Agano la Kale 2022
Oktoba 10–16. Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20: “Kabla Sijakuumba Katika Tumbo Nilikujua”


“Oktoba 10–16. Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20: ‘Kabla Sijakuumba Katika Tumbo Nilikujua,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Oktoba 10-16. Yeremia 1–3; 7; 16–18–30; 20,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Nabii akiongea na wanaume

Yeremia, na Walter Rane

Oktoba 10–16

Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20

“Kabla Sijakuumba Katika Tumbo Nilikujua”

Mzee David A Bednar alisema: “Mojawapo ya njia ninazomsikia [Bwana] ni katika maandiko. Maandiko ni sauti ya Bwana iliyorekodiwa awali” (“Msikilize Yeye katika Moyo Wako na katika Akili Zako,” ChurchofJesusChrist.org).

Andika Misukumo Yako

Kwanza, Yeremia hakufikiria iwapo angekuwa nabii mzuri. “Tazama, siwezi kusema,” alipinga wakati Bwana alipomwita mara ya kwanza (Yeremia 1:6). Bwana alimhakikishia, “Nimetia maneno yangu kinywani mwako” (mstari wa 9), Yeremia alihisi kuwa yeye ni “mtoto” asiye na uzoefu (mstari wa 6), lakini Bwana alielezea kwamba alikuwa amejiandaa zaidi kuliko alivyofikiria—alikuwa ametawazwa kwa wito huu hata kabla ya kuzaliwa (ona mstari wa 5). Hivyo Yeremia akaweka kando woga wake na akakubali wito. Aliwaonya wafalme na makuhani wa Yerusalemu kwamba utakatifu wao wa kujifanya hautawaokoa kutokana na uharibifu. “Mtoto” ambaye alidhani kuwa hawezi kusema alikuja kuhisi neno la Mungu “moyoni [mwake] kama moto uwakao” na hakuweza kunyamaza (Yeremia 20:9).

Hadithi ya Yeremia ni hadithi yetu pia. Mungu alitujua, pia, kabla hatujazaliwa na alituandaa kufanya kazi Yake hapa duniani. Miongoni mwa mambo mengine, kazi hiyo ni pamoja na jambo ambalo Yeremia aliliona mapema: kukusanya watu wa Mungu, mmoja mmoja, “kuwaleta Sayuni” (Yeremia 3:14). Na hata kama hatujui nini cha kufanya au kusema, hatupaswi “kuogopa…; kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, asema Bwana” (Yeremia 1:8, 19).

Kwa ajili ya muhtasari wa kitabu cha Yeremia, ona “Yeremia” katika Kamusi ya Biblia.

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Yeremia 1:4–19; 7:1–7; 20:8–10

Manabii wameitwa kusema neno la Bwana.

Unaposoma katika Yeremia 1:4–19 kuhusu wito wa Yeremia kuwa nabii, tafakari jukumu la manabii katika maisha yako. Unajifunza nini kuhusu manabii kutoka kwenye maneno ya Bwana kwa Yeremia? (ona pia Yeremia 7:1–7). Mahubiri ya Yeremia mara nyingi yalikataliwa (ona Yeremia 20:8, 10). Unajifunza nini kutoka kwa maneno ya Yeremia katika Yeremia 20:9? Weka mawazo haya akilini wakati wote wa masomo yako ya mafundisho ya Yeremia. Ni kipi unachopata katika mafundisho haya ambacho inakuhimiza kufuata manabii wetu wa siku za mwisho?

Yeremia 1:5

Mungu alinijua kabla sijazaliwa.

Kabla ya kuzaliwa kwa Yeremia, Mungu alimjua na akamchagua, au kumteua mapema, kutimiza utume maalum hapa duniani (ona Yeremia 1:5). Kwa nini unafikiri ilikuwa muhimu kwa Yeremia kujua hivi?

Mungu pia alikujua kabla hujazaliwa na alikutawaza kwa majukumu maalum (ona Alma 13:1–4; Mafundisho na Maagano 138:53–56; Ibrahimu 3:22–23). Je! Maarifa haya yanaweza kuleta tofauti gani katika maisha yako? Ikiwa umepokea baraka yako ya patriaki, unaweza kuipitia kwa maombi na kumwuliza Mungu jinsi ya kutimiza kile alichoamua mapema ufanye.

Ona pia Mada za Injili, “Julikana Tangu Zamani,” “Kubala Kuzaliwa,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

mtu amesimama katika tangi la maji la kale

Watu katika Israeli ya kale walitumia mabirika kuhifadhi maji yenye thamani.

Yeremia 2; 7

“Wameniacha mimi chemchemi ya maji ya uzima.”

Katika eneo kame ambalo Waisraeli waliishi, watu walihifadhi maji yenye thamani katika mabwawa ya chini ya ardhi yaliyoitwa matangi. Kwa nini kupokea maji kutoka kwenye chemchemi itakuwa bora kuliko kutegemea matangi? Inamaanisha nini kuacha “chemchemi ya maji yaliyo hai”? Unafikiria “matangi yaliyovunjika” yaliyotajwa katika Yeremia 2:13 yanaweza kumaanisha nini? Unaposoma Yeremia 2 na7, angalia jinsi watu walivyokuwa wanaacha maji ya uzima ya Bwana, na fikiria juu ya jinsi unavyopokea maji ya uzima maishani mwako.

Yeremia 7 inaelezewa kwa wale ambao walikuwa wakiingia “lango la nyumba ya Bwana … kumwabudu Bwana” (Yeremia 7:2). Walakini licha ya mwonekano wa nje kwa kujitolea, walikuwa na hatia ya uovu mkubwa (ona mstari wa 2–11). Ni jumbe gani unahisi Bwana anaweza kuwa nazo kwa ajili yako katika mstari wa 21–23?

Yeremia 3:14–18; 16:14–21

Bwana atawakusanya watu Wake.

Wakati Yeremia alitabiri juu ya kukusanyika kwa Israeli iliyotawanyika, alisema itakuwa kubwa zaidi kuliko Kutoka Misri (ona Yeremia 16:14–15). Katika roho kama hiyo, Rais Russell M. Nelson alisema: “Ulitumwa duniani wakati huu sahihi … kusaidia kukusanya Israeli. Hakuna chochote kinachotokea katika dunia hii sasa ambacho ni muhimu zaidi ya huku [kukusanyika]. … Kukusanya huku hakuna budi kumaanisha kila kitu kwako” (Russell M. Nelson na Wendy W. Nelson, “Tumaini la Israeli” [ibada ya vijana duniani kote, Juni 3, 2018, nyongeza katika New Era na Ensign, 2018,12, ChurchofJesusChrist.org

Unapojifunza Yeremia 3:14–18; 16:14–21, ni nini kinachokuhimiza juu ya mkusanyiko wa Israeli wa siku za mwisho? Mistari hii inapendekeza nini juu ya jinsi gani mkusanyiko unatokea? Ni umaizi gani wa ziada unaupata katika ujumbe mzima wa Rais Nelson uliotajwa hapo juu?

ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Yeremia 1:5.Unaweza kuutumia mstari huu kuongea kuhusu maisha yetu pamoja na Baba wa Mbinguni kabla ya kuzaliwa. Nyenzo kama “I Lived in Heaven” (Children’s Songbook, 4) na “Utangulizi: Mpango wa Baba yetu wa Mbinguni” (katika Hadithi za Agano Jipya, 1–5) zinaweza kusaidia. Ni kwa jinsi gani kujua kuhusu maisha ya awali kunaathiri jinsi tunavyoishi maisha ya Duniani?

Yeremia 2:13; 17:13–14.Ili kuwasaidia wanafamilia kuona mistari hii, unaweza kuonyesha kinachotokea unapoweka maji kwenye chombo kilichopasuka au kilichovunjika. Je! “Chemchemi ya maji ya uzima” na “tangi la maji lililovunjika” vinaweza kuwakilisha nini? Yeremia 2:13. Je! Tunakunywaje maji ya uzima ya Bwana?

Yeremia 16:16.Rais Russell M. Nelson amelinganisha wavuvi na wawindaji katika mstari huu na wamisionari wa siku za mwisho (ona “Kukusanywa kwa Israeli Iliyotawanyika,” Ensign au Liahona, Nov. 2006, 81). Wanafamilia wangeweza “kutafuta” vitu kwenye nyumba yenu na kuzungumza juu ya jinsi unaweza kusaidia “kuvua samaki” na “kuwinda” kwa ajili ya Israeli iliyotawanyika.

Yeremia 18:1–6.Kuchunguza mistari hii, unaweza kujadili au kuonyesha jinsi ufinyanzi unavyofanyika. Je, ni ujumbe upi Bwana anao kwa ajili ya Israeli katika Yeremia 18:1–6? Je, inamaanisha nini kuwa udongo mikononi mwa Bwana? (ona pia Isaya 64:8). Kwa hadithi nyingine inayotulinganisha na udongo wa mfinyanzi, ona ujumbe wa Mzee Richard J. Maynes “Shangwe ya Kuishi Maisha Yanayolenga kwa Kristo” (Ensign au Liahona, Nov. 2015, 27–30).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Israel, Israel, God Is Calling,” Nyimbo za Kanisa, na. 7.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia hadithi. Mwokozi mara nyingi alifundisha kwa kutumia hadithi. Fikiria hadithi kutoka kwenye maisha yako mwenyewe ambazo zinaweza kufanya kanuni za injili kuwa hai. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 22.)

udongo kwenye gurudumu la mfinyanzi

“Angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli” (Yeremia 18:6).