa taji ya miiba na akifanyiwa dhihaka na askari

Kufanyiwa Dhihaka kwa Kristo, na Carl Heinrich Bloch

Septemba 26–Oktoba2

Isaya 50–57

“A meyachukua Masikitiko Yetu na Amejitwika Huzuni Zetu”

Isaya 50–57 ina lugha ya kupendeza ambayo watoto unaowafundisha wanaweza wasiielewe. Unapojiandaa kufundisha, tafakari ukweli rahisi ambao maneno haya yanafundisha na jinsi utakavyowasaidia watoto kujifunza.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Muhimize kila mtoto kushiriki jinsi wanavyojua kwamba Yesu Kristo anawapenda. Waombe kushiriki kile wanachofanya ili kuonesha kwamba wanampenda Yesu.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Isaya 53:4

Yesu Kristo aliteseka kwa ajili yangu kwa sababu Ananipenda.

Kupitia dhabihu Yake ya kulipia dhambi, Yesu Kristo aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu na kujichukulia juu Yake “masikitiko” yetu na “huzuni zetu.” Ni jinsi gani utawashuhudia watoto juu ya Upatanisho wa Mwokozi?

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya Mwokozi akiteseka msalabani na katika Bustani ya Gethsemane (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 56, 57, au sura 51–53 katika Hadithi za Agano la Kale). Waombe watoto waelezee kile wanachokiona katika picha na kushiriki kile wanachojua kuhusu kile kinachotendeka. Kwa nini Yesu Aliteseka kwa ajili yetu?

  • Wasomee watoto kutoka Isaya 53:4: “Ameyachukua masikitiko yetu na amejitwika huzuni zetu.” Waoneshe watoto kitu kizito (au picha ya kitu hicho) na waalike wajifanye kunyanyua kitu kizito. Eleza kwamba “masikitiko” na “huzuni” (au kukosa furaha) vinaweza kuwa vizito na vigumu kubeba. Shuhudia kwamba Yesu Kristo atatusaidia kubeba vitu hivi kwa sababu Yeye anatupenda.

Isaya 55:6

Ninaweza kumtafuta Bwana na kumlilia Yeye.

Tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa inamaanisha nini “kumtafuta” Yesu katika maisha yetu yote.

Shughuli Yamkini

  • Ficha picha ya Yesu mahali fulani chumbani, na waalike watoto kuitafuta. Soma maneno “Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana” kutoka Isaya 55:6. Waombe watoto wataje baadhi ya njia wanazoweza kumtafuta Bwana—ambayo ina maana kwamba wanajitahidi kujifunza kuhusu Yeye na kuja karibu na Yeye. Kila wakati mtoto anapotoa jibu, ficha picha tena na mwalike mtoto “kuitafuta”.

  • Wasaidie watoto wajifunze maneno kwenye wimbo “Seek the Lord Early” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,108) au wimbo mwingine kuhusu kuja karibu na Mwokozi. Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kuchagua kitu watakachofanya ili “kumtafuta … Bwana.”

  • Soma kirai “Mwiteni, maadamu yu karibu” kutoka Isaya 55:6. Je, ni kwa jinsi gani tunamwita Baba wa Mbinguni? Waombe watoto wazungumze kuhusu kile wanachosema katika sala zao. Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda na anawasikia wakati wanaposali.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Isaya 51–52

Bwana ananialika mimi “kujivika nguvu [yangu].”

Katika Isaya51 na52, Bwana alitumia virai kama vile “amka,” “simama,” na “jivike nguvu” ili kuwapa msukumo watu Wake kuishi kufikia uwezekano wao wa kiungu. Fikiria ni jinsi gani vifungu hivi vya maneno vinaweza kuwapa msukumo watoto unaowafundisha.

Shughuli Yamkini

  • Kabla ya darasa, andika ubaoni vifungu kadhaa vya maneno kutoka Isaya 51–52 ambavyo vinaelezea matendo ambayo Bwana anataka watu Wake wafanye, kama vile “ Inueni macho yenu,” “Amka,” “Simama,” “Jikung’ute mavumbi,” na “Pigeni kelele za furaha” (Isaya 51:6,17; 52:2,9). Waruhusu watoto wafanye zamu kuigiza moja ya vifungu hivyo wakati wengine darasani wakijaribu kubahatisha tendo hilo linamaanisha nini. Baada ya kila zamu, waoneshe watoto kifungu cha maneno katika maandiko na jadili pamoja nao maana ya kiroho ya kifungu hicho. Bwana anatuomba tufanye nini? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya kila moja ya mambo haya?

  • Waalike watoto wasome Isaya 51:1, 4,7 na bainisha nani Bwana anazungumza naye na nini Yeye anawataka wao wafanye. Je, nini maana ya “kumsikiliza” Bwana? Ili kueleza kwa mfano, muombe mmoja wa watoto kutoa maelekezo rahisi ambayo wengine wanapaswa kuyafuata. Kwa nini wakati mwingine ni vigumu kumsikiliza na kumtii Bwana? Je, tunawezaje kumwonesha Bwana kwamba “tunamsikiliza” Yeye?

Picha
sanamu ya Kristo akiwa amebeba msalaba

Kwa sababu ya Upendo, na mchongaji Angela Johnson

Isaya 53:3–9

Yesu Kristo alijichukulia juu Yake dhambi zangu na huzuni zangu.

Je, unawezaje kuyatumia maneno ya Isaya kuwasaidia watoto waelewe kwa kina zaidi kile Mwokozi alichofanya kwa ajili yao?

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha kadhaa zikielezea mateso na kifo cha Yesu Kristo (ona, kwa mfano, Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 56, 57, 58). Someni pamoja Isaya 53:3–6,9, na waalike watoto kutafuta vifungu vya maneno ambavyo vinaelezea matukio katika picha. Shuhudia kwamba maelfu ya miaka kabla ya Yesu Kristo kuteseka kwa ajili yetu, manabii kama Isaya walikuwa wakifundisha kuhusu matukio haya muhimu. Kwa nini ingekuwa muhimu watu kujua mambo haya miaka mingi kabla? (ona Alma 39:15–19).

  • Waalike watoto wasome Isaya 53:4–7 na watafute maneno ambayo yanaelezea kile Mwokozi alichoteseka kwa ajili yetu. Waombe waandike maneno haya ubaoni. Kwa nini Yeye aliteseka “masikitiko,” “huzuni,” na “maovu”? (Ona pia Alma 7:11–12). Shiriki na watoto jinsi Mwokozi alivyokusaidia kubeba masikitiko na huzuni zako. Waruhusu kushiriki jinsi wanavyojisikia kuhusu Mwokozi na kile alichofanya kwa ajili yao.

Isaya 55:7–9

Njia za Bwana zi juu sana kuliko njia zangu.

Wakati tunapoelewa kwamba mawazo na njia za Bwana zi juu kuliko zetu, inakuwa rahisi kumtumaini Yeye.

Shughuli Yamkini

  • Waulize watoto ni nani wangemwendea kama wamepata tatizo kubwa na kwa nini. Soma pamoja na watoto Isaya 55:8–9, na waombe wasikilize sababu za kwa nini tunapaswa kutafuta mwongozo wa Bwana wakati tunapohitaji msaada.

  • Chora ubaoni anga na ardhi, na uzipe majina Mbingu na Dunia. Kisha waalike watoto wasome Isaya 55:9 ili kutafuta kile Bwana alichokifananisha na mbingu na dunia na waombe waweke majina haya mengine kwenye michoro. Inamaanisha nini kwamba njia na mawazo ya Bwana zi “juu sana” kuliko zetu? Kwa nini ni muhimu kwetu kujua hili?

  • Jadili pamoja na watoto baadhi ya njia za Bwana ambazo zi juu sana kuliko zetu. Kwa mfano, ni ipi njia Yake ya kuwatendea wenye dhambi? (ona Marko 2:15–17). Je, ni ipi njia Yake ya kuwaongoza wengine? (ona Mathayo 20:25–28). Je, ni kwa jinsi gani njia Zake zimetofautiana na njia za watu wengine? Waambie watoto jinsi ulivyojifunza kutumainia njia za juu na mawazo ya juu ya Bwana.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Pendekeza kwa watoto kwamba waweke lengo ambalo litawasaidia kuja karibu na Yesu Kristo, kwa kuzingatia jambo walilojifunza darasani leo. Waalike kushiriki lengo hilo pamoja na mwanafamilia.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto wadogo wajifunze kutoka kwenye maandiko. Ili kuwasaidia watoto wadogo kujifunza kutoka kwenye maandiko, fokasi katika mstari mmoja au hata kifungu kimoja cha maneno muhimu tu. Wakati mwingine unaweza kusoma kifungu na kuwaalika watoto kusimama au kuinua mikono yao juu wakati wanaposikia neno fulani au kifungu unachotaka kukizingatia.

Chapisha