Agano la Kale 2022
Oktoba 10–16. Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20: “Kabla Sijakuumba katika Tumbo Nalikujua”


“Oktoba 10–16. Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20: ‘Kabla Sijakuumba katika Tumbo Nalikujua’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Oktoba 10–16. Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20: ,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

nabii akizungumza na wanaume

Yeremia, na Walter Rane

Oktoba 10–16

Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20

“Kabla Sijakuumba katika Tumbo Nalikujua”

“Lengo la kila mwalimu wa injili … ni kufundisha mafundisho safi ya injili, kwa mwongozo wa Roho, ili kuwasaidia watoto wa Mungu kujenga imani yao kwa Mwokozi na kuwa zaidi kama Yeye” (Kufundisha katika njia ya Mwokozi, jalada la mbele).

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Andika kwenye vipande vya karatasi maneno machache muhimu kutoka kwenye usomaji wa wiki hii wa Yeremia, kama vile nabii, maji yaliyo hai, kukusanyika, na udongo wa mfinyanzi. Weka karatasi ndani ya chombo na waalike watoto wachukue moja na kushiriki mawazo yoyote waliyonayo kuihusu. Wasaidie waone jinsi maneno yanavyohusiana na jambo ambalo Yeremia alifundisha.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Yeremia 1:5

Baba wa Mbinguni alinijua kabla sijazaliwa.

Kwa sababu tuliishi na Mungu kabla ya kuja duniani, Yeye anatujua, hata kama sisi hatuwezi kukumbuka. Unawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa ukweli huu muhimu?

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto Yeremia 1:5, na eleza kwamba Mungu alimjua nabii Yeremia kabla hajazaliwa. Mwambie kila mtoto, binafsi, kwamba Baba wa Mbinguni alimjua pia kabla hajazaliwa na kwamba Yeye alimleta kila mmoja wetu hapa kwa dhumuni.

  • Waoneshe watoto picha ya kichanga na waulize watoto ikiwa wanafahamu mahali ambapo kichanga huyu aliishi kabla ya kuzaliwa. Imbeni pamoja wimbo unaofundisha kuhusu maisha yetu kabla ya kuzaliwa tukiwa pamoja na Mungu, kama vile “I Am a Child of God” au “I Lived in Heaven” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3,4). Zungumza kuhusu hisia za kiroho zinazoletwa na wimbo. Toa ushuhuda wako kwamba sote hapo awali tuliishi na Baba wa Mbinguni na kwamba Yeye alituleta hapa duniani.

Yeremia 1:7

Manabii wameitwa kuzungumza maneno ya Bwana.

Wito wa Yeremia unaonesha kitu ambacho Bwana anawataka manabii wafanye. Unawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha kuimarisha hamu yao ya kumfuata nabii aliye hai?

Shughuli Yamkini

  • Waoneshe watoto picha ya nabii aliye hai na waalike kushiriki kile wanachojua kuhusu yeye. Je, manabii wanafanya nini? Wasomee watoto kitu ambacho Bwana alisema kwa nabii mwingine, Yeremia, katika Yeremia 1:7. Waalike watoto watembee mahali pamoja wakati ukisoma “utakwenda kwa wote nitakaokutuma kwao” na kujifanya kuzungumza wakati unaposoma “nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.” Shiriki ushuhuda wako kwamba manabii hufanya na kusema kile Bwana anachoamuru.

  • Onesha picha za manabii kutoka kwenye maandiko (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, majarida ya Kanisa, na Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waruhusu watoto wakuambie kile wanachokifahamu kuhusu manabii hawa. Kwa ufupi waambie watoto kuhusu jambo kila mmoja alilofanya ili kusaidia kwenye kazi ya Mungu. Toa ushuhuda wako kwamba manabii wameitwa na Mungu kuzungumza maneno Yake na kuwatumikia watu Wake.

Yeremia 16:16

Ninaweza kuwasaidia watoto wa Baba wa Mbinguni kurudi Kwake.

Akinukuu Yeremia 16:16, Rais Russell M. Nelson alisema, “Wamisionari wetu wamewatafuta wale Waisraeli waliyotawanyika; wamewawinda ‘ndani ya mashimo ya miamba’; na wamewavua kama vile siku za kale” (“The Gathering of Scattered Israel,” Liahona, Nov. 2006,81).

Shughuli Yamkini

  • Unaposoma Yeremia 16:16, waalike watoto wajifanye kuvua samaki au kuwinda. Eleza kwamba wavuvi na wawindaji katika mstari huu huwakilisha wamisionari. Waalike watoto wajifanye kuwa wamisionari. Wamisionari hufanya nini? Tunawezaje kuwasaidia?

  • Tengeneza mchezo wa kuoanisha kwa kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Wakati mtoto anapopata picha inayofanana, zungumzeni kuhusu nini picha ile huonesha kuwa tunaweza kufanya ili kuwasaidia watoto wa Baba wa Mbinguni kurudi kwake.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Yeremia 1:4–19

Manabii wameitwa kuzungumza neno la Bwana.

Ni jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto waimarishe imani yao, na uelewa wa jukumu la manabii katika ufalme wa Mungu?

Shughuli Yamkini

  • Chagua mistari muhimu kutoka Yeremia1 ambayo hufundisha kweli za msingi kuhusu manabii, kama vile mistari 5, 7, 10, na19. Mwalike kila mtoto kuchagua moja ya mistari, kuusoma na kushiriki jambo analojifunza kuhusu manabii kutoka kwenye mstari huo. Waalike vijana wachache kushiriki shuhuda zao juu ya Joseph Smith.

  • Onesha picha ya nabii aliye hai na imbeni pamoja wimbo kuhusu manabii, kama vile “We Listen to a Prophet’s Voice” (Nyimbo za Kanisa, na.22). Wasaidie watoto watengeneze orodha ya mambo ambayo nabii aliye hai ametuomba kufanya. Chagua ujumbe wa mkutano wa hivi karibuni kutoka kwa nabii na wasaidie watoto watafute ushauri katika ujumbe wake. Ni kwa jinsi gani tunamfuata nabii? Jadili jinsi ushauri kutoka kwa manabii unavyotusaidia kumfuata Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo vyema zaidi.

  • Onesha video “Why Do We Have Prophets?” (ChurchofJesusChrist.org), na waulize watoto jinsi ambavyo wangeelezea kwa rafiki kwa nini ni baraka kuwa na nabii aliye hai (ona Makala ya Imani 1:6,9). Waalike watoto kushiriki hisia zao kuhusu nabii aliye hai.

Yeremia 16:14–15

Ninaweza kuwa sehemu ya kukusanya Israeli.

Ujumbe kuhusu kukusanya Israeli unaopatikana katika Yeremia 16:14–15 unaweza kutoa fursa kubwa ya kuzungumza na watoto kuhusu kazi ya umisionari na historia ya familia. Hii ni njia moja ambayo “tunasimama kama mashahidi wa Mungu” (Mosia 18:9).

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Yeremia 16:14, na waombe watoto kushiriki maelezo ya kina wanayokumbuka kuhusu jinsi “Bwana … alivyowatoa wana wa Israeli kutoka nchi ya Misri” (ona Kutoka14). Waalike wasome Yeremia 16:15 kutafuta ni tukio gani Yeremia alisema lingekuwa hata la kukumbukwa zaidi ya hilo. Eleza kwamba Israeli ilikuwa imetawanyika kote duniani, lakini Mungu aliahidi kuwakusanya tena Kwake na kwenye Kanisa Lake. Hii huitwa kukusanywa kwa Israeli. Ni jinsi gani hii inafanana na kuwakomboa watu kutoka utumwani?

  • Shiriki kauli hii kutoka kwa Rais Russell M. Nelson: “Wakati wowote unapofanya kitu chochote kinachomsaidia mtu yeyote—upande wowote wa pazia—kuchukua hatua kusonga mbele kuelekea kufanya maagano na Mungu na kupokea ibada zao muhimu za ubatizo na za hekaluni, wewe unasaidia katika kukusanya Israeli” (Russell M. Nelson na Wendy W. Nelson, “Tumaini la Israeli” [ibada fupi ya vijana duniani kote, Juni 3, 2018], nyongeza katika New Era na Ensign, Agosti 2018,15, ChurchofJesusChrist.org Tunawezaje kusaidia kuikusanya Israeli?

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu kazi ya umisionari, kama vile “I Hope They Call Me on a Mission” au “Called to Serve” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 169,174), au onesha video “Your Day for a Mission” (ChurchofJesusChrist.org). Waulize watoto kile wanachojifunza kutokana na wimbo au video hii kuhusu kwa nini mtu angechagua kuhudumu misheni.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto wapeleke nyumbani nakala ya ukurasa wa shughuli ya wiki hii na kucheza mchezo wa kuoanisha pamoja na familia zao. Wahimize wazungumze na familia zao kuhusu jinsi kazi ya umisionari ilivyowabariki.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto kumtambua Roho. Muziki mtakatifu mara zote hukaribisha ushawishi wa Roho Mtakatifu. Unapoimba na watoto, chukua muda kuwasaidia kutambua hisia za kiroho ambazo huthibitisha ukweli wa kile wanachojifunza.