Agano la Kale 2022
Oktoba 3–9. Isaya 58–66: “Mkombozi Atakuja Sayuni”


“Oktoba 3–9. Isaya 58–66: ‘Mkombozi Atakuja Sayuni,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Oktoba 3–9. Isaya 58–66,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Famila: 2022

Picha
Yesu akifundisha ndani ya sinagogi

Yesu katika Sinagogi huko Nazareti, na Greg K. Olsen

Oktoba 3–9

Isaya 58–66

“Mkombozi Atakuja Sayuni”

Unaposoma Isaya 58–66, fikiria jinsi maneno ya Isaya yanavyokupa furaha na tumaini la baadaye.

Andika Misukumo Yako

Mwanzoni mwa huduma yake ya duniani, Yesu Kristo alitembelea sinagogi huko Nazareti, kijiji ambacho Yeye alilelewa. Hapo Alisimama kusoma kutoka kwenye maandiko, akafungua kitabu cha Isaya, na kusoma kile tunachojua sasa kama Isaya 61:1–2. Kisha akatangaza, “Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.” Hii ilikuwa mojawapo ya matamko ya moja kwa moja ya Mwokozi kwamba Yeye ndiye Mpakwa Mafuta, ambaye “atawaponya waliovunjika moyo” na “kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao” (ona Luka 4:16–21). Maandiko haya kwa kweli yalitimizwa siku hiyo. Na, kama vile unabii mwingi wa Isaya, unaendelea kutimizwa katika siku zetu. Mwokozi anaendelea kuwaponya wote waliovunjika moyo ambao huja Kwake. Bado kuna mateka wengi ambao kwao wokovu lazima uhubiriwe. Na kuna mazuri ya baadaye ya kujiandaa kwa ajili yake—wakati ambapo Bwana “ataumba mbingu mpya na dunia mpya” (Isaya 65:17) na “kusababisha haki na sifa mbele ya mataifa yote” (Isaya 61:11). Kusoma Isaya kunatufungua macho yetu kwa kile Bwana amekwisha kifanya, kile anachofanya, na kile atakachowafanyia watu Wake.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Isaya 58:3–12

Kufunga huleta baraka.

Mistari hii inaonyesha kwamba kwa Waisraeli wengi wa zamani, kufunga ilikuwa mzigo zaidi kuliko baraka. Wengi wetu tunaweza kujilinganisha na hali hiyo wakati mwingine. Kama ungependa kupata maana zaidi na kusudi la kufunga kwako, soma Isaya 58:3–12 kupata majibu ya Bwana kwa swali “Kwa nini tunafunga?” Katika uzoefu wako, ni kwa jinsi gani kufunga kunaweza kufungua minyororo ya uovu” na “kuvunja kila nira”? (Isaya 58:6). Ni kwa namna gani kufunga kumekuletea baraka zilizoelezwa katika Isaya 58:8–12? Ni kwa jinsi gani Isaya 58:3–12 inaathiri mawazo yako juu ya kufunga?

Katika ujumbe wake, ““Je, Saumu Niliyoichagua, Siyo ya Namna Hii?Liahona, Mei 2015, 22–25), Rais Henry B. Eyring alishiriki mifano kadhaa ya jinsi watu walivyobarikiwa kwa mfungo na matoleo. Ni kwa jinsi gani umeshuhudia baraka kama hizo katika maisha yako?

Ona pia Mada za Injili, “Mfungo na Matoleo” (topics.ChurchofJesusChrist.org).

Isaya 59:9–21; 61:1–3; 63:1–9

Yesu Kristo ni Mwokozi na Mkombozi wangu.

Katika Isaya 58–66 utapata marejeleo mengi juu ya misheni ya upatanisho wa Yesu Kristo. Hapa kuna mifano michache, pamoja na maswali ya kukusaidia kuyatafakari.

  • Isaya 59:9–21. Je! Unawezaje kufupisha hali ya kiroho ya watu walioelezewa katika mstari wa 9–15? Ni nini kinachokuvutia juu ya maelezo ya “mwombezi” katika mistari wa 16–21 na agano ambalo Yeye hufanya na wale wanaomwendea Yeye?

  • Isaya 61:1–3. Je! Yesu Kristo amekubariki vipi katika njia zilizoelezewa katika mistari hii? Amekuletea “habari njema gani”? Je! Amekupaje uzuri badala ya majivu?

  • Isaya 63:7–9. Je! ni “fadhili gani za Bwana” ambazo unaweza kuzitaja? Je! Ni hisia gani kwa Mwokozi ambazo mistari hii inashawishi moyoni mwako?

Je! Unapata marejeo gani mengine kwa Mwokozi katika Isaya 58–66?

Ona pia Mosia 3:7; Mafundisho na Maagano 133:46–53.

Picha
mwanamke akiwasha taa ya mafuta ya udongo kutoka kwa taa iliyoshikiliwa na mikono ya mwanadamu

“Bwana atakuwa nuru ya milele kwako” (Isaya 60:19). Zawadi ya Nuru, na Eva Timothy

Isaya 60; 62

“Bwana atakuwa nuru ya milele kwako.”

Isaya 60 na62 sema juu ya nuru na giza, macho na kuona, kufundisha juu ya jinsi injili ya Yesu Kristo itakavyoibariki dunia katika siku za mwisho. Tafuta dhana hizi hususani katika Isaya 60:1–5, 19–20; 62:1–2. Unaposoma sura hizi, tafakari jinsi Mungu anavyowakusanya watoto Wake toka gizani kuja kwenye nuru Yake. Jukumu lako ni lipi katika kazi hii?

Ona pia 1 Nefi 22:3–12; 3 Nefi 18:24; Mafundisho na Maagano 14:9; Bonnie H. Cordon, “Ili Wapate Kuona,” Liahona, Mei 2020, 78–80.

Isaya 64:1–5; 65:17–25; 66

Kristo atatawala duniani wakati wa Milenia.

Isaya alisema juu ya siku ambapo “taabu za kwanza zimesahauliwa” (Isaya 65:16). Wakati unabii huu una utimilifu kadhaa, kwa maana yake kamili, siku hiyo bado inakuja—wakati Yesu Kristo atakaporudi duniani na kuanzisha enzi ya amani na haki iitwayo Milenia. Isaya alielezea siku hii ya baadaye katika Isaya 64:1–5; 65:17–25; 66. Angalia ni mara ngapi alitumia maneno kama “furahi” na “kufurahia.” Tafakari kwa nini kurudi kwa Mwokozi itakuwa siku ya furaha kwako. Je, unaweza kufanya nini kujiandaa kwa ajili ya ujio Wake?

Ona pia Makala ya Imani 1:10; Russell M. Nelson, “Siku za Baadaye za Kanisa: Kuuandaa Ulimwengu kwa Ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi,” Ensign, Apr. 2020, 13–17.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Isaya 58:3–11.Wanafamilia wanaweza kuelewa vizuri ujumbe wa Isaya juu ya kufunga ikiwa wataigiza aina ya kufunga ilivyoelezewa katika Isaya 58:3–5 na aina ya kufunga ilivyoelezewa katika Isaya 58:6–8. Je! Tunawezaje kufanya kufunga kwetu kuwe kama “mfungo ambao [Mungu] amechagua”? Je! Ni baraka gani tumeziona kutokana na mfungo?

Isaya 58:13–14.Je! Kuna tofauti gani kati ya “kupata raha [yetu] wenyewe” na kutafuta “kufurahia … katika Bwana” siku ya Sabato? Tunawezaje kuifanya Sabato kuwa “ya kufurahisha”?

Isaya 60:1–5.Unaposoma Isaya 60:1–3, wanafamilia wangeweza kuwasha taa wakati mistari inataja nuru na kuizima wakati mistari inapotaja giza. Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo ni kama nuru kwetu? Je! Isaya aliona nini kitatokea wakati watu wa Mungu wakishiriki nuru ya injili? (Ona Isaya 60:3–5).

Isaya 61:1–3.Je! Mwokozi ametimizaje unabii wa Isaya katika mistari hii? Unaweza kuwaalika wanafamilia kutafuta picha za Mwokozi ambazo wanahisi zinaonyesha mambo haya ya misheni Yake (picha zinaweza kupatikana katika majarida ya Kanisa au Kitabu cha Sanaa za Injili). Unaweza pia kuimba wimbo kuhusu jinsi Mwokozi anatubariki, kama vile “I Feel My Savior’s Love” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa “When He Comes Again,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Andaa Mazingira yako. Mazingira yetu yanaweza kuathiri uwezo wetu wa kujifunza. Tafuta mahali pa kusoma maandiko ambapo unaweza kuhisi ushawishi wa Roho. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 15.)

Picha
Yesu akiwa angani

“Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia.” (Isaya 60:1). Nuru na Uzima, na Mark Mabry

Chapisha